(Masomo maalumu yahusuyo faida za matoleo).
Jifunze kutoa sadaka!!, jizoeze kutoa sadaka, jitaabishe kutoa sadaka!!.
Utoaji si agizo la washirika bali hata viongozi (wachungaji, waalimu, wainjilisti na watu wote wanaoujenga mwili wa Kristo), pasipo kujali Umri wala kipato. Hili ni agizo la Bwana YESU lenye baraka na laana nyuma yake (soma Mathayo 25:31-46).
Sadaka inayotolewa katika misingi ya Neno la Mungu, inafanya mambo makubwa zaidi ya yale tuyajuayo.
Sadaka inayotolewa katika msingi wa Neno la Mungu, inameza sadaka nyingine zilizotolewa na upande wa ibilisi.
Ile fimbo ya Musa ilibidi aitoe na kuitupa, ndipo ilipoweza kumeza zile fimbo nyingine za wachawi wa Farao.
Sasa zile fimbo zilizomezwa, laiti zingeendelea kuwepo zingeleta madhara mengine kwani zilikuwa ni za kichawi, na zilitumika na wachawi kwa shughuli za kichawi.
Sasa ilimgharimu Musa kuitoa fimbo yake kwanza ili imeze zile nyingine. Vile vile iliwagharimu wachawi kutoa fimbo zao za gharama ili wahindane na Musa.
Vile vile kuna mambo mengine yanahitaji tu matoleo yatatuke..(Kasome Waamuzi 20:20-40).
Sasa wale waganga wa Misri walizigharimia zile fimbo zao, hazikutokea tu… huenda walizinunua kwa fedha na kuzifanyia matambiko mengi.
Kitabu cha Matendo ya Mitume kinatuonyesha jinsi waganga wanavyougharimia uganga wao.
Matendo 19:17 “Habari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa.
18 Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao.
19 Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote; wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha hamsini elfu”
Hapo anasema gharama ya vile vitabu vya uganga vilivyochomwa ilikuwa ni elfu 50.
Sasa tukisema elfu 50, kwenye vichwa vya wengi inadhaniwa ni shilingi za kitanzania, zinazotosha tu gharama ya nauli kutola mkoa mmoja hadi mwingine..La!.
Kujua thamani halisi ya vipande vya fedha elfu 50…rejea kile kiasi Yuda alichoongwa ili amsaliti Bwana YESU, maandiko yanasema alipewa kiasi cha vipande 30 tu vya fedha na vipande hivyo vilitosha kununulia shamba (ambalo hatujui ni hekari ngapi) lakini tunajua ni hekari nyingi maana zilitumika kama eneo la makaburi..soma Mathayo 27: 3-7.
Sasa piga hesabu kama vipande 30 vya fedha ya Yuda vimenunua shamba, na hapo vitabu vya waganga gharama yake ni vipande vya fedha elfu 50..gawanya hapo uone waganga waliugharimia uganga wao kiasi gani…
Utaona hapo ni zaidi ya mashamba 1,600 na kama shamba moja litauzwa tu kwa gharama ya shilingi za kitanzania milioni moja…basi jumla yake vile vitabu vyote ni zaidi ya BILIONI MOJA.
Kwahiyo wale waganga waligharimia mabilioni kuusimamisha uganga wao!!!…..
Halafu wewe na mimi kuigharimia injili kidogo tu tunaona tabu!!!!…..Fikiri mara mbili…fikiri mara mbili!!!.
Jenga ufalme wa Mungu, kwani shetani anajenga ufalme wake kwa kasi na gharama.
Bwana atusaidie.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Biblia inamaana gani iliposema “Dhambi ilipozidi, Neema ilizidi kuwa nyingi Zaidi”.
Kupiga ramli ni nini katika biblia?
About the author