Theolojia ni nini?. Na je ni sahihi kuisoma?

Theolojia ni nini?. Na je ni sahihi kuisoma?

Theolojia ni elimu ya kujifunza sifa za Mungu na mapenzi yake na jinsi anavyohusiana na ulimwengu na wanadamu kwa ujumla.

Neno Theolojia limezaliwa kutoka katika maneno mawili ya kigiriki ‘theos’, na ‘logos’

Theos likiwa na maana ya Mungu, na logos ni neno/wazo/elimu/maarifa.

Hivyo tukiunganisha maneno hayo, ni sawa kusema theolojia ni mafundisho au maarifa au elimu kuhusu Mungu.

Ni utafiti kuhusu  Mungu katika mpangilio na mtiririko maalumu wa kiutafiti. Ukweli ni kwamba theolojia haiwezi kumfafanua Mungu katika ufasaha wote, ikiwa mtu ataitegemea  theolojia tu kumjua Mungu, ukweli ni kwamba amepotea, lakini ikiwa itasomwa vema (si kwa lengo la kitaaluma), bali kwa lengo la kupanua upana wa fikra kuhusu Mungu na maandiko, inafaa sana katika uelewa wa nyanja mbalimbali, hususani kwa wale viongozi na waangalizi kama vile wachungaji, na wahubiri. Si lazima isomwe kwenye vyuo maalumu, mtu yeyote akitia nia kujifunza theolojia anaweza jifunza, kwa kupitia mafundisho mengi, majadiliano na waalimu walio na upeo mpana wa biblia, semina, na kujisomea mwenyewe n.k.

Na Haya ni matawi makuu ya theolojia katika kuichambua biblia.

1) Theolojia ya biblia.

Imejikita katika kutafiti Maudhui au fundisho kuu la biblia, inaangazia jinsi gani vitabu mbalimbali kwenye biblia, vinavyoelezea mpango wa Mungu katika nyakati tofauti tofauti tangu mwanzo hadi mwisho. Mfano kujifunza MAAGANO, katika agano la kale na jipya yalivyotenda kazi na jinsi Yesu alivyoanza kutambulishwa tangu Edeni kama mzao wa mwanamke, hadi nyakati za manabii Isaya 53, hadi wakati wa kutokea kwake duniani Luka 24:27.

Upo umuhimu wa kuijua hii theolojia kwasababu itakupa kujua kiini cha biblia ni nini? Zipo habari nyingi, hadithi nyingi, nyimbo nyingi, mifano mingi, lakini ni vema ujue maudhui zao ni zipi ili usijikute unatoka nje ya shabaha ya imani.

2) Theolojia ya kimpangilio

Inaegemea kujifunza biblia katika migawanyo maalumu ya mada, kwa mfano,

Fundisho la Mungu (theolojia),

Fundisho La Yesu Kristo (Kristolojia),

Fundisho La Roho Mtakatifu (pneumatolojia),

Fundisho La wokovu (Soteriolojia),

Fundisho La kanisa,(Ekleziolojia)

La Siku za mwisho.(Esokatolojia)

La mwanadamu (Anthropoloja)

La malaika (Angeolojia)

3) Theolojia ya vitendo

Inajikita kujifunza jinsi maagizo ya kiblia yanavyoweza kutendewa kazi katika,, huduma kwa mfano kuhubiri na kufundisha , katika uangalizi wa kichungaji, katika umisheni, na katika taratibu za kiibada, na katika kutoa mashauri ya kikristo kama vile kuwaonya wenye matatizo ya kiroho,  kifikra, vifungo n.k.

4) Theolojia ya historia.

Inaangazia jinsi gani imani ya kikristo imekuwa ikipiga hatua katika vipindi mbalimbali vya kihistoria, inaangazia mabaraza mbalimbali ya makanisa yaliyokaa katika kujadili fundisho na misingi ya imani. Kwamfano lile baraza la Nikea (325WK). Mpaka nyakati za matengenezo mfano akina Martin Luther, calvin, na wengine.

Hii inakusaidia kujua historia na chimbuko la imani yetu, na sababu ya ukristo kuonekana katika muundo huu leo.

5) Theolojia ya kimaadili.

Hii inaegemea katika ukristo na jamii, kwamfano mtazamo wa ukristo katika maeneo ya kijamii mfano ndoa, biashara, taratibu za kijamii, haki za kibinadamu, vita, na usafi wa kimaisha.

Kwa mfano kuelewa fundisho hili kutamsaidia mkristo kuangaza nuru yake vema katika ulimwengu.

Zipo theolojia nyingine kama vile theolojia za tafsiri, za kulinganisha, za kifalsafa. n.k. Kwasababu ya upana wa theolojia, haya ni  matawi baadhi tu, kati ya mengi. Hivyo, kama watu wa Mungu, pamoja na kutegemea Bwana kutufunulia mwenyewe maandiko, upo pia wakati ambao hatuna budi kuyamulika maandiko kiundani (Kitheolojia), tukiwa na lengo la kumjua Mungu na sio kuwa wasomi, au wanataaluma.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mwanazuoni ni mtu gani kibiblia?

Kwanini kuna tafsiri nyingi za Biblia, na tafsiri ipi ni sahihi?

Yesu anapoitwa mwana wa Azali, maana yake nini?

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments