Kutoka 10:1 “BWANA anasema atampa Farao moyo Mgumu, asimtii, je! hapo Bwana Atamhukumu Farao kama mkosaji siku ile?”

Kutoka 10:1 “BWANA anasema atampa Farao moyo Mgumu, asimtii, je! hapo Bwana Atamhukumu Farao kama mkosaji siku ile?”

JIBU: Ndio atamuhukumu kama mkosaji, na ndio maana utaona zile adhabu zote zilimpata!! Hata kufiwa na mtoto wake wa kwanza…Na baada ya kufa kama hakupewa moyo wa kutubu, basi bado ataenda jehanamu ya moto. Kumbuka Moyo wa kutubu na moyo wa kumtafuta Mungu, ni Mungu mwenyewe ndio anaotoa sio sisi tunaoamua kwa juhudi zetu..ndio maana Bwana Yesu alisema katika

 “Yohana 6:44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka;”

Umeona hapo? Nguvu ya mtu kumfuata Mungu ni Mungu mwenyewe ndiye anayekujalia..vinginevyo haiwezekani kumtafuta Mungu wala kumfuata.Sasa Kwanini Mungu amjalie Musa moyo mlaini wa kumkubali na Farao ampe moyo mgumu wa kumkataa??..hatujui na wala hatuwezi kumuuliza Mungu hayo maswali, ndivyo ilivyompendeza yeye, ni sawa na tumuulize Mungu alitokea wapi?? Hayo ni maswali tusiokuwa na majibu nayo….Yapo juu ya upeo wa fikra zetu. Na ndio maana mtume Paulo alisema katika.. 

Warumi 9.13 “Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.

14 Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!

15 Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye.

16 Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu.

17 Kwa maana maandiko YASEMA JUU YA FARAO, ya kwamba, nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.

18 BASI, KAMA NI HIVYO, ATAKAYE KUMREHEMU HUMREHEMU, NA ATAKAYE KUMFANYA MGUMU HUMFANYA MGUMU.

19 Basi, utaniambia, MBONA ANGALI AKILAUMU? Kwa maana NI NANI ASHINDANAYE NA KUSUDI LAKE?

20 La! Sivyo, Ee binadamu; WEWE U NANI UMJIBUYE MUNGU? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?” 

Unaona hapo? Biblia inasema pia wapo watu ambao hawajakusudiwa uzima wa milele, watu ambao majina yao hayajaandikwa katika kitabu cha uzima kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu (Ufunuo 17:18 na Ufunuo 13:8)..Swali ni Ni wakina nani hao?? Jibu ni kwamba Hatuwajui, Mungu ndie anayewajua…sisi sio kazi yetu kuwafahamu, jukumu tulilopewa ni kuhubiri injili kwa kila kiumbe kana kwamba wote wote wamekusudiwa uzima wa Milele,…Na kujitahidi kuishi kulingana na maagizo yake na amri zake,ili tuwe na uhakika sisi sio miongoni mwa hilo kundi lililoandikiwa kupotea milele.Kwasababu dalili kuu inayotambulisha kuwa umekusudiwa uzima wa milele ni pale mtu anapoitii na kubadilika, kadhalika dalili kubwa inayoweza kumtambulisha kama mtu huyo hajakusudiwa uzima wa milele, ni pale anapoupinga wokovu ndani ya moyo wake. 

Ubarikiwe!


Mada zinazoendana:

KWA MUNGU ASIYEJULIKANA.

SIFA TATU ZA MUNGU.

MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU:

WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU

FUVU LA KICHWA.

ANGALIA JINSI USIKIAVYO:


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments