Fitina maana yake nini kwenye biblia?

Fitina maana yake nini kwenye biblia?

Fitina ni nini?

Katika biblia Fitina maana yake ni “kufanya mageuzi au mapinduzi”. Mtu ambaye anataka kufanya mapinduzi labda ya kimamlaka, kutokana na kwamba labda hakubaliani na serikali yake, au mamlaka yake, na hivyo akakusanya watu kadhaa na kutafuta kuiangusha serikali, kwa lugha ya kibiblia mtu huyo anafanya fitina.

Katika biblia (Agano la kale) tunaona mifano ya watu kadhaa waliofanya fitina katika biblia..

  • SHALUMU:

Huyu Shalumu, alimng’oa  Mfalme Zekaria kwenye kiti chake kwa hila, na yeye akatawala mahali pake

2Wafalme 15: 10 “Na Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya fitina juu yake, akampiga mbele ya watu, akamwua, akatawala mahali pake……

15 Basi mambo yote ya Shalumu yaliyosalia, na fitina aliyoifanya, tazama, yameandikwa katika kitabu-chatarehe cha wafalme wa Israeli.”.

  • HOSHEA:

Huyu naye alimng’oa madarakani mfalme Peka wa Israeli kwa kumuua na kutawala mahali pake.

2Wafalme 15:30 “Na Hoshea mwana wa Ela akafanya fitina juu ya Peka mwana wa Remalia, akampiga, akamwua, akatawala mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.”

Na wengine wengi ambao unaweza kuwasoma katika mistari hii..(2Wafalme 17:4, 2Wafalme 21:23, 2Nyakati 13:6)

Katika agano jipya pia tunaona mifano ya baadhi ya watu waliofanya fitina.

  • BARABA:

Huyu Baraba, alipanga kunyanyuka kinyume na mamlaka iliyokuwa inatawala, akataka kufanya mapinduzi…Na pia aliua watu kadhaa katika harakati zake hizo za mapinduzi..

Luka 23: 18  “Wakapiga kelele wote pamoja, wakisema, Mwondoe huyu, utufungulie Baraba.

19  Naye ni mtu aliyetupwa gerezani kwa ajili ya FITINA iliyotokea mjini, na kwa uuaji”

Na katika kanisa la Kristo pia kuna fitina za shetani.

Fitina ndani ya kanisa la Kristo ipoje?..Ni pale mtu anapotaka KULIPINDUA NENO LA MUNGU, na kulisimamisha lake.

Warumi 16:17  “Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale WAFANYAO FITINA na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.

18  Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu”.

Asilimia kubwa ya watu WANAOLIPINDUA NENO LA MUNGU, na kulisimamisha lao, ni ili tu wapate faida Fulani, labda fedha, ndio biblia inasema hapo, watu wa namna hiyo hawamtumikii Kristo bali matumbo yao. Hawa wanaweza kuupindua Uponyaji wa Yesu uliopo katika JINA LAKE, na kulazimisha uwe katika Maji, au mafuta..lengo lao wala si kwasababu wana huruma sana, lengo lao ni ili wauze hayo maji na mafuta mengi wapate pesa, ndio maana yanawekwa kwa kiwango kidogo lakini bei kubwa.

Tumeonywa tujihadhari nao.. tusichukuliwe na fitina zao.

Hali kadhalika wapo wahubiri wanaomfitini Kristo, na kutafuta kuchukua nafasi yake, ili waabudiwe au waonekane ni miungu-watu, hawa nao pia tumeonywa tujiepushe nao.

Je umeokoka?. Kama bado unasubiri nini tubu leo na kumpokea Kristo, unyakuo upo karibu

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Nini tofauti kati ya Husuda, faraka na uchafu?

Hazama ni nini katika biblia?(Ezekieli 16:12, Kutoka 24:47)

MATUNDA 9 YA ROHO MTAKATIFU

RUDI KUMPA MUNGU UTUKUFU.

KITABU CHA UZIMA

KITABU CHA UCHAWI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments