Zamani nilipokuwa mdogo nilijaribu kufanya zoezi ambalo lilikuwa ni hatarishi kwangu. Nilidhani, kila “balbu” ilihitaji kitu kinachoitwa “Umeme”tu bila kujua ni umeme kiasi gani unahitajika ili uwake. Hivyo, siku hiyo nikachukua nyaya mbili, nikazichomeka moja kwa moja kwenye soketi, lengo langu ni zile nyaya nitakapozigusanisha sasa na balbu nione ikiwaka, nifurahie.
Lakini nilipozigusanisha tu zile waya na balbu, matokeo yalikuwa ni tofauti na nilivyotarajia. Balbu ile ilipasuka. Na kwa neema za Mungu tu vile vipande vilivyorukwa havikuniingia machoni, vinginevyo leo hii ningekuwa kipofu.
Shida ni nini? Nilidhani kilichohitajika ni umeme tu, ilimradi umeme. Na hiyo yote nikwasababu nilikurupukia kitu ambacho sijafahamu kanuni zake kwanza, Ni kwanini watu wanaitanguliza ile holder kwanza kabla ya kuiunganisha na umeme..! sikuwa na muda wa kufuatilia.
Mambo kama hayo yanaendelea leo hii rohoni, Watu wanajaribu kumfanyia Mungu ibada bila kufahamu kanuni sahihi ambazo Mungu anataka zifuatwe. Na matokeo yake ndio hapo tunaishia kuona matokeo hasi kama sio kuadhibiwa na Mungu kabisa..
Katika biblia tunaona kulikuwa na watoto wawili wa Haruni, ambao walijaribu kufanya zoezi kama hili. Wenyewe waliingia hemani pa Mungu, na kuvukiza uvumba kinyume na utaratibu wa Mungu, na Mungu akawaua saa ile ile kwa kuwashushia moto na kuwateketeza kabisa,. Biblia inatuambia kosa walilolifanya lilikuwa ni KUTUMIA MOTO WA KIGENI, kuvukiza uvumba.
Walawi 10:1 “Na Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakatwaa kila mtu chetezo chake, wakatia moto ndani yake, wakatia na uvumba, nao wakatoa moto wa kigeni mbele ya Bwana, ambao yeye hakuwaagiza.
2 Kisha moto ukatoka hapo mbele za Bwana, nao ukawala, nao wakafa mbele za Bwana.
3 Ndipo Musa akamwambia Haruni, Jambo hili ni hilo Bwana alilolinena, akisema, Nitatakaswa mimi”
Moto wa kigeni ulikuwa ni upi? Ni moto wowote ambao ulitoka nje ya madhabahu ya Mungu. Utakumbuka wakati ule makuhani walipotaka kufanya upatanisho wa makosa na dhambi za watu, walikuwa wanaagizwa wachinje wanyama, Sasa moto uliokuwa unawateketezea hao wanyama ndio ulikuwa unaitwa moto wa madhabahuni, moto huo wa makaa haukuzimwa mchana wala usiku, uliwaka daima.
Sasa huo ndio waliokuwa wanauchukua makuhani, na kwenda nao ndani ya hema, kisha wanaweka uvumba uliosagwa vizuri, juu yake na kuvukiza. Pale moshi na harufu ya uvumba ule unapopanda juu, basi Mungu alikuwa anawasemehe makosa yao, waliomkosea.
Sasa hawa wana wawili wa Haruni, wao walidharau kanuni hii ya Mungu, wakadhani kinachohitajika ni Moto ilimradi moto tu,.. Wakauacha moto wa madhabahuni,ambapo upo pale hemani daima, wakaenda chukua moto wanaoujua wao kutoka huko nje, hatujui pengine waliutolea kwenye majiko yao ya nyumbani, hatujui, wakauleta nyumbani mwa Mungu, kisha wakaweka uvumba juu yake, ili wamvukizie Mungu kwa kupitia huo. Kilichotokea ni kuuliwa badala ya kupewa rehema.
Tunapaswa tujue kuwa wakati wowote tunapomfanyia Mungu ibada ya aina yoyote ile, tujiulize je tumefuata taratibu zake? Tunapowasilisha maombi yetu kwake je, tupo ndani ya wokovu? Je na sisi ni watakatifu? Kama sio ni heri tuache tu, kwasababu maombi yanayowekwa juu ya moto wa madhabahuni ya Mungu ni yale watakatifu tu, na si ya wengine, biblia inasema hivyo katika.
Ufunuo 8:3 “Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na MAOMBI YA WATAKATIFU wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.
4 Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika”.
Unaona? Hivyo kama wewe si mtakatifu, na unasema mimi ninasali, ninashiriki meza ya Bwana, ninaimba kwaya,, ninatawadha watakatifu miguu, ninamtolea Mungu.. ujue kuwa unaweka moto mgeni madhabahuni pa Mungu. Na upo hatarini sana kupigwa kama sio kuuliwa kabisa.
Huu ni ule wakati ambao Mungu anataka waabuduo halisi, wa kumwabudu yeye katika Roho na kweli. Na sio katika uongo, kama waliofanya akina Anania na Safira wakafa.
Yohana 4:23 “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli”.
Mungu hataki ukristo feki, ndugu yangu, anasema ukitaka kuwa moto kuwa moto, au uwe baridi kabisa, kuliko kuwa vuguvugu, unasema umeokoka na bado unaendelea kuvaa vimini, na suruali, unavaa milegezo, unajichubua ngozi yako, unakunywa pombe, unazini. Hayo mambo si ya wakati wake huu, ambao Mungu anataka aabudiwe katika Roho na Kweli. Na wala usiyajaribu kwa Mungu, kwasababu unaweza ukadhani unampendeza Mungu, kumbe ndio unajitafutia mapigo kama ilivyokuwa kwa Nadabu na Abihu.
Kama hujaokoka kwa kumaanisha, basi okoka leo, Yesu aingie maishani mwako, dhamiria kabisa kuacha matendo yako maovu unayoyafanya, kisha ukabatizwe kama hukubatizwa na yeye mwenyewe atakupokea na kukusamehe, na ibada yako itaipokea na kukubariki.
Bwana atupe macho ya kuona..
Ubarikiwe.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengin
Mada Nyinginezo:
Kama tunaokolewa kwa neema kwanini wokovu tuupate kwa nguvu?
Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?
Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?
About the author