Ndoa ni nini? Je ndoa za kibinadamu ni zipi na ndoa ya kimbinguni ni ipi?
karibu tujifunze masomo ya ndoa na elimu ya ndoa na mafunzo ya ndoa kwa mapana.
Ndoa ni muunganiko wa kimwili kwa namna ya roho kati ya watu wawili wa jinsia mbili tofauti. Kuna aina mbili za Ndoa. Zipo ndoa za kibinadamu na ndoa ya kimbinguni.
Ndoa za kibinadamu zinahusisha Mume mmoja na mke mmoja…Lakini Ndoa ya kimbinguni inahusisha Mume mmoja (Aitwaye Yesu Kristo) na mke wake mmoja aitwaye Kanisa.
Ndoa za kibinadamu.
Kama tulivyotangulia kusema hapo juu..Ndoa hii ni muunganiko wa kimwili baina ya watu wawili wa jinsia mbili tofauti. Ndoa ya kwanza ilifungishwa na Mungu mwenyewe pale Edeni…baada ya Adamu kukabidhiwa Hawa aliyetoka ubavuni mwake. Na ilihusisha Mume mmoja na mke mmoja…Hakuumbwa Adamu mmoja na wakina Hawa wengi…au Hawa mmoja na wakina Adamu wengi. Kama ingekuwa ni hivyo basi Ndoa ya mume mmoja na wake wengi ingekuwa halali..au ya mke mmoja waume wengi.
Mathayo 19:3 “Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?
4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe”.
Na kuna tofauti kati ya ndoa na harusi..Ndoa ndio kama tulivyoizungumza hapo juu kwamba ni muunganiko wa kimwili watu wawili wa jinsia mbili tofauti. Lakini harusi ni sherehe au karamu inayofanywa baada ya ndoa kufungwa.
Sasa kuna maswali machache yafuatayo ya kujiuliza: Maswali haya yanalenga kwa urefu juu ya masomo ya ndoa na mafunzo ya ndoa/Elimu ya ndoa
Biblia haijaweka sharti la kwamba kila mtu ni lazima aoe au aolewe. Zaidi ya yote ni vizuri mtu kutokuoa kabisa au kutokuolewa kwa ajili ya kuifanya kazi ya Mungu. Biblia inasema hivyo katika..
1 Wakorintho 7:32 “Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;
33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.
34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
35 Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine”
Kuna faida kubwa ya kutokuoa au kutokuolewa kwaajili ya kuifanya kazi ya Mungu..lakini kama sio kwasababu hiyo ni heri kuoa au kuolewa. Kwasababu Ndoa ina faida kubwa sana, na ina baraka na heshima. Mtu aliyefunga ndoa takatifu. Kuna Baraka za kipekee na Neema kutoka kwa Mungu anazipokea zaidi ya yule ambaye hajaoa au hajaolewa. Hivyo ni vizuri kuoa au kuolewa..(hususani Unapozidi kuelewa upana juu ya ndoa ni nini na majukumu yako baada ya ndoa hiyo utabarikiwa sana kuliko kawaida )
lakini pia ni vizuri kutooa au kutokuolewa kwaajili ya ufalme wa mbinguni.
Maswali mengine ya muhimu ya kujiuliza kuhusu elimu ya ndoa/mafunzo ya ndoa ni kama yafuatayo.
Kama utakuwa umeyafuatilia hayo masomo ya ndoa hapo juu na kuzifungua link hizo kwa umakini utakuwa umeelewa kwa sehemu kubwa ndoa ni nini?. Hivyo kama umedhamiria kuoa au kuolewa..Basi kumbuka jambo moja na la muhimu kuwa “Ndoa inapaswa iheshimiwe na watu wote.”. Sio iheshimiwe na wewe tu na mpenzi wako peke yenu!.. Hapana bali watu wote..Ikiwa na maana kuwa ukifanya jambo lolote litakaloifanya ndoa yenu isiwe na heshima, watu wakaidharau…Hiyo tayari ni dhambi! mbele za Mungu.
Waebrania 13:4 “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu”.
Ukishaoa au kuolewa huo sio wakati wa kutanga tanga huku na huko kuzungumza zungumza habari za ndoa yenu..huko ni kuiondolea heshima ndoa yenu! na ni dhambi..Ukishaoa sio wakati wa kuudhiana mpaka kutupiana maneno au kupigana hadi watu wa nje wanawaona..huko ni kuivunjia heshima ndoa…ambapo ni dhambi! n.k
Ukishaoa sio wakati wa kukaa kwenye vibaraza vya mizaha, na vijiweni kuzungumza kama mtu ambaye hajaoa au hajaolewa, na wala si wakati wa kuvaa kama kahaba, au mhuni huko ni kuivunjia heshima ndoa ambako ni dhambi na kujitafutia laana. Ni lazima ufahamu ndoa ni nini!
Kama hujafahamu Agano lililopo katika ndoa ni heri ukasubiri kwanza, kuliko kukurupuka na kuoa au kuolewa na kisha kuiharibu ndoa na kuangukia Hukumu.
Yapo mengi ya kuzungumzia juu ya ndoa ni nini, lakini hapa hatuwezi kuyaandika yote, naomba ufungua link hizo nilizokupatia hapo juu au hizi hapa chini, yapo maelezo marefu na ya kutosha kuhusu ELIMU YA NDOA.
Bwana akubariki sana.
Na kama hujampa Yesu Kristo maisha yako.. Nakushauri ufanye hivyo sasa. Mahusiano ya kwanza ya kutafuta kabla ya kuoa au kuolewa ni mahusiano yetu sisi binafsi na Yesu Kristo. Huyo ndiye tumaini la wokovu wetu na mwokozi wa kila mwenye mwili. Na biblia inasema pia itatufaidia nini tuupate ulimwengu mzima na tupate hasara ya nafsi zetu..
Hivyo kila kitu kitapita…hata baada ya kifo hakutakuwa na kuoa wala kuolewa..Ni mambo mengine yatafuata. Hivyo ni muhimu sana kwanza kutafuta uhusiano binafsi na Yesu Kristo kabla ya mambo yote..Na huo tunaupata kwa kumwamini, na kutubu dhambi zetu zote kwa kukudhamiria kutozifanya tena..Na kubatizwa..na Roho Mtakatifu atatuongoza katika kweli yote.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Maranatha!
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo:
Je! Ni sahihi kwa mkristo kuoa/kuolewa na mtu wa imani nyingine?
About the author