Dhabihu ni nini?

Dhabihu ni nini?

Dhabihu kwa jina lingine ni “kafara”, zilikuwepo sadaka za kafara na vile vile zilikuwepo zisizo za kafara.

Katika agano la kale, kafara zilizokuwa zinatolewa kwa Mungu ni kafara za wanyama, kama kondoo, mbuzi na ng’ombe.

Ambapo, mtu binafsi au Taifa zima litamsogeza huyo mnyama mbele za Bwana katika hema yake, na kuhani atamchukua huyo mnyama kama ni ng’ombe, au mbuzi au kondoo na kumchinja na kutwaa damu yake na kufanya upatanisho kwa huyo mtu au kwa Taifa, na kutwaa baadhi ya viungo na kuvichoma juu ya madhabahu.

Sasa sadaka ya namna hiyo ndiyo inayoitwa dhabihu.

Zilikuwepo sadaka nyingine ambazo hazikuwa dhabihu.

Kwamfano sadaka za unga, sadaka za mazao, sadaka za fedha, sadaka za nguo, za malimbuko n.k hizo hazikuitwa dhabihu.. Dhabihu ni sadaka ya kafara inayohusisha mnyama kuchinjwa na damu kumwagika.

Leo hii tumezoea kusema “tunaenda kumtolea Bwana dhabihu tukimaanisha sadaka zetu za fedha..lakini kiuhalisia hizo sio dhabihu tunazotoa bali ni sadaka tu!. Na zina baraka zake kubwa tu!, Lakini haziitwi dhabihu, ingawa hatutendi dhambi pia kuziita hivyo.

Sasa swali ni je! Mpaka leo hii tunapaswa tutoe sadaka za dhabihu? Yaani kafara za wanyama?

Jibu ni la! Katika agano jipya hatuna tena sadaka za dhabihu za wanyama, hatuhitaji tuchinje ng’ombe ili tupate kibali fulani au baraka fulani kutoka wa Mungu.

Kadhalika hatuhitaji damu ya kuku, au ya mbuzi, kupata ulinzi fulani wa kiMungu.

Jambo hilo liliwezekanika katika agano la kale, chini ya maagizo maalumu ya Bwana.
Lakini kwa sasa Agano jipya, hatuna hicho tena,

Sasa tunayo dhabihu moja ambayo imeshatolewa inayotufanya tusiwe na haja ya dhabihu za wanyama.

Na dhabihu hiyo Mwanakondoo Yesu Kristo, ambaye alitolewa sadaka kama kafara kwa ajili yetu, na damu yake ndio inayotupa upatanisho sisi na Mungu.

Sadaka nyingine za fedha, mazao, mavazi n.k tunaweza kuzitoa, lakini dhabihu ilishatolewa, na Mungu karidhika na hiyo, na hakuna nyingine yoyote tunaweza kumtolea ikamridhisha.

Waebrania 10:3 “Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka.

4 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

5 Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema,
Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari;

6 Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo;

7 Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu.

8 Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati),

9 ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili.

10 Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu”.

Umeona hapo?. Kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu tumepata utakaso, hivyo Kristo ndio dhabihu iliyo hai leo.
Sasa swali ni kosa leo kuchinja kafara za wanyama?

Jibu ni ndio! kama wakristo hatupaswi leo kushiriki ibada zozote za kafara!. Wengi leo wanasema ni wakristo lakini vijijini kwao wanatoa kafara!..pasipo kujua kuwa wanamtolea dhabihu shetani na si Mungu.

Bwana atujalie neema yake, tuzidi kumjua yeye zaidi na mapenzi yake.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Mahali pa juu palikuwa ni wapi kama tunavyosoma katika biblia?

Swali: Kurushwa upesi kunakozungumziwa katika Danieli 9:21 ndio kupi?

Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ya namna gani?

Sadaka ya kutikiswa ilikuwaje?

Kwanini Yesu aliwakataza mitume wake kumdhihirisha?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Crispus Nyanje
Crispus Nyanje
2 months ago

Bwana Yesu apewe Sifa, nasema Bwana Yesu awabarki kwa mafundisho haya yamejuza mambo ambayo singeliyajua. Mungu awabariki