Kibiblia ni neno lenye maana ya wale funza, ambapo hutokea palipo na mzoga, au uozo. Hivyo popote ukutanapo na Neno hilo, huashiria/humaanisha, uharibifu au maiti, au kaburi,
Kwamfano ukisoma;
Ayubu 17:14 Ikiwa nimeuita uharibifu, Wewe u baba yangu; Na kuliambia buu, Wewe u mama yangu, na umbu langu;
Buu kama lilivyotumika hapo ni kaburi, Ayubu akimaanisha katika hatua aliyofikia, kaburi, na uharibifu ni kama familia yake (baba yake, mama yake na dada yake), kama tunavyojua familia ni kitu cha karibu sana na mtu, ndivyo Ayubu alivyojiona katika hali aliyokuwa amepitia.
Maana yake, kifo kilikuwa karibu na yeye zaidi hata ya familia yake.
Sehemu nyingine inasema;
Ayubu 25:6 iuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!
Mwandishi akimaanisha mwanadamu ni sawa na mzoga, (yaani mwili wenye uharibifu usio na umilele).
Neno hili utalisoma pia katika vifungu hivi;
Kutoka 16:20,24, Kumbukumbu 28:39, Ayubu 7:5.
Katika maeneo mengine kwenye biblia linatajwa moja kwa moja kama funza. (Isaya 66:24)
Hii ni hatma ya kila mwanadamu asiye na Mungu, yeye ni buu, haijalishi atakuwa na afya leo, anapesa zote ulimwenguni, anacheo kikubwa au elimu, maisha yake bila Yesu Kristo kumwokoa, ni buu tu (maiti, kaburi, )..atakufa na kuishia jehanam ya moto. Lakini akiokoka, hata ajapokufa, ataishi, siku ya ufufuo ikifika, atafufuliwa na kubadilishwa mwili wake na kupewa mwili mwingine wa utukufu, kisha Kwenda kuishi na Kristo milele na milele mbinguni.
Ikiwa haujaokoka, bado na upo tayari kufanya hivyo leo, basi basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya toba upokee msamaha wa dhambi leo >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Msikwao ni mtu gani Na nini tunajifunza katika neno hilo? (Zaburi 69:8).
Jehanamu ni nini?
Shetani anaishi wapi, Je! Amefungwa au yupo kuzimu?
Print this post
Swali: Katika Mathayo 24:27, tunaona “UMEME” ukitajwa, Je kipindi cha Bwana YESU umeme ulikuwepo?
Jibu: Turejee..
Mathayo 24:27 “Kwa maana kama vile UMEME utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu”.
Umeme unaozungumziwa hapo ni ule “MWANGA WA RADI” unaoonekana nyakati za Mvua… Kwaasili “Radi” ni “Umeme” na si Moto. Na tangu Uumbaji Radi zipo,
Ayubu 28:26 “Hapo alipoiwekea mvua amri, Na njia kwa UMEME WA RADI”.
Soma pia Ayubu 37:15, Zaburi 77:18, Zaburi 135:7, Yeremia 10:13, Yeremia 51:6, Danieli 10:6 na Nahumu 2:4 na Luka 10:18.
kwahiyo hapo maandiko yamemaanisha kuwa kama vile Radi imulikavyo kutoka mashariki hata magharibi ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu.
Na kwanini Umeme umetumika kufunua ujio wa YESU?.. Ni kwasababu ya Nguvu ya Umeme, na kasi ya Umeme.. Kikawaida Radi huwa inapiga sehemu ya juu iliyoinuka nan a inaweza kupasua mti wa Mbuyu ulio mkubwa vipande viwili chini ya dakika moja..
Na YESU KRISTO atarudi kwa nguvu hizo hizo, na kupakanyaga mahali pa juu pa dunia palipoinuka (Amosi 4:13)
Isaya 22:5 “Kwa maana siku ya kutaabika, SIKU YA KUKANYAGWA, SIKU YA FUJO INAKUJA, itokayo kwa Bwana, Bwana wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima”.
Je umempokea YESU?.. na kumfanya Bwana na Mwokozi wa maisha yako? Na kuishi maisha matakatifu ya kumpendeza yeye?.. Kama bado unasubiri nini?.. Ni heri ukayasalimisha maisha yako kwa YESU leo, kwamaana siku hizi tuishizo ni siku za hatari na dakika yoyote ule mwisho unafika.
MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.
TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!
Kwa namna gani mauti hufanya kazi ndani yetu na uzima kwa wengine? (2Wakorintho 4:12).
FUNGUO ZA UZIMA, MAUTI NA KUZIMU.
NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?
Turejee..
Yohana 13:1 “Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo”.
“Upeo” ni kiwango cha mwisho cha Jambo… Kwamfano ukitazama juu, upeo wa macho yako unaishia kuona nyota zaidi ya hapo huoni kingine.. kwahiyo tunaweza kusema upeo wa kuona kwetu angani ni nyota..
Vile vile tunapofikiri kumhusu MUNGU, (kwa namna gani hana mwanzo wala mwisho) tunafikia kikomo cha kufikiri, tunafika mwisho wa Upeo wetu wa kufikiri (hatuwezi kufikiri zaidi ya hapo na kupata majibu).. na mambo mengine yote yana upeo wake..
Sasa hapa Bwana YESU aliposema kuwa “aliwapenda watu wake Upeo”.. maana yake alitupenda kiwango cha juu kabisa cha UPENDO, ambacho baada ya hicho hakuna kingine…
Upendo wa YESU kwetu ni MKUU mno, kina cha upendo wake, urefu wa upendo wake, mapana mapana ya upendo wake na kimo cha upendo wake hakielekezeki..
Waefeso 3:18 “ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; 19 na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu”.
Waefeso 3:18 “ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina;
19 na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu”.
Mahali pengine anasema hivi..
Yohana 5:13 “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake”.
Ni rahisi mtu kuutoa uhai wake kwaajili ya mtoto wake, au mzazi wake au ndugu yake yoyote wa damu, lakini ni ngumu mtu kuutoa uhai wake kwaajili ya Rafiki.. Kwasababu marafiki hawatabiriki, leo anaweza kuwa rafiki yako kesho msaliti wako, na adui..
Mtu anaweza kutoa msaada kwa rafiki yake lakini si UHAI, na mtu kama huyo akitokea basi upendo wake ni mkubwa sana!… na hapa Bwana YESU anajitaja yeye, kwamba anautoa uhai wake kwaajili ya rafiki zake, na tena si rafiki mmoja, bali wengi, ijapokuwa anajua kuwa katikati ya marafiki wapo wanafiki na wasaliti, lakini anautoa uhai wake kwaajili yao wote.. hakika huo ni UPEO wa mwisho kabisa wa Upendo.
Biblia inasema mtu ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe..lakini YESU ametufanya sisi kuwa rafiki zake na ametupenda kuliko ndugu.
Mithali 18:24 “Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; LAKINI YUKO RAFIKI AAMBATANAYE NA MTU KULIKO NDUGU”.
Neno la Mungu linazidi kutufundisha juu ya huu UPEO WA UPENDO WA YESU, kuwa hakuna chochote kilichopo duniani, wala kilichopo mbinguni, wala mahali pengine popote kitakachoweza kutuondolea Upendo wa YESU kwetu,.. YESU mwokozi ataendelea kutupenda na hakuna mtu atakayetuchonganisha naye..
Warumi 8:33 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. 34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea. 35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? 36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. 37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. 38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Warumi 8:33 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.
37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Sasa kama tunapendwa kwa upendo mkuu namna hii kwanini na sisi TUSIPENDEKEE??…Kwanini tusiitikie vyema huu upendo kwa kumpa yeye maisha yetu, na muda wetu na mioyo yetu?..
Utajibu nini siku ile, utajiteteaje siku ile, kama leo ukiudharau upendo huu mkuu?.. Ni heri ukampokea YESU leo kama bado hujafanya hivyo, kwa kutubu na kupokea Roho Mtakatifu.
MAAJABU YA AGANO LA UPENDO WA KRISTO.
JE UMEUFIKIA ULE UTUKUFU HALISI WA MANA?
UPENDO WA KRISTO WATUBIDISHA;
JE! UMEFIKIA VIGEZO VYA KUWA BABA ROHONI?
Yohana 11:44
[44]Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
Nakusalimu Katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Nataka tujifunze jambo moja Kwa Lazaro aliyefufuliwa…
Kama tunavyojua mtu huyu alikufa, akazikwa na akaoza pia..lakini Bwana Yesu alipofika kaburini Alifanya muujiza mkubwa wa kumfufua.
Na kweli Lazaro alitoka kaburini akiwa mzima kabisa bila shida yoyote…Lakini wengi wetu tunaishia hapo, na kusema Bwana Ametenda muujiza…Lakini Yesu alipomwangalia aliona bado akatoa agizo akisema mfungueni mkamwache aende zake.. Maana yake ni kuwa ufufuo, ulimpa uzima kweli lakini sio uhuru..
Ilihitaji afunguliwe, maana kaburi lilimfunga mikono yake, miguu yake pamoja na uso wake…hata alipofufuka bado liliacha mizizi yake kwa mtu.
Ufufuo unafananishwa na wokovu, Mtu anapomwamini Yesu anakuwa tayari amefufuka kutoka katika wafu…lakini hilo peke yake halitoshi, bado Anakuwa na kamba za makaburini (maisha ya kale), hivyo anapaswa afunguliwe…
Ukiokoka haimaanishi, tabia za kale zote zitaondoka siku hiyo hiyo, unahitaji kukubali kufunguliwa, ili uwe huru kwelikweli..
Sanda, zilizomzinga Lazaro, uso wake, miguu, mikono, kama wavu wa bui-bui, hutembei, Hushiki wala huoni…ndio maisha Ya wakristo wengi baada ya kuokoka yalivyo..
Zile tabia za kale wanaendelea nazo, uchungu, wivu, hasira, uadui, maumivu, vinyongo, hofu, wasiwasi, wanashindwa kuendelea mbele kwasababu hawatoi nafasi ya kufunguliwa…
Angalia hapo Bwana Yesu anasema..”Mfungueni, mkamwache aende zake…”
Hasemi jifungue…bali mfungueni…yapo mambo huna budi kukubali kusaidiwa ili upone..
Ndio hapo Mungu akaweka…Kanisa.
Ambapo..
Utakutana na wachungaji.. kukusimamia na kukulisha mpaka utakapokomaa Na kukua vizuri kiroho…kuishi bila kanisa yaani mwenyewe mwenyewe tu, ni sawa na kutembea na sanda lako,
Kumbuka Bwana anatarajia umzalie matunda mara baada ya wokovu wako…yapo majukumu ya kufanya baada ya kuokoka..lakini ikiwa miguu na mikono na uso umefungwa unatarajia nini hapo?
Kubali kufundishika, Kubali kuchungwa, kubali mashauri na kuonywa, kubali kuombewa, kubali kuishi na ndugu (katika Bwana), kubali kusoma Neno, kuomba na wenzako utafunguliwa sana.. zaidi ya kuridhika tu na wokovu ulioupokea ukidhani utazalisha chochote katika hali hiyo hiyo ya kiroho ambayo upo peke yako peke yako.
Mara nyingine hata maono yako huwezi kuyafikia kwasababu umefungwa miguu yako. usisonge mbele.. Ogopa sanda, kama vile unavyoogopa mauti.
Ukijiona una tabia ambazo haziendani Na hali mpya ya wokovu ulioupokea basi ndio wakati wa kushughulika na sanda lako, kwa kutii na kufuata hayo maagizo. Jiwajibishe, tendea kazi wokovu Wako, kwasababu kila mtu anawajibu wa kufanya hivyo.
Hofu ya Bwana ni nini? (2Wakorintho 5:11)
Sheria ya uhuru ni ipi? (Yakobo 2:12)
Kutawa ni nini? Sawasa na Luka 1:24
WhatsApp
1Wakorintho 9:27 “BALI NAUTESA MWILI WANGU na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa”.
Kuutesa mwili kunakozungumziwa hapa si kujiumiza kwa viboko na mapigo… bali ni kuuzuia mwili kupata vitu viupendavyo, ili makusudi kutimiza mapenzi ya MUNGU.
Mfano wa vitu ambavyo vikizidi sana kufanyika katika mwili vinaathiri mbio za kiroho ni pamoja na VYAKULA NA USINGIZI vipo na vingine vingi lakini hivi ndio vikuu..
1. VYAKULA
Kula kila wakati kwa kipindi kirefu bila kuwa na vipindi vya KUFUNGA kunaathiri ukuaji wa kiroho na kuna mambo ambayo hayatatokea, kwani Biblia imesema mambo mengine hayawezekaniki isipokuwa kwa kufunga na kuomba..
Mathayo 17:19 “Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa? 20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. 21 [LAKINI NAMNA HII HAITOKI ILA KWA KUSALI NA KUFUNGA.]”
Mathayo 17:19 “Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa?
20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
21 [LAKINI NAMNA HII HAITOKI ILA KWA KUSALI NA KUFUNGA.]”
Kwahiyo Mtu mwenye desturi ya kufunga mara kwa mara na kuomba anakuwa anautesa mwili wake lakini anakuwa anapata faida kubwa rohoni
2. USINGIZI.
Mtu anayejizuia kulala kwa lengo la kuutafuta uso wa Mungu kwa Maombi, pia anahesabika kuwa anautesa mwili, na faida yake pia ni kubwa..
Marko 14:37 “Akaja akawakuta wamelala usingizi, akamwambia Petro, Je! Simoni, umelala? Hukuweza kukesha saa moja? 38 Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu”.
Marko 14:37 “Akaja akawakuta wamelala usingizi, akamwambia Petro, Je! Simoni, umelala? Hukuweza kukesha saa moja?
38 Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu”.
Na mwisho kumbuka, kujizua kufanya dhambi kama uzinzi, ulevi, sio kuutesa mwili, bali ndio kuupa mwili pumziko..kwasababu dhambi ni sumu ya mwili pia, dhambi inauharibu mwili… Mtu anapojizuia kutenda dhambi katika mwili, mwili wake hauteseki badala yake ndio unajengeka zaidi, kwahiyo usichanganye kutotenda dhambi na kuutesa mwili.
Ukiona dhambi kama Ulevi au Uzinzi au nyingine yoyote inakufanya mateka, kiasi kwamba usipoifanya mwili wako unateseka basi ni dalili ya kuwa bado utakaso kamili haujaingia maishani mwako, hivyo ni wakati wa kumgeukia Bwana kwa moyo wote kwa kutubu, kubatizwa kwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU na kisha kupokea Roho Mtakatifu,
Na ile sheria ya Roho wa uzima itakuweka huru mbali na dhambi, BUREEEEE kabisa..
Warumi 8:2 “Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti”.
Bwana atusaidie tuitese miili yetu kwa kufunga na kuzuia usingizi, ili tupate muda wa kukesha na kuomba kwa faida ya roho zetu.
Nini maana ya “Andiko huua, bali Roho huhuisha (2Wakorintho 3:6)
SI KWA UWEZA WALA KWA NGUVU BALI KWA ROHO YANGU, ASEMA BWANA.
Je kuna haja gani ya kuamini biblia iliyoandikwa na watu?
Swali: Hofu ya Bwana inayotajwa katika kitabu cha 2Wakorintho 5:11, ni hofu ya namna gani?
2Wakorintho 5:11 “Basi tukiijua HOFU YA BWANA, twawavuta wanadamu; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tumedhihirishwa katika dhamiri zenu pia”.
“Hofu ya Bwana” au “Hofu ya Mungu”.. Ni hali ya kuhofia Hukumu ya Mungu ijayo..
Tukianzia mstari wa juu kidogo katika maandiko hayo tunasoma kuwa kila mtu itampasa kusimama mbele ya kiti cha hukumu na kupokea malipo ya kazi yake.
2Wakorintho 5:9 “Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye. 10 Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya”.
2Wakorintho 5:9 “Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye.
10 Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya”.
Na mahali pengine Biblia inasema kila atatoa habari zake mwenyewe..
Warumi 14:12 “Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu”.
Hivyo hiyo hali na kutafakari mambo yajayo, kwamba tutasimama mbele ya kiti cha hukumu, inazaa hofu, na hofu hiyo ndio ijulikanayo kama “Hofu ya Bwana” au “Hofu ya Mungu”.. Na wakati mwingine hofu hii haimpeleki mtu kuogopa hukumu ijayo baada ya kifo, bali hata akiwa hai, kwasababu pia Mungu anaweza kumhukumu mtu bado akiwa hai, kwa kuruhusu madhara yampate.
Mfano wa watu katika maandiko walioonekana kuwa na Hofu ya Mungu, ni Yule mnyang’anyi aliyeangikwa msalabani pamoja na Bwana.
Luka 3:39 “Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi. 40 Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, WEWE HUMWOGOPI HATA MUNGU, nawe u katika hukumu iyo hiyo? 41 Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa. 42 Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako”.
Luka 3:39 “Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi.
40 Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, WEWE HUMWOGOPI HATA MUNGU, nawe u katika hukumu iyo hiyo?
41 Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa.
42 Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako”.
Na mfano wa Mtu/Watu katika maandiko waliotajwa kukosa Hofu ya Mungu kabisa ni wale watu wa Sodoma na Gomora na wenyeji wa nchi ya Gerari..
Mwanzo 20:10 “Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Umeona nini hata ukatenda jambo hili? 11 Ibrahimu akasema, Kwa sababu naliona, Yakini hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu”.
Mwanzo 20:10 “Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Umeona nini hata ukatenda jambo hili?
11 Ibrahimu akasema, Kwa sababu naliona, Yakini hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu”.
Na sisi ni lazima tuwe na “Hofu ya Mungu” siku zote, ili tuikwepe huku ya Mungu..kwani madhara ya kukosa hofu ya Mungu ni makubwa.. Tukiwa na hofu ya Mungu ndani yetu, tutajitenga na dhambi kwa namna yoyote ile.
Bwana atusaidie.
Nyakati za Mwisho na Tumaini la Utukufu kwa Mwamini Mpya
IFANYE KAZI YA MUNGU PASIPO HOFU!
Hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
UMEPATA UHAKIKA WA KUTOKUINGIA HUKUMUNI KATIKA SIKU ILE?
SWALI: Sheria ya uhuru ni ipi inayozungumziwa na mtume Yakobo kulingana na maandiko?
Yakobo 2:11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. 12 Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.
Neno hili pia utaliona likitajwa na mtume Yakobo katika vifungu vingine vya juu.
Yakobo 1:25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.
Katika biblia zipo sheria kuu mbili
Sheria ya dhambi na mauti ndio ile ya torati, ambayo kazi yake kubwa ni kufichua uovu, kushtaki makosa, lakini haimfanyi mtu kuwa huru, kwa mfano sheria inasema usizini, mtu atakataa kuzini, sio kwasababu hapendi uzinzi, lakini kwasababu sheria imesema tu hivyo, anaogopa adhabu atakapotenda hiyo dhambi atauawa.
Lakini sheria ya Roho wa uzima, ni sheria ya Mungu, isipokuwa hii mtu anavuviwa na Roho Mtakatifu, nguvu ya kuishi sawasawa na matwaka ya Mungu, bila shuruti Fulani, ni ya uhuru. Mfano labda sheria inasema usiue, mtu haui sio kwasababu sheria imesema, lakini kwasababu moyoni mwake hiyo nia, tamaa, au kiu ya kuua haipo, hivyo hata kama sheria isingesema hilo jambo lisingekubalika ndani yake, Hivyo mtu kama huyu tunasema ni huru na sheria, hayupo ki-sheria, sheria haimtawali ijapokuwa sheria yenyewe ipo.
Mtu akishaokoka, anakutana na sheria mpya ya Mungu, ambayo hiyo ni lazima ifuatwe na ishikwe, lakini inakuwa ya uhuru, sio tena ya kifungo, kwasababu Roho Mtakatifu anamsaidia huyo mtu kuiishi..
Ndio hiyo inayoitwa sheria ya uhuru, kwenye kitabu cha Yakobo.
Maana yake ni nini? Sisi kama waamini, Mungu anatarajia tuonyeshe matunda ya Imani yetu katika upendo, huruma, na matendo mema, kwasababu tunaye Roho.
Hivyo inapotokea, hayo hayaonekani, sheria itatuwajibisha, kutuhukumu, au vinginevyo hatukupokea sheria hiyo ya uhuru.. Ni sawa, na mtu aende kuua watu ovyo bila sababu yoyote,
Mtu huyu atahukumiwa, sawa tu na yule ambaye amesukumwa na sababu fulani, labda kisasi, hasira, wivu, chuki n.k.,
Hivyo sisi waamini, tulipokuwa huru na dhambi, hatupaswi kufikiri kuwa ndio tuna uhalali wa Kutenda dhambi. Kinyume chake, tujue kuwa ipo sheria yetu ya uhuru, itakayotuhukumu, kama tu vile wale wengine walivyohukumiwa kwa sheria ya dhambi na mauti (torati).
Ndicho alichokisema mtume Yakobo..
Kwa hitimisho ni kuwa sheria ya uhuru, ni sheria tunayoitimiza kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Ambayo hiyo pia itatuhukumu. Hivyo wewe kama mwamini, hakikisha wokovu wako unathibitika kwa kazi zake njema, chini ya upendo
Kama Bwana anawajua walio wake tangu asili kwanini tunahubiri injili? (Warumi 8:29)
Fahamu maana ya Warumi 7:25 je tunatumikia sheria ya dhambi?
Silaha za Nuru ni zipi? (Warumi 13:12)
Kitabu cha Waraka wa kwanza wa Yohana ni kitabu ambacho kilielekezwa mahususi kwa makundi matatu (3) ya watu, Watoto, vijana, na Wababa. Sasa sio Watoto au vijana au wababa kimwili, Hapana, bali alikuwa anazungumzia ngazi hizo katika roho, yaani Kundi la Watoto kiroho, vijana kiroho na wababa kiroho.
1Yohana 2:12-14
12 Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. 13 Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba. 14 Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
Na kila mmoja wao ameelezwa sifa zao, zinazowafanya wawe vile. Kwamfano Watoto kiroho, anasema ni kwasababu wamesahewa dhambi, lakini pia wamemjua Baba, tafsiri yake ni nini? Kwa mtu ambaye ni mchanga kiroho, anapokuja kwa Kristo, jambo la kwanza, ambalo atalipitia kwenye maisha yake, ni kutuliwa mizigo, mizito ambayo alikuwa anasumbuka nayo, ambayo asili yake ni dhambi. Ndio hapo ataanza kujiona mwepesi, anapokuja kwa Kristo, anajiona huru, katika kifungoni, anajiona na amani ambayo hajui chanzo chake ni nini, anajiona anapendwa,..Na ndivyo ilivyo upendo wa Mungu kwa huyu mtu unakuwa wa kipekee sana, ndio sababu kwanini anasema nimewaandikia nyinyi Watoto wadogo kwasababu mmesamehewa dhambi zenu, na mmemjua Baba. Hayo ni mambo mawili ambayo walio wa changa kiroho huyapitia.
Lakini kwa vijana, anasema nimewaandikia kwasababu mmemshinda yule mwovu. Hatua hii ya ujana ni ya kipindi cha ukuaji kiroho, hapa mara nyingi mwamini hukutana sana na majaribu ya shetani, mapingamizi makubwa, vita vya kiimani, misukosuko kwa sababu ya Kristo. Kiroho mtu kama huyu huitwa kijana, kwasababu wakati huu, ijapokuwa atasongwa lakini huwa haachi kumng’ang’ania Mungu, moto wake hauzimiki, hata kidogo, kama ni maombi, kasi huwa ni ile ile, usomaji Neno haupungui, hata akiumwa haiwi vyepesi kumwacha Mungu, kwasababu ni wakati wa Nguvu za Mungu nyingi Kutenda kazi ndani yake, na kumshinda mwovu kotekote.
Lakini Wababa kiroho, sifa yao pia ni tofauti na hao wengine, Sifa yao ni kuwa “ wamemjua yeye aliye tangu mwanzo”.
Maana yake ni nini? Kwanini hasemi kwasababu mmehubiri sana?, au kwasababu mmedumu sana ndani ya Kristo? Bali kwasababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo?
Kumfahamu Mungu, tangu mbali, ni kigezo kikuu sana cha ukomavu rohoni. Mpaka mitume kuitwa baba zetu, ni kwasababu walipewa kumwona Mungu kutokea mbali, tofauti na waandishi na makuhani..Ndio maana waraka tu huu ulipoanza anasema..
1Yohana 1:1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima;
Hili lilikuja kudhihirika pale Yesu alipoanza kuwaeleza mambo yake mwenyewe aliyoandikiwa tangu, Torati ya Musa, Zaburi na Manabii, jinsi alivyokuwepo na watu wake, jangwani, kupitia ule mwamba, Mana, nyoka wa shaba, jinsi alivyo mtokea Ibrahimu kama Melkizedeki, jinsi alivyojidhihirisha kwao kwa namna mbalimbali kupitia tumbo la Samaki kwa Yona n.k. lakini hawakumwelewa.
Luka 24:44
44 Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. 45 Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.
Sasa, mtu akishamwona Mungu kwa namna hiyo, basi Mungu kwake hawi wa “matukio” bali wa wakati wote. Yaani alikuwa nasi jana, yupo nasi leo, na atakuwa nasi hata milele.. Watoto wachanga kiroho, hawawezi kumwona Mungu jana, wenyewe Mungu wao, ni wa matukio ya leo.
Maeneo matatu ambayo macho yako yanapaswa yafunguke kuhusu, kumjua Mungu tangu mwanzo.
Hivyo ile uwe Baba, ni lazima umjue Mungu aliyekuwepo tangu Mwanzo, usiwe mtu wa matukio ya leo leo, kama mtu uliyeokoka jana, Kaa chini, tafakari sana, hatua moja baada ya nyingine ya maisha yako, anzia kwenye maandiko uone jinsi Mungu alivyokuwa na watu wake tangu zamani, ambao wengine kwa kukosa kumjua wakawa wanalalamika tu, wanaishi kiwepesi wepesi, na hatimaye kumsulubisha, lakini wale waliomjua waligeuzwa na kuwa mitume wake,
Kuwa baba rohoni.
Mungu akubariki.
Shalom.
Je umewaonea utungu watoto wako?
Kwa jina lake Ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.
LAKINI SISI HATUKUIPOKEA ROHO YA DUNIA.
SWALI:Je? ni sahihi kwa watu wa MUNGU kutumia majina ya wanyama kuwaita wengine.mfano “We kenge njoo hapa”, kama YESU alivyo tumia mbweha katika
luka 13:32.
JIBU: Katika biblia tunaona watu wakiitwa kwa majina mbalimbali ya wanyama mfano mbwa mwitu (Mathayo 7:15), kondoo(Yohana10:27), nyoka(Mathayo 13:34). Lakini pia mbweha, Njiwa, nguruwe, Simba, mbuzi.
Sasa ni vema kufahamu makusudio ya watu/jamii kuitwa hivyo yalikuwa ni nini, hayakuwa kwa lengo la kutukana, au kukejeli, au kudharau..
Hapana Bali kwa lengo la kuonyesha tabia ya mtu, jinsi ilivyo hilo tu.
Kwamfano Yesu alipomuitwa Herode Mbweha, hakuwa na kusudi la kumtukana, au kumdharau, bali alikuwa Anaeleza tabia zake zilizo mfano wa mbweha, ambaye anatabia ya kuvizia na kurarua wanyama wadogo na kuwaua. Maana hivyo ndivyo Herode alivyokuwa, jambo lililoonekana Hata kwa baba zake Kipindi Yesu anazaliwa walimwinda ili wamuue.
Sasa Ikiwa mtu atajulikana kwa namna kama hiyo, kibiblia sio tusi.
Lakini kinyume chake watu hutumia Majina ya wanyama kuwatukana Wengine, au kuwaabisha, au kuonyesha dharau kinyume chao, chuki au hasira, hayo biblia imekataza…na ni dhambi
Kusema “wewe kenge njoo hapa”..Moja kwa moja kauli hiyo inaonyesha chanzo chake ni hasira, dharau au chuki.
Waefeso 4:29
[29]Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.
Wakolosai 3:8
[8]Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.
Mathayo 5:22
[22]Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
Hivyo chunga kinywa chako. Kila Neno ulisemalo pima makusudi yaliyo nyuma yake.
VILIO VINAVYOUFIKIA MOYO WANGU.
JAWA SANA MOTO ULAO
USIWAOGOPE WAZAMZUMI
SWALI: Naomba kufahamu tunaposema Bwana Yesu asifiwe tunamaanisha nini? Na ni nani anayepaswa kuisema hiyo salamu, na kwanini wengine wanasema ‘shalom’ badala yake?
JIBU
‘Bwana Yesu asifiwe’ ni kauli inayotangaza kustahili kwa Yesu sifa kwa ile kazi njema aliyoifanya Hapa duniani.
Yesu ndiye Mtu pekee ambaye alikubali kuingia gharama ya kuacha enzi na mamlaka Mbinguni, na kuja kuishi hapa duniani kwa kusudi moja tu la kutukomboa sisi,katika dhambi zetu, akateswa na kujaribiwa sana, akafa baadaye akafufuka na hata sasa yupo hai ameketi kama mpatanishi wa sisi na Mungu,..
Kiasi kwamba kwa kupitia Yeye tunapokea msamaha wa dhambi, tunaponywa magojwa, tunamseta shetani, tunabarikiwa, tunawasiliana na Mungu moja kwa moja bila vikwazo vyovyote kwa damu yake.
Mtu Kama huyu ni lazima astahili kusifiwa..ndio maana inakuwa ni salamu ya Wakati wote BWANA YESU ASIFIWE..
Kwasababu ya nuru tuliyo ipata kwa kazi yake njema ya ukombozi.
Je ni nani anayepaswa kuisema?
Hakuna mtu anayekatazwa kuisema, lakini mtu asipojua kwanini Yesu asifiwe basi anaisema kwa unafki, Na Mungu hapendi unafiki. Kwamfano mtu ambaye hajaokoka, halafu anasema Bwana Yesu asifiwe, ni sharti ajiulize asifiwe kwa lipi wakati hakuna chochote kilichofanya na yeye katika maisha yake..
Ni sawa na mtu aliyeokoka aseme shetani asifiwe.. atasifiwa kwa jambo gani hapo wakati hakuna ushirika wowote alio nao na shetani. Lakini mganga wa kienyeji Akisema hivyo hiyo ni kweli kwasababu kuna faida amezipata Kwa shetani.
Salamu hii pia, au kauli hii, ni sahihi kutumika katika matamshi ya kiibada..mfano kwenye mahubiri, mafundisho, nyimbo, maombezi N.k. kwasababu katika Maeneo haya kazi za Yesu hudhihirishwa.
Lakini shalom Ni neno la kiyahudi linalomaanisha ‘Amani’. Ni Neno ambalo mtu yeyote anaweza kulitumia awe ameokoka au hajaokoka kwasababu ni Neno la kilugha zaidi kuliko kiimani. Ni sawasawa na sisi tunavyosema, ‘habari yako’. Mtu yeyote anaweza kutumia hilo neno. Lakini Bwana Yesu asifiwe ni Neno la kiimani ambalo anayestahili kulitamka ni mtu aliyemwamini Yesu tu.