Maisha ya mwilini mara nyingi hubeba mafundisho ya rohoni, ndio maana Bwana Yesu alitumia sana mifano ya kidunia kuwafundisha siri za ufalme wa mbinguni.
Katika jamii ili mtu aitwe profesa au daktari(kitaaluma) anapaswa awe ni msomi wa kukaa darasani kwa muda mrefu, awe na ujuzi lakini pia na uzoefu wa tafiti nyingi..yaani kwa ufupi haiwezekani ukaitwa daktari(kitaaluma) halafu usiwe msomi wa elimu za juu.
Lakini kuna udaktari ambao mtu anaweza kupewa kwa kutunikiwa, na mara nyingi huu huja pale mtu anapotoa mchango fulani mkubwa katika jamii…mtu kama huyu anaweza kutunukiwa udaktari hata kama yale mafunzo ya ndani ya kitaaluma hana.
Sasa kiroho ni vivyo hivyo unaweza pia ukawa mkufunzi, mwenye ukomavu mkubwa, zaidi ya mababa zako wa kiroho, hata zaidi ya wachungaji wako, au maaskofu wako, au wazee wako wa kiimani, kwa namna gani?
Mstari ufuatao unatupa jibu;
Zaburi 119:99-100
[99]Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo. Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.
[99]Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote,
Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo. Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.
Ukitafakari huo mistari, utaona ni mwanafunzi anayejisifia kuwa ana akili zaidi ya waalimu wake…sio kwamba ameshahitimu, hapana bado yupo chini ya waalimu wake lakini akili zake zimewapita, bado ni kijana lakini ufahamu wake umeshawazidi wazee wake.
Imewezekanikaje?
JE anasoma sana? Au ana kiwapa cha asili tofauti na wengine? Hapana…anasema kwasababu shuhuda za Mungu ndizo anazozitafakari, lakini pia anayashika mahusia ya Mungu .
Hiyo ndio siri yake, usiku na mchana ni kufikiri juu ya “KWELI”, Yaani Neno la Mungu, na na namna ya kulifanya kuwa sehemu ya maisha yake..(kujiepusha na dhambi.)
Hiyo ndio namna inayomkomaza mtu kiroho kwa haraka sana kuliko hata maarifa mengi ambayo wengi hudhani, au mafunuo mengi, au kuhubiri kwingi, au kufundisha kwingi…
Mtu mmoja anaweza akawa na uelewa mkubwa, mwalimu mzuri, mtume mwenye ushawishi mkubwa, lakini bado asimkute mwanafunzi wake ambaye maisha yake anajitahidi kuliishi Neno la Mungu.
Hivyo ndivyo Mungu anavyowatambua wakufunzi wake (kiroho), uwezo wa “kumcha Mungu” haijalishi utapoteza sifa nyingine zote za maarifa,mafunuo, lakini akiwa na hiyo huyo amefika mbali sana.
Kwasababu Biblia inasema hakuna mwisho wa usomi, (kujua maarifa), ila mtu akizingatia kumcha Mungu na kuziishika amri zake, ni zaidi ya usomi wa vitabu vyote.
Mhubiri 12:12-13
[12]Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili. [13]Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
[12]Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili.
[13]Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa;
Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
Tuwekeze nguvu zetu zote katika kuliishi Neno na neema ya Mungu itusaidie..
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
JE! UNATAKA UITWE MSOMI NA MUNGU?
USIKWEPE CHUO CHA UTAKATIFU.
HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU.
Print this post
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, karibu katika kuyatafakari maneno ya uzima
Tengeneza picha Mungu amekutokea amesimama mbele yako, wakati ukiwa na mawazo ya kumwangukia chini umsujudie, unashangaa yeye moja kwa moja anakuwa wa kwanza kuinama na kukusafisha miguu yako…
Hivi utajisikiaje? Ukweli ni kwamba hutajisikia huru hata kidogo, kwa ufupi hutakubali kitendo hicho kifanywe na yeye kutoka na ukuu wake, na heshima yake iliyozidi vyote, ni sawa na uone baba amemnunulia mtoto wake zawadi halafu yeye ndio anayekuwa wa kwanza kumshukuru mtoto, tena kwa kumwinamia..ni wazi kuwa hilo halijakaa sawa, au mtu aliyeibiwa mali zake nyingi, halafu amekutana na aliyemwibia badala ya mwenye mali kungojea kuombwa msamaha, yeye ndio anajionyesha kama ni mkosaji kwake…unaona ni jambo ambalo halina uhalisia, halikubaliki kifikra hata kidogo…
Kwa namna ya kawaida hali kama hizi akitendewa mtu hawezi kuridhia…lakini Mungu anatutendea sisi na anasema kama hutakubali kutendewa naye hivyo kamwe hutuna ushirika naye.
Ndicho kilichotokea kwa mitume na Petro. Wakati ule walipomwona Bwana Yesu, anashika kitambaa na maji kisha akaanza kuwaosha na kuwapangusa miguu yao…Petro hakuweza kuridhia akasema Bwana hutanitawadha miguu kamwe. Lakini Yesu akamwambia usipokubali huna ushirika nami.
Yohana 13:8
[8]Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.
Hii ni kufunua nini…
Ni lazima tumjue Kristo, ni kweli anasimama kwetu kama mfalme, kama Bwana, kama Mungu…tunamwabudu…lakini pia anasimama kama mtumishi wetu..Ni jambo ambalo hatuwezi kuingia akilini lakini ndivyo alivyo, amependa yeye kuwa hivyo kwetu.
Ni mfalme mwenye taji la kifalme lakini wakati huo huo pia mfalme aliyebeba kitambaa cha kuwasafisha watu miguu.
Hiyo ndio sifa ya ufalme wake. Amesimama kama muumba wetu tumwabuduye, lakini pia anatutumikia, katika kutuponya magonjwa yetu, kutulisha, kutuvisha, kutuombea, kutulinda, kutufuta machozi, na kuchukua mizigo yetu mfano wa punda na hata kufanya mambo ambayo sisi hatuwezi stahimili akitufunulia yote kwa jinsi anavyojishusha na kujishughulisha sana na mambo yetu…. Na mfano tukitataa yeye asituhudumie hivyo anasema wazi kuwa hatuna ushirika naye.
Maana yake ni fahari yake kututendea hayo, wala yeye hayahesabu kuwa ni kitu.
Anatufundisha nini?
Tuwe watumishi pia wa wengine kwa namna hiyo, kama yeye alivyo kwetu…kujitoa kwake sio kutimiza wajibu bali ni fahari yake ambayo isipokubaliwa inaharibu moja kwa moja mahusiano.
Kumsaidia mpendwa mwenzako iwe ni furaha..kujinyenyekeza kwake isiwe ni sababu za umri au cheo bali fahari..Kumwombea iwe ni fahari yako, kumsikiliza iwe ni furaha yako…hivyo ndivyo Bwana anavyotaka.. na ndivyo alivyomwambia Petro.
Yohana 13:12-17
[12]Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea? [13]Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. [14]Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. [15]Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo. [16]Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka. [17]Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda.
[12]Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea?
[13]Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.
[14]Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi.
[15]Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.
[16]Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka.
[17]Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda.
Neema ya Bwana itusaidie.
Shalom.
WEWE NI ZAO LA MAHUSIANO NA USHIRIKA.
USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU UKAE NANYI NYOTE.
WENGINE WANAKESHA KWAAJILI YAKO.
Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu
Wimbo ulio bora 2:15
15 : Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana mizabibu yetu yachanua.
Kitabu cha wimbo ulio Bora ni kitabu kinachoeleza asili ya upendo wa Kristo kwetu na jinsi tunavyopaswa kuuitikia.
Kuwa urefu wa masomo yaliyo nyuma ya kitabu hiki fungua hapa >>> NYAKATI TOFAUTI- TOFAUTI ZA UPENDO.
Lakini kwenye mstari huu, tunaona ni kama vile mtu kwa lugha ya picha anaona mbweha “ Wadogo” wamevamia shamba lake la mizabibu inayochanua na hivyo hawapuuzii kwasababu ya udogo wao, bali anatoa tamko la kukamatwa na kuondolewa…ili shamba lake linalochanua liwe salama.
Kimsingi mbweha si mnyama anayekula nyama tu, bali hula pia mizazibu, na mingine kuiharibu.
Hii ni kufunua nini katika hali zetu za rohoni..
Adui akishaona mahusiano Yetu na Kristo yanazaa matunda, huinua vitu Vidogo vidogo ili kuharibu mahusiano wakati mwingine unaweza usione kama vina madhara sana au vina nguvu sana, lakini katika eneo la kiroho kitu kidogo kina nguvu sawa na kitu kikubwa…
Hivi ndio vinavyoitwa mbweha wadogo..
Mambo Kama haya ni kama vile kuendekeza vishawishi vya dhambi kwenye maisha yako.
Kwa mfano wewe ni binti halafu kila siku unaona wanaume wanazungumza na wewe maneno ya mizaha, sasa kama usipokemea tabia hiyo, ukaona ni kawaida, tabia hizo ndogo ndogo ndizo zinazopelekea mtu baadaye kuanguka kwenye dhambi za uzinzi.
Samsoni, alipoona ushawishi wa delila unaendelea, badala aukatishe yeye akapuuzia mwisho wa siku akatekwa..
Hao ni mbweha wadogo wanaoharibu shamba lako, kila kichocheo na kishawishi kiwe kidogo kiasi gani usikipuuzie.
Wakati mwingine kuendekeza uvivu wa kiroho, yaani kupuuzia maombi, kupuuzia ibada, kidogo kidogo hupelekea kupoa kiroho, na hatimaye unajikuta kabisa umerudi duniani..mpaka unajiuliza nimefikaje hapa? Ni kwasababu uliendekeza uvivu wa kiroho..ulisema. nitaomba kesho, nikesha kesho, nitamtumikia Mungu mwezi ujao..mwishowe ukawa hivyo ulivyo leo…
Angalia ni eneo lipi la maisha yako limevamiwa na hawa mbweha wadogo, kisha chukua hatua za haraka kurekebisha.
Shalom
Mwandishi wa kitabu cha wimbo uliobora.
Nini maana ya Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, (Wimbo 2:7)
Pambaja ni nini katika Biblia kama tunavyosoma katika kitabu cha Wimbo ulio bora 1:2?
Kuba ni kitu chenye umbo la duara kinachofunika kwa juu, ni kama paa lililopinda. Lenye mwonekano unaofanana na nusu ya mpira au bakuli lililogeuzwa juu chini.
Mifano ya kuba:
unaweza kuona kwenye ujenzi wa Misikiti mingi na baadhi ya Makanisa na majengo ya kale
Tukirudi kwenye biblia Enzi za kale, ilidhaniwa kuwa dunia ina kuba kwa juu, yaani kifuniko. Ambao ndani yake jua, mwezi na nyota hutembea..
Neno hilo utalisoma katikq vifungu hivi;
Ayubu 22:14
[14]Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione;
Naye yuatembea juu ya kuba ya mbingu.
Amosi 9:6
[6]Yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi ya kuba yake juu ya nchi; yeye ndiye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA ndilo jina lake.
Kumbuka, ujumbe unaowasilishwa hapo ni kueleza ukuu uliozidi wa Mungu, katika uumbaji wake na mamlaka yake.
Nini maana ya Israeli?
Binti za Yerusalemu wanaotajwa katika kitabu cha Wimbo ulio Bora 1:5 ni akina nani?
Hiba ni nini? (Wimbo 3:10)
UNAJISIKIAJE, KUTEMBEA NA SANDA?
JIBU: Maana yake ni “yeye ashindanaye na Bwana”
Siku ile Yakobo alipotokwa na Mungu, kisha akashindana naye usiku kucha bila kumwacha, ndipo yule mtu akamuuliza jina lako nani, akasema Yakobo, akaambiwa hutaitwa tena hilo jina Yakobo, bali Israeli.
Mwanzo 32:28
[28]Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.
Au kwa namna nyingine tafsiri yake ni
“mtu anayeng’ang’ana na Mungu mpaka kuona matokeo”
Ndio jina ambalo kabila zake zote ziliitwa. Leo hii tunaposema taifa la Israeli, tunamaanisha taifa la washindanaji.
Lakini Israeli kwa agano jipya si hii ya mwilini tu.. bali ile ya rohoni ambayo imeundwa na Yesu Kristo mwenyewe..
Warumi 2:28-29
[28]Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili; [29]bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.
[28]Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;
[29]bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.
Maana yake ikiwa umempokea Kristo, wewe tayari ni mwisraeli/myahudi.
Na kama ni mwisraeli, jua asili ya jina lako..kuwa wewe ni mtu wa kung’ng’ana na Mungu…sio mtu mwepesi mwepesi…
Usimrajie Mungu katika vitu virahisi rahisi, huyo ndio sababu kwanini tunakuwa na mifungo na mikesha, kudumu uweponi mwa Bwana wakati mwingi, kumtafuta Bwana, sio kwamba yeye ni mgumu kupatikana hapana, bali kwa asili hataki wana walioitwa kwa jina hilo wawe walegevu,
Wengi hulalamika, mbona sioni uwepo wa Mungu, mbona sioni amani ya kutosha ndani, siono furaha ya wokovu, ukiwauliza vipi juhudi yako rohoni…mmoja atasema ratiba yangu huwa ni maombi ya dk 10 kwa siku, kusoma Neno dk 10.. Sasa mtu kama huyu hawezi kuhudumiwa vema na Mungu ikiwa ameokoka…
Ndugu jitambue wewe ni nani! Ikiwa ni mwisraeli, simama kama mtu shupavu kung’ang’ana na Mungu wako, nje ya hapo, tafuta jina lingine na mungu mwingine mwenye vigezo vyake vya kukuhudumia, lakini kama ni waisraeli wa Kristo, basi ni watu wa kuliitia jina la Bwana bila kukoma (Luka 18)
NINI MAANA YA UKOMBOZI?
Urujuani ni nini? (Wimbo 3:10)?
PALE MAOMBI YANAPOGEUKA KUWA MAPAMBANO.
Wimbo 3:10 “Nguzo zake alizifanyiza za fedha, Na mgongo wake wa dhahabu, Kiti chake kimepambwa urujuani, GARI LAKE LIMENAKISHIWA NJUMU, Hiba ya binti za Yerusalemu”.
Neno hili pia tunalisoma katika 1Nyakati 29:2..
1Nyakati 29:2 “Basi kwa uwezo wangu wote nimeiwekea akiba nyumba ya Mungu wangu, dhahabu kwa vitu vya dhahabu, na fedha kwa vitu vya fedha, na shaba kwa vitu vya shaba, na chuma kwa vitu vya chuma, na miti kwa vitu vya miti; vito vya shohamu, na vya kujazia, VITO VYA NJUMU, na vya rangi mbalimbali, na mawe ya thamani ya kila namna, na marimari tele.
“Njumu” ni malighafi za “kung’ara ng’ara/ kuwaka-waka” Tazama picha juu, mfano wa vazi lililonakshiwa na Njumu..
Na gari la Mfalme Sulemani kulingana na maandiko hayo ya Wimbo 3:10, lilikuwa limenakshiwa na malighafi hizo za kung’ara ng’ara, hivyo lilikuwa linavutia sana, lakini pamoja na kunakshiwa kwa vito hivo vyote vya thamani lakini bado sifa za binti Yerusalemu zilikuwa bora zaidi.
Kufahamu kwa kina Gari/Machela ya Sulemani jinsi ilivyokuwa na rangi ya Urujuani ilikuwaje fungua masomo chini ya somo hili, Bwana akubariki..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.
Machela ni nini (Wimbo ulio bora 3:7)
MAANA YA KUISHI NA MKE KWA AKILI.
MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.
WhatsApp
Swali: Katika kitabu karibia chote cha Wimbo uliobora tunaona wakitajwa sana Binti za Yerusalemu je, hawa walikuwa ni mabinti wa aina gani?..au ni wa mji wa Yerusalemu kama Biblia inavyosema hapo?
Jibu: Turejee..
Wimbo 1:5 “Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, ENYI BINTI ZA YERUSALEMU, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani.”
Sehemu nyingine Biblia inawaasa hawa Binti za Yerusalemu kutoyachochea mapenzi ..
Wimbo 2:7 “Nawasihi, enyi BINTI ZA YERUSALEMU, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe”.
Sasa swali hawa Binti za Yerusalemu ni akina nani?
“Binti za Yerusalemu” au kwa lugha nyingine “Binti Sayuni” ni lugha ya mithali inayowakilisha “Jamii nzima ya watu wa Israeli”… na si Mabinti waliopo Yerusalemu tu peke yao..la! bali jamii yote ya wana wa Israeli.
Turejee maandiko yafuatayo ili tuweze kulielewa hili vizuri…
Zekaria 9:9 “Furahi sana, EE BINTI SAYUNI; piga kelele, EE BINTI YERUSALEMU; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda.”
Unabii huu ulimuhusu Bwana YESU kipindi anaingia Yerusalemu, ambapo jamii ya watu wote walipomwona walikata majani ya mitende na kutandaza njiani ili apite..
Yohana 12:15 “Nayo siku ya pili yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu; 13 wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, HOSANA! NDIYE MBARIKIWA AJAYE KWA JINA LA BWANA, MFALME WA ISRAELI! 14 Naye Yesu alikuwa amepata mwana-punda, akampanda, kama vile iliyoandikwa, 15 Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda. 16 Mambo hayo wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba walimtendea hayo”.
Yohana 12:15 “Nayo siku ya pili yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu;
13 wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, HOSANA! NDIYE MBARIKIWA AJAYE KWA JINA LA BWANA, MFALME WA ISRAELI!
14 Naye Yesu alikuwa amepata mwana-punda, akampanda, kama vile iliyoandikwa,
15 Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda.
16 Mambo hayo wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba walimtendea hayo”.
Umeona hapo?.. waliooimba Hosana! Hosana! si tu mabinti waliokuwepo Yerusalemu bali “ni jamii yote na marika yote!”.. ikifunua kuwa Binti za Yerusalemu ni jamii nzima wa Israeli, kuzidi kulithibitisha hilo soma pia Mika 4:8, 2Wafalme 19:20-21, Isaya 37:22, na Isaya 62:1.
Na sisi kama wakristo (wakike na kiume) tunahesabika kama Israeli ya Rohoni, hivyo sisi sote pasipo kujalisha jinsia zetu, marika yetu wala nafasi zetu, maadamu tu tumempokea YESU tunafahamika kama Binti Sayuni, au Binti za Yerusalemu.
Na Biblia inatuonya Binti za Yerusalemu, mji wa Mungu tujiepushe na dhambi, hususani Uasherati wa rohoni na mwilini.
Uasherati wa rohoni ni ibada zote za sanamu.. Je umempokea BWANA YESU KRISTO?.
Fahamu kuwa hizi ni siku za Mwisho na YESU amekaribia sana kurudi.
DANIELI: Mlango wa 2
MAAJABU YA AGANO LA UPENDO WA KRISTO.
JE UMEJIFUNZA ULE WIMBO MPYA?
Tunasahau sana maisha yetu ya sirini, na kuweka nguvu kubwa, katika kuonekana kwetu kwa nje mbele za watu, hatujui kuwa Darasa kubwa la Mungu kwa mwanadamu lipo katika maisha yake ya sirini. Na Mungu humlipa mtu kwa hayo na si mengine.
Mathayo 6:4….na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Kujazi maana yake ni kulipa.
Ikiwa na maana, unayoyatenda sasa iwe ni mema au mabaya kwa siri, malipo yake utayaona baadaye kwa wazi.
Yusufu, kabla ya kuwekwa kuwa msimamizi wa mali yote ya Farao, alitumika kama wakili mwaminifu katika nyumba ya potifa, kwa muda mrefu. Baadaye Mungu akamlipa kwa kumpa Misri yote.
Yuda mpaka kuingiwa na shetani, hadi kumuuza Bwana wake, ni matokeo ya wizi aliokuwa anaufanya kwa siri kwa muda mrefu.
Daudi kabla ya kujazwa mafuta ya kumwangusha Goliathi, ni maisha ya sirini ya Imani aliyokuwa anayadhihirisha kule maporini kwa Mungu wake, mbele ya simba na dubu walipokuwa wanakuja kulishambulia Kundi. 1 Samweli 17:34-37)
Vilevile, kwa mtu yeyote yule, kupata kibali, kutumiwa na Mungu, kuinuliwa viwango vya kiroho..hutegemea sana hali zetu za sirini zinazoendelea sasa, Kwamfano utakuta labda huyu ni mwanakwaya, au mtumishi wa Mungu, lakini katika maisha yake ya sirini, anajichua, ni mzinzi, anakunywa pombe, Lakini kwa nje, anajionyesha kuwa ni mwema, anautunza ushuhuda wake, anavaa mavazi ya kujisitiri, anaongea kwa staha, ana juhudi katika utumishi, akidhani kuwa hilo ndio litamshawishi Mungu kumwongezea neema.
Ukweli ni kwamba hapo anapoteza nguvu, kwasababu tusipokuwa waaminifu katika madogo ya sirini, Bwana Yesu hawezi kutuaminisha katika makubwa.. Tabia mbaya za sirini, zinaharibu huduma zetu, utumishi wetu wa baadaye.
Mtu anataka apandishwe labda cheo kazini, lakini katika nafasi hiyo hiyo ya chini, anaiba, mwingine anataka apewe cheo lakini pale pale alipo hawajali watu walio chini yake, ni mwenye wivu, . Unategemea vipi Mungu amlipe mtu kama huyu?
Kabla hujalipwa na Mungu, unakuguliwa kwanza na Mungu.
Shughulika na maisha yako ya binafsi ya sirini, kwasababu hayo ndiyo yanayokueleza utakuwa nani mbele za watu baadaye.
Nini cha kufanya..
Mwalike Bwana, akuchunguze, sirini mwako, Mawazo yako, tabia zako, matendo yako. Kisha mwombe akuponye, na baada ya hapo anza kutendea kazi uliyoyaomba.
Simamia andiko hili;
Zaburi 139:23-24
23 Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu; 24 Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele
Mungu akubariki.
USIIHARIBU TABIA YAKO KWA MAZUNGUMZO YAKO.
NIONYESHE MARAFIKI ZAKO, NIKUAMBIE TABIA ZAKO.
HII NDIO TABIA YA WATU WA KEILA, USIIGE
Swali: Neno Hiba linamaanisha nini kwenye Biblia kwa mujibu wa andiko hili, Wimbo 3:10.
Wimbo 3:10 “Nguzo zake alizifanyiza za fedha, Na mgongo wake wa dhahabu, Kiti chake kimepambwa urujuani, Gari lake limenakishiwa njumu, HIBA ya binti za Yerusalemu”.
“Hiba” kama ilivyotumika hapo inamaanisha “Mapenzi ya Kina (yale yaliyozama kabisa)”
Kwahiyo hapo kwa Kiswahili chepesi kabisa mstari huo unaweza kusomeka hivi.. “..Gari lake limenakishiwa njumu, MAPENZI YA DHATI ya binti za Yerusalemu”
Mstari huu unaelezea Machela ya Mfalme Sulemani (yaani kiti chake kinachotumika kumbebea, anaposafiri) jinsi kilivyopambwa vizuri, na jinsi kilivyo na ufahari, lakini hayo yote si kitu zaidi ya Upendo wa dhati.
Hivyo Upendo wa dhati unaotoka kwa hadhira ya binti za Yerusalemu ni bora kuliko fedha na dhahabu, na huo unaeleza zaidi uthamani wa kitu kuliko mapambo mengine yote.
Je umempa YESU maisha yako?
Je kunena kwa Lugha mpya kukoje?
UWEZO WA KIPEKEE.
TUNALINDWA NA NGUVU ZA MUNGU.
FAIDA NYINGINE YA MAOMBI YA KUSHUKURU.
NAO WAKAMSHINDA KWA DAMU YA MWANA-KONDOO.
Ulishawahi kujiuliza, kwanini Mungu atumie namna ya “wingi”, alipomuumba mwanadamu, na sio, “umoja”, kama alivyokuwa anafanya kwenye uumbaji wa vitu vingine?
Mwanzo 1:26-28
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba
Anasema na “tumfanye” mtu kwa mfano wetu, na si “nimfanye mtu”? Ni kuonyesha hali ya asili ya anaye muumba, kwamba si wa kibinafsi, bali ya kimjumuiko..asili yake ni jumuiya. Ijapokuwa ni Mungu mwenyewe ndio aliyemuumba mwanadamu, lakini wazo lake aliwashirikisha Malaika zake, ambao walikuwepo kabla yetu sisi..Ndio maana ya hiyo “na tumfanye mtu”
Ni kufunua kuwa sisi ni zao la muunganiko, na ushirika, na ndivyo ambavyo tunaweza pia kuzaa, au kufanikiwa katika namna hiyo hiyo.. Ndio maana, hata sisi tukitaka kumleta mwanadamu mwenye asili yetu, sio jambo la mtu binafsi kujitakia pekee yake, ni lazima mwanamume, atakutana na mwanamke, kila mmoja atachangia alichonacho, na mwishowe, anatokea kiumbe kama wao. Hiyo ni kanuni..sisi kuwepo ni kazi ya “mchango” iliofanywa na watu wawili.
Hata katika maendeleo yetu, na mafanikio yetu. Jambo lolote tukitaka lifanikiwe, ni sharti tukubali michango.. Haiwezekani mtu kusimama mwenyewe mwenyewe kufanikisha kila jambo., Ukuaji wa kiroho, unahitaji kanisa, ukutanapo na watakatifu wenzako,(wawili, watatu, mia) ndipo unajengwa na kukua, tofauti na kujisukuma mwenyewe mwenyewe, hakuna mafanikio .
Vilevile na katika maendeleo ya mambo mengine yote ya mwilini na rohoni, wanaofanikiwa, ni watu wenye kuruhusu, michango, kusaidiwa, kujihusianisha, kujishusha, kujengwa, kufundishwa, kushauriwa, kuwezeshwa, na wengine..Na hatimaye kufanikiwa..Mafanikio ya moyoni yaani furaha, amani, utulivu, ni mahusiano mazuri na mema uliyonayo na wengine, katika ushirika wa Roho Mtakatifu.
Mwanadamu kamili, huishi kwa mahusiano. Kuanzia sasa usipuuzie mahusiano, Jenga mizizi yako vema, tafuta kwa bidii kuishi kwa amani na watu wote (Waebrania 12:14). Kwasababu wewe ni zao la Mahusiano, tangu mwanzo.