NAYE NENO ALIFANYIKA MWILI.

NAYE NENO ALIFANYIKA MWILI.

Je unaielewa vyema hii sentensi? “..Naye Neno alifanyika Mwili”.

Yohana 1:14 “Naye NENO alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli”.

Je ulishawahi kuzungumza na mtu kwa simu?.. Je anapozungumza na wewe huwa unamwona?? Au unayasikia MANENO YAKE TU?.. Ni wazi kuwa humwoni ila unasikia MANENO YAKE.

Lakini atakapokujia na kusema nawe ana kwa ana..hapo utakuwa UNAMWONA na pia UNAYASIKIA MANENO YAKE YANAYOTOKA KATIKA KINYWA CHAKE.

Hivyo tunaweza kusema kuwa wakati anaongea nawe kwenye simu yalikuwa ni Maneno tu (Pasipo yeye kumwona), lakini alipokujia na kusema nawe ana kwa ana yalikuwa ni Maneno yale yale isipokuwa yanatoka ndani ya mwili unaoonekana..KWA LUGHA NYINGINE TUNAWEZA KUSEMA NI MANENO YALIYOUVAA MWILI.

Na siri ya UUNGU wa YESU, inaanzia hivyo hivyo… Kwamba hapo Mwanzo Mungu alisema nasi kwa NENO LAKE pasipo yeye kuonekana… Lakini baadaye yeye mwenyewe akaja katika mwili na kuonekana na kusema MANENO YALE YALE kupita mwili unaoonekana…

Mtume Paulo kaielezea vizuri hiyo siri katika 1Timotheo 3:16

1Timotheo 3:16 “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. MUNGU ALIDHIHIRISHWA KATIKA MWILI, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu”.

Lakini sio tu Mtume Paulo aliyefunuliwa hiyo siri, bali pia Mtume Yohana, aliyekuwa mwanafunzi wa BWANA YESU, alifunuliwa hiyo siri ya MUNGU kudhihirika katika mwili..

Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

2  Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika…………

14 NAYE NENO ALIFANYIKA MWILI, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.”

Na huyu Neno aliyevaa mwili alikuwa si mwingine Zaidi ya BWANA YESU KRISTO, MKUU WA UZIMA!!!.

Tena Mtume huyu huyu Yohana kazidi kuliweka hili wazi katika nyaraka yake nyingine aliyoiandika kwa watu wote.. na kusema kuwa lile NENO lililokuwa linasikiwa zamani, limefanyika mwili, na wakaushika ule mwili na kuupapasapasa (yaani mwili wa BWANA YESU).

1Yohana 1:1 “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima”

Kumbe hili Neno lilianza kwa kusikiwa, baadaye likaonekana (maana yake lilivaa mwili)..na Mitume wakalipapasa (maana yake waliushika mwili wa BWANA YESU) kabla na baada ya kufufuka.

Kwahiyo KRISTO ni Neno la MUNGU na ni MUNGU pia aliyeuvaa mwili, ni Mungu pamoja nasi (Imanueli) ndio maana katukuka kuliko vitu vyote na viumbe vyote.

Je umemwamini na kumpokea maishani mwako?..kama bado fahamu kuwa hakuna njia nyingine yoyote ya kufika mbinguni isipokuwa kwa njia ya yeye. Na pia hakuna mtu wala malaika, wala kiumbe kingine chochote kitakachoweza kukupenda wewe au mimi katika viwango atupendavyo BWANA YESU.

Sasa ni heri umtumainie huyu YESU ambaye si mnafiki katika upendo, mwanadamu anaweza kukunafikia, mchungaji anaweza kukunafikia, lakini YESU, ni wa UPENDO USIO NA UNAFIKI NDANI YAKE. Yasikilize maneno yake, yakubali na yapokee.

BWANA AKUBARIKI.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?

“WOKOVU WETU U KARIBU NASI KULIKO TULIPOANZA KUAMINI”

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

Biblia imemaanisha nini iliposema “hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu”

Roho Mtakatifu ni nani?.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments