Msikwao ni mtu gani Na nini tunajifunza katika neno hilo? (Zaburi 69:8).

Msikwao ni mtu gani Na nini tunajifunza katika neno hilo? (Zaburi 69:8).

Jibu: Turejee..

Zaburi 69:8 “Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu”.

Msikwao ni Kiswahili cha “Mgeni aliyetoka nchi nyingine”… Mtu aliyetoka Taifa lingine na kuingia katika Taifa lisilo lake ndio anayeitwa “Msikwao”.

Hivyo katika hilo andiko, aliposema nimekuwa Msikwao kwa wana wa mama yangu, maana yake amekuwa kama mgeni asiye wa nchi ile mbele ya ndugu zake (wana wa mamaye).

Maneno hayo Daudi aliyaandika kumhusu yeye, lakini pia yalikuwa ni unabii wa maisha ya Bwana YESU KRISTO. Ukisoma Zaburi nyingi za Daudi zilikuwa ni unabii wa maisha ya BWANA YESU, Kwa mfano Zaburi ya 22 ule mstari wa kwanza unasema…

Zaburi 22:1 “Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu?”

Maneno hayo utayaona Bwana YESU anayataja alipokuwa pale msalabani (soma Mathayo 27:46).

Vile vile unabii wa Yuda kumsaliti Bwana YESU, umeandikwa katika Zaburi 41:9..

Zaburi 41:9 “Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake.”

Na Bwana YESU anakuja kunukuu maneno hayo katika Yohana 13:18…

Yohana 13:18 “Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu Ameniinulia kisigino chake”

Sasa tukirejea katika Zaburi hiyo ya 69, ilikuwa inaelezea maisha ya BWANA YESU KRISTO, kwamba kuna wakati ataonekana mbele ya ndugu zake kama mtu aliyetoka nchi ya mbali, maana yake hata ndugu zake watamkataa.. (na ndugu zake wa kwanza ni Taifa la Israeli, na wa pili ni ndugu zake wa damu).

Utauliza ni wakati gani ndugu zake walimwona kama mtu wa ajabu asiye wa kwao (msikwao)?..

Marko 3:21 “Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili”.

Soma pia Yohana 7:5.

Hivyo Zaburi hiyo ya 69 ni unabii wa maisha ya Bwana YESU asilimia zote… Na tunazidi kulithibitisha hilo katika mstari unaofuata wa 9, ambao tunaona baadaye Bwana YESU anakuja kuurejea..

Zaburi 69:8 “Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu.

9 MAANA WIVU WA NYUMBA YAKO UMENILA, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata”.

Utaona hapo aliposema “Wivu wa nyumba yako umenila”.. panakuja kujifunua katika Yohana 2:16-17.

Yohana 2:1 “Akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.

17  Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, WIVU WA NYUMBA YAKO UTANILA.”

Ni nini tunajifunza?..

Kikubwa tunachojifunza ni UNABII uliopo katika kitabu cha Zaburi, kwamba kumbe sehemu kubwa ya kitabu hiko ni unabii wa maisha ya BWANA YESU, ili kutumiza yale maneno yake aliyoyasema katika Luka 24:44. 

Luka 24:44  “Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii NA ZABURI”.

Hivyo tukisoma kitabu hiko kwa uongozo wa ROHO MTAKATIFU, Tutaona mambo mengi sana yamhusuyo YESU.

Lakini pia mambo mengi yaliyoandikwa katika kitabu hiko yanatuhusu pia sisi, kwani Kristo akiwa ndani yetu nasi tunafanana na yeye, na hivyo sehemu ya maandiko hayo pia yanatimia juu ya maisha yetu..

Maana yake ni kwamba kama KRISTO alionekana Msikwao mbele ya ndugu zake kwasababu anafanya mapenzi ya Baba wa mbinguni, hali kadhalika na sisi tutakutana na vipindi kama hivyo tukiwa katika kuyafanya mapenzi ya Mungu, hivyo endapo yakitokea hayo hatuna budi kusimama na kujitia moyo, kwasababu tayari yalishatabiriwa.

Yohana 16:32 “Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.

33  Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; LAKINI JIPENI MOYO; MIMI NIMEUSHINDA ULIMWENGU”.

BWANA YESU AKUBARIKI.

KUMBUKA KUSOMA NENO LA MUNGU KILA SIKU!!!!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KWANINI DAUDI ALIKUWA NI MTU ALIYEUPENDEZA MOYO WA MUNGU?

MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.

Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?

NENO LA MUNGU NI UFUNUO MKAMILIFU.

NGUVU YA UPENDO WA KRISTO.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments