Tukiachilia mbali, Eneo linaloitwa Arabuni ambalo limetajwa sana katika biblia, .
Kama tunavyosoma katika vifungu vifuatavyo..
2Nyakati 9:14 “mbali na ile waliyoileta wachuuzi na wafanya biashara; tena wafalme wote wa Arabuni, na maliwali wa nchi wakamletea Sulemani dhahabu na fedha”.
Isaya 21:13 “Ufunuo juu ya Arabuni. Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala, Enyi misafara ya Wadedani”.
Yeremia 25: 13 “Ufunuo juu ya Arabuni. Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala, Enyi misafara ya Wadedani”.
Wagalatia 1:17 “wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu; bali nalikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski”.
Wagalatia 4:25 “Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto”.
Eneo ambalo walikuwa wanaishi jamii ya watu wa kiarabu.. Au kwa jina lingine linaitwa Arabia.Tazama picha juu.
Lakini Neno hili limetajwa kwa namna nyingine, katika biblia kama tunavyosoma katika vifungu vifuatavyo
2Wakorintho 1:22 “naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu”.
2Wakorintho 5:5 “Basi yeye aliyetufanya kwa ajili ya neno lilo hilo ni Mungu, aliyetupa arabuni ya Roho”.
Waefeso 1:3 “Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.
14 Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake”.
Sasa Mungu alipotugawia ahadi zake za uzima wa milele na nyinginezo, hakutaka kutupa mikono mitupu tu hivi hivi bila uthibitisho wowote, Hivyo ili kututhibitishia kuwa ahadi zake ni kweli alitupa uhakika huo kwa kutugawia Roho Mtakatifu, kama garantii au tunaweza kusema, kuponi, ya kuwa ahadi zake tutafikia, au atatutimizia.. Sasa hiyo garantii/kuponi ndio inayoitwa arabuni.
Ukipokea Roho Mtakatifu basi unayo arabuni ya uzima wa milele, kama alivyowaahidia wale waliomwamini.
Ukipokea Roho Mtakatifu basi una uhakika kuwa wewe ni mbarikiwa wa Mungu, hakuna laana yoyote inayoweza kukaa juu yako.
Ukipokea Roho Mtakatifu basi maombi yako ni hakika kuwa yanasikiwa na kujibiwa mbinguni, sawasawa na ahadi za Yesu kwa wote waliomwamini.
Lakini ukiwa huna Roho Mtakatifu, na unasema umeokoka, bado mbinguni hutaenda..Kama vile maandiko yanavyosema..
Warumi 8:9 “…Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”.
Hivyo kama na wewe unataka upate hii arabuni(garantii) ya urithi wa ahadi za Mungu zote za mwilini na rohoni,, basi ni sharti umpokee Roho Mtakatifu. Na mtu anampokea Roho Mtakatifu kwa kuzaliwa mara ya pili.
Mtu anazaliwaje mara ya pili?
Pale unapotubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, , na baada ya kutubu ukawa tayari kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, sawasawa na Mdo 2:38, hapo utakuwa tayari umeshazaliwa mara ya pili.
Na moja kuwa moja, kuanzia huo wakati na kuendelea Roho anashuka ndani yako..Na unakuwa tayari umeshapokea garantii hiyo(arabuni) ya kuwa wewe ni mwana wa ahadi… Hivyo kama hutarudi nyuma utaendelea tu kuishi katika maisha matakatifu ya wokovu ya kumpendeza Mungu na kudumu katika ushirika wa Mungu..Ni uhakika kuwa hata ukifa usiku huo huo, wewe ni wa mbinguni tu mrithi wa ahadi zote za Mungu..
Hivyo kama hujaokoka, basi anza sasa kufuata hatua hizo kwa moyo wako wote..Kama unahitaji leo kumpa Yesu maisha yako basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba.>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Na ikiwa utahitaji kubatizwa usisite kuwasiliana nasi kwa namba hizi +255789001312: Ubatizo ni bure, na unafanyika pindi tu mtu anapotubu dhambi zake..Hakuna madarasa ya kupitia, wala hakuna kutoa fedha, kwasababu biblia haitufundishi kanuni hizo..
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Yuko azuiaye sasa hata atakapoondolewa! ni nani huyo?
USIFIKIRI FIKIRI.
KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE.
https://wingulamashahidi.org/ikabodi-maana-yake-ni-nini/
AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.
UNYAKUO.
About the author