ZUMARIDI NI MADINI GANI?

ZUMARIDI NI MADINI GANI?

Zumaridi ni aina ya madini yenye rangi ya kijani,

Madini haya kimwonekano ni mazuri sana,
Matumizi ya madini haya ni kama yale ya Marijani (Rubi) pamoja na Yakuti (Sapphire). Yote haya kazi yao ni moja ambayo ni kutengenezea vito vya thamani kama vile saa, pete na vitu vingine vya urembo.

Kimwonekani madini ya Zumaridi ni mazuri mno, na ni ya gharama kubwa, kama ilivyo Rubi na Yakuti.

Katika biblia madini haya ya Zumaridi yametajwa mara kadhaa.

Sehemu mojawapo na ya muhimu yalipotajwa ni katika kile kiti cha Enzi, ambapo ule upinde uliokizunguka Kile kiti cha Enzi, ulikuwa na mwonekano mithili ya madini hayo ya Zumaridi.

Ufunuo 4:3 “na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi”.

Mistari mingine inayozungumzia mawe hayo ni pamoja na Kutoka 28:18, Kutoka 39:11, Ezekieli 27:16, Ezekieli 28:13 na Ufunuo 21:19.

Biblia imetumia mawe haya kufunua uzuri uliopo katika Enzi yake, Enzi ya Mungu ni nzuri sana, mbinguni kuna makao mazuri sana tumeandaliwa, ni mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia. Hapo maandiko yanasema “upinde ulikizunguka mithili ya Zumaridi”..kumbe sio Zumaridi, bali mithili ya Zumaridi, maana yake ni kwamba uzuri wa mambo yaliyopo mbinguni, hauelezeki.

Biblia imetumia tu lulu na madini ya kidunia, kutusaidia angalau tulate picha, ya ni nini kilichopo kule.

Je unao uhakika wa kwenda mbinguni?.Kama hauna basi huna budi kuutafuta, kwasababu mbinguni si pa kukosa.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

YAKUTI NI MADINI GANI?

INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

Marijani ni nini katika biblia(Ayubu 28:18,Mithali 8:11)?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments