Tikiko ni mmoja wa washirika waliohudumu na mtume Paulo katika kazi injili. Ijapokuwa si mtu anayejulikana sana..lakini ametajwa sehemu kadha wa kadha katika vitabu vya agano jipya.
> Anatajwa kama mmoja wa watu waliomua kufuatana na Paulo katika ziara za injili maeneo mbalimbali (Makedonia na Asia).
Matendo ya Mitume 20:3-4
[3]Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, na Wayahudi kumfanyia vitimvi, alipotaka kwenda Shamu kwa njia ya bahari; basi akaazimu kurejea kwa njia ya Makedonia.
[4]Watu hawa wakafuatana naye, Sopatro Mberoya, mwana wa Piro, na Aristarko na Sekundo, watu wa Thesalonike; na Gayo mtu wa Derbe, na Timotheo; na Tikiko na Trofimo watu wa Asia.
> Paulo anamtaja pia kama Mhudumu mwaminifu katika Bwana. Maana yake aliupima uaminifu wake, akauthbitisha kuwa hauna unafiki, mpaka akamfanya kama mbeba taarifa zake za kihuduma kwa makanisa.
Waefeso 6:21
[21]
Basi ninyi nanyi mpate kuzijua habari zangu, ni hali gani, Tikiko, ndugu mpendwa, mhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisheni mambo yote;
Wakolosai 4:7-8
[7]Tikiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mjoli wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote;
[8]ambaye nimemtuma kwenu kwa sababu iyo hiyo, ili mjue mambo yetu, naye akawafariji mioyo yenu;
> Lakini pia kwa jinsi Paulo alivyomtaja tunaweza kusema alisimama kama mwangalizi-mwenza wa viongozi wa makanisa.
2 Timotheo 4:12
[12]Lakini Tikiko nalimpeleka Efeso.
Tito 3:12
[12]Wakati nitakapomtuma Artema kwako au Tikiko, jitahidi kuja kwangu huku Nikopoli; kwa maana huku nimekusudia kukaa wakati wa baridi.
Hivyo ijapokuwa si mtu aliyemaarifu, lakini alifanyika nguzo si tu katika mafanikio ya huduma ya mtume Paulo lakini pia kwa makanisa ya Mungu.
Je! Makanisa yetu yaweza kuwa akina Tikiko, watu waaminifu kwa viongozi wao, na kwa kanisa la Kristo?
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Je mwanamke Fibi, alikuwa ni askofu wa makanisa, kama mitume?
Silwano ni nani,kama tunavyomsoma kwenye biblia?(1Petro 5:12)
Rudi Nyumbani
About the author