SWALI: Shalom naomba kujua nini maana ya huu mstari “Roho za manabii huwatii manabii? (1Wakorintho 14:34)
JIBU: Labda tusome kuanzia juu kidogo ili tupate picha kamili mstari huo ulikuwa unamaana gani..
1Wakorintho 14:26 “Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.
27 Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.
28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.
29 Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue.
30 Lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze.
31 Kwa maana ninyi nyote mwaweza kuhutubu mmoja mmoja, ili wote wapate kujifunza, na wote wafarijiwe.
32 NA ROHO ZA MANABII HUWATII MANABII.
33 Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu”.
Ukisoma hapo utaona kuna ustaarabu ulizuka miongoni mwa wakristo wa kanisa la Korintho. Walipokuwa kutanika kanisani, kila mtu alikuwa na neno la kusema, kila mtu alikuwa na wimbo wake spesheli wa kumwabudu Mungu, kila mtu alikuwa na ufunuo wake, kila mtu alikuwa na fundisho lake jipya la kuliwasilisha kanisani, kila mtu alikuwa na lugha na tafsiri yake mwenyewe..
Embu tengeneza picha, kila mtu kanisani anazo karama zote, wote wanataka kufundisha kwasababu wamepokea mafunuo, wote wanataka kutabiri kwasababu ni manabii, wote wanataka kufasiri lugha, wote wanataka kuwa waongozaji kwaya n.k…
Utagundua jambo kama hilo likiwepo kanisani, ni wazi kuwa hakutakuwa na kujengana tena, bali mavurugano tu, kwasababu hakuna utaratibu, hivyo hata kuielewa sauti ya Mungu itakuwa ni shida.
Kwamfano tengeneza picha umeenda kwenye shule yenye waalimu wengi, halafu kila mwalimu anataka afundishe masomo yote, hesabati, yeye, kemia yeye, baolojia yeye, na mwingine hivyo hivyo, jiulize wanafunzi wataelewaje? Hawawezi kuelewa bali watachanyikiwa, ni wapi wajifunze, au mwalimu yupi wamsikilize…
Halikadhalika na katika kanisa la wakorintho, Paulo aliwaagiza, wasiwe na utaratibu huo, hata kama imetokea watu 10 au 20 au 50 katika kanisa wamepewa ufunuo kwa wakati mmoja, hawapaswi wanene wote, bali wawape ruhusa walau wawili au watatu tu, na hao wengine wabakie kupambanua..
Na kama ikitokea hao ambao hawajapewa nafasi ya kunena na bado wanang’ang’ania tu wanene na wao, wanapaswa wakumbuke huo msemo wa Paulo kwamba “ROHO ZA MANABII HUWATII MANABII”
Maana yake ni kuwa kama wao ni manabii, wanapaswa watii utaratibu wa manabii wenzao uliowekwa. Hata kama wao hawajapewa nafasi. Kwasababu Mungu sio Mungu wa machafuko,. Na vilevile kama ikatokea mwingine aliyeketi amefunuliwa jambo kubwa zaidi, basi yule wa kwanza, anapaswa awe radhi kumpisha mwenzake, na yeye atulie, kwasababu mambo yote yanafanywa kwa lengo la kulijenga kanisa, na sio kwa lengo la mashindano, au kwa lengo la kutoa mafunuo mengi, ambayo yatafanya kanisa likose shabaha ya kujua kusudi la Mungu ni nini.
Hata sasa, utaratibu huu unapaswa uwe mwendelevu katika makanisa, sio maono yote au mafunuo yote watu waanaoonyeshwa na Mungu yanapaswa yafundishwe ndani ya kanisa kwa wakati huo huo, hapana, vinginevyo tutazama kwenye machafuko na mikanganyiko mingi, bali vichaguliwe viungo viwili au vitatu katika vyenye karama hiyo, kisha sisi wengine tubakie kupambua, na hao wengine wapewe nafasi wakati mwingine..Ili tuweze kumwelewa Mungu.
Lakini kama ikitokea mmojawetu anataka kujiona na yeye ni lazima ya kwake isemwe, akumbuke usemi ule..”Roho za Manabii, huwatii manabii”. Awe tayari kuwatanguliza wenzake kwanza, Kwasababu Mungu si Mungu wa machafuko bali wa utaratibu.
Bwana akubariki
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengin
Mada Nyinginezo:
Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; Mstari huu unamaana gani?.
SI KWA UWEZA WALA KWA NGUVU BALI KWA ROHO YANGU, ASEMA BWANA.
About the author