Sosthene ni mmoja wa wahudumu wa injili Katika agano jipya. Mshirika mmojawapo wa mtume Paulo, katika kazi ya kuitetea injili.
Katika kitabu cha matendo anatajwa kama mkuu wa sinagogi, kule Korintho
Matendo ya Mitume 18:17
[17]Nao wote wakamshika Sosthene, mkuu wa sinagogi, wakampiga mbele ya
kiti cha hukumu. Wala Galio hakuyaona mambo hayo kuwa ni kitu.
> Alikuwa ni mmoja wa wayahudi(washika-sheria), waliokutana na injili ya Paulo na kuamini.
Paulo alipofika Korintho Mungu alimtokea katika maono na kumwambia asiogope aendelee kuhubiri kwasababu katika Mji huo anao “watu wake wengi”
Hivyo aliendelea kuhubiri kwa ujasiri mwingi kwa muda wa mwaka mmoja na nusu na watu wengi sana miongoni mwa wayahudi waliamini ikiwemo huyu Sosthene na Krispo.
Matendo 18:9-11
[9]Bwana akamwambia Paulo kwa maono usiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze,
[10]kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu.
[11]Akakaa huko muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha kati yao neno la Mungu
Baadaye wayahudi wenye wivu waliamka kinyume cha Paulo, na kumpeleka mbele ya Galio liwali ili ashitakiwe kwa kuleta machafuko ndani ya dini yao.
Lakini Galio akawatawanya kwasababu kesi yao haikuwa ya uhalifu au dhuluma bali ya mambo ya kiimani..Ambayo kwa mujibu wa sheria za kirumi hazisikilizwa kwenye mahakama zao.
Hivyo wayahudi kuona Paulo hajahukumiwa, wakamkata huyu Sosthene mkuu wa Sinagogi na kumpiga mbele ya kiti cha hukumu. Na hiyo yote ni kutokana na kwamba aliisapoti huduma ya Paulo, pengine aidha kwa kumruhusu ahubiri injili ndani ya masinagogi yao au kwa kutochukua hatua zozote stahiki dhiki ya injili ya mtume Paulo.
Lakini pia tunakuja kuona baadaye Paulo wakati anaandika waraka kwa Wakoritho anamtaja Sosthene kama mshirika mwenza wa utume wa Kristo.
1 Wakorintho 1:1
[1]Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu,
Hiyo ni kuonyesha kuwa alikuja kuwa nguzo hasaa kwa watakatifu wa Korintho. Mpaka Paulo anamtaja kama mshirika mwenza.
Ni Nini cha kujifunza katika habari ya Sosthene?
Ni kuonyesha uweza wa Mungu wa kugeuza watu wa aina zote. Kikawaida kwa taratibu za kiyahudi mpaka mtu ameaminiwa kuwa mkuu wa sinagogi, maana yake ni kuwa mtu huyo amethibitishwa kuijua na kuishiya torati kwelikweli na nidhani zote za kiyahudi na taratibu zao.
Kwahiyo kwa mtu kama Sosthene kubadilika ghafla na kuwa mfuasi wa injili, haikuwa rahisi, ilihitaji neema ya Mungu kubwa, ndio maana kwa wayahudi alionekana kwa mwasi wakampiga sana.
Bwana anataka tusibague wa kuwahubiri injili, kwasababu injili ni uweza wa Mungu(Warumi 1:16), Umwonapo imamu mhubirie, Shehe mhubirie, Buddha mhubirie, baniani mhubirie, padri, askofu, mganga wa kienyeji..wahubirie kwasababu hapo ulipo kuna “watu wa Mungu wengi sana” hujua ni yupi Bwana aliyemkusudia kuwa chombo chake kama Sosthene.We hubiri tu.
Bwana akubariki
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MKUU WA GIZA.
Tikiko ni nani kwenye biblia?
Mhunzi ni nani? (Isaya 54:16)
About the author