Mungu ni Mungu tu!.
Watu wengi tunadhani, tunaweza kumuudhi Mungu au kumkomoa Mungu kiasi cha kumgharimu kupoteza kitu fulani, pale tunapofanya jambo lisilompendeza..
Biblia inasema hivi..
Ayubu 35:6 Ikiwa umefanya dhambi, umefanya nini juu yake? Yakiwa makosa yako yameongezeka, wamfanyia nini yeye?
7 Ikiwa u mwenye haki, wampa kitu gani? Au yeye hupokea nini mkononi mwako?
8 Uovu wako waweza kumwumiza mtu kama wewe; Na haki yako yaweza kumfaa mwanadamu.
Unaona, Kumbe hata haki zetu, au matendo yetu mazuri, hayamwongezi Mungu kitu chochote, hayamwongezei umri wa kuishi, kwa yeye tayari ni wa milele, hayamwongezei afya, wala chochote kile kizuri kwasababu vitu vyote vinatoka kwake.
Warumi 11:36 “Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina”.
Tukisema, tujiue, hakumbadilishi yeye kuwa Mungu, tukisema hatumpendi bado hakumfanyi yeye kutokuwa Mungu, hata tukisema hayupo, ndio kabisa hakuubadilishi uungu wake. Ndege wataendelea kumsifu, jua litaendelea kuangaza majira yake, anga litaendelea kuwa la blue.
Hivyo tunachopaswa kufanya ni kujinyenyekeza mbele zake tu, haijalishi leo hii tunapitia magumu mengi kiasi gani, au mazuri mengi kiasi gani, tukiwa wanyenyekevu mbele zake, wakati wake ukifika tutauna wema aliotuwekea sisi tunaomtumainia ..Kuzielewa njia zote za Mungu hiyo haiwezekani, hata tupambane vipi, lakini tunachojua tu ni kuwa anatuwazia mawazo mazuri siku zote,
Yeremia 29:11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
Hivyo ndugu yangu unausoma ujumbe huu pengine, bado hujaokoka, wakati uliokubalika ndio sasa, usiache leo ipite bila kuyasalimisha maisha yako kwa Kristo. Ukimaanisha na kudhamiria kweli kutubu, hapo ulipo haijalishi upo sehemu gani, Kristo atayageuza maisha yako mara moja, na kukupa badiliko la ajabu ambalo litakufanya ulistaajabie maisha yako yote..
Kama upo tayari kufanya hivyo basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, . NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, kuanzia huu wakati, Kwasababu Mungu ameshaipokea toba yako . Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako sawasawa na Matendo 2:38.
Mungu ni Mungu tu!
Ubarikiwe sana.
Mada Nyinginezo:
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
CHUKIZO LA UHARIBIFU
UTENDAJI KAZI WA MPINGA-KRISTO.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
JINSI SODOMA NA GOMORA ILIVYOKUWA INAVUTIA SANA..
About the author