Je Mahari ina ulazima wowote?

Je Mahari ina ulazima wowote?

SWALI: Je ulipwaji wa Mahari ina ulazima wowote?..je ni Agizo la kibiblia? Na kama ni hivyo Je! Adamu alitoa mahari kwa nani ili ampate Hawa?

JIBU: Ndoa ya kwanza ilifungishwa na Mungu mwenyewe…Na hakukuhusika mahari wala viapo…Hiyo yote ni kwasababu Hawa hakuwa na Baba wala Mama…

Lakini sasa wake zetu wanao wazazi wao..hatuwatoi ubavuni mwetu kama Adamu alivyompata Hawa..Hatuna budi kuwatoa kutoka kwa wazazi wao…Na wazazi wao waliwalea na kuwatunza kwa gharama zao.

Hivyo sio vyema kuwaiba kutoka kwa wazazi wao na kuwafanya wetu…Hatuna budi kufuata taratibu za kuwatoa kutoka kwao na kuwaleta kwetu…Na taratibu hizo zinahusisha ulipwaji wa mahari. Ulipwaji wa mahari hakumaanishi kumnunua huyo mwanamke…hapana! Bali kumthaminisha Yule binti kwamba hajaokotwa tu.

Laiti kama tungekuwa tunawapata wake zetu kama Adamu kwamba Mungu anatuletea usingizi na kuwatoa kutoka ubavuni mwetu..hapo kungekuwa hakuna haja ya mahari wala ndoa kanisani..hapo mahari ina ulazima wowote?..haina ulazima kwasababu wametoka kwetu(kwenye miili yetu kama Adamu)…lakini tulio nao hawajatoka kwetu wametoka kwa wengine… Hivyo ni lazima mtu upitie hatua za kuposa, na kuposa kuna taratibu zake ikiwemo mahari,

Luka 2:4  “Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;

5  ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba”.

Hivyo hatua hiyo ikishavukwa kinachofuata sasa ni kwenda kanisani…Tulipowatoa! tumewatoa katika jamii..watu wote walikuwa wanajua binti Yule hajaolewa..hivyo binti kwa idhini yake sasa hana budi kwenda kukiri mbele ya umati wa jamii ya watu wake na mbele ya kanisa la Kristo na mbele ya Mungu kwamba amekubali kwa idhini yake mwenyewe kuolewa na kijana huyo..Na kijana naye vivyo hivyo anatamka kwa kukiri..kuwa ushuhuda..Na hapo ndipo Mungu anapoiridhia kuwa ni ndoa takatifu ya kikristo.

Hivyo ndoa na mahari ni mambo ya kimaandiko kabisa hata Bwana wetu Yesu Kristo aliingia gharama ili kututoa katika ulimwengu…Ilimgharimu uhai wake ili tu atupate sisi bibi-arusi wake..

Bwana akubariki.

Je umeithamini gharama Kristo aliyoingia ili akupate wewe?..Damu yake ilimwagika pale msalabani kwaajili yako na yangu..ili sisi tuwe mali yake yeye…tuondoke katika ulimwengu tukaishi naye..Kama hujaokoka unasubiri nini?..siku ile utakuwa mgeni wa nani kule au utakuwa mfano wa wale wanawali wapumbavu tunaowasoma katika kitabu cha Mathayo 25?..Uchaguzi ni wako, mlango wa rehema bado upo wazi.

Maran atha. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

Je! Ni halali kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto?

Je! Ni sahihi kwa mkristo kuoa/kuolewa na mtu wa imani nyingine?

WAZAZI WA YOHANA NA YAKOBO.

JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI AU KUTOA TALAKA?

KILEMBA CHA NEEMA, JE! UMEMVIKA MWANAO?

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments