AKIKI NA YASPI NI MADINI GANI?

AKIKI NA YASPI NI MADINI GANI?

Akiki ni aina ya madini inayokaribia kufanana kimwonekano na madini ya Marijani (Rubi). Kwa lugha ya kiingereza madini ya Akiki yanajulikana kama “Sardius”. (Tazama picha juu).

Na madini ya Yaspa ni aina nyingine ya madini, ambayo rangi yange ni ya kahawia (Tazama picha chini), mawe haya kwa kiingereza ndio yanayojulikana kama “JASPER”. Kimwonekano ni mawe mazuri kama yalivyo Akiki na Marijani.

Mawe haya (Akiki na Yaspi) yametajwa katika biblia kuwakilisha Utukufu wa Mungu.

Ufunuo 4:2 “Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti;

3 na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la YASPI NA AKIKI, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi.

4 Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu”.

Mwonekano wa Mungu ulikuwa ni Mithili ya Madini haya ya Yaspi na Akiki, kumbuka hapo biblia inasema ni “Mithili” na sio Mwonekano halisi. Biblia imetumia madini yetu ya kidunia yaliyo mazuri kuuelezea utukufu wa Mungu, lakini kiuhalisia Utukufu wa Mungu ni mkuu na mzuri kuliko mawe hayo, mwonekano wake hauwezi kulinganishwa na chochote. Lakini biblia imetumia mfano wa mawe hayo kuuwakilisha utukufu wa Mungu, ili tuweze kujua kuwa kwa Mungu kuna uzuri.

Vile vile tunasoma mji ule mpya ushukao mbinguni (Yerusalemu Mpya), umepambwa kwa mawe hayo mazuri (Akiki na Yaspi).

Ufunuo 21:17 “Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika.

18 Na majenzi ya ule ukuta wake YALIKUWA YA YASPI, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.

19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa YASPI; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi;

20 wa tano sardoniki; WA SITA AKIKI; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto”.

Maandiko yanasema pia shetani kabla ya kuasi, alikuwa amepambwa na kufunikwa na haya mawe ya thamani.

Ezekieli 28:13 “Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, AKIKI, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, NA YASPI, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.”

Hivyo kwa hitimisho ni kwamba Mbinguni ni kuzuri na si pa kukosa, tukose kila kitu katika haya maisha lakini tusiikose mbingu, kwasababu maandiko yanasema mambo tuliyoandaliwa huko jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia.

Bwana atubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Kwanini madhabahu zilitengenezwa kwa mawe yasiyochongwa?

ZUMARIDI NI MADINI GANI?

KWA HIYO NDUGU, VUMILIENI, HATA KUJA KWAKE BWANA.

KUSAMBAA KWA ROHO YA MPINGA-KRISTO.

Ufisadi una maanisha nini katika biblia?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments