Daawa ni madai, au mashitaka, malalamiko, au hukumu.
Kwamfano pale mwenzako anapokukosea, au amekudhulumu, au amekutukana au amekufanyia jambo baya, na unataka kwenda kumshitaki , sasa hilo shitaka au madai ndio kwa jina lingine linaitwa Daawa.
1Wakorintho 6:1 “Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu?
2 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?
3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya”?
Unaona, biblia inatushauri sisi kama watakatifu tukiwa na daawa/shitaka juu ya ndugu zetu wa kikristo, hatupaswi kuyapeleka kwa watu wasioamini watusaidie kuamua, badala yake tunapaswa tuyawasilishe mbele ya kanisa, sisi kwa sisi wenyewe tuyaamue, Kwasababu Mungu mwenyewe ametupa jukumu hilo la kuhukumu mambo ya mwili kwa haki, kwasababu hata huko tutakapokwenda tutawahukumu malaika pia biblia inatuambia ..Hivyo basi, hakuna sababu ya kupelekana mahakamani, ili watu waioamini watusaidie kutoa hukumu, wakati sisi wenyewe tupo na tunayo hukumu ya haki zaidi ya wale wengine kule. Hivyo daawa zetu zote, zinapaswa ziamuliwe na kanisa.
Mistari mingine inayoeleza juu ya Neno hili, ni kama ifuatayo:
Ayubu 31:13 “Kama nimeidharau daawa ya mtumishi wangu, au ya kijakazi changu, Waliposhindana nami;
14 Basi Mungu atakapoinuka nitafanya nini? Naye atakapozuru, nitamjibuje?
15 Je! Huyo aliyenifanya mimi ndani ya tumbo, siye aliyemfanya na yeye? Si yeye mmoja aliyetufinyanga tumboni”?
Kumbukumbu 16:19 “Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza daawa ya wenye haki”.
Kumbukumbuku 17:8 “Ikiwa limezuka neno lililo zito kukupita wewe, katika maamuzi kati ya damu na damu, na kati ya daawa na daawa, na kati ya pigo na pigo, nayo yashindaniwa katika malango yako; ndipo nawe uondoke, ukwee uende mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako”;
Mengine ni hii: (2Samweli 15, Ayubu 5:8, 23:4,29:16,35:14)
Hiyo ndio tafsiri ya Neno hilo, pia angalia tafsiri ya maneno mengine chini..
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Jabari ni nini, kama linavyotumika kwenye biblia?
Areopago ni nini? Kwanini mtume Paulo walimpeleka huko?
MAMBO MENGINE HAYATOKI ISIPOKUWA KWA KUFUNGA.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 8 (Kitabu cha Ezekieli)
TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
About the author