Ni kwa nini tunasema tunamwabudu MUNGU aliye hai ,Je! wale wanaomwabudu shetani sio mungu wao aliye hai?

Ni kwa nini tunasema tunamwabudu MUNGU aliye hai ,Je! wale wanaomwabudu shetani sio mungu wao aliye hai?

JIBU: Embu tutafakari mfano huu, utatusaidia kupata majibu ya maswali yetu. Tunajua kuwa Dunia tunayoishi sasa hivi ni dunia ya utandawazi na kugunduliwa kwa Kompyuta kumefanikisha kurahisisha mambo mengi sana, Komputa sasa inAaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu pekee angeweza kufanya, unaweza ukaiuliza swali lolote na ikakusaidia kupata sehemu kubwa ya majibu yako, inaweza kukusaidia kufanya mahesabu yako, inaweza ikakusaidia kuwasiliana na mtu mwingine aliye mbali, inaweza ikakuonyesha picha, inaweza ikakuhifadhia kumbukumbuku zako, inaweza ikakusaidia kutafiti, na hata kufanya kazi n.k. Kwa ufupi komputa sasa tunaweza kusema ni chombo ambacho kina ufanisi mkubwa karibia na mwanadamu, tunaweza kusema kina uhai fulani, Na uhai huo ni wazi kabisa hakijapewa na mwingine zaidi ya mwanadamu. 

Lakini pamoja na hayo tunajua hata kiwe na ufanisi mkubwa kiasi gani, bado tu uhai wake hauwezi kuwa halisi kama wa mwanadamu mwenyewe, vipo vitu vingi kitashindwa kufanya ambavyo mwanadamu angeweza kufanya, kwamfano Komputa haiwezi kufariji, haiwezi kupima hisia za mtu, komputa haiwezi kuonyesha fadhili, komputa ukiiomba chakula haiwezi kukupa, komputa haiwezi kuona mambo ya mbeleni ili kuchukua tahadhari n.k..yenyewe inaongozwa na kwa yale tu mwanadamu aliyoyapachika ndani yake, nje ya hapo haiwezi kujichagulia mambo yake yenyewe. Vivyo hivyo tukirudi kwa Mungu wetu.

Tunajua sisi sote tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, na kama vile alivyo hai, na sisi basi tutakuwa hai, lakini uhai tulionao si kama ule wa kwake, sisi ni mfano wa Komputa zilizotengenezwa na Mungu, tunaouwezo wa kuonyesha tabia zote za Mungu lakini haimaanishi tutakuwa na ule uhai halisi kabisa kama wa Mungu mwenyewe, wa kufikia hatua ya kuweza hata kuumba, kufanya kila kitu, kuona mambo yote ya mbeleni yanayokuja, kuchipusha chakula ardhini, hatuwezi pia kujihakikishia uzima wetu wa milele kama sio kutoka kwake. Hivyo tunavyosema Tunamwabudu Mungu aliye HAI, tunamaanisha Mungu awezaye kufanya mambo yote, Mungu anayetoa uhai katika mambo yote, Mungu ambaye hashindwi na lolote,Shetani hawezi kuumba chochote,japo anaishi, hajui hata kesho yake itakuwaje sasa ataitwaje mungu aliye hai? Yeye kapewa tu sehemu ya uhai kama sisi tulivyopewa, hawezi kusema sasa nataka jua lizime, au leo mimea yote duniani ikauke,hana uwezo huo hivyo hawezi kuitwa Mungu aliye hai.. Neno zuri labda linaweza kumstahili yeye kuitwa nao hao wanaomwabudu ni “mungu aliyepewa pumzi”, lakini sio Mungu aliye hai aliye hai ni mmoja tu! anayekaa mbingu za mbingu.

Isaya 46:9 “kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi; 10 nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote. 11 Nikiita ndege mkali kutoka mashariki, mtu wa shauri langu toka nchi iliyo mbali; naam, nimenena, nami nitatekeleza; nimekusudia, nami nitafanya.”

 Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

JINA LA MUNGU NI LIPI?

USILITAJE BURE JINA LA BWANA!

NINI MAANA YA ELOHIMU?

SIKU ZA MAPATILIZO.

UPENDO


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments