Inaaminiwa na wengi wetu kuwa Mariamu, mama, aliyemzaa Bwana wetu Yesu Kristo, alikuwa ni mwanamke wa kipekee sana, na aliyebarikiwa zaidi ya wanawake wengine wote, na kabla hajapata Neema ya kumzaa Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa ni mtu mkuu sana, na anayependwa sana na aliyeheshimika sana…Lakini je! ni kweli maandiko yanasema hivyo?
Tukisoma maandiko kitabu cha Luka 1: 1.42 inasema “akapaza sauti kwa nguvu akasema, UMEBARIKIWA WEWE KATIKA WANAWAKE, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa”.
Maneno hayo yalizungumzwa na Elizabeth, mama yake Yohana Mbatizaji baada ya kukutana na Mariamu, Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu akambariki na kumwambia UMEBARIKIWA WEWE KATIKA WANAWAKE.
Sasa jambo la muhimu la kuzingatia hapo ni hilo neno “KATIKA” Hakusema “kuliko wanawake wote” hapana bali “katika”
Ikiwa na maana kuwa katika wanawake waliobarikiwa na yeye (Mariamu) ni mmoja wapo..na sio kwamba yeye kabarikiwa kuliko wote..
Wakati Fulani mwanamke mmoja alimtaja Mariamu kuwa kabarikiwa sana, mbele ya umati mkubwa wa watu na mbele ya Bwana Yesu, lakini Bwana alimrekebisha pale pale na kumwambia HERI walisikiao Neno la Mungu na kulishika..
Sasa maana ya neno heri ni “amebarikiwa yeye”
Luka 11:27 “Ikawa alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake, akamwambia, Heri {limebarikiwa} tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya. Lakini yeye alisema, Afadhali, heri{wamebarikiwa} walisikiao neno la Mungu na kulishika”.
Kwa lugha nyepesi katika mstari huo tunaweza kusema “…Mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake akamwambia; amebarikiwa mwanamke Mariamu aliyekuzaa, lakini Bwana akasema amebarikiwa zaidi mwanamke Yule alisikiaye Neno la Mungu na kulishika”
Kwahiyo unaweza ukaona hapo ingekuwa Mariamu amebarikiwa kuliko wanawake wote, Bwana Yesu asingemkosoa huyu mwanamke aliyekuja Kumtangaza Mariamu hadharani kuwa ni mbarikiwa.
Na pia kumbuka Bwana Yesu hakutabiriwa kutokea katika ukoo wa Mariamu, bali ukoo wa Yusufu Mumewe Mariamu..ndio maana ukisoma pale mwanzo wa kitabu cha Mathayo utaona ukoo wa Bwana Yesu Ulianzia kwa Ibrahimu na ukaishia kwa Yusufu mumewe Mariamu, na haukuanzia kwa Ibrahimu na kuishia kwa wazazi wake Mariamu. Hivyo unaweza ukaona ni neema tu Mariamu kumzaa Bwana.
Kwahiyo ni muhimu kufahamu hilo ili tusije tukamwona Mtu Fulani ni wa kipekee sana katika maandiko zaidi ya mwingine, Imefikia wakati watu wanamaabudu Marimu, bila hata hofu ya Mungu, mwanamuhisisha katika ibada zao na kumtolea shukrani kana kwamba yeye ni Kristo. Hata Nabii Eliya biblia inatuambia alikuwa ni mtu mwenye tabia moja na sisi (Yakobo 5:17). Mfano kama biblia isingeandika vile leo hii si ajabu tungewaona watu wamemfanya leo kuwa ni mtu wa nne katika uungu wa Mungu.
Ni YESU KRISTO, peke yake aliye Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana ndiye aliyekuwa wa kipekee zaidi ya wengine wote duniani…
Sasa tukirudi kwenye kiini cha somo ambacho tutaona ni jambo gani lililomfanya Mariamu, apate neema ya kumzaa Mwokozi wa Ulimwengu Yesu Kristo.
Awali ya yote Biblia takatifu haijaelezea maisha ya nyuma ya Mariamu kabla ya kumzaa Bwana wetu Yesu Kristo..Lakini tukiyachunguza maandiko kwa undani tunaweza tukapata dondoo chache za maisha yake ya nyuma jinsi yalivyokuwa..
Sasa kabla ya kumsoma Mariamu hebu tuwasome kidogo Wanawake wachache kwenye maandiko waliopewa neema ya kuzaa baadhi ya MASHUJAA..
Tukianza na mwanamke wa Kwanza wakati wa kipindi cha Waamuzi, aliyekuwa (Mke wa mtu mmoja aliyeitwa Manoa) Tunasoma hivi..
Waamuzi 13: 2 “Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; NA MKEWE ALIKUWA TASA, hakuzaa watoto. 3 Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini UTACHUKUA MIMBA, NAWE UTAMZAA MTOTO MWANAMUME. 4 Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi; 5 kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti”.
Waamuzi 13: 2 “Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; NA MKEWE ALIKUWA TASA, hakuzaa watoto.
3 Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini UTACHUKUA MIMBA, NAWE UTAMZAA MTOTO MWANAMUME.
4 Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;
5 kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti”.
Mwanamke huyu ndiye aliyemzaa shujaa Samsoni…Sasa ukiyachunguza kwa makini maisha yake utagundua alikuwa ni Mwanamke aliyekuwa MNYONGE kwa sababu alikuwa tasa..wakati wanawake wengine wana watoto yeye hakuwa na mtoto hata mmoja na umri wake umeshakwenda…Na inaelekea alikuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu akimwomba Mungu usiku na mchana, na pengine alimwekea nadhiri Bwana kwamba endapo atapata mtoto wa kiume atampatia Bwana kama sadaka. Hivyo aliendelea kubakia katika hali hiyo hiyo paka siku malaika wa Bwana alipomtokea na kumwambia atazaa mtoto wa kiume (Samsoni) ambaye atawaokoa watu wake Israeli na maadui zao. Huyu Samsoni biblia inasema alikuwa ni Mnadhiri wa Bwana tangu tumboni mwa mama yake.
Tukirudi tena kwenye maandiko tunamwona mwanamke mwingine aliyezaa Shujaa..Na huyu si mwingine zaidi ya Hana mke wa Helkana. Huyu naye hakuwa na mtoto kwa muda mrefu na zaidi ya yote, mke mwenza alikuwa akimtesa na kumchokoza mara kwa mara kutokana na hali yake ya utasa..Hivyo kwasababu ni mcha Mungu na alikuwa mwenye haki alimwekea Bwana nadhiri kwamba endapo atapata Mtoto wa kiume atamweka wakfu kwa Bwana maisha yake yote…na Bwana alimkumbuka akampa Neema ya kumzaa Nabii Samweli, aliyekuja kuwa nabii mkubwa sana Israeli na Mwamuzi. Na hivyo Bwana akautoa UNYONGE wake akampatia Faraja yake dhidi ya dhiki na mateso aliyokuwa anayapitia kwa muda mrefu.
Hivyo Hana alifurahi sana mpaka akazungumza maneno haya..
1 Samweli 2: 1 “Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia Bwana, Pembe yangu imetukuka katika Bwana, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia wokovu wako; 2 Hakuna aliye mtakatifu kama Bwana; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu. 2 Samwli 2:3 “Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani. 4 Pinde zao mashujaa zimevunjika, Na hao waliojikwaa wamefungiwa nguvu. 5 Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha. Naam, huyo aliyekua tasa amezaa watoto saba, Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika. 6 Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu. 7 Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu. 8 HUMWINUA MNYONGE KUTOKA MAVUMBINI, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake”.
1 Samweli 2: 1 “Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia Bwana, Pembe yangu imetukuka katika Bwana, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia wokovu wako;
2 Hakuna aliye mtakatifu kama Bwana; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.
2 Samwli 2:3 “Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.
4 Pinde zao mashujaa zimevunjika, Na hao waliojikwaa wamefungiwa nguvu.
5 Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha. Naam, huyo aliyekua tasa amezaa watoto saba, Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika.
6 Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.
7 Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu.
8 HUMWINUA MNYONGE KUTOKA MAVUMBINI, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake”.
Ukisoma mstari wa 8 unasema “HUMWINUA MNYONGE KUTOKA MAVUMBINI” Ikifunua kuwa hapo kwanza Hana alikuwa mnyonge lakini Bwana alimwinua kutoka mavumbini, alikuwa chini na sasa Bwana kamwinua juu sana..alikuwa hana mtoto lakini sasa kamzaa shujaa Samweli n.k
Tukimtazama mwanamke wa Mwisho katika maandiko ambaye naye pia alizaa Shujaa…alikuwa ni Elizabethi aliyekuwa ndugu yake Mariamu. Huyu Elizabeth naye alikuwa ni Tasa, hakuwa na Mtoto mpaka alipokuwa mzee, yeye pamoja na Mume wake Zakaria walikuwa ni wacha Mungu.. Na zaidi ya yote mume wake alikuwa ni Kuhani hivyo walikuwa wakiomba dua usiku na mchana kuhusu hali yao..Siku moja malaika alimtoke Zakaria na kumwambia mkewe aliye Tasa atachukua Mimba, na atazaa mtoto ambaye atawarejesha wengi kwa Bwana.. Na huyu mtoto tunakuja kumwona si mwingine zaidi ya YOHANA MBATIZAJI, ambaye alitabiriwa kuja kwa roho ya Eliya..Shujaa wa Bwana aliyetabiriwa kuitengeneza njia ya Bwana. Habari yake inapatikana katika (Luka mlango wa kwanza wote).
Sasa tabia za wanawake wote hawa watatu,: Yaani Mke wa Manoa, Hana, pamoja na Elizabethi utaona kuwa walikuwa ni wanawake wanyonge na wacha Mungu, na watulivu, na waliodharaulika… Hakuna hata mmoja aliyekuwa na heshima katika jamii ya watu wake wanaowazunguka, walikuwa ni wanawake wasio na uzao, kwa mfano Hana, hakuwa na watoto lakini bado alikuwa anamcha Mungu, alikuwa hakosi zamu za kwenda kuabudu Yerusalemu…Hivyo kwa mienendo yao inayompendeza Bwana na ya utulivu, na ya kusubiri kwa muda mrefu, Bwana akawapa neema ya Kuzaa MASHUJAA..
Na sio hao tu, tazama maisha ya Sara ambaye alikuwa mgumba kwa miaka mingi, mwanamke aliyemcha Mungu na mume wake mpaka kufikia hatua ya kumwita mumewe bwana. Mwanamke aliyedharauliwa na wanawake wengine wote lakini yeye ndiye alikuyekuja kumzaa Isaka. Vivyo hivyo tunaowaona akina Rebeka mambo yale yale, Raheli ambaye alikuja kumzaa Yusufu, mambo yale yale n.k. Kupitia makala iliyo hapo juu, https://www.fakewatch.is/product-category/richard-mille/rm-011/ tunaweza kukupendekezea nguo za hivi punde zaidi. kwa urefu, rangi na mitindo mbalimbali kwa kila tukio kutoka kwa chapa unazozipenda.
Sasa mpaka hapo tumeshaanza kupata picha ya MWANAMKE MARIAMU jinsi alivyokuwa naye alikuwa ni mwanamke wa dizaini gani?? Kwa kuwasoma maisha ya hao wanawake watatu waliotangulia unaweza ukapata picha kuwa Mariamu naye sio kwamba alikuwa ni mwanamke aliyekuwa na kila kitu, au aliyekuwa na heshima…Hapana! Utaona tabia yake na maisha yake ni lazima itakuwa yanafanana na hao wanawake watatu waliomtangulia… Inawezekana yeye hakuwa Tasa kwasababu alikuwa ni Bikira lakini alikuwa ni mjonge mahali Fulani.. alikuwa ni mwanamke aliyedharaulika…pengine familia yao ilikuwa inajulikana ni duni tu, na pengine ilikuwa haina jina…Pengine wabinti wenzake walikuwa wanafanikiwa na kuzaa watoto wenye sifa, yeye alijitunza tu! Alikuwa anachekwa kama Hana, alikuwa ni mdhaifu, na alikuwa hana umaarufu wowote, pengine alikuwa hana uzuri sana wa kuvutia kama mmojawapo ya wanawake wa kidunia waliokuwepo kipindi kile, lakini alikuwa mcha Mungu…
Lakini ulipofika wakati. Bwana akautazama unyonge wake..akamkirimia kumzaa SHUJAA WA MASHUJAA, na MFALME WA WAFALME haleluya!! Malaika wa Bwana akatumwa kama alivyotumwa kwa mke wa Manoa, akatumwa kama alivyotumwa kwa Zekaria Mume wa Elizabethi, akaambiwa atachukua mimba kwa uwezo wa Roho na kumzaa Bwana Yesu. Hivyo Bwana akawa amemwondolea unyonge wake, na yeye akajihisi ni mwanamke kati ya wanawake waliobarikiwa..ndio maana utakuja kuona akisema…
Luka 1: 46 “Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, 47 Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu; 48 Kwa kuwa ameutazama UNYONGE WA MJAKAZI WAKE. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa; 49 Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu. 50 Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha. 51 Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao; 52 Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; NA WANYONGE AMEWAKWEZA. 53 WENYE NJAA AMEWASHIBISHA MEMA, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu”.
Luka 1: 46 “Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
47 Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;
48 Kwa kuwa ameutazama UNYONGE WA MJAKAZI WAKE. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;
49 Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu.
50 Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha.
51 Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
52 Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; NA WANYONGE AMEWAKWEZA.
53 WENYE NJAA AMEWASHIBISHA MEMA, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu”.
Unaona anasema hapo “wanyonge amewakweza” ikiwa na maana kuwa hapo kwanza naye pia alikuwa mnyonge.
Ni jambo gani la kujifunza kwa Mariamu na wanawake hawa wengine?
Katika hali zao za Unyonge walimngojea Bwana na kumtumainia kwa saburi, na pili walijua Bwana ndiye anayeshusha na ndiye anayepandisha…Walipoona tabu nje! Bwana ndiye aliyekuwa kimbilio lao, Hana hakuzunguka kwa wapunga pepo kupata utatuzi wa tatizo lake, wala Elizabethi hakuwatafuta waganga wamtatulie tatizo lake la kukosa mtoto, walijua ni Bwana ndiye aliyewafunga matumbo yao na ipo siku yatafunguka..hivyo waliendelea kukaa katika njia zake..
Hakuna hata mmoja unaona akimlaumu Mungu katika hali yake ya unyonge aliyokuwa anapitia, wote walikuwa katika hali ya utulivu mpaka ulipofikia wakati wa Ahadi zao kutimia wote walizaa mashujaa..Ukimsoma pia Sara na Rebeka na Raheli na Ruthu aliyekuwa bibi yake Daudi..utaona jambo hilo hilo, wote walikuwa ni wanawake wavumilvu na hawakuiacha njia yao ya haki na mwisho wakazaa mashujaa.
Hivyo Dada/Kaka unayesoma ujumbe huu, ukitaka kuzaa Shujaa katika maisha yako epuka manunguniko, epuka njia za mkato, kubali kudharauliwa na kuwa mnyonge, kubali kuonekana sasa wewe ni mshamba katika Kristo,kubali kuonekana tasa usiyeweza kufanya chochote maadamu unamcha Mungu usiogope. kwasababu utafika wakati Bwana atalikumbuka teso la kijakazi wake kama Mariamu alivyosema.
Unapokosa kitu sasa usiwalaani waliokuwa nacho, wabariki,ukikosa mtoto sasa usiwalaani wanaokulaani, usizunguke kwa waganga, wala usiuache UTAKATIFU wako, ishi maisha yanayompendeza Mungu kila siku,ukijiepusha na mambo yote mabaya ya ulimwengu, kwasababu Mungu anao wakati wake na majira yake, na ukifika wakati Bwana atakufurahisha kama alivyomfurahisha Mariamu , atautoa unyonge wako kama alivyoutoa wa Mariamu na wengine.
Isaya 54: 1 “Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema Bwana”.
Bwana akubariki.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
MIRIAMU NI NANI
DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI:
JINSI MWISHO ULIVYOKARIBIA.
MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI.
VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.
Rudi Nyumbani
Print this post
Kama tunavyosoma biblia baada ya wana wa Israeli kuingia katika nchi ya Ahadi, hawakuwa na Mfalme, kila mtu alifanya jambo aliloliona ni jema machoni pake, ndivyo Biblia inavyosema katika…
Waamuzi 17: 6 “Siku hizo hapakuwa na mfalme katika israeli; kila mtu alifanya hayo aliyoyaona kuwa ni mema machoni pake mwenyewe”.
Lakini tunasoma pamoja na kuwa hawakuwa na Mfalme wala serikali yoyote inayotawala juu yao, waliishi kwa amani na Furaha, hakukuwa na mtu aliyemtawala mwenzake, wala aliyekuwa juu ya mwenzake, wote walikuwa sawa. Na walikaa katika hali hiyo kwa mamia ya miaka kwasababu ndivyo Bwana Mungu alivyopenda waishi katika hali hiyo, kwamba asiwepo aliye mkuu zaidi ya mwingine, yeye Bwana ndiye atakayekuwa Mkuu kwao na Mfalme wao.
Unaweza ukajiuliza leo hii mfano Taifa lisiwe na Raisi, wala mawaziri, wala serikali ya uongozi, litakuwaje!! kwamba kila mtu anafanya kile akionacho kuwa ni chema machoni pake, Ni wazi kuwa Taifa la namna haliwezi kusimama, ni taifa litakalo jaa vurugu, mauaji, dhuluma, uonevu, ubeberu, na mambo mengine mabaya yataonekana tu, kwasababu hakuna viongozi juu yao..
Lakini haikuwa hivyo kwa Wana wa Israeli, baada ya kutoka Misri, hawakuwa na Mfalme wala Raisi, wala mawaziri, lakini walikaa kwa utulivu na kwa utaratibu.. Kwasababu Mungu mwenyewe alikuwa katikati yao kama Roho Mtakatifu (Mfalme wao asiyeonekana kwa Macho). Akiwaamua na kuwaongoza katika utulivu na uhuru..kwa namna isiyoweza kuelezeka na kuchunguzika Ndio maana biblia inasema katika…
2 Wakoritho 3:17 Basi “BWANA” ndiye Roho; walakini ALIPO ROHO WA BWANA, hapo ndipo PENYE UHURU.”
Nataka uone hapo maandiko yanaposema kuwa “BWANA NDIYE ROHO”…Ikimaanisha kuwa Roho Mtakatifu ndiye Bwana Yule Yule, sio nafsi nyingine ya tatu hapana ni Yule Yule Bwana..Hata katika hali ya kawaida huwezi kumtenganisha mtu na Roho yake, wewe na Roho yako ni kitu kimoja, Roho yako sio nafsi yako ya tatu hapana! Roho yako ni wewe mwenyewe! Ndio maana na hapa maandiko yanasema “BWANA NDIYE ROHO” Na hakuna mahali popote katika maandiko matakatifu yamemtaja kuwa Mungu ana nafsi tatu. Hapana Mungu ni mmoja ana nafsi moja na Roho yake ni moja..Ndio maana na sisi wanadamu hatuna nafsi tatu, bali tuna nafsi moja, na Roho moja na mwili mmoja kwasababu katuumba kwa mfano wake na sura yeke yeye mwenyewe mwenye nafsi moja na Roho moja na mwili mmoja.
Sasa Kumbuka “BWANA NDIYE ROHO”… Roho Mtakatifu ndiye Yule Yule Yesu Kristo akifanya kazi katika Roho,..alipokuwa hapa duniani alikuwa anafanya kazi katika mwili, lakini ili kwamba ajiletee faida kubwa zaidi ilimpasa aondoke ili aje tena katika roho..ndio maana utaona alisema “bado kitambo kidogo hamnioni na tena bado kitambo kidogo mtaniona”, akimaanisha kuwa atakuja tena kwetu kwa njia nyingine bora zaidi itakayomfanya aingie ndani yetu, na ndio hiyo njia ya Roho, ambayo ndio ukamilifu wake kwetu sisi .
Na tukisoma pia kitabu cha Ufunuo mlango wa pili na wa tatu, tunaona Bwana Yesu Kristo akitoa ujumbe kwa Yale makanisa saba, Lakini mwanzo wa kila kanisa utaona anajitambulisha kuwa ni Bwana Yesu ndiye anayezungumza maneno yale lakini mwisho wa ujumbe utaona anasema “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”.. Hebu tuchukue mfano wa kanisa moja la Thiatira.
Mwanzoni mwa ujumbe anasema Ufunuo 2:18-19 “Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu,[YESU KRISTO] yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana. Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.”..
Sasa huyu ni Bwana Yesu ndiye anayeyazungumza maneno hayo, lakini mwishoni mwa Barua hatuoni akimalizia kama alivyoanza, kwamba badala ya kusema “mwenye masikio na asikie neno hili ambalo Mwana wa Mungu anayaambia makanisa” badala yake anasema “mwenye masikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.. Kwahiyo ni dhahiri kuwa “BWANA NDIYE ROHO” kama MTUME PAULO alivyosema.Hivyo ni muhimu kufahamu haya, ili kujiwekea vizuri msingi wa kumwelewa Bwana wetu Yesu Kristo na uweza wake, na utendaji kazi wake sasa katikati ya kanisa.
Lakini tukiendelea kwenye kile kipengele cha pili cha ule mstari kinachosema ““BWANA” ndiye Roho; walakini ALIPO ROHO WA BWANA, hapo ndipo PENYE UHURU.”
Nataka tukiangalie hicho kipengele kinachosema “ALIPO ROHO WA BWANA HAPO NDIPO PENYE UHURU”
Kwa kulinganisha na habari ile ya wana wa Israeli baada ya kutoka Misri, tunaona Bwana hakuwaweka chini ya Utumwa mwingine walipoingia kaanani, hakuwaweka tena chini ya wafalme kama farao, wala chini ya majemedari, wala hakuruhusu tena warudie maisha ya kiutumwa katika nchi ya Ahadi waliyokuwa wanaiendea. Bwana alikuwa Mfalme wao wa Amani, alikuwa katikati yao kama Roho. Akiwaweka katika utulivu, na uhuru wa hali ya juu. Bwana aliwalinda na roho mbaya za ugomvi, mateso, chuki, visasi, ubeberu, na maadui wote, fitina, dhiki, mashindano, ubinafsi…waliishi wote kama ndugu wa familia moja, na mataifa yote duniani yaliwaogopa kwa umoja huo uliokuwa katikati yao,..
Bwana aliwalinda kwa ile Hekima ya NZIGE, kama Mfalme Sulemani alivyoizungumza katika Mithali zake..Akisema nzige ni wadudu walio na akili nyingi sana.
Mithali 30: 27 “NZIGE HAWANA MFALME; Lakini huenda wote pamoja VIKOSI VIKOSI”.
Bwana aliwapa uhuru wa hali ya juu, kiasi kwamba kila mtu aliweza kufanya alilolitaka. Kulikuwa hakuna Taifa lingine duniani lililojiendesha bila mfalme, mataifa yote ya ulimwengu yalilishangaa Taifa la Israeli lenye mamilioni ya watu kipindi hicho linajiendesha pasipo mfalme na bado linafanikiwa kuliko mataifa yote, linapigana na maadui zake na kuwashinda.
Lakini tunaona maandiko yanasema baada ya miaka mingi kupita, kikainuka kizazi kingine ambacho hakikuutaka uhuru ule Bwana aliowapa na badala yake wakataka kuwa na Mfalme kama mataifa mengine, Na kwasababu walilisisitiza hilo jambo kwa nguvu Bwana akawapa haja ya mioyo yao, lakini hawakujua kuwa wamemkataa Bwana mwenyewe ambaye alikuwa katikati yao kama Roho awapaye uhuru, amani, furaha,upendo, raha na heri katika ile nchi ya Ahadi, wao wakataka uongozi wa kibinadamu…Japo Bwana aliwaonya kuwa mfalme watakayemchagua atatwaa binti zao na kuwafanya wajakazi wake, atatwaa mali zao na kuzifanya zake, atawalipisha kodi na atawashurutisha waishi kama wanavyotaka wao, lakini wao bado walimkataa Roho mtakatifu na kutaka uongozo wa wanadamu.
1Samweli 8:1-22
“1 Hata Samweli alipokuwa mzee, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli. 2 Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza aliitwa Yoeli; na jina la wa pili Abiya; walikuwa waamuzi katika Beer-sheba. 3 Ila wanawe hawakuenda katika njia zake, bali waliziacha, ili wapate faida; wakapokea rushwa, na kupotosha hukumu. 4 Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama; 5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote. 6 Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba Bwana. 7 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao. 8 Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe. 9 Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki. 10 Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya Bwana. 11 Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake. 12 Naye atawaweka kwake kuwa maakida juu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake. 13 Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji. 14 Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake. 15 Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi Wake. 16 Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng’ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe”. 17 Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu; nanyi mtakuwa watumwa wake. 18 NANYI MTALIA SIKU ILE KWA SABABU YA MFALME WENU MLIYEJICHAGULIA; BWANA ASIWAJIBU SIKU ILE. 19 Walakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu; 20 ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu. 21 Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa Bwana. 22 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti yao, ukawafanyie mfalme. Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, Enendeni kila mtu mjini kwake”.
“1 Hata Samweli alipokuwa mzee, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli.
2 Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza aliitwa Yoeli; na jina la wa pili Abiya; walikuwa waamuzi katika Beer-sheba.
3 Ila wanawe hawakuenda katika njia zake, bali waliziacha, ili wapate faida; wakapokea rushwa, na kupotosha hukumu.
4 Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama;
5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote.
6 Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba Bwana.
7 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao.
8 Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe.
9 Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki.
10 Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya Bwana.
11 Akasema, Mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake.
12 Naye atawaweka kwake kuwa maakida juu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake.
13 Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji.
14 Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake.
15 Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi Wake.
16 Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng’ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe”.
17 Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu; nanyi mtakuwa watumwa wake.
18 NANYI MTALIA SIKU ILE KWA SABABU YA MFALME WENU MLIYEJICHAGULIA; BWANA ASIWAJIBU SIKU ILE.
19 Walakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu;
20 ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu.
21 Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa Bwana.
22 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti yao, ukawafanyie mfalme. Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, Enendeni kila mtu mjini kwake”.
Mstari wa 18 unasema ..“NANYI MTALIA SIKU ILE KWA SABABU YA MFALME WENU MLIYEJICHAGULIA; BWANA ASIWAJIBU SIKU ILE.”
Unaona hapo?. Baada ya Israeli kujitwalia mfalme ndio ulikuwa mwanzo wa matatizo kwa taifa lile, tunakuja kusoma baadaye hao hao wafalme ndio waliokuwa wakwanza kuweka vinyago tena Israeli kama walivyokuwa kule Misri. Israeli ikaanza kudhoofika kidogo kidogo mpaka kufikia hatua ya Mungu kuchukizwa nao kwa sanamu zao na kutawanywa katika mataifa yote ulimwenguni.
Mambo hayo ni kivuli cha mambo yanayoendelea sasa, Mfalme wetu ni YESU KRISTO, ambaye hapo kwanza alikuja katika mwili, akatufundisha katika mwili, lakini sasa yupo katikati yetu katika ROHO anatuonya katika roho, anatuita kutoka katika utumwa wa dhambi na kutuingiza katika Uhuru wa Roho. Kwasababu BWANA NDIYE ROHO, na alipo Roho hapo ndipo penye uhuru.
Na kanisa leo limetoka katika kutawaliwa na ROHO MTAKATIFU na kuzama katika utawala wa kibinadamu, Sio Roho tena anaamua bali ni mitazamo ya wanadamu, sio tena karama za Roho zinazoongoza kanisa bali ni vyeo vinavyoongoza kanisa, kiasi kwamba ukiwa mchungaji mkuu, au kasisi, au padre, papa au shemasi, au askofu basi wewe unaweza ukasimama badala ya YESU KRISTO DUNIANI, Unaweza ukasamehe dhambi, unaweza ukawabariki watu katika dhambi zao, n.k..ndio maana hakuna, uhuru, umoja,wala amani, wala usafi,wala utakatifu ndani ya kanisa, kwasababu Kristo katupwa nje! Haiwezekani kupaa kama nzige, wakati kuna uongozi mwingine zaidi ya ROHO MTAKATIFU, Wana wa Israeli baada ya kumkataa Bwana kama Mfalme wao, ndio vyanzo vya matatizo yote ndani ya Taifa la Israeli vilipoanzia, wakaanza kujiweka watumwa wao kwa wao.
Kwahiyo Biblia inatuonya tutuoke huko, kwenye kamba za dini na udhehebu, zilizoacha uongozi wa Roho Mtakatifu (Yesu Kristo) na kuingiza uongozi wa wanadamu, Tumgeukie Mfalme wetu Yesu Kristo ambaye leo hii katika mwisho wa nyakati anatuonya “yeye aliye na sikio alisikie Neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”..Toka katika dhambi, rudi katika Neno, toka katika uvuguvugu ambao Bwana kasema atakutapika, toka katika ulevi, toka katika anasa za ulimwengu huu, rushwa, uasherati, usengenyaji, utukanaji, uuaji, ushirikina na mambo mengine yote yanayofanana na hayo..
2 Wakorintho 6 : 14 “…kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. 18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,”
2 Wakorintho 6 : 14 “…kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,”
Rudi katika kamba za kimadhehebu kwasababu hayo yote yameshahukumiwa. Tafuta Roho Mtakatifu kwasababu huo ndio MUHURI WA MUNGU. Biblia inasema hivyo katika waefeso 4:30, ikiwa na maana kuwa ukipokea Roho Mtakatifu ndani yako, basi wewe tayari ni kazi iliyokamilika. Mungu kashakutia alamu kuwa wewe ni wa kwake. Na pasipo Roho Mtakatifu hakuna uhuru wala hakuna unyakuo. Dini wala udhehebu havikuhakikishii hilo isipokuwa Yesu Kristo peke yake. Tubu leo uoshwe dhambi zako na Bwana atakupa Roho wake.
Bwana akabariki.
SIRI YA KUASI KATIKA KANISA LA MUNGU.
UTAMBUE UJUMBE WA SAA UNAYOISHI.
ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:
MWANZI ULIOPONDEKA.
Ni kweli sisi kama wakristo tunaomngojea Bwana ni wajibu wetu kila siku kuelekeza macho yetu mbinguni, tukichunguza katika maandiko yale yatupasayo kufahamu juu ya siku hizi za mwisho na kuangalia dalili zote zinazoeleza kuja kwa pili kwa Kristo, Na kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa maandiko utagundua kuwa hichi kizazi tunachoishi ndio kile kizazi kilichotabiriwa na Bwana kushuhudia kuja kwa pili kwa Kristo. Kwasababu kuu mbili kwanza ni kizazi kilichoshuhudia kuchipuka tena kwa “mtini” (yaani Taifa la Israeli), Pili: Tunaishi katika kanisa la 7, na la mwisho, ambalo ni moja ya yale makanisa 7 tunayasoma katika kitabu cha (Ufunuo 2&3), litaisha na unyakuo. Na hakutakuwa na kanisa lingine zaidi ya hilo. Na kanisa hili lilianza mwanzoni mwa karne ya 20, (yaani mwaka 1900) na litaisha na kunyakuliwa kwa kanisa.
Kadhalika biblia inatabiri pia katika wakati wa mwisho, kabla ya kuondoka kwa bibi-arusi wa Kristo na kwenda mbinguni kwenye karamu ya mwanakondoo, ni sharti kwanza IMANI ionekane ndani ya huyu bibi-arusi (Luka 18:8). Ni imani itakayomfanya anyakuliwe, vinginevyo kanisa halitaweza kuenda mahali popote kama halitafikia viwango hivyo vya ukamilifu Mungu analotaka liwe nalo. Hivyo ili hayo yote yatokee ni sharti kuwepo na uamsho na uvuvio mkubwa sana wa Roho Mtakatifu kabla ya huo wakati kufika ili wateule wawezi kufikia kiwango hicho cha ukamilifu Bwana anachotaka kukiona katika kanisa.
Na ndio ukija kusoma katika kitabu cha Yoeli 2: 23 utaona Inasema hivi;
“Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi MVUA YA MASIKA, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na MVUA YA VULI, kama kwanza.”
Unaona hapo? Biblia inazungumzia juu ya MVUA YA MASIKA na MVUA YA VULI au kwa tafsiri nyingine mvua hizi zinajulikana kama MVUA ZA KWANZA, na MVUA ZA PILI. Au mvua za sasahivi na mvua za baadaye..Sasa mvua ya kwanza Bwana aliiachilia katika ile siku ya Pentekoste, mwanzo kabisa wa kanisa na mwanzo wa ukristo, (Matendo 2), lakini ipo mvua ya mwisho ambayo Bwana ataiachilia tena katika dunia nayo itakuwa ni kwa ajili ya kulitimiliza kanisa, kwa ajili ya kuondoka hapa duniani. Na utukufu wake ni sharti uwe mkubwa kuliko ule utukufu wa lile kanisa la kwanza. Biblia imetabiri hivyo. Katika Hagai 2:9
“Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema Bwana wa majeshi…”
Hivyo mambo yatakayoambatana na uamsho huo mkubwa ambao upo mbio kutokea ni mambo ambayo hayajazoeleka kuyaona katika wakati wowote wa kanisa tangu lianze siku ile ya Pentekoste hadi sasa. “Zile nguvu za zamani zijazo” za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu ndio zitaonekana hicho kipindi, Sehemu ya pili ya ule unabii wa Yoeli aliotabiri juu ya siku za mwisho zitakavyokuwa ndio zitakwenda kuonekana katika kipindi cha majira hayo kama tunavyosoma:
Matendo 2:16-21.
“16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli, 17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto. 18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri. 19 Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi. 20 Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri. 21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.”
“16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,
17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri.
19 Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi.
20 Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri.
21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.”
Ukisoma katika maandiko hayo sehemu moja ya unabii huo utaona umetimizwa, kwamfano sehemu ya ndoto, maono, kutabiri, lakini sehemu nyingine bado yaani sehemu ya ishara za juu mbinguni, na nchi, damu, moto,jua kuwa giza n.k.. Sasa hicho kipengele kilichobakia, kitatimizwa katika kipindi hicho cha uamsho huo wa mwisho wa kanisa. Kadhalika ukisoma kitabu cha Ufunuo 10, utaona pia zipo ngurumo 7 ambazo sauti zake hazijiandikwa mahali popote katika biblia nazo hizi zitafunuliwa katika hicho kipindi karibu na ukamilifu wa kanisa takatifu la Mungu. Ujumbe utakaotolewa na hizo ngurumo 7, utakuwa ni ujumbe wa kumkamilisha bibi-arusi wa Kristo tu peke yake, na si mtu mwingine aliye nje ya mpango wa wokovu. Kwao jumbe hizo zitasikika kama ngurumo tu, hawatuaelewa chochote.
Hivyo tukiyafahamu hayo, tunajua kabisa huu ni wakati wa kujiweka tayari na kwamba mambo hayo siku yoyote yanatokea. Lakini Sasa embu turudi katika kiini cha somo letu la leo.
Kuna wakati wanafunzi wa Bwana baada ya kuona kuwa Kristo sasa ameshashinda na kupewa mamlaka juu ya vitu vyote baada ya kufufuka kwake kutoka katika wafu, wanafunzi wake wakatanuka vichwa vyao wakidhani kuwa ule ndio wakati Mungu aliokuwa anauzungumzia tangu zamani wa Bwana kuwapigania Israeli na kuwarudishia ufalme wao ambao ulikuwa umetwaliwa na wapagani kuwa muda mrefu ndio wakati sasa umefika Israeli watapata raha, na kwamba Bwana atakwenda kuwaangamiza watu wote na mataifa yote yasiyomcha Mungu.
Hivyo hiyo ikawafanya wale wanafunzi wahamishe mawazo yao yote katika kutafuta kufanya mapenzi ya Mungu kwa wakati waliokuwepo na kuwafanya wafikirie mambo ya mwisho wa dunia. Walitaka mambo yaishe haraka haraka, hawakutaka kusikia kitu kingine chochote kinachohusu wokovu, hawakuwa na muda wa kufikiria kuokoa nafsi za watu ili zisiangamie huo muda utakapofika, wao walifikiria juu ya jamii ya watu wao tu, hawakujali na watu wengine ambao hawakuwahi kuisikia kweli, watu wa mataifa ambao laiti na wao wangeijua kweli ya wao wasinge abudu sanamu.
Kumbuka Mitume waliyajua maandiko na kuelewa kuwa siku masihi wao atakapokuja kuuchukua ufalme basi atawaokoa na maadui zao wote waliokuwa waliowatesa kwa miaka mingi. Ni kweli kabisa hilo jambo lilitabiriwa na ni lazima lije kutokea, katika siku hizi za mwisho lakini lile lilikuwa sio jukumu lao kuliharakisha.
Matendo 1:6-8 “6 Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?”
Unaona walijua kabisa hilo. Lakini jibu lake lilikuwa ni hili..
“7 Akawaambia, SI KAZI YENU kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. 8 LAKINI MTAPOKEA NGUVU, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa MASHAHIDI WANGU katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”
“7 Akawaambia, SI KAZI YENU kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.
8 LAKINI MTAPOKEA NGUVU, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa MASHAHIDI WANGU katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”
Ndugu tukiyaelewa hayo maneno vizuri yatatusaidia sisi tunaoishi katika kipindi hichi ambacho tunaona kweli wakati wa mavuno upo karibu, na siku yoyote Bwana anarudi kama walivyoona mitume kwa kipindi chao. Je! na sisi kwa kulijua hilo tutahamisha mawazo yetu ya kumtumika Mungu, mawazo yetu ya kumzalia Mungu matunda ya kazi, na kustarehe na kusema tunangojea huo uamsho wa mwisho ufike sisi tuondoke?. Tuna relax tukingojea hizo sauti za ngurumo 7 zifunuliwe?. Tunangojea mpaka Mvua ya pili ishuke ndio tuanze kumtumika Mungu? Na huku hatutaki kutazama hali za watu waliokatika dhambi huu wakati, hatutaki kuyajua mapenzi ya Mungu kwetu sisi sasa hivi ni nini?..Sisi muda wote Ngurumo 7 zitafunuliwa,..ngurumo 7 zitafunuliwa.
Lakini Bwana Yesu vivyo hivyo anatuambia na sisi watu wa leo
“Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. 8 LAKINI MTAPOKEA NGUVU, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”
“Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.
8 LAKINI MTAPOKEA NGUVU, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”
Ndugu, njia za Mungu HAZITAFUTIKANI, hujui leo na kesho Mungu kaipanga vipi, au kaamua kipi kianze au kipi kiishe, Mfalme Sulemani alijaribu kufanya hivyo kuzichunguza njia za Mungu ajue mwanzo wake na mwisho wa njia zake, lakini alishindwa na mwisho wa siku alimalizia na kusema:
Mhubiri 9: 17 basi, niliiona kazi yote ya Mungu, ya kuwa haitafutikani na mwanadamu kazi inayofanyika chini ya jua; kwa sababu mwanadamu na akijisumbua kadiri awezavyo kuitafuta, hata hivyo hataiona; naam, zaidi ya hayo, mwenye hekima ajapodhania ya kuwa ataijua, lakini yeye hataweza kuiona.
Pia Mtume Paulo anasema:
Warumi 11:33 Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala NJIA ZAKE HAZITAFUTIKANI!.
Mwisho kabisa ikiwa Bwana ametupa na sisi nguvu ya kuwa mashahidi wake, hatuna budi sasa kufiria kumzalia Mungu matunda kwa wingi iwezekanavyo, na kuacha kupoteza muda mrefu kungojea mambo ambayo huna uhakika ni muda gani yatatokea. Kumbuka watu wengi wanaokaa katika hali hiyo ya kusubiria kipindi Fulani cha uvuvio kifike na huku hawana muda na shamba la Mungu sasa huwa hawafiki mbali. Kwasababu wanaishi kama watu waoteaji tu, na si kama watu wa Imani. Soma.
Mhubiri 11: 4 “Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna. 5 Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote. 6 Asubuhi panda mbegu zako, Wala jioni usiuzuie mkono wako. Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa,kama ni hii au hii,au kama zote zitafaa sawasawa.”
Mhubiri 11: 4 “Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna.
5 Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote.
6 Asubuhi panda mbegu zako, Wala jioni usiuzuie mkono wako. Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa,kama ni hii au hii,au kama zote zitafaa sawasawa.”
Tenda kazi ya Mungu bila kuangalia msimu, au wakati unaofaa Bwana huwa analaani miti ile inayosubiria msimu ndio izae, kumbuka ule mtini Bwana Yesu alioulaani ambao alitarajia akute matunda juu yake na akakosa hivyo akaulani. Biblia inasema haukuwa umezaa kwasababu ulikuwa sio msimu wake wa kuzaa, kama Bwana angeenda katika kipindi cha msimu wake ni wazi kuwa angekuta matunda, lakini njaa ilimshika kabla ya msimu kufika. Hivyo usitegemee msimu, mwisho wa siku utajikuta huzai chochote. Anza kutafuta kufanya mapenzi ya Mungu sasa angali LEO IPO, KWASABABU KESHO SI YAKO.
Ubarikiwe sana.
HISIA YA MUNGU ILIYO MBAYA KULIKO ZOTE.
HERI, WALE MUNGU ASIOWAHESABIA MAKOSA YAO.
IELEWE SAUTI YA MUNGU.
VITA BADO VINAENDELEA
Ulishawahi kuitazama kwa ukaribu ile nyota ya asubuhi? Kama ulishawahi kuifuatilia na ukaona tabia yake utagundua ni ya kipekee sana, kwasababu ndio nyota pekee inayochelewa kupotea asubuhi na ndio nyota pekee inayotangulia kuonekana wakati wa jioni kabla ya nyingine… Ukiifuatilia kwa makini utagundua kuwa hii nyota ya asubuhi ndio ile ile nyota ya jioni na iko moja tu!.
Sasa jambo la kipekee sana kuhusu hii nyota ni kwamba licha tu ya kuwa inachelewa kupotea asubuhi na kuwahi kuchomoza jioni…lakini pia HUWA INAONEKANA MCHANA. Mchana kweupe wakati kukiwa hakuna mawingu nyota hii inaonekana, Mimi binafsi nikiwa na watu kadhaa tuliwahi kulithibitisha hilo..Wakati juu kukiwa hakuna mawingu, anga la Blue tumewahi kuiona hii nyota zaidi ya mara moja.
Kwa kawaida unaweza ukadhani ni jambo lisilowezekana lakini lipo!..kwasababu hata mimi mwanzo sikuwahi kutegemea kuona nyota yoyote mchana saa saba…lakini ilitokea nikaiona siku hiyo, na sikuwa mwenyewe tulikuwa wengi nao pia waliiona, na siku inayofuata iliendelea kuonekana. Sasa hii nyota kulingana na dunia inavyosogea na yenyewe huwa inasogea…asubuhi inaweza ikaonekana mashariki, mchana ikaonekana juu ya utosi jioni ikaonekana magharibi..inabadili eneo kulingana na mzunguko wa dunia. Ukipata muda ifuatilie nyota hii, utagundua haya yote na mengine zaidi ya haya.
Sasa katika maandiko Bwana amefananishwa na hii NYOTA YA ASUBUHI. Kutokana na tabia ya nyota hiyo ilivyo…Kama tu vile sehemu nyingine Bwana Yesu alivyofananishwa na SIMBA WA YUDA, alifananishwa na simba kutokana na tabia ya samba ilivyo, kwanza Simba ni mnyama aliye na nguvu kuliko wanyama wengi, na mwenye ujasiri kuliko wanyama wote, na sehemu nyingine anajulikana kama Mfalme wa mwituni..kadhalika na Bwana wetu Yesu Kristo, aliposhinda mauti pale Kalvari, alipewa nguvu, na heshima na uweza na ufalme wa dunia yote na mbingu zote, kama vile Simba alivyo mfalme wa mwituni, kadhalika na Bwana wetu Yesu Kristo alifanyika Mfalme wa ulimwengu wote.
Sasa tukirudi katika ILE NYOTA YA ASUBUHI, utaona kuwa licha tu ya kung’aa asubuhi na jioni, lakini pia inang’aa mchana, hivyo inang’aa katika vipindi vyote vya siku, yaani asubuhi, mchana na jioni na usiku. Biblia inasema:
Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ILE NYOTA YENYE KUNG’AA YA ASUBUHI.
Ikimfunua BWANA wetu YESU KRISTO, ambaye yeye ameshinda na kukaa katika NURU ISIYOWEZA KUKARIBIWA, aling’aa milele iliyopita, anang’aa nyakati hizi na atang’aa milele…
1 Timotheo 6: 14 “..hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; 15 ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana; 16 ambaye yeye PEKE YAKE HAPATIKANI NA MAUTI, AMEKAA KATIKA NURU ISIYOWEZA KUKARIBIWA; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele”.
1 Timotheo 6: 14 “..hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;
15 ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana;
16 ambaye yeye PEKE YAKE HAPATIKANI NA MAUTI, AMEKAA KATIKA NURU ISIYOWEZA KUKARIBIWA; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele”.
Amina.
Wakati nyota nyingine zote zinang’aa jioni na asubuhi kufifia, Nyota ya Yesu Kristo haififii kamwe, NURU YAKE HAIHARIBIKI, (Haifunikwi) wakati wanadamu mashuhuri, watu maarufu, watu wakuu, na wafalme wa dunia wanakuja na kuondoka, lakini Yesu Kristo Mfalme wa Wafalme na Bwana wa mabwana anadumu milele, vizazi na vizazi hapungui nguvu, wala uweza, wala mamlaka..ANANG’AA HATA MCHANA KWEUPE..anatoa NURU isiyoweza kufunikwa na nuru nyingine, Je! Unajua kuwa mtu pekee anayeshikilia namba moja kwa umaarufu duniani kwa wakati wote ni YESU KRISTO??…Kama hujui hilo nenda kasome kwenye vitabu vya rekodi ya dunia,.. (hata mambo ya ulimwengu huu tu yanamtangaza) Ndio maana Bwana Yesu alisema yeye ndiye NURU YA ULIMWENGU. Ikiwa na maana kuwa hakuna Nuru nyingine zaidi yake. Mbingu na nchi zitapita lakini Yesu ni yeye yule jana na leo na hata milele. Haleluya!
Yohana 1: 9 “Kulikuwako NURU HALISI, amtiaye NURU KILA MTU, akija katika ulimwengu. Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua”.
Umeona hapo? Anasema kulikuwako na NURU halisi, ikiwa na maana kuwa zilikuwepo nuru nyingine lakini hazikuwa halisi, na Nuru hii halisi, ina uwezo wa kumtia Nuru kila mtu , ikiwa na maana kuwa ina uwezo wa kumfanya kila mtu kuwa kama yeye alivyo.
Ndugu yangu, Yesu Kristo Mkuu wa Uzima anataka watu wote, tuwe kama yeye, anataka wote tung’ae kama yeye, anataka tuangaze hata mchana kweupe, kusiwepo na chochote kinachoweza kutuzima, milele na milele, na ndio maana maandiko pia yanasema katika..
Mithali 4:18 “Bali njia ya wenye haki ni kama NURU ING’AAYO, Ikizidi kung’aa HATA MCHANA MKAMILIFU”.
Unaona hapo wenye haki, yaani wote waliyoikubali NURU HALISI (YESU KRISTO), biblia inasema watang’aa hata mchana Mkamilifu. Siku ile watakapomaliza kazi yao hapa ulimwenguni, ndio watadhihirika mng’ao wa utukufu wao ulivyo. Watakuwa kama miale ya Moto, watang’aa kuliko jua. Bwana hataki maisha yako leo yawe hivi kesho yanyauke, anataka uishe milele.
Danieli 12:3 “Na walio na hekima WATANG’AA KAMA MWANGAZA WA ANGA; na hao waongozao wengi kutenda haki WATANG’AA KAMA NYOTA MILELE NA MILELE”.
Mathayo 13: 40 “Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia. 41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, 42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. 43 Ndipo wenye HAKI WATAKAPONG’AA KAMA JUA katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie”.
Mathayo 13: 40 “Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia.
41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,
42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
43 Ndipo wenye HAKI WATAKAPONG’AA KAMA JUA katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie”.
Je! Na wewe leo umetiwa nuru na ile Nuru halisi (Yesu Kristo)? Je! Umemkabidhisha maisha yako leo? Siku tunazoishi ni za hatari, Kristo anakaribia kurudi kulichukua kanisa lake, na kukusanya ngano ghalani na makapi kuyakusanya kwenda kuchomwa moto. Yesu Kristo ndiye Nuru ya ulimwengu, na ukombozi kwa mwingine yoyote isipokuwa yeye..Tubu leo, ukabatizwe kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, naye Bwana atakutia Muhuri wa Roho wake Mtakatifu.
Ubarikiwe!
TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.
DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?
UMEFUNULIWA AKILI?
VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.
Siku ile unapofanyika kuwa mtoto wa Mungu, yaani siku ile unayotubu kwa kuamua kabisa kuyasalimisha maisha yako kwa Bwana Yesu, siku ambayo unageuka na kusema maisha yangu sasa ni kwa Bwana, ya kale yamepita. Na ukazingatia kufuata maagizo yote yanayoambata na wokovu wako yaani kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO. siku hiyo ambayo Roho wa Mungu anaangia ndani yako na kukushuhudia kuwa wewe ni mwana wake. Basi kuanzia siku hiyo unauhakika kuwa jina lako lipo katika kitabu cha uzima na umevuka toka mautini na kuingia uzimani (1Yohana 3:14), na kufanyika kuwa mrithi wa ahadi zote za Mungu.
Lakini ili uonekane kuwa umestahili kupokea URITHI huo utakaokuja kufunuliwa kwa wana wote wa Mungu siku ile ya mwisho ya unyakuo, ni lazima kwanza kwa namna moja au nyingine upitie njia kama aliyopitia BWANA YESU KRISTO alivyokuwa hapa duniani. Ni lazima Bwana aisafishe kwanza nyumba yake, na mambo yote machafu. Hatuwezi kuwa warithi na tabia zetu chafu tulizotoka nazo huko ulimwenguni. Hatuwezi kuwa wasengenyaji, halafu kule tukawe warithi wa uzuri Mungu aliwaandalia watakatifu wake, hatuwezi tukawa na viburi halafu tuingie uzimani hivi hivi kiwepesi, hatuwezi tukawa watukanaji, wawakaji wa tamaa, waabudu sanamu, waongo halafu tukamilikishwe mambo matukufu makuu namna ile kiwepesi wepesi tu. Ni sharti kwanza hayo yote yasafishwe. Na yakishasafishwa sasa hatuna budi kukionja kikombe cha mateso kama kile alichokinywa Bwana.
Kama YESU alikuwa ni mkamilifu bila dhambi yoyote [yeye aliyekuwa mti mbichi] lakini alionja sehemu ya HUKUMU YA MUNGU kwa ajili ya makosa yetu, itakuwaje kwa sisi tulio miti mikavu?. Hatuwezi kuikwepa hukumu yake. Hivyo kwa mtu yeyote aliye mwaminio wa kweli HUKUMU hii pia lazima ipite juu yake. Ambayo hiyo inakuja hapa hapa duniani. Tofuati na Hukumu ya watu waovu, yao itakuja baada ya kifo. Ambapo huko hakuna kutubu, mtu akishaonekana amesimama mbele ya Kiti cheupe cha Enzi cha mwanakondoo basi jua mtu huyo moja kwa moja ni kwenye ziwa la moto, kwasababu huko hakuna tena msamaha.
Hivyo hukumu hii ya Mungu itakuja juu ya mwaminio kwa namna zote mbili: Yaani pale ATAKAPOFANYA KOSA kadhalika na pale ATAKAPOISHI MAISHA MASAFI YA HAKI. Katika zote mbili hukumu ya Mungu lazima itamfiikia.
1) MTAKATIFU ATAKAPOISHI MAISHA YA HAKI:
“1Petro 4: 4.13 Lakini kama MNAVYOYASHIRIKI MATESO YA KRISTO, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. 14 MKILAUMIWA KWA AJILI YA JINA LA KRISTO NI HERI YENU; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. 15 Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine. 16 Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo. 17 KWA MAANA WAKATI UMEFIKA WA HUKUMU KUANZA KATIKA NYUMBA YA MUNGU; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje? 18 NA MWENYE HAKI AKIOKOKA KWA SHIDA, YULE ASIYEMCHA MUNGU NA MWENYE DHAMBI ATAONEKANA WAPI? 19 Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu”.
“1Petro 4: 4.13 Lakini kama MNAVYOYASHIRIKI MATESO YA KRISTO, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.
14 MKILAUMIWA KWA AJILI YA JINA LA KRISTO NI HERI YENU; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.
15 Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine.
16 Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.
17 KWA MAANA WAKATI UMEFIKA WA HUKUMU KUANZA KATIKA NYUMBA YA MUNGU; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?
18 NA MWENYE HAKI AKIOKOKA KWA SHIDA, YULE ASIYEMCHA MUNGU NA MWENYE DHAMBI ATAONEKANA WAPI?
19 Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu”.
Unaona? Kama vile Bwana Yesu alivyopitia makwazo, na majaribu mazito namna ile mpaka kufikia hatua ya kudhihakiwa na kutukanwa, na kutemewa mate, na huku hajafanya jambo lolote listahililo kutendewa mambo hayo, hakutenda dhambi yoyote kustahili msalaba, hakumdhulumu mtu yeyote kustahili kupigwa makofi, lakini aliyapitia hayo, sio kwamba alimkosea Mungu, hapana, bali Mungu aliridhika kumfanya ayapitie yale, ili aitimize HUKUMU ile juu yake ili mbele zake aonekane kama amestahili kuzipokea Ahadi zote alizokuwa amemwahidia za kumfanya awe mrithi wa vyote. Biblia inasema..
Isaya 53: 4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; LAKINI TULIMDHANIA YA KUWA AMEPIGWA, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. 5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu;…….. 9 Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa na hila kinywani mwake. 10 LAKINI BWANA ALIRIDHIKA KUMCHUBUA; AMEMHUZUNISHA; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake; 11 Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao”.
Isaya 53: 4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; LAKINI TULIMDHANIA YA KUWA AMEPIGWA, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu;……..
9 Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa na hila kinywani mwake.
10 LAKINI BWANA ALIRIDHIKA KUMCHUBUA; AMEMHUZUNISHA; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake;
11 Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao”.
Kama tunavyoona maandiko yanasema “TULIMDHANIA KUWA AMEPIGWA NA MUNGU”..Bwana Yesu kupitia majaribu kama yale mpaka kusulibiwa kwa aibu msalabani watu walidhani kuwa Mungu ndiye aliyemlipizia maovu yake, ya kujifanya kuwa yeye ni sawasawa na Mungu. Lakini Mungu alimuhukumia adhabu ile kwa ajili yetu, “Mungu aliridhika kumchubua na kumuhuzunisha” ili mwisho wa siku aje kuona wingi wa uzao Mungu alimwandalia kwa kupitia yeye, ili baadaye aje kuona matunda ya taabu yake biblia inasema hivyo, jinsi atakavyomiliki mataifa mengi na wafalme wengi. Na ndio maana mpaka sasa unaweza kuona ni jinsi gani KRISTO anamiliki kila kitu sasa hivi, Jina lake linaitwa kila mahali duniani kote, katika vizazi vyote na hapo bado ufalme wake haujaanza, siku ukija kuanza duniani ndipo tutamwelewa vizuri yeye ni kwanini anaitwa BWANA WA MABWANA na MFALME WA WAFALME.
Vivyo hivyo na sisi ambao tutakuwa warithi pamoja na yeye. Kusudi kwamba tuonekane tumestahili kuzirithi hizo ahadi nono ambazo Mungu kawaandalia watoto wake, yapo mambo tutayapitia kwa ajili ya imani yetu. Ni kweli inajulikana kila mahali kuwa mtu akiwa mwenye haki, hawezi kuudhiwa au kushitakiwa kwa namna yoyote ile, lakini kwa mkristo ni kinyume chake. Mungu kaiweka hivyo kwa makusudi yake, hiyo ndiyo HUKUMU yake kwa wana wake.
Kwa mfano unaweza ukashangaa hapo mwanzo ulikuwa ni fisadi, lakini ulipomwamini Kristo tu na kuacha ufisadi, badala ya wale wanaoupinga wakufurahie ghafla unashangaa ndio wanaanza kukuchukia, ulikuwa ni mhubiri feki, wa injili za juu juu tu, za kuwachekesha watu madhabahuni, lakini ulipoamua kuchukua uamuzi wa kusimama katika imani, na kuanza kuihubiri ile injili ya mitume,sasa badala ya kufurahiwa ghafla makasisi wenzako wanaanza kukuangalia vibaya na kukutenga, na kukukataza kuhubiri mbele ya makanisa yao. Ulipokuwa katika dhambi ndugu na marafiki hawakuwa na neno lolote juu yako. Lakini siku ulipoamua kumfuata Kristo badala wakufurahie umekuwa mtu mwema, ndio kwanza wanaanza kukuzungumzia vibaya, wanaanza kukuchukia bila sababu, wanaanza kukuwekea vinyongo, wanaanza kukuwekea mitego isiyo na sababu ukitazama kosa lako hulioni.
Mtume Paulo aliliona hilo tangu zamani na kusema
2Timotheo 3:12 “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu WATAUDHIWA”.
Wafilipi 1: 29 “Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake;”
Hivyo ndugu mkristo, usishangae wala usiogope unapoyapitia haya, kwasababu ya Imani yako, unapopigwa, unapofungwa, unapotengwa, unapoachwa jua tu hiyo ni hukumu ya Mungu inapita juu yako, hata mitume walipitia kadhalika na wakristo wenzako duniani wanapitia hivyo hivyo ili siku ile uonekane kuwa umestahili kupata vinono vya ufalme ule usikuwa na mwisho kama Bwana Yesu yalivyomkuta ni sharti upitie hapo..Jua tu hivyo ni vya kukutengenezea TAJI bora utakapoingia katika ufalme ule. Wakati mwingine utashangaa kuona misiba ya watu wako wa karibu, au utapoteza vile uvipendavyo kwasababu umeamua tu kumfuata Kristo, utapitia njaa, utapitia shida, n.k. Lakini kuwa na uhakika kuwa hujapoteza lolote, hiyo ni hukumu ya Mungu itakayopita juu yako kwa muda.
Sasa biblia ndio inakuja kusema IKIWA MWENYE HAKI ATAOKOKA KWA SHIDA NAMNA HIYO?. Asiye mcha Mungu na mwenye dhambi ataonekania wapi?. Ndugu hukumu za Mungu si za kuzitamani kabisa. Ikiwa huyu ambaye anamcha Mungu leo hii unamwona yupo katika dhiki,na pengine taabu. Ikiwa watakatifu ndio unawaona kuwa wenyewe ndio watu wa bahati mbaya. Wewe ambaye sasa huna habari na Mungu siku ile utaonekania wapi? Ni nani atakayasimama badala yako kukutetea siku ile?.
Leo hii watu wanaowadhihaki watakatifu na kusema hawana uelekeo wowote, wana shida, wamepoteza dira ya maisha, maisha yao ni ya dhiki, hawana mbele wala nyuma, hawajui hata wale wayahudi walimwambia hivyo hivyo Bwana Yesu. Walisema ngoja sasa tumuue tuone huyo baba yake kama atakuwa na uwezo wa kumshusha msalabani, . Na walipoona hajashushwa msalabani waliendelea kudhihaki, hakisema huyo Mungu mbona hamsaidii? lakini hawakujua kuwa Mungu ndiye aliyeridhika kumchubua,.Ikiwa Bwana Yesu ambaye hakuwa na dhambi aliupata ule ufalme kwa taabu vile, sisi ambao leo hii tunaudharau wokovu na njia ya msalaba tutaonekania wapi siku ile.?.
2) MTAKATIFU ATAKAPOMKOSEA MUNGU.
Leo hii watakatifu wakimkosea Mungu kwa kosa linaloweza kuonekana kuwa dogo, inawagharimu adhabu kubwa sana hata wakati mwingine kupoteza maisha yao kama ilivyokuwa kwa Hanania na safira (Matendo 5), kwa kosa kutokutimiza tu nadhiri zao walikufa wote wawili pale pale.
Kumbukumbu 8: 5 “Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa kama vile baba amrudivyo mwanawe, ndivyo Bwana, Mungu wako, akurudivyo”.
Sasa hao walio waasherati, na waabudu sanamu, na washirikina, na wenye dhambi wote ambao hawataki sasa kuyasalimisha maisha yako kwa Bwana. siku ile watastahimili vipi ile hukumu?. Pengine utatoka leo kuzini na usione chochote, utatoka leo kuua na jambo lolote baya lisikutokee, utakwenda kulawiti na ubaya wowote usikupate. Utakwenda kuloga na usikutwe na ubaya wowote, Sio kwasababu Mungu hakuoni au wewe ni mtu wa kipekee sana kwake zaidi ya Yule anayemcha yeye na kupitia mabaya. Hapana fahamu tu jambo moja, Hukumu ya waovu sio sasa. Bali ni baada ya dunia hii yote kuisha. Siku ile mataifa yote yatakaposimama mbele ya kiti cha huku cheupe cha enzi cha mwanakondoo na kila mmoja atakapotoa hesabu ya mambo yake yote aliyokuwa anayafanya hapa duniani. Sio kutamani kuwepo siku hiyo. Kumbuka watakatifu wale walimwamini Kristo wakati huo hawatakuwepo.
Huu si wakati wa kuchekezea maisha yako, Kila mtu anajua kuwa haya ni majira ya kurudi kwa Bwana Yesu mara ya pili duniani, Kila mtu anajua kuwa dhiki kuu ipo mlangoni kuanza, na Yule mpinga-kristo kunyanyuka. Sasa unasubiri nini usitengeneze maisha yako sasa?.
Ikiwa mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi?.
Ni furaha yangu, ukigeuka sasa angali muda upo.
Tafadhali hubiri habari njema hizi kwa wengine.
UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI.
AYUBU 28 : HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?
‘’MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI’’..NA NDIVYO ILIVYO KWA UASHERATI
JE! WEWE NI MBEGU HALISI?
2 Wakorintho 3:2 “NINYI NDINYI BARUA YETU, iliyoandikwa mioyoni mwetu, INAJULIKANA NA KUSOMWA NA WATU WOTE;”
Maisha tunayoishi sisi ni BARUA ya Kristo, watu watutazamapo, wanapata ujumbe hata kabla ya sisi kuzungumza lolote,. Na matendo yetu ndiyo maandishi, na siku zetu ndizo kurasa, Tangu tulipompa Bwana maisha yetu, siku hiyo hiyo tunaanza kuandika kurasa njema za barua zetu.
Injili yenye matunda Kristo anayoyataka haihubiriwi kwa maneno matupu! Hapana bali inahubiriwa kwa matendo..Matendo yetu ndiyo yanayohubiri injili kuliko kingine chochote, Matendo yetu ndiyo yanayomtangaza Kristo kuliko kitu kingine chochote. Tunaweza tukawa na uwezo mzuri wa kuhubiri au kuongea lakini kama matendo yetu hayaendani na tunachokizungumza basi injili tunayoihubiri ni BURE!!.
Unaweza ukawa unahudhuria kanisani kila siku, unasaidia watu, lakini kama maisha yako ya siri ni machafu, kama maisha yako ya pembeni ni ya kiasherati, au ni mtazamaji wa pornography, au mfanyaji masturbation au mtukanaji, au mwizi, au mwuaji, au unacheza kamari, au mtu wa hasira usiyesamehe basi wewe ni barua yako ni mbaya, haijalishi unalitaja jina la Kristo mara ngapi..
Maisha yetu yanapaswa yahubiri injili kwa watu wa nje kiasi kwamba mtu akikuona tu anajua moja kwa moja Yule ni Mkristo hata kabla hujazungumza lolote, akikuona juzi, jana na leo maisha yako ni yale yale masafi, hata kabla hajazungumza na wewe Neno moja anakiri moyoni kwamba wewe ni mwanafunzi wa Kristo.
Sio lazima tuonekane tumebeba biblia, au tumevaa kanzu, au tumevaa kama watu wa dini au tusikiwe tunaimba mapambio, au tuonekane tunaenda kanisani kila siku, au tusikiwe tukisali kila siku hapana! Hiyo ni vizuri lakini hata pasipo hayo mambo, pasipo watu kutusikia tukisali, au tukiimba, au tukienda kanisani n.k inapaswa wakituona tu, ndani ya muda mfupi wameshajua sisi ni watu wa namna gani, washajua kuwa sisi milki ya Yesu Kristo.
Unaweza usiwe unaongea kama watu wa kidini, lakini inapasa mtu akikutazama tu maisha yako, siku mbili tatu,lazima kuwe kuna kitu ndani yake kinamshuhudia kwamba wewe ni mwana wa Mungu. Kwa jinsi maisha yako yanavyoangaza Nuru, na kuonekana Barua inayosomeka vyema.
Mathayo 5:16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona MATENDO YENU mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni…
Unaona? Kitu Bwana Yesu anachosema hapo ni kwamba nuru ya mtu inaangaza kwa matendo yake, na si kitu kingine na hichi ndicho watu wanachokitazama.
Hebu tujifunze kidogo Kitabu cha ESTA.
Esta alikuwa ni Myahudi lakini alizaliwa katika nchi ya Babeli, wakati wana wa Israeli wapo utumwani, hakuwahi kufika nchi yake Israeli.. aliishi na Kaka yake aliyeitwa Mordekai, baada ya wazazi wake kufa (ambapo Baba yake Esta alikuwa ni mjomba wake Mordekai). Walikuwa wanamcha Mungu yeye na Mordekai, lakini ilipofika wakati Mfalme wa Uajemi anatafuta malkia mwingine sehemu ya Malkia Vashti aliyemvunjia heshima Mfalme, Mordekai alimpandisha Esta kwenda kushindania hiyo nafasi ya umalkia miongoni mwa wanawali watakaochaguliwa na mfalme, Lakini jambo la kimiujiza ni kwamba Mordekai wala Esta hawakujitambulisha kuwa wao ni watu kutoka taifa gani wala Imani yao ni Imani gani…Na chakushangaza ni kwamba japo kuwa Esta hakuidhihirisha Imani yake mbele ya nyumba ya Mfalme wa Uajemi, lakini kwa matendo yake TAYARI WALE WALIOKUWA WANAWACHAGUA WANAWALI, WALISHAMSOMA ESTA NA KUGUNDUA KUWA NI MTU WA KIMUNGU, MWENYE TABIA NJEMA. Na kama ni msomaji wa Biblia utaona kuwa Ni Esta peke yake ndiye aliyepata kibali mbele ya Mfalme kuwa MALKIA kati ya wale wanawali wengine.
Sasa Ni nini tunachoweza kujifunza hapo?? Hata pasipo Kutaja DINI YAKO,WALA DHEHEBU LAKO, WALA IMANI YAKO, watu wanaweza kukusoma tu na kugundua wewe ni mtu wa namna gani? Watu wanaweza wakakusoma tu na kugundua Barua yako ni barua ya namna gani. Kwa mwenendo wako tu hata pasipo kusema BWANA ASIFIWE! au BWANA ATUKUZWE!
Sasa tukirudi kwenye kitabu cha Esta, tunaweza tukajifunza jambo lingine kubwa sana..
JE! Unajua kuwa kitabu cha ESTA ndio kitabu pekee cha Biblia ambacho kuanzia mwanzo wake hadi mwisho wake hakuna Neno “BWANA” wala neno “MUNGU”? Kama hujui hilo nenda kapitie tena biblia yako na utaligundua hilo. Sasa Jambo hilo linafunua nini? Japokuwa kitabu cha Esta hakijamtaja mahali popote Bwana wala neno Mungu halionekani, lakini tukisomapo kile kitabu tunamwona Mungu kwa sehemu kubwa sana na uwezo wake, na bila shaka watu wote tunafahamu kuwa ni kitabu takatifu cha Mungu…ikifunua jambo lile lile kwamba unaweza usionekane unalitaja jina la Bwana Mahali popote pale lakini watu WASOMAPO BARUA YAKO WANAMWONA MUNGU kwa kiwango kikubwa. Na hicho ndicho Mungu anachotaka. Simaanishi kuwa usilitaje jina la Bwana mahali popote hapana, ni wajibu wetu sote kufanya pia na hayo.
Mungu Hataki tuwe kama wanafki kama mafarisayo, ambao kwa nje, tunaonekana ni wakidini lakini kwa ndani ni wachafu. Malkia Esta hakubeba Torati na kuingia nayo kwa Mfalme ndipo akubalike, hakujidhihirisha kwamba yeye ni Myahudi, mwana wa Ibrahimu, na kwamba anamwabudu Mungu wa aliyeziumba Mbingu na nchi..hakufanya hayo yote, yeye aliingia tu mbele ya mfalme na barua ya maisha yake, na utii wake, unyenyekevu wake, upole wake, usikivu wake, na utulivu wake, na tabia yake njema, aliingia na tabia yake ya kuwa na kiasi, ya mtu asiye na majivuno, asiye na kiburi, asiyekuwa na tamaa, aliingia na tabia yake ya kuridhika, na kutotamani mambo makubwa, aliingia na tabia yake ya kutokusengenya, ya kutokuwa mwashetati, hiyo ndiyo iliyomfanya apendwe na Mfalme, hiyo ndiyo iliyomfanya akubalike..Hiyo ndiyo iliyomfanya Barua yake isomeke vyema mbele za Mfalme, na Ufalme wa Uajemi wote, na hiyo ndiyo iliyomfanya KITABU CHAKE JAPOKUWA HAKINA JINA LA BWANA MAHALI POPOTE LAKINI KIMEINGIA KATI YA VITABU 66 VYA BIBLIA.
Kaka/Dada uliye mkristo usomaye ujumbe huu, ifanye barua yako isomeke vyema, kusudi kwamba watu wakishauona mwenendo wako, roho zao zipate kuponywa. Mwenendo tu wa mtu ni nguvu tosha ya kumgeuza mtu kama vile Neno linavyoweza kumgeuza mtu. Wakati mwingine ndoa yako inamatatizo na umehangaika huku na kule, umefunga na kusali, lakini bado mume wako anazidi kuwa mwovu, anazidi kuwa mlevi, mke wako hana nidhamu, hamchi Mungu, watoto wako ni watukutu hawataki kukutii, wazazi wako ni waashirikina, wanagombana, wametengana..Na wewe ni mkristo umejaribu kuomba, hata wakati mwingine kuwashuhudia lakini bado hakuna mabadiliko..Tatizo linaweza kuwepo katika mwenendo wako, wanapokutazama hawaoni kitu cha kuwavutia kuwa kama wewe. Lakini ikiwa mwenendo wako utaubalishwa na kuishi maisha ya nidhamu na utakatifu na kumcha Mungu, basi fahamu kuwa hiyo ni injili tosha ya kuwafanya wao wabadilike. Embu soma vifungu hivi vinavyosema juu ya familia.
1Petro 3:1 “Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 2 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.”
1Petro 3:1 “Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;
2 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.”
Unaona hapo? Hivyo ndugu ikiwa bado hujamkabidhi Bwana Yesu maisha yako, mpe leo, Tubu mgeukie kwasababu yeye ndiye Njia ya kufika mbinguni, hakuna mwingine, njia nyingine za kidini, kidhehebu, mtu binafsi, n.k zote zinaishia mautini..Yesu ndiye mwokozi, Siku tunazoishi ni siku za Mwisho, zilizotabiriwa. Na Neema inakaribia kurudi Israeli, na Kristo kulichukua kanisa lake, je! umo miongoni mwa watakaoenda na Bwana??
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo izidi kuwa nawe!!
Tafadhali “share” kwa wengine,
Mungu akubariki.
MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.
HADITHI ZA KIZEE.
UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.
MADARAKA YA WAKATI MKAMILIFU.
LULU YA THAMANI
Kwa muda mrefu Mfalme Sulemani aliingia katika kuchunguza hekima ya viumbe vyote duniani, mimea yote na kazi zote za wanadamu zinazofanywa chini ya jua hili ili kutoa jawabu moja ambalo kwa hilo litamfanya mwanadamu aweze kufungua milango yote ya BARAKA,na MAARIFA na UZIMA na AMANI katika siku zake zote aishizo hapa duniani. Mfalme Sulemani aliingia katika utafiti huo wa hali ya juu kwa wa muda mrefu sana, tangu ujana wake akiongozwa na ile hekima iliyokuwa ndani yake, biblia inasema alijaribu hata “upumbavu” mambo yasiyopaswa kufanywa na mtu yeyote wa Mungu, lakini yeye alifanya kwa kusudi tu la kulivumbua hilo jawabu pengine linaweza likawa limejificha ndani yake.. Jawabu ambalo litampa mwanadamu wepesi wa maisha, amani, furaha ya kudumu, utulivu, kuridhika,uzima, upendo n.k.
Uchunguzi huu wa Sulemani tunaweza kuusoma katika kitabu cha Mhubiri tukianzia mwanzoni kabisa tunaona Sulemani akieleza jinsi alivyoutia moyo wake kutafuta na kuchunguza hekima ili kupata jawabu hilo moja, hivyo ilimgharimu kujaribu kitu kimoja kimoja kinachoweza kutamanika hapa duniani, na kila alichokijaribu na kuona sio chenyewe chenye ufunguo wa maisha kwa kwa mwanadamu alisema ni UBATILI, hivyo akaendelea na kingine, kadhalika alipoona hicho nacho hakiwezi kumsaidia mwanadamu alisema ni UBATILI..hivyo akakiacha akaendelea na kingine, hivyo hivyo mpaka alipofanikiwa kujaribu kila kitu unachoweza kukifahamu hapa chini ya jua, hakuna ambacho hakukijaribu, mpaka kwa wachawi na miungu migeni alifika, hakuna kitu ambacho hakukijaribu Sulemani, alijaribu vyote, lakini vyote aliona ni ubatili na upotevu ni sawa na kuufuata na kujilisha Upepo, mpaka tunapokuja kusoma sasa kwenye sura ya mwisho kabisa ya kitabu cha Mhubiri baada ya Sulemani kwenda huku na kule, kufanya hichi na kile, kujaribu hichi na kile, ndipo mwisho wa siku anakuja kulipata JAWABU lenyewe alilokuwa analitafuta kwa muda mrefu, tangu ujana wake, lililomgharimu hata kuipoteza nafsi yake katika mambo yasiyompasa kuyafanya ili tu alipate na hatimaye akalipata jawabu hilo..Haikuwa kazi rahisi..
Ni sawa na wewe leo unakwenda kutafuta nguo yenye nyuzi za rangi 10 iliyoandikwa karatu katika soko la mitumba, itakugharimu kuchambua mtumba mmoja hadi mwingine mpaka uipate, na hiyo haitakuwa kazi ya kuisha ndani ya siku moja, utafukua mitumba na mitumba soko zima na pengine unaweza usiipate.
Ndicho kilichomgharimu Sulemani kuipata hiyo kanuni ya mwanadamu ya kuishi hapa duniani kwa wepesi na furaha na amani, kwa lugha ya kisayansi tunaweza kusema FORMULA ya maisha ya mwanadamu ambayo katika hiyo mwanadamu atakuwa na uwezo wa kufungua milango yote migumu ya maisha yake ya sasa na ya baadaye ambayo hapo kwanza kwa kuikosa hiyo ndio iliyomfanya mwanadamu awe mtu wa kutangatanga huko na kule, ajisumbue kwa hili na lile, ajitese kwa hichi na kile. Lakini sasa akishaifahamu hii kanuni basi maisha yake yatakuwa matamu yenye raha na mafanikio.
Na jawabu hili tunakuja kuliona mwishoni kabisa mwa kitabu alichokiandika SULEMANI cha Mhubiri..Sulemani anasema
Mhubiri 12: 13 “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; MCHE MUNGU, NAWE UZISHIKE AMRI ZAKE, MAANA KWA JUMLA NDIYO IMPASAYO MTU. 14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni KILA KAZI, pamoja na KILA NENO LA SIRI, likiwa jema au likiwa baya”.
Mhubiri 12: 13 “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; MCHE MUNGU, NAWE UZISHIKE AMRI ZAKE, MAANA KWA JUMLA NDIYO IMPASAYO MTU.
14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni KILA KAZI, pamoja na KILA NENO LA SIRI, likiwa jema au likiwa baya”.
Unaona jumla mambo yote yampasayo mtu ni hii KUMCHA MUNGU, NA KUZISHIKA AMRI ZAKE.Basi!!..kwa hilo kila mlango utafunguka, ambao mwanadamu alikuwa anajitesa kwayo.
Sasa sisi tunaoishi kizazi hiki, tumesharahisishiwa mambo yote, leo hii unahangaika kutafuta mali ukidhani kuwa huko ndiko utapata jawabu la maisha yako, ndugu Sulemani alizitafuta sana tena kwa lengo la kupata jawabu kama hilo hilo unalolitafuta wewe, lakini hakuliona mwisho wa siku akasema ni UBATILI na UONGO..
Mhubiri 7: 27 “Tazama, asema Mhubiri, mimi nimeyaona hayo kwa kulinganisha hili na hili, ili kuitafuta jumla; 28 ambayo bado nafsi yangu nikali nikiitafuta, nisiione;….”
Mhubiri 7: 27 “Tazama, asema Mhubiri, mimi nimeyaona hayo kwa kulinganisha hili na hili, ili kuitafuta jumla;
28 ambayo bado nafsi yangu nikali nikiitafuta, nisiione;….”
Leo hii unatafuta kuzitii tamaa zako za macho na anasa,kila mwanamke mzuri unataka awe wako, kila mwanaume mwenye utajiri unataka awe mume wako, ukidhani kuwa utapata raha nafsini mwako, na hivyo maisha yako yatakuwa mepesi ukidhani kuwa hiyo ndio maana ya maisha. dada/kaka Sulemani alishalijaribu hilo nalo kwa ajili yetu, ili aone kama kweli humo ndani yake kuna jambo la maana sana la kumfaa mwanadamu lakini alingundua ndani yake kuna ubatili na mauti, yeye alikuwa na mamia ya wake na Masuria lakini hata kimoja hakuona kama kinao uwezo wa kutoa jawabu la maisha ya mtu hapa duniani.
Unadhani siku ukishajenga nyumba na kuwa na familia nzuri ndio siku utakayofurahia maisha yako?. Na hivyo leo hii unazunguka huku na kule unajitabisha kwa hili na lile ili uifikie hiyo furaha?. Ndugu ni vizuri kufanya hivyo lakini fahamu kuwa hilo sio jawabu la maisha yako.
Unaona kuwa ulevi ndio furaha ya maisha ya mwanadamu, hilo nalo lilishajaribiwa lakini alisema halina manufaa yoyote ya kumwokoa mwanadamu. Embu sikiliza walau kidogo maneno haya ya Sulemani aliyosema:
Mhubiri MLANGO 2 “1 Nikauambia moyo wangu, Haya, nitakujaribu kwa njia ya furaha basi ujifurahishe kwa ANASA. Na tazama, hayo nayo yakawa ubatili. 2 Nikasema juu ya kicheko, Ni wazimu; na juu ya furaha, Yafaa nini? 3 Moyoni mwangu nikapeleleza jinsi ya kuuburudisha mwili KWA MVINYO, na (moyo wangu ukali ukiniongoza kwa hekima) jinsi ya kushikana na upumbavu, HATA NIYAONE YALIYO MEMA YA KUWAFAA WANADAMU, ILI WAYAFANYE HAYO CHINI YA MBINGU SIKU ZOTE ZA MAISHA YAO. 4 Nikajifanyizia kazi zilizo kubwa; nikajijengea nyumba; nikajipandia mashamba ya mizabibu; 5 nikajifanyizia bustani na viunga, na kuipanda humo miti yenye matunda ya kila namna; 6 nikajifanyizia birika za maji, ya kuunyweshea mwitu mlimopandwa miti michanga. 7 Nami nikanunua watumwa na wajakazi, nikawa na wazalia nyumbani mwangu; tena nikawa na mali nyingi za ng’ombe na kondoo, kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; 8 TENA NIKAJIKUSANYIA FEDHA NA DHAHABU, NA TUNU ZA KIFALME NA ZA KUTOKA KATIKA MAJIMBO. Nikajipatia waimbaji, waume kwa wake, nao wale ambao wanadamu wanawatunuka, masuria wengi sana. 9 Basi nikawa mkuu, nikaongezeka kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; pia hekima yangu nikakaa nayo. 10 Wala sikuyanyima macho yangu cho chote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote; maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote, na hii ilikuwa sehemu yangu katika kazi yangu yote. 11 Kisha nikaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu, na taabu yote niliyotaabika katika kuzitenda; na tazama, YOTE NI UBATILI NA KUJILISHA UPEPO, WALA FAIDA HAKUNA CHINI YA JUA”.
Mhubiri MLANGO 2
“1 Nikauambia moyo wangu, Haya, nitakujaribu kwa njia ya furaha basi ujifurahishe kwa ANASA. Na tazama, hayo nayo yakawa ubatili.
2 Nikasema juu ya kicheko, Ni wazimu; na juu ya furaha, Yafaa nini?
3 Moyoni mwangu nikapeleleza jinsi ya kuuburudisha mwili KWA MVINYO, na (moyo wangu ukali ukiniongoza kwa hekima) jinsi ya kushikana na upumbavu, HATA NIYAONE YALIYO MEMA YA KUWAFAA WANADAMU, ILI WAYAFANYE HAYO CHINI YA MBINGU SIKU ZOTE ZA MAISHA YAO.
4 Nikajifanyizia kazi zilizo kubwa; nikajijengea nyumba; nikajipandia mashamba ya mizabibu;
5 nikajifanyizia bustani na viunga, na kuipanda humo miti yenye matunda ya kila namna;
6 nikajifanyizia birika za maji, ya kuunyweshea mwitu mlimopandwa miti michanga.
7 Nami nikanunua watumwa na wajakazi, nikawa na wazalia nyumbani mwangu; tena nikawa na mali nyingi za ng’ombe na kondoo, kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu;
8 TENA NIKAJIKUSANYIA FEDHA NA DHAHABU, NA TUNU ZA KIFALME NA ZA KUTOKA KATIKA MAJIMBO. Nikajipatia waimbaji, waume kwa wake, nao wale ambao wanadamu wanawatunuka, masuria wengi sana.
9 Basi nikawa mkuu, nikaongezeka kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; pia hekima yangu nikakaa nayo.
10 Wala sikuyanyima macho yangu cho chote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote; maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote, na hii ilikuwa sehemu yangu katika kazi yangu yote.
11 Kisha nikaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu, na taabu yote niliyotaabika katika kuzitenda; na tazama, YOTE NI UBATILI NA KUJILISHA UPEPO, WALA FAIDA HAKUNA CHINI YA JUA”.
Unaona hapo ndugu mimi na wewe hatupaswi kuyajaribu hayo yote ambayo tayari yalishajaribiwa na kuonekana kwamba hayawezi kutupatia sisi furaha na uzima wowote ndani yetu. Tuufuate ushauri wa wenye hekima, tuufuate ushauri wa mababa, tuufuate ushauri wa walitutanguliza zamani wazee wetu ambao kwa hekima za Mungu waliona na kufundishwa mengi Ndio maana Suleimani akaitwa akaitwa MUHUBIRI.. Usidanganyike na wahubiri wengine wanaokutumainisha katika mambo ya ulimwengu huu, Tumsikilize Muhubiri huyu aliyetiwa mafuta na Mungu mwenyewe na kuitwa MUHUBIRI,na ndio maana Sulemani alisisitiza sana katika mithali zake akisema..
Mithali 7: 1 “Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako. 2 Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako. 3 Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako”.
Mithali 7: 1 “Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako.
2 Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako.
3 Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako”.
Mithali 4: 10 “Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu; Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi. 11 Nimekufundisha katika njia ya hekima; Nimekuongoza katika mapito ya unyofu. 12 Uendapo, hatua zako hazitadhiikika, Wala ukipiga mbio hutajikwaa”.
Mithali 4: 10 “Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu; Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi.
11 Nimekufundisha katika njia ya hekima; Nimekuongoza katika mapito ya unyofu.
12 Uendapo, hatua zako hazitadhiikika, Wala ukipiga mbio hutajikwaa”.
Yesu pekee ndio jawabu la maisha yako, haijalishi utahangaika wapi, utasumbuka wapi, utajitaabisha na nini, leo ni rahisi kupuuzia lakini utafika wakati ambao utaona hivyo vitu ulivyovitaabikia havikukupa jawabu la maisha yako hapo ndipo utapozikumbuka zile hekima ulizopewa na mababa ukazikataa. Na kumbuka ukishafika huo wakati huwezi tena kuwa na raha, utajikuta tu unayachukia maisha yako. Kwasababu umeshachelewa, na wala huna nguvu tena ya kumshinda yule mwovu kwasababu siku za maisha yako zimeshakwenda..
Mwanadamu huwa akishafika hatua hiyo ni ngumu tena kumgeukia Mungu kwasababu anakuwa ameshachanganyikiwa rohoni hajui ni wapi tena pa kuanzia,ni wapi pa kumalizia, japo atajifanya kuwa anafuraha kwa nje lakini ndani yake huzuni na hofu vimemjaa kwasababu alipuuzia hekima za mababa angali akiwa kijana, hakumkumbuka muumba wake siku za ujana wake, hata hekima za kidunia zinasema Samaki mkunje angali mbichi..Akishakauka ukijaribu kufanya hivyo atavunjika kama kijiti badala ya kukunjika..ndivyo itakavyokuwa hali yake mtu yule anayeupuuzia wokovu sasa..
Sulemani anasema tena “1 Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.(Mhubiri 12:1)”.
Unaona hapo zipo siku ZILIZO MBAYA, kadhalika zipo siku ZISIZO NA RAHA ndani yake zitakuja huko mbeleni kwa kila mwanadamu ambaye hamkumbuki muumba wake katika siku za ujana wake.
Wewe ni kijana unayesoma hii habari, yatafakari yote ambayo yalimgharimu Sulemani kuyafanya wakati mwingine hata mambo yasiyompendeza Mungu ili kusudi kwamba tu avumbue jumla ya maisha yako, unende katika kanuni ya maisha iliyo sahihi..
Na sasa JUMLA hiyo ipo wazi mbele ya macho yetu, siku ile hutakuwa na udhuru tena, ukisema nilitanga tanga kutafuta raha na amani na ndio maana niliingia katika anasa na ushirikina, Sulemani atakuhukumu siku ile kwa kutokutii sauti ya Mungu inayozungumza na wewe kupitia injili yake.
TUBU sasa, mpe YESU KRISTO maisha yako, acha dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kutozifanya tena na sio kimazoea, kisha ukabatizwe katika ubatizo ulio sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi katika jina la YESU ili upate ondoleo la dhambi zako, kisha kuanzia hapo Bwana mwenyewe atakupa Roho wake Mtakatifu kukusaidia kuushinda ulimwengu na kumcha Yeye kila siku. Na maisha yako yatakuwa SALAMA katika mikono yake yeye aliyekupa huo uzima, siku zako zilizobakia hapa duniani.
Ni maombi yangu utafanya hivyo leo.
TUSIFUNGWE NIRA PAMOJA NA WASIOAMINI.
KWANINI TUWE WENYE BUSARA KAMA NYOKA?
DHAMBI YA ULIMWENGU
Mhubiri 12: 1 “MKUMBUKE MUUMBA WAKO SIKU ZA UJANA WAKO, KABLA HAZIJAJA SIKU ZILIZO MBAYA, Wala HAIJAKARIBIA MIAKA utakaposema, MIMI SINA FURAHA KATIKA HIYO”.
Biblia inasema “Mkumbuke” ikiwa na maana kuwa ni wakati ambao kuna “kusahau” wakati wa kupumbazwa na mambo mengi, …Na huo wakati si mwingine zaidi ya wakati wa UJANA. Na biblia inasema pia zitakuja nyakati au siku zilizo mbaya, ambazo zitakuwa sio za furaha, nyakati zisizofaa tena kumgeukia yeye,..
Tafakari kwa makini hiyo sentesi “Mkumbuke muumba wako kabla hazijaja siku !!” Ina maana sio kila wakati unafaa katika kumgeukia Mungu..Ni rahisi kusema nitakapokuwa MZEE nitamgeukia Mungu, au nitakapofikia kipindi Fulani au nitakapokuwa nimezidiwa sana, au nitakapokuwa nimefilisika sana, au nitakapokuwa katika ugonjwa wa kufisha, au siku nitakayokaribia kufa ndiyo nitakuwa karibu na Mungu. Ndugu hiyo ni hatari sana neema ya Mungu haiotewi. yeye anasema “mkumbuke Muumba wako kabla hazijaja siku zilizo mbaya”..zingatia hilo neno kabla!! Kabla!!,.Kumbuka Wengi wanaopata Neema ya kuokolewa katika hizo nyakati zilizo mbaya ni wale tu ambao hawajawahi kabisa kuisikia injili hapo nyuma, mfano wa Yule muhalifu aliyesulibiwa na Kristo pale Msalabani. Hivyo usiliweke hilo akilini kwa sisi wa kizazi hiki ambacho injili ya Kristo inahubiriwa kila siku barabarani lakini hatutaki kusikia au tunapuuzia tukitumaini itafika siku tu tumtafuta Mungu..Hilo tuliondoe akilini.
SASA HIZO SIKU ZILIZO MBAYA(au siku za matatizo) NI ZIPI? AMBAZO TUMEONYWA TUMKUMBUKE MUUMBA WETU KABLA HAZIJAFIKA??
Ukizidi kusoma mistari inayofuata utaona hizo siku siku mbaya zinazozungumziwa hapo ni zipi. Ukiwa na nafasi binafsi utasoma, sura yote ya 12,lakini kwasasa tutaangalia vipengele hivyo vikuu. 1)KABLA JUA, NA NURU, NA MWEZI, NA NYOTA, HAVIJATIWA GIZA; (Mhubiri 12:1-14)
Hapo anazungumzia siku ya Bwana inayotisha, ambayo ipo mbioni kuijilia dunia nzima,.Biblia inasema tumkumbuke Bwana kabla hiyo siku haijafika, siku ambayo Jua litatiwa giza, na mwenzi hautatoa nuru yake, na nyota za mbinguni zitakapoanguka…Siku ya kutisha ya hasira ya Mungu mwenyezi.
Amosi 5: 18 “Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? NI GIZA, WALA SI NURU. 19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma. 20 Je! SIKU YA BWANA HAITAKUWA GIZA, WALA SI NURU? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga”
Amosi 5: 18 “Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? NI GIZA, WALA SI NURU.
19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
20 Je! SIKU YA BWANA HAITAKUWA GIZA, WALA SI NURU? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga”
Amosi 8: 9 “Tena itakuwa siku hiyo, asema Bwana MUNGU, nitalifanya JUA LITUE WAKATI WA ADHUHURI, NAMI NITAITIA NCHI GIZA WAKATI WA NURU YA MCHANA. 10 Nami nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo, na nyimbo zenu zote kuwa vilio; nami nitatia nguo za magunia katika viuno vyote, na upaa katika kila kichwa; nami nitayafanya haya kuwa kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, na mwisho wake kama siku ya uchungu.”
Amosi 8: 9 “Tena itakuwa siku hiyo, asema Bwana MUNGU, nitalifanya JUA LITUE WAKATI WA ADHUHURI, NAMI NITAITIA NCHI GIZA WAKATI WA NURU YA MCHANA.
10 Nami nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo, na nyimbo zenu zote kuwa vilio; nami nitatia nguo za magunia katika viuno vyote, na upaa katika kila kichwa; nami nitayafanya haya kuwa kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, na mwisho wake kama siku ya uchungu.”
Unaona sisi watu wa kizazi hichi, tunaishi karibu na siku hizo, mambo yote yanathibitisha hilo, siku yoyote mwisho unafika, kwani katika kalenda ya kibiblia tunaishi katika kanisa la mwisho linalojulikana kama Laodikia (Ufunuo 3).Na ndio kanisa hilo litakaloshuhudia mambo yote. Unyakuo pamoja na dhiki kuu. 2) KABLA YA KURUDI MAWINGU BAADA YA MVUA; (Mhubiri 12:2)
Kabla ya kurudi mawingu baada ya Mvua, inafunua “kipindi cha njaa kuanza” Kama vile Farao alivyoambiwa na Bwana itakuja miaka 7 ya neema, ya mvua tele na kisha baada ya hiyo itaanza miaka mingine 7 ya njaa, isiyokuwa na Mvua, kupanda wala kuvuna. Ndio kitu kile kile Biblia inachokizungumzia hapa, kwamba baada ya mvua mawingu yatarudi na kuanza vipindi vya njaa, Biblia inatabiri pia siku za mwisho Bwana ataleta njaa juu ya nchi, si njaa ya chakula bali njaa ya KUKOSA KUYASIKIA MANENO YA MUNGU.
Amosi 8: 11 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana. 12 Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huko na huko, kulitafuta neno la Bwana, wasilione. 13 Siku hiyo wanawali wazuri na wavulana watazimia kwa kiu”.
Amosi 8: 11 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana.
12 Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huko na huko, kulitafuta neno la Bwana, wasilione.
13 Siku hiyo wanawali wazuri na wavulana watazimia kwa kiu”.
Neno la Mungu linatuonya TUMKUMBUKE MUUMBA WETU KABLA HIZO SIKU HAZIJAFIKA, Na hizo siku zimeshaanza kujitokeza duniani…Tunaona sasa Njaa ya Neno la Mungu imeanza kuongezeka..
3) KABLA HAIJAKATIKA KAMBA YA FEDHA; (Mhubiri 12:6)
Kabla ya uchumi wako binafsi kuanguka, Unaona hapo?? usiseme siku nitakapoishiwa fedha au nitakapokuwa naumwa sana ndipo nitakapomgeukia Mungu, au siku nitakapokaribia kufa..Bwana hadhihakiwi, yeye anasema TUMKUMBUKE KABLA HIZO SIKU HAZIJAFIKA, ikiwa na maana kuwa kama tutamkataa leo kwa makusudi tukiwa katika hali nzuri, hatakuwa na sisi wakati wa matatizo. Tukimkana leo yeye wakati wa ujana wetu, na yeye atatukana sisi wakati wa matatizo yetu, kumbuka Watakaompata katika hali za matatizo ni wale tu ambao hawakuwahi kuisikia injili hapo kabla, lakini kama ulishawahi kuisikia na unaipuuzia hakutakuwa na nafasi ya pili wakati matatizo yatakapokukumba. 4) KABLA MAVUMBI KUIRUDIA NCHI KAMA YALIVYOKUWA, NAYO ROHO KUMRUDIA MUNGU ALIYEITOA. (Mhubiri 12:7)
Biblia inasema katika Waebrania 9:27 “MTU AMEANDIKIWA KUFA MARA MOJA NA BAADA YA KIFO HUKUMU”..Ndugu, hakuna maombi yoyote yanayoweza kumsaidia mtu baada ya kufa, Mafundisho ya Toharani hayapo katika biblia takatifu, ni mafundisho ya Yule mwovu, ili kuwafariji watu kuwa baada ya kufa unaweza ukaombewa na ukatolewa katika maumivu ya moto, hakuna kitu kama hicho, baada ya kifo ni hukumu ndivyo Neno linavyosema, ndio maana hapa Bwana anatuonya
“mkumbuke Muumba wako kabla roho yako haijamrudia yeye” ikiwa na maana kuwa baada ya kufa hakuna nafasi yoyote ya kumgeukia Mungu, au kuokoka na lile ziwa la Moto, kama ulimkataa yeye katika enzi za uhai wako.
Ujana wako unaweza usiwe tu ujana wa mwili wako, bali hata ujana wa akili yako, Na ujana wa akili yako ndio huu, ambao unaweza ukapata nafasi ya kusikiliza Neno la Mungu, Siku ile hutasema hukusikia, Leo hii mkumbuke Muumba wako, kabla ya siku za matatizo kufika, kabla ya vipindi vya njaa, shida, mauti, kabla ya kurudi kwa pili kwa Kristo, kabla ya Mpinga-Kristo kunyanyuka, kabla ya siku ya ghadhabu ya Mungu kumiminwa, uukumbuke msalaba, usiwe miongoni mwa hao wanaodhihaki ambao biblia inasema “Mungu amewaletea nguvu ya upotevu” wauamini uongo ili wapotee. Ujana wako unautumiaje?, nguvu zako unampa nani?.
Biblia inasema nimewaandikia ninyi vijana kwasababu mna nguvu ya kumshinda shetani, hii ikiwa na maana kuwa utafika wakati hizo nguvu hutakuwa nazo za kumpinga shetani maisha mwako kama hutakuwa ndani ya Kristo. Embu jaribu kifikiria unapata faida gani leo unavyoishi katika hayo maisha ya dhambi?. Huoni kama upo katika hatari kubwa sana. Tubu angali bado upo katika siku njema, siku za neema, siku ambazo bado hazijawa mbaya, tuipishe ghadhabu ya Mungu ambayo hivi karibuni inakwenda kumiminwa katika dunia nzima.
Ni maombi yangu kuwa Bwana atakujali kufanyika kiumbe kipya.
Ubarikiwe.
Mada Zinazoendana:
CHUKIZO LA UHARIBIFU
JE! WEWE NI MWANA WA IBRAHIMU?.
UMUHIMU WA KUZALIWA MARA YA PILI.
JIRANI YAKO NI NANI?
UMUHIMU WA KUISHI MAISHA YAMPENDEZAYO MUNGU SASA.
Upendo ni kiini cha ukristo na pia ni KILELE CHA UKRISTO. Mungu hajaufunua Upendo kama moja ya tabia zake, kwa mfano hajasema mahali popote kuwa yeye ni mwenye upendo kama anavyosema juu ya tabia zake nyingine alizonazo, mfano Mungu muweza yote, au Mungu mwenye nguvu, Mungu wa rehema, au Mungu mwenye mamlaka n.k. hapana bali anapofikia kwenye suala la Upendo anasema “MIMI NI UPENDO”, yaani yeye kama alivyo ni UPENDO na si kama moja ya tabia zake..Hivyo hulifanya hili Neno upendo katika mtazamo wa rohoni kuwa na tafsiri pana zaidi kuliko sisi tunavyoweza kulichukulia.
1Yohana 4:16 “Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. MUNGU NI UPENDO, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake”.
Upendo ule unaozungumziwa kwenye biblia sio upendo wa kusema nakupenda kimdomo na wala si upendo wa kihisia bali ni upendo UNAOTENGENEZWA ndani ya moyo wa mtu, kwasababu chanzo chake si mwanadamu bali ni Mungu. Hivyo sio wa kutokea tu ndani ya siku moja, pale mtu anapozaliwa mara ya pili. Na ndio maana ukisoma katika kitabu cha 2Petro 1:1-10, utaona kuwa Upendo unachukua hatua ya mwisho kabisa baada ya mtu kupita hatua zote sita za kuelekea ukamilifu, upendo ndio unatokea mwishoni,
2 Petro 1: 5 “Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na WEMA, na katika wema wenu MAARIFA, 6 na katika maarifa yenu KIASI, na katika kiasi chenu SABURI, na katika saburi yenu UTAUWA, 7 na katika utauwa wenu UPENDANO WA NDUGU, na katika upendano wa ndugu, UPENDO. 8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo”.
2 Petro 1: 5 “Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na WEMA, na katika wema wenu MAARIFA,
6 na katika maarifa yenu KIASI, na katika kiasi chenu SABURI, na katika saburi yenu UTAUWA,
7 na katika utauwa wenu UPENDANO WA NDUGU, na katika upendano wa ndugu, UPENDO.
8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo”.
huwezi kurukia hatua ya mwisho ukasema kuwa unao upendo wakati hatua zile 6 bado hujazikamilisha ndani yako.Maana ile hatua ya mwisho ni Mungu mwenyewe. Hivyo ili kufikia hatua hiyo ya juu kabisa kileleni Mungu alipo, mahali ambapo utakuwa karibu sana na Mungu katika roho kuliko pengine popote ni hapo utakapoufikia Upendo wa Mungu ndani yako. Na hivyo ili kufika hapo inahitaji BIDII na si vinginevyo. Hiyo haiji kwa kuombewa wala kwa kuwekewa mikono. Biblia inasema ni kwa jitihada na bidii. Kama inavyosema:
1Petro 1: 1.22 “Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi JITAHIDINI kupendana kwa moyo. Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele”. “Zaidi ya yote iweni na JUHUDI NYINGI katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.” (1Petro 4:8).
1Petro 1: 1.22 “Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi JITAHIDINI kupendana kwa moyo. Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele”.
“Zaidi ya yote iweni na JUHUDI NYINGI katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.” (1Petro 4:8).
Unaona biblia inasema pia katika:
1Yohana 4:20. “Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. NA AMRI HII TUMEPEWA NA YEYE, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake”.
Pamoja na hayo biblia inatuambia hata tukiwa na uwezo wa kuzungumza lugha za malaika hata tukiwa na imani timilifu ya kuweza kuhamisha milima, hata tukitoa mali zetu kuwapa maskini, hata tukitoa miili yetu iungue kwa moto lakini kama hatutakuwa na huo Upendo unaozungumziwa kwenye Neno la Mungu..hatuwezi kuwa kitu mbele za Mungu.
Ukiangalia hayo kwa ukaribu utaona upendo ni kitu cha utofauti na kile tunachokidhania Upendo wa Mungu ni jambo linalojengeka ndani ya mtu katika kipindi cha muda, hivyo inahitaji bidii ya kulipalilia ili liumbike, vinginevyo itakuwa ni ngumu kulifikia..Embu turudi pale kwenye 1Wakoritho 13 tuone biblia inasema nini juu ya Upendo mkamilifu..
“4 Upendo HUVUMILIA, HUFADHILI; UPENDO HAUHUSUDU; upendo HAUTAKABARI; HAUJIVUNI; 5 HAUKOSI KUWA NA ADABU; HAUTAFUTI MAMBO YAKE; HAUONI UCHUNGU; HAUHESABU MABAYA; 6 HAUFURAHII UDHALIMU, BALI HUFURAHI PAMOJA NA KWELI; 7 HUVUMILIA YOTE; HUAMINI YOTE; HUTUMAINI YOTE; HUSTAHIMILI YOTE. 8 Upendo HAUPUNGUI NENO WAKATI WO WOTE; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika”.
“4 Upendo HUVUMILIA, HUFADHILI; UPENDO HAUHUSUDU; upendo HAUTAKABARI; HAUJIVUNI;
5 HAUKOSI KUWA NA ADABU; HAUTAFUTI MAMBO YAKE; HAUONI UCHUNGU; HAUHESABU MABAYA;
6 HAUFURAHII UDHALIMU, BALI HUFURAHI PAMOJA NA KWELI;
7 HUVUMILIA YOTE; HUAMINI YOTE; HUTUMAINI YOTE; HUSTAHIMILI YOTE.
8 Upendo HAUPUNGUI NENO WAKATI WO WOTE; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika”.
Unaona unaweza kutoa mali zako zote kuwapa maskini, lakini je! uvumilivu upo ndani yako?, Tumaini lipo ndani yako? kustahimili mabaya kwa ajili ya Kristo kupo ndani yako? Adabu njema ipo ndani yako? majivuno yameondoka ndani yako?. Kuamini yote unayoambiwa na Mungu kupo ndani yako,? Unaweza ukasaidia maskini sana lakini je! Uchungu upo ndani yako? Unaweza ukawa na karama ya kunena kwa lugha na kuona maono, na kutabiri, lakini je! Unahesabu mabaya kwa ndugu yako n.k??.
Sasa hivi vyote vikiungana na kuonekana ndani ya mtu ndio Neno Upendo wa Mungu linaumbika. Lakini huwezi kusema wewe hauhusudu kama hutaonyesha bidii ya kutokufanya hivyo..kama wewe ni wa kukaa kuwazungumzia vibaya wengine, na bado ni mkristo, hata kama utakuwa una karama kubwa kiasi gani basi mbele za Mungu wewe si kitu ndivyo biblia inavyosema. Kama hutaonyesha bidii katika uvumilivu kwenye mambo yote kwanza kwa ajili ya imani yako na kwa ajili ya kudhulumiwa au kuonewa huwezi kusema upendo wa Mungu upo ndani yako.
Hivyo ni wajibu wetu sisi sote (mimi na wewe), kuonyesha bidii kuutafuta upendo kwasababu ndio kifungo cha ukamilifu, ndio kilele cha ukristo wetu. Na hii inakuja Kwa kuvitunza kwa bidii hivyo vigezo vilivyotelewa hapo juu, mpaka kufikia hatua ya vyenyewe kujengeka ndani yetu na kuwa ni TABIA yetu. Sasa tukishafikia hatua hiyo biblia inasema hapo sisi ni watu wakamilifu sana.
Wakolosai 3:14 “Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu”.
Tunapaswa tuyatawale maisha yetu kwa kanuni za Neno la Mungu, kwa bidii, kuonyesha zile tabia zinazoambatana na Upendo wake. Kila siku tukiyarekebisha maisha yetu, na kutengeneza upya pale tulipojikwaa jana, ikiwa tulishindwa kuwavumilia ndugu zetu au marafiki zetu kwa mabaya waliyotutenda na kukataa kuwasamehe, ni wakati wa kujirekebisha, kufanya bidii kusamehe, ikiwa tulikuwa tunatafuta mambo yetu wenyewe, tunapaswa tufanye bidii kubadilika, ikiwa tulikuwa hatufadhili tunapaswa pia tufanye bidii kufadhili, na kuwa na adabu ili tuonekane kuwa ni watoto wa Mungu. Na kufikia hatua ya kupendana sisi kwa sisi pasipo unafki,
1Yohana 4: 12 “Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote.
Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, NA PENDO LAKE LIMEKAMILIKA NDANI YETU”.
Hivyo sisi sote tuzidi kuonyesha bidii katika kupendana mpaka tumfikie Bwana mwenyewe ambaye ni UPENDO.Kama Bwana wetu Yesu alivyofikia.
LENGO LA SHETANI KWA WATOTO WA KIZAZI HIKI.
UKOMA NA UJANE ULIO NDANI YAKO, UMEUPATIA TIBA?
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
USIACHE KUJIFUNZA NENO LA MUNGU
KAMA UNAPENDA MAISHA, NA KUTAKA SIKU YAKO IWE NJEMA.
Yohana 19: 16 “Basi ndipo alipomtia mikononi mwao ili asulibiwe; nao wakampokea Yesu. 17 Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha. 18 Wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja naye, mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati. 19 Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI”
Yohana 19: 16 “Basi ndipo alipomtia mikononi mwao ili asulibiwe; nao wakampokea Yesu.
17 Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha.
18 Wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja naye, mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati.
19 Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI”
Bwana Yesu alisema mimi ndimi NJIA, na KWELI na UZIMA..mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi (Yohana 14:6). Litafakari hilo neno “ILA KWA NJIA YA MIMI” Kumbuka aliposema ILA KWA NJIA YA MIMI hakumaanisha kuwa wafuasi wake au washabiki wake.Hapana alimaanisha kitu kingine kabisa tofauti na hicho.
Tuchukue mfano leo hii, mwanariadha maarufu duniani, ambaye amepokea tuzo bora kuliko wote duniani…atoe sentensi aseme “mtu hawezi kuifikia tuzo niliyo nayo mimi isipokuwa kwa njia yangu mimi” je! Kwa sentensi hiyo unadhani atakuwa anamaanisha kuwa ili mtu awe kama yeye anapaswa awe mshabiki wake au mfuasi wake??…Ni wazi hamaanishi hivyo, utagundua kuwa anamaanisha kwamba mtu akitaka kuwa kama yeye, ni lazima kwanza awe mwanariadha kama yeye, na pili awe na bidii kama za kwake, ajue mbinu anazozitumia za yeye kufanikiwa..
Unaona kwahiyo NJIA ya mwanariadha sio kuwa mshabiki wake wala mfuasi wake bali ni kuwa na bidii kama ya kwake, kufanya mazoezi magumu kama aliyoyafanya yeye, kujitoa kama alivyojitoa yeye, kutokata tama kama yeye asivyokata, kukubali kupitia changamoto zote kama alizozipitia yeye pasipo kukata tamaa n.k…Kwahiyo utagundua kuwa kumbe Kupata tuzo kama aliyoipata yeye sio jambo jepesi ni zaidi na kuwa mshabiki wake au kuwa mfuasi wake.
Kadhalika na Bwana Yesu aliposema mtu haji kwa Baba ila kwa njia yake yeye…hakumaanisha tuwe wafuasi wake, au washabiki wake, kwamba tumshabikie kila mahali tueleze sifa zake na umahiri wake tu, halafu inatosha, hapana alimaanisha kuwa ili mtu afike kwa Baba kama yeye atakavyofika, hana budi kupitia njia kama alizopitia yeye, na si njia nyingine yeyote.. Ilikuwa ili aipate tuzo iliyo bora ilimpasa, kudharaulika, kutukanwa, kutemewa mate kwa ajili ya Imani, kutengwa, kuchukiwa pasipo sababu na zaidi ya yote ilimpasa siku moja ABEBE MSALABA WAKE aelekee Golgotha.
“17 AKATOKA, HALI AKIJICHUKULIA MSALABA WAKE, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha.”
Na yeye akasema mtu yeyote akitaka kumfuata na apitie njia hiyo hiyo, akubali kuchukiwa, akubali kutemewa mate, akubali kudharaulika kwa ajili ya Imani, akubali kukataliwa, akubali kuyaacha mambo ya ulimwengu hata ikiwezekana ndugu, wazazi na jamii na Mwisho wa yote na yeye pia akubali KUBEBA MSALABA WAKE kuelekea Golgotha yake kama yeye alivyofanya. Kwasababu hawezi kuwaambia watu wabebe misalaba yao na wakati yeye mwenyewe habebi.
Ni njia ngumu lakini ndio Mungu aliyoichagua, tukitaka kufika kwa Baba mbinguni hatuna budi tupitie hiyo…hakuna njia nyingine ya Mkato, ni lazima tubebe Misalaba yetu. Ndio maana Bwana Yesu alisema mara nyingi kila mahali..
Mathayo 16: 24 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, MTU YE YOTE AKITAKA KUNIFUATA, NA AJIKANE MWENYEWE, AJITWIKE MSALABA WAKE, ANIFUATE. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona”.
Na kama Mungu, alivyompa Bwana wetu Yesu Kristo nguvu ya kushinda majaribu mazito kama yale, nguvu hiyo hiyo atatupa sisi endapo tutakubali kumfuata yeye kwa mioyo yetu yote na kwa roho zetu zote. Endapo tutaikubali hii njia ya msalaba iliyodharaulika..
Bwana baada ya kudharaulika kwa ajili ya Imani, mwisho wa siku aling’aa kama jua, Biblia inasema aliidharau aibu,na hivyo Mungu akamuadhimisha mno, akamkirimi jina lile lipitalo kila jina.
Wafilipi 2: 8 “tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. 9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; 10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; 11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba”.
Wafilipi 2: 8 “tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba”.
Bwana atusaidie tusiwe WASHABIKI WAKE au WAFUASI WAKE, bali tuwe watu tunayoiendea njia yake, tukiwa ni walevi na bado tunajiita wakristo sisi bado ni washabiki, tukiwa tunaenda kanisani na bado tunasengenya sisi bado tu ni washabiki, gharama za mbio hatuzijui, ikiwa bado tunavaa nusu uchi na mavazi yasiyostahili mbele za Mungu, bado sisi ni washabiki hatutaweza kufika kwa Baba wanaofika kwa Baba ni wale wanaoiendea NJIA YA BWANA YESU KRISTO, yeye hakuwa mlevi, hakuwa mtukanaji, hakuwa mwizi, hakuwa mwabudu sanamu, hakuwa mwasherati, hakuwa mfuasi wa mambo ya ulimwengu huu. Hiyo ndiyo njia tunayowekewa tuifuate, kama Mwana wa Mungu kapitishwa kwa hiyo, unadhani sisi wengine tutatengenezewa njia nyingine mbadala ya mkato?? Hapana njia ni moja tu, na imeshawekwa na kuthibitishwa na Mungu nayo ni njia ya YESU KRISTO.
Hivyo kama hujampa Bwana Yesu Maisha yako, usikawie kufanya hivyo, nyakati hizi tunazoishi ni za hatari, muda unakaribia kusimamishwa, na umilele kuanza, Bwana asirudi leo na kukukuta upo hivyo ulivyo, asikukuta katika hali hiyo ya uvuguvugu uliyo nayo, Mkabidhi leo maisha yako kikamilifu, kwa kudhamiria kabisa kutoka moyoni mwako, Kuanza maisha mapya na UKAIFUATE NJIA YA MSALABA, na yeye mwenyewe atakuwezesha kuiendea, Na kuumaliza mwendo salama. Ili siku ile uwe na ujasiri wa kusimama mbele zake.
Wafilipi 1: 6 “..yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;
Bwana akuangazie Neema yake.
Tafadhali, Tangaza habari njema za ufalme popote pale ulipo.
UNAMCHUKULIA YESU KWAKO KAMA NANI?
MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU:
NJIA MUNGU ALIYOIWEKA KWA KILA JAMBO:
FUVU LA KICHWA