Kila mwamini ameitwa kuieneza injili ya Yesu Kristo. Ambayo huitwa habari njema.
Mathayo 28:19-20
[19]Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
[20]na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Habari njema ni nini? Ni habari za wokovu kwa mwanadamu, ulioletwa na kupitia mtu mmoja Yesu Kristo kwa tendo la kufa na kufufuka kwake kaburini.
Kama tulivyotangulia kuona hapo juu, kuwa siku Yesu alipoondoka hakutuacha bila wajibu, bali kila mmoja wetu alipewa sehemu ya huduma katika shamba lake. Ya kuenenda ulimwenguni kote kuwafanya watu kuwa wanafunzi wake.
Kazi hii sehemu nyingine anaifananisha na talanta, ambayo amempa kila mwamini na anataka kila mmoja aizalishe (Mathayo 25:14-30), sehemu nyingine anaifananisha na matunda, anasema sisi ni matawi na yeye ni mzabibu kwamba tumzalie matunda, (Yohana 15:1-7),sehemu nyingine nyingine anaiita posho, huku yeye akijiita bwana, na sisi mawakili wake, akitutaka tutoe posho kwa wakati kwa watu wake, (Luka 12:42-48)
Sasa ukiangalia utaona sehemu zote hizo tunazofananishwa nazo, kama mtu hajafanya chochote au hajazalisha chochote, haachwi hivi hivi, bali kuna aidha kuondolewa sehemu ya thawabu yake, au kukataliwa kabisa.
Ndio maana ni lazima tujue mwamini yoyote yule, ni lazima aishi maisha ya kuwashuhudia wengine injili.
Warumi 10:14 Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?
Ni lazima ujue kuwa hukumu ipo na kuzimu pia ipo, na inawameza wengi, Na watu hawawezi kuokoka tu wenyewe hivi hivi bila kusikia injili kama wewe ulivyosikia. Tengeneza picha unamwona baba yako, au mama yako kwenye ziwa la moto, halafu anakuambia laiti ningelijua ukweli nisingekuwa huku, utajisikiaje? Ukilijua hili basi huruma ya ki-Mungu itakujaa tu ndani yako, na utasukumwa kujitoa kuwaendea wenye dhambi, kama Kristo alivyotujia sisi, kutoka mbinguni, na kama mitume walivyowaendea watu, ili kuhakikisha wanaokoka.
Luka 15:7 Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu
Mungu hufurahi malaika pia hufurahi, wanapoona roho za watu zinaokoka,duniani, Hivyo sisi kama wana wa Mungu ni wajibu wetu kuyatenda yale tu ambayo yanamfanya Baba yetu afurahi, na hilo si lingine zaidi ya kutoka na kwenda kuwashuhudia watu injili.Hapo tunaufanya moyo wa Mungu hufurahi sana.
Ni ukweli usiopingika kuwa kila mmoja wetu kuna mahali Mungu amemtoa mpaka hapo alipomfikisha, anayo mengi ya kushuhudia kuhusu uzuri wa Kristo.
Wazia yule kichaa ambaye alikuwa katika hali mbaya kule makaburini, uchi, usiku na mchana, ameshindikana kwa vifungo vyote. Lakini Yesu alipokutana naye saa ile ile alipona, akataka kuambatana na Yesu, lakini Yesu akamwambia nenda nyumbani kwa watu wako uwasimulie matendo makuu ambayo Mungu amekutendea, Na tunaona alikwenda kusimulia yote mji ule, na watu wengi wakamwamini Kristo, kwa ushuhuda wake tu.
Marko 5:20 Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu
Hata wewe, wazia uzuri ulioupata pindi ulipompokea Kristo, utamani pia mwingine aupate, na huo ndio upendo, umeonja uzuri wa Kristo unakwenda kuwaambia na wengine mfano tu wa yule mwanamke pale kisimani.
Sawasawa na agizo ambalo Yesu alimwagiza yule mtu ambaye aliteswa Na mapepo akamfungua. (Marko 5:19-20)
Hii ni njia bora, ambayo utapata nguvu ya kikanisa, kwasababu mule akutanapo na vipawa mbalimbali vya Mungu, hurahisisha zaidi moyo wake, kuamini ujumbe uliompelekea.
Ishi maisha yanayomuhakisi Kristo. Kwasababu matendo yako ni injili kuwa wengine kumgeukia Kristo. (1Petro 3: 1-2)
Hivi Ni kama vitabu, kanda, luninga, na kwa dunia ya sasa, Vitu kama whatsapp, websites, panaweza pakawa mahali Ambapo injili yetu kupaa sana na kuwavuta wengi ndani ya ufalme. Ulimwengu wa sasa, upo mtandaoni, hivyo tumia fursa hiyo, kushea mafundisho, mahubiri sahihi ya Neno la Mungu kwa marafiki zako, familia, ndugu, majirani, huko huko Mungu ataanza kazi ya wokovu ndani yao.
Haya ni mambo ya kukumbuka kila uendapo kushuhudia, ili usishindwe na hofu.
Usiwe na hofu ikiwa huoni mwitikio wowote, kwa yule unayemweleza habari ya wokovu, fahamu kuwa ipo mbegu imemwingia ambaye itakuja kumea tu kwa wakati wake.
Uinjilisti wa wawili huwa mrahisi zaidi ya ule wa mmoja (isipokuwa unao uzoefu). Yesu aliwatuma wanafunzi wake wawili wawili, alijua ujasiri utaongezeka lakini wangeweza kufanya zaidi, pale mmoja anapochoka anamtia nguvu mwenzake. Vivyo hivyo na wewe katika hatua za awali ongozana na kiongozi wako, au mshirika mwenza katika kazi ya injili.
Yohana 3:16
Warumi 3:23
Warumi 6:23
Warumi 10:9–10
2 Wakorintho 5:17
Kwa mwongozo wa namna ya kutembea katika baadhi ya vifungu hivyo, pitia hili fundisho >>> NJIA/BARABARA YA WOKOVU NDANI YA KITABU CHA WARUMI.
Mafundisho ya ziada
KWANINI TUNAPASWA KWENDA KUIHUBIRI INJILI KWA UJASIRI WOTE?
IHUBIRI INJILI, KILA MAHALI KWASABABU AKUZAYE NI MUNGU.
HEKIMA NANE(8) ZA KIUINJILISTI, KATIKA KUWAVUA WATU KWA KRISTO.
JE UDHAIFU WANGU UNAWEZA KUZUIA INJILI?
KUTOKUIHUBIRI INJILI,KUNA MADHARA GANI?
KWANINI KILA MWAMINI ANAPASWA AWE MHUBIRI WA INJILI
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
About the author