Nini maana ya kurarua mavazi? (Mwanzo 37:34).

Nini maana ya kurarua mavazi? (Mwanzo 37:34).

Kurarua mavazi ni utamaduni wa wayahudi na watu wa zamani kuonyesha hisia zao kwa kuyararua (kuchana) sehemu ya mavazi yao kama isha ya Toba (kujishusha) au  maombolezo au majuto.

      1. Ishara ya kushuka (kunyenyekea) na kutubu.

Mfalme Yosia alipokiona kitabu cha Torati alitambua Israeli wamefanya dhambi kulingana na yaliyoandikwa kule, hivyo akajishusha mbele za Mungu Soma 2Wafalme 22:11-15..

Vile vile Mfalme Ahabu baada ya kutamkiwa hukumu yake na Mungu kwaajili ya shamba la Nabothi alilomdhulumu na tena kumwua..Ahabu alijishusha mbele za Mungu kwa kuyararua mavazi yake..

1Wafalme 21:27 “Ikawa, Ahabu alipoyasikia maneno hayo, akayararua mavazi yake, akavaa magunia mwilini mwake, akafunga, akajilaza juu ya magunia, akaenda kwa upole”.

      2. Maombolezo.

Kwamfano utaona baada ya Yakobo kupokea taarifa za kifo cha mwanae Yusufu (ambaye kimsingi hakufa) aliyararua mavazi yake kama ishara ya kuhuzunika na kumwombolezea..

Mwanzo 37:34 “Yakobo akararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni, na kumlilia mwanawe siku nyingi”

Utasoma tena tukio kama hilo katika Mwanzo 37:29 pale Rubeni alipopata taarifa za kifo cha ndugu yake. Na pia 2Samweli 13:29-31, Esta 4:1, na Ayubu 1:20.

      3.Majuto

Utaona Mwamuzi Yeftha baada ya kukutana na mwanae, anaijutia nadhiri aliyoiweka kwa kurarua mavazi yake..

Waamuzi 11:35 “Ikawa alipomwona akayararua mavazi yake, akasema, Ole wangu! Mwanangu, umenitweza sana, nawe u mmoja miongoni mwa hao wanisumbuao; kwa kuwa mimi nimemfunulia Bwana kinywa changu, nami siwezi kurejea nyuma”.

Lakini je kiroho kurarua mavazi ni kufanya nini? Na je mpaka sasa tunapaswa tuyararue mavazi yetu kwa namna ya kimwili kama walivyofanya wayahudi zamani pindi tunapopitia maombolezo, au tunapotaka kutubu au kunyinyenyekeza kwa Mungu?

Jibu tunalipata katika kitabu cha Yoeli 2:13.

Yoeli 2:13 “Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea;

13 RARUENI MIOYO YENU, WALA SI MAVAZI YENU, MKAMRUDIE BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.

14 N’nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa Bwana, Mungu wenu?”

Umeona?.. Kumbe kurarua mavazi ni kutubu!.. Na kwamba tunapotubu na kugeuka na kubadili njia zetu, mbele za Mungu ni sawa na tumeyararua mavazi yetu!.

Je leo umeurarua moyo wako?,  Umetubu kwa kumaanisha kabisa kuacha njia ile mbovu?…

Isaya 66: 2 “….lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu”.

Kujua maana ya “Kuvaa mavazi ya magunia” basi fungua hapa >>Nguo za magunia katika biblia ni zipi?

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.

MAVAZI YAPASAYO.

USIYAACHE MAVAZI YAKO NA KWENDA UCHI!

FAHAMU JINSI MUNGU NA SHETANI WANAVYOZUNGUMZA NA WATU.

YEYE AJAYE ATAKUJA WALA HATAKAWIA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments