SWALI: Mtume Paulo alikuwa anamaanisha nini aliposema..”Wengine wanahubiri habari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitina; na wengine kwa nia njema.”(Wafilipi 1:15)? Huko kuhubiri injili kwa husuda ndio kukoje?
JIBU: Ili kuelewa Paulo alimaanisha nini ni vema tukaisoma habari yote tokea juu..
Wafilipi 1:12-18
[12]Lakini, ndugu zangu, nataka mjue ya kuwa mambo yote yametokea zaidi kwa kuieneza Injili;
[13]hata vifungo vyangu vimekuwa dhahiri katika Kristo, miongoni mwa askari, na kwa wengine wote pia.
[14]Na wengi wa hao ndugu walio katika Bwana, hali wakapata kuthibitika kwa ajili ya kufungwa kwangu, wamezidi sana kuthubutu kunena neno la Mungu pasipo hofu.
[15]Wengine wanahubiri habari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitina; na wengine kwa nia njema.
[16]Hawa wanamhubiri kwa pendo, wakijua ya kuwa nimewekwa ili niitetee Injili;
[17]bali wengine wanamhubiri Kristo kwa fitina, wala si kwa moyo mweupe, wakidhani kuongeza dhiki za kufungwa kwangu.
[18]Yadhuru nini? Lakini kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anahubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi.
Waraka huu Paulo aliuandika akiwa gerezani..Sasa akiwa huko kifungoni kulizuka makundi mawili ya watu ambao walianza kuihubiri injili kama ile ile aliyoihubiri..
Kundi la kwanza lilikuwa na Nia njema kwa Bwana kama ile aliyokuwa nayo Paulo. Kuzihurumia roho za watu na kuifanya kazi ya injili kwa kujitoa kwa upendo bila kujali kama wanapata faida yoyote au la..
Lakini kundi la pili lilikuwa la tofauti..lilianza kuhubiri kwalengo la kumkomoa Paulo na kutaka kujionyesha kuwa na wao wana mamlaka kama yake..N hiyo yote ni kwasababu ya kukua na kujulikana sana kwa huduma ya Paulo ulimwenguni..Hivyo wivu ulipowajaa wakatumia fursa ya kufungwa kwake kuhubiri injili kwa lengo la kumuonyesha Paulo hana chochote cha ziada kushinda wao.
Na wengine wakawa wanahubiri huku wakimnenea habari mbaya ili tu kumzidishia vifungo vyake kwa maaskari.
Lakini cha ajabu ni kuwa taarifa hizo zilipokewa tofauti na Paulo..badala ya kuchukia ndio kwanza akafurahia..kwasababu hata kwa njia hiyo injili inahubiriwa na watu wanaokoka..
Ni jambo gani tunaweza kujifunza kwa Paulo na hao wahubiri injili kwa fitina..
Hiyo ni kuonyesha kuwa injili inaweza kuhubiriwa na mtu yeyote na ikaleta matokeo yale yale ya wokovu..hata sasa wapo wahubiri wengi wa uongo wanawavuta watu wa Kristo..lakini hilo haliwafanyi wao kupokelewa na Kristo siku ile ya hukumu..
Bwana Yesu aliliweka wazi hilo katika;
Mathayo 7:21-23
[21]Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
[22]Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
[23]Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Hivyo tuwe makini na kuhubiri kwetu..Je Nia yetu ni kwa Bwana? au kwa lengo la kushindana na mtumishi fulani au mtume fulani au mchungaji fulani au nabii fulani…
Vivyo hivyo…Sisi kama wahubiri hatuna haja ya kurudisha mashambulizi pale tunapoona watumishi wa uongo wanashindana nasi..ikiwa injili wanayoihubiri ni ya kweli basi sisi tufurahie matunda kama alivyofanya Paulo..hayo mengine tumuchie Mungu atayahukumu mwenyewe siku ile..
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Ni kwa namna gani malaika wa mbinguni wanaweza kutuhubiria sisi injili?
Je! Watu ambao hawajawahi kusikia injili kabisa siku ya mwisho watahukumiwa?
About the author