Je Adamu na Hawa waliokoka?

Je Adamu na Hawa waliokoka?

Biblia haielezi moja kwa moja kama waliokoka, au hawakuokoka, kwasababu Neno “Kuokoka”, tunalisoma kwenye agano jipya, likimaanisha kukombolewa kutoka katika uharibifu wa hukumu ya Mungu kwasababu ya dhambi kwa kupitia kifo cha Yesu Kristo mwokozi wetu.

Lakini tunaweza kufahamu watu wa agano la kale waliokolewa, kwa kutii kwao ile ahadi ya Mungu aliyoahidi ya kumletea mkombozi duniani baadaye, yaani Yesu Kristo. Hivyo wote waliotembea katika mpango huo wa Mungu, waliokoka. Na mpango wa Mungu wote ulimuakisi Yesu Kristo.

Kwamfano ile safina aliyoijenga Nuhu ilikuwa ni Yesu Kristo, Ule mwamba walionywea wana wa Israeli jangwani ulikuwa ni Kristo, wote waliokataa kuunywea walimkataa Kristo, (1Wakorintho 10:4), Yule nyoka wa shamba alikuwa ni Kristo waliokataa kuitazama, walimkataa Kristo(Yohana 3:14), zile mbao mbili (Amri 10), zilikuwa ni Kristo waliozikataa kuzitii, walimkataa Kristo.  Yule melkizedeki aliyemtokea Ibrahimu alikuwa ni Kristo, wale malaika wawili walioshuka sodoma kuhubiri alikuwa ni Kristo ndani yao, waliowatii walimtii Kristo. Wale wanyama waliochinjwa na damu zao kunyunyizwa katika madhabahu kwa ajili ya upatanisho wa  dhambi za watu walimfunua Kristo, wote waliotii,. Walimtii Kristo ajaye.

Hivyo kila mahali walipotembea, Kristo alijidhirisha kwao kwa lugha ya maumbo na vivuli, na mifano, na maagizo, ili wamwamini yeye. Kwahiyo wote waliomtii katika nyakati zote, waliingizwa katika jopo la watu ambao Kristo atakapofunuliwa basi wataokolewa. Ndio maana baada ya Yesu kufufuka katika wafu miili mingi ya watakatifu ikatoka makaburini, wakahamishiwa peponi, rahani mwa Yesu, kwani hapo kabla watakatifu wote waliokufa walikuwa chini makaburini.

Hivyo kwa msingi huo, tutachunguza kama Adamu na Hawa walimtii Kristo au la, baada ya anguko. Biblia inatuonyesha walipojiona wapo uchi, hawakuendelea kufurahia anguko lile, bali walijificha, kuonyesha majuto ya dhambi zao, ndipo Mungu akamchinja mnyama Yule, akawavika vazi lake. Sasa Mnyama Yule alimfunua Kristo,(Mwanzo 3:21) lakini kama wangekataa basi wasingeweza kuokoka, ndio maana Yesu alisema..pia maneno haya haya kwetu sisi wa siku za mwisho, tuvikwe vazi lake, ili aibu yetu iondoke.

Ufunuo 3:18  Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na MAVAZI MEUPE UPATE KUVAA, AIBU YA UCHI WAKO ISIONEKANE, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona

Halikadhali, biblia inataja uzao wa mwanamke kwamba utauponda kichwa uzao wa nyoka. Kuashiria kuwa Hawa hakuwa mwana wa Adui (Mwanzo 3:15). Bali ni zao mbili tofauti kabisa.

Lakini pia watoto wao, mpaka sethi, tunaona walifundishwa njia ya kumtolea Bwana sadaka, na sadaka zile zilikuwa ni Kristo katika maumbo. Ni wazi kuwa wasingeweza kufanya vile kama hawakupokea au kuona kwa wazazi wao.

Na sababu nyingine ya mwisho, Kristo anatajwa kama mwana wa Adamu, hata katika vizazi vile vilivyoorodheshwa anatajwa kama “wa Adamu” (Luka 3:23-38). Asingeitwa hivyo wa Adamu  kama angekuwa ni wa ibilisi,. Mungu hawezi anza na mguu usio sahihi. Atashinda mwanzo, vilevile atashinda mwisho.

Kwa hitimisho ni kwamba Adamu na Hawa hawakupotea, bali walimwamini Kristo, baada ya anguko.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?(Opens in a new browser tab)

Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?(Opens in a new browser tab)

Nini Maana ya Adamu?

Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments