YEYE AJAYE ATAKUJA WALA HATAKAWIA.

YEYE AJAYE ATAKUJA WALA HATAKAWIA.

Waebrania 10:37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, YEYE AJAYE ATAKUJA, wala hatakawia”.

Angalia muda unavyokimbia, angalia majira yanavyobadilika, angalia maasi yanavyoongezeka kwa kasi.. Je! yote haya unajua ni ishara ya nini?..Si ya kitu kingine bali  ya YEYE AJAYE!!.. Ndio! Yupo mmoja anayekuja! na yupo karibu sana..

Gari likipita huwa linaacha vumbi!, lakini ikitokea vumbi linatangulia kabla ya gari kufika basi ni upepo unavuma kuelekea mbele, na una mbio kuliko gari lenyewe!.

Na YESU KRISTO anakuja, na ishara zake zinatangulia mbele yake!..zina mbio kabla ya kuwasili kwake, Uvumi wa ujio wake unatufikia kabla ya yeye kuwasili.

Zifuatazo ni sifa za “Yeye ajaye”

        1. Yeye ajaye anakuja kutoka Juu mbinguni.

Yohana 3:31 “YEYE AJAYE kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote”.

       2. Yeye ajaye ana nguvu kuliko manabii wote.

Mathayo 3:11 “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali YEYE AJAYE nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake…”.

      3. Yeye ajaye Ni Mbarikiwa na amejaa utukufu.

Mathayo 21:9 “Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, YEYE AJAYE kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni”.

      4. Yeye ajaye Anakuja Upesi wala hakawii.

Waebrania 10:37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, YEYE AJAYE ATAKUJA, wala hatakawia”.

>Jiulize!…Utajisikiaje siku umeamka asubuhi unajiandaa kwenda kazini, halafu ghafla unapokea taarifa za kuwa KRISTO kashawachukua watu wake, na wewe umebaki?

> Utajisikiaje umeamka vizuri na unaelekea shuleni, halafu unapata taarifa kuwa unyakuo wa kanisa umepita na wewe umeachwa?

> Utajisikiaje ule muda unapewa taarifa kuwa Kanisa limenyakuliwa na jana tu uliyasikia mahubiri na hukuzingatia??..

>Tafakari utakuwa katika hali gani utakapoanza kutafakari mambo yatakayoupata ulimwengu baada ya hapo?..Kwamaana maandiko yanasema baada ya hapo itakuwa ni dhiki kuu na  hukumu kwa wanadamu na mlango wa rehema utakuwa umefungwa!.

Isaya 26:21 “Kwa maana, tazama, Bwana anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao…”.

Zaburi 96:13 “Mbele za Bwana, kwa maana anakuja, Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu wake”

Wakati huo watu watatamani kuingia katika mlango wa Neema lakini watakuwa wamechelewa…kwasababu mwenye nyumba (YESU) atakuwa ameshasimama na ameufunga mlango, hakuna anayeingia wala anayetoka..

Luka 13:23  “Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,

24  Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba WENGI WATATAKA KUINGIA, WASIWEZE.

25  Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;

26  ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.

27  Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.

28  Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje”.

Kwanini leo usijitahidi kuingia katika mlango ulio mwembaba???… hao marafiki watakusaidia nini siku ile au watakushauri nini utakapoukosa unyakuo?.. hizo mali zitakutetea vipi wakati huo?… hizo fasheni za kidunia na huo urembo utakupa kibali gani nyakati hizo?… Kumbuka YEYE AJAYE, ANAKUJA WALA HATAKAWIA!!

Ni heri ukayasalimisha maisha yako kwa YESU leo, maana hizi ni nyakati za hatari!.. na muda wowote parapanda inalia!.

Ufunuo 22:20 “Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu”

Ikiwa unahitaji kumpokea YESU basi fungua hapa kwa mwongozo >>>KUONGOZWA SALA YA TOBA

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

ANAKUJA KAMA “MWIVI” NA SI KAMA “ASKARI” FANYIKA CHOMBO CHA THAMANI.

MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.

Je mapepo au majini yanaweza kuviingia vitu visivyo na uhai?

MWANAMKE, USIFUNGUE MLANGO WA MAPEPO KUKUINGIA!.

LIITE JINA LA BWANA KATIKA NYAKATI MBALIMBALI ZA MAISHA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments