1Wakorintho 1:26 “Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;”
Kwanini Mtume Paulo, alisisitiza kwamba tuangalie sana mwito wetu? Ni Kwasababu kwenye mwito ndipo watu wengi, tunapokosa shabaha, tukidhani Mungu anahitaji kwanza ujuzi fulani, au ukubwa fulani ndipo atuite tumtumikie, au tunadhani wale wenye vyeo vikubwa ndio hao Mungu anawatumia sana katika kazi yake.
Wito wa Mungu, ni tofauti na wito wa kibinadamu, Mungu akikuita, jambo la kwanza analolifanya kwako ni kukufagia kwanza, ikiwa wewe ni mtu mwenye ujuzi, au cheo fulani, au elimu fulani kubwa, ni anaondoa kwanza huo ujuzi wako kwake, anakufanya kuwa si kitu chochote, ndipo sasa akutumie, vinginevyo ukienda na cheo chako kwake, ukadhani hicho ndicho kitakachomshawishi yeye atembee na wewe, ujue kuwa umepotea.
Tumtazame, Musa, yeye alikuwa mrithi wa Farao, alikuwa anayo elimu kubwa ambayo hakuna asiyejua hilo , Biblia inatuambia Musa alifundishwa hekima yote ya ki-Misri na alikuwa pia ni mjuzi wa kipekee sana katika kuongea.
Warumi 7:22 “Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo”.
Na kumbuka kwa wakati ule taifa kama Misri ni sawa na Marekani ya leo, ni taifa lililokuwa linashikilia uchumi wa ulimwengu mzima.
Lakini tunaona Mungu alipoanza kumvuta kwake, alikimbilia kule jangwani, na huko akawa anachunga mifugo ya mkwe wake Yethro, kwa muda mrefu sana wa miaka 40, wakati wote huo, Mungu hakujionyesha kwake, wala kujidhihirisha, unaweza ukajiuliza ni kwanini ichukue muda wote huo? hiyo yote ni Mungu alikuwa anamwondolea kwanza ule utashi wake aliokuwa anajiona anao, ule ujuzi wake, ambao hapo mwanzo alidhani pengine ndio angeutumia huo kuwaokoa wana wa Israeli, lakini ikawa ni kinyume na matazamio yake, aliendelea kukaa katika hali hiyo hiyo kwa muda wa miaka 40 mizima.
Na wakati ambapo hata ule ujuzi wake wa kuzungumza umekufa, hapo ndipo Mungu alipomwita, na ndio maana utaona alipoitwa na Mungu jambo la kwanza alimwambia kuwa yeye sio Mnenaji, yaani hana uwezo tena kwa kuzungumza siasa majukwaani, kama alivyokuwa nao kule mwanzoni,
Kutoka 4:10 “Musa akamwambia Bwana Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito. 11 Bwana akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, Bwana”?
Kutoka 4:10 “Musa akamwambia Bwana Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito.
11 Bwana akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, Bwana”?
Unaona? Musa huyu huyu, biblia inatuambia alikuja kuwa MPOLE kuliko watu wote waliokuwa duniani wakati ule. Kutoka kuwa muuaji, mpaka kuwa mtu mpole sana zaidi ya watu wote, si jambo jepesi inahitaji kujishusha kwa Mungu kweli kweli.
Hesabu 12:3 “Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.”
Mtu kama huyo ndio Mungu alitembea naye. Na kanuni za Mungu huwa hazibadiliki, akisema hivi, ndivyo ilivyo, hata sasa, Mungu hatembei na watu wanaojiona kuwa ni bora kuliko wengine, hawatumii watu wanaojiona wana elimu kubwa au washupavu kuliko wenzao, hawatumii kamwe watu wanaojiona ni vigogo kuliko wenzao, Na kama akitaka kukutumia basi jiandae kufanywa kama Musa,. Jiandae kushushwa kwanza. Vinginevyo sahau kutumiwa na Mungu.
Na ndio maana ukiendelea pale utaona anasema..
1Wakorintho 1:26 “Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; 27 bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; 28 tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; 29 mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu”.
1Wakorintho 1:26 “Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;
27 bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;
28 tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;
29 mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu”.
Ndivyo ilivyo watu wasiokuwa na utashi wowote ni rahisi sana wao kutumiwa na Mungu kuliko watu wenye vyeo au wenye elimu kubwa za kidunia, kwasababu hao hawana cha kujisifia mbele za Mungu. Na watu wa namna hii ndio Mungu anaowafunulia siri zake nyingi.
Luka 10:21 “Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza”.
Halikadhalika, watu wasio na elimu kubwa za theolojia ndio wanaokuwa katika nafasi kubwa ya kutumiwa na Mungu kuliko hao wengine, kwasababu hawa hawana cha kutegemea isipokuwa uongozo wa Roho Mtakatifu, lakini hao wengine watategemea elimu zao za dini ndio ziwasapoti, au ziwalinde, au ziwape heshima.
Vivyo hivyo na sisi pia tunapaswa tuutafakari sana mwito wetu, tujiulize je Mungu tumempa nafasi ya ngapi katika maisha yetu, Je! Ni kweli tumeshusha viburi vyetu na kuvua ujuzi wetu, ili kumruhusu yeye atutumie? Au tumejikweza kwake na kujiona sisi ni wa kipekee sana kisa tuna elimu, au tuna vyeo, au tuna heshima kuliko wengine.
Tuutafakari mwito wetu, ili tujue ni wapi Mungu anataka tutembee naye, na tuanze kujishusha kuanzia sasa.. Kwasababu kiburi ni adui mkubwa wa utumishi wa Mungu. Tukitaka tutumiwe na Mungu tushushe kwanza viburi vyeo, na kujiona sisi ni sawa na watu wengine wote.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo:
IMESALIA RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU.
TAFAKARI SANA KABLA YA KUAMUA HATIMA YAKO.
KUMTUMIKIA MUNGU, KUNAWEZA KUWE KINYUME NA MATARIJIO YAKO.
JE! JICHO LAKO LINAONA NINI KATIKATI YA MAJARIBU?
Je ni sahihi kuweka walinzi kulinda mali zetu?
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Je ni sahihi kwa sisi tuliookoka na tunaomtegemea Mungu kuweka walinzi kulinda mali zetu au mali za kanisa?. Kwasababu Biblia inasema Bwana asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure (Zab.127:1).
JIBU: Si dhambi kuweka walinzi au kuweka ulinzi katika mali zako, tena ni jambo la busara zaidi na la hekima. Unapokuwa na biashara yako au kazi yako ambayo ni halali inayompendeza Mungu, na ndani yake una mali nyingi, basi ni hekima kuweka ulinzi na pia kuifunga na kuhakikisha haitachukuliwa au kuibiwa kirahisi. Sio dhambi kabisa kufanya hivyo.
Kitu pekee ambacho si sawa na hakimpendezi Mungu, ni sisi kutegemea hao walinzi kama ndio msaada wetu na tegemeo letu la mwisho. Hapo ndipo linapokuja hilo neno..
Zaburi 127:1 “Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure”.
Kinyume chake ni kweli, Bwana akiijenga nyumba wajengao hawafanyi kazi bure, kadhalika Bwana akiulinda mji wakeshao hawakeshi bure. Vile vile Bwana akiwa upande wetu kwa chochote tukifanyacho, hicho tunachokifanya hakitakuwa bure.
Ipo mifano kadha wa kadha katika biblia ya kujifunza, lakini itoshe tu leo kujifunza juu ya Nehemia, mtumishi wa Mungu. Wakati alipopata maono ya kwenda kuukarabati mji mtakatifu Yerusalemu, alikutana na vizuizi vingi, vya watu kuyapinga hayo maono..Hivyo ikampelekea kuingia katika hatari kubwa hata kufikia kupoteza maisha yake, lakini yeye alikuwa anamcha Mungu, na kumtegemea..na alimtegemea kwa kila kitu, lakini ulipofika wakati wa kuijenga nyumba ile hakuwa na budi ya kumwomba Mungu na pia kuweka walinzi huku anaifanya kazi ile… Lengo ni ili wasirudishwe nyuma na maadui zao..
Nehemia 4:7 “Lakini ikawa, Sanbalati, na Tobia, na Waarabu, na Waamoni, na Waashdodi, waliposikia ya kuwa kazi ya kuzitengeneza kuta za Yerusalemu inaendelea, na ya kuwa mahali palipobomoka panaanza kuzibwa, basi wakaghadhibika mno; 8 wakafanya shauri wote pamoja kuja kupigana na Yerusalemu, na kufanya machafuko humo. 9 BALI SISI TULIMWOMBA DUA MUNGU WETU, TENA TUKAWEKA WALINZI, MCHANA NA USIKU, KWA SABABU YAO, ILI KUWAPINGA”.
Nehemia 4:7 “Lakini ikawa, Sanbalati, na Tobia, na Waarabu, na Waamoni, na Waashdodi, waliposikia ya kuwa kazi ya kuzitengeneza kuta za Yerusalemu inaendelea, na ya kuwa mahali palipobomoka panaanza kuzibwa, basi wakaghadhibika mno;
8 wakafanya shauri wote pamoja kuja kupigana na Yerusalemu, na kufanya machafuko humo.
9 BALI SISI TULIMWOMBA DUA MUNGU WETU, TENA TUKAWEKA WALINZI, MCHANA NA USIKU, KWA SABABU YAO, ILI KUWAPINGA”.
Umeona, waliomba dua na pia wakaweka walinzi, lakini pamoja na kuweka walinzi, tumaini lao lote halikuwa kwa hao walinzi, bali walimtumainia Mungu, hivyo hawakukesha bure katika kuujenga huo mji na kuulinda, ndio maana mpaka leo kipande hicho cha ukuta kulichojengwa na Nehemia kipo Israeli, pale Yerusalemu maelfu ya miaka imepita bado sehemu ya ukuta ipo mpaka leo. (Tazama picha juu).
Hao waliweka walinzi na kukesha kuulinda na kuujenga mji, na mpaka leo sehemu ya ukuta ipo, kazi yao haikuwa bure..Lakini kama wangeweka walinzi na kuujenga huku wakizitumainia nguvu zao, hapo lingetimia hilo neno.. “Bwana asipoulinda mji yeye aulindaye afanya kazi bure”..Ni wazi kuwa wangeshambuliwa na maadui zao na huo mji wanaoujenga wasingemaliza.
Kwahiyo tunajifunza, tuwapo na kitu chochote ambacho Mungu katubariki kwa hicho, basi hatuna budi kukitunza na kukilinda kwa kadiri tuwezavyo, Sio hekima wala akili kuacha milango wazi ya nyumba yako usiku, au kuacha wazi mlango wa sehemu ya biashara yako mpaka asubuhi ukiamini kuwa hakuna atakayeingia na kuzichukua mali zako. Nakuambia ukweli ukija asubuhi hutakuta chochote, kwasababu unamjaribu Mungu.
Itokee bahati mbaya umesahau kufunga mlango wa maingilio ya sehemu za mali zako, hapo Bwana ataingilia kati kuzilinda mali hizo utazikuta salama kimiujiza miujiza tu, haijalishi zipo mazingira gani… lakini kamwe usimjaribu Mungu kwa kuacha kukilinda kile ulicho nacho, huku ukisema Mungu atazilinda tu..hapo utakuwa unamjaribu Mungu na unatenda dhambi..
Na sio vitu vya mwilini tu ambavyo tunajukumu la kuvilinda, bali hata vitu vya rohoni, ambavyo ndio vya muhimu zaidi. Na cha kwanza kabisa cha kukilinda ni WOKOVU mtu alioupata..
Biblia inasema..
Ufunuo 3:11 “Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako”.
Na pia inasema..
Mithali 4:23 “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. 24 Kinywa cha ukaidi ukitenge nawe, Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe. 25 Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa”
Mithali 4:23 “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
24 Kinywa cha ukaidi ukitenge nawe, Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.
25 Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa”
Umeona?..baada ya kumpokea Yesu sio wakati wa kujilegeza na kusema nipo salama!..bali ndio wakati wa kukilinda kile ulichokipokea..kwasababu WIZI wa rohoni upo!!…shetani anatafuta kwa hali na mali kuiba vile vya rohoni tulivyopewa na Mungu.
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba ulinzi wa vitu vya rohoni na mwilini unapaswa uwe tabia ya kila mkristo, kama vile ilivyo tabia ya Mungu kutulinda sisi, yeye ijapokuwa ametupa tayari wokovu lakini bado anawatuma malaika wake kutuzunguka kutulinda pande zote usiku na mchana, hivyo na sisi hatuna budi kulinda vile tulivyopewa.
Bwana atubariki.
Kama hujampokea Yesu, nakushauri ufanye hivyo leo, hizi ni siku za Mwisho, na parapanda inakaribia kulia na Kristo kuchukua watu wake, kwenda nao mawinguni, Je! Utakuwa wapi siku hiyo?
MTEGO HUTEGWA BURE, MBELE YA MACHO YA NDEGE YE YOTE.
Swali: Je Ni sahihi kwa Mkristo kupeleka kesi mahakamani?
Je! Ni sahihi kutumia maji ya upako,katika kufanya maombezi?
Je ni sahihi kumtenga mtu anapofanya dhambi kanisani?
Je! Ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu uliyemzidi umri?
Bwana YESU asifiwe sana, karibu tujifunze Neno la Mungu.
Awali ya yote ni vizuri tukaweka msingi kwanza wa kufahamu nini maana ya Sabato.
Sabato maana yake ni pumziko/kuacha kufanya kazi/ kustarehe/kuingia rahani mwako. Mungu alifanya kazi yake ya kuumba kwa muda wa siku sita mfululuzo kama tunavyosoma katika kitabu cha Mwanzo, na ilipofika siku ya saba kazi yote ilikuwa imeshamalizika, ndipo akastarehe/ akapumzika, hivyo akaibariki siku hiyo na kuifanya kuwa kama kumbukumbu la pumziko lake, na baadaye akawaagiza wana wa Israeli walipokuwa kule jangwani kwamba kila itakapofika siku hiyo waifanye kuwa ni sabato yao.
Lakini Sabato haikuwa ile siku yenyewe ya saba, bali sabato ilikuwa ni lile pumziko lenyewe, Lakini “SABA” yenyewe inawakilisha pumziko la Mungu, kwasababu katika saba ndipo Mungu aliingia katika pumziko lake. Na ndio maana ukisoma kwenye biblia, Mungu hakuiwekea sabato yake mipaka kwamba iwe tu ni katika siku ya saba ,hapana.. Bali utaona alikwenda mpaka kwenye mwaka wa Saba, ilikuwa kila mwaka wa saba, hakuna kupanda, wala kwenda kufanya kazi yoyote mashambani, bali waipumzishe ardhi, watulie majumbani kwao. Utalisoma hilo katika..
Walawi 25:1 “Kisha Bwana akanena na Musa katika mlima wa Sinai, na kumwambia, 2 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika nchi niwapayo, ndipo hiyo nchi itashika Sabato kwa ajili ya Bwana. 3 Panda shamba lako miaka sita, na miaka sita lipelee shamba lako la mizabibu, na kuyachuma matunda yake; 4 lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ni Sabato kwa Bwana; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu.
Walawi 25:1 “Kisha Bwana akanena na Musa katika mlima wa Sinai, na kumwambia,
2 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika nchi niwapayo, ndipo hiyo nchi itashika Sabato kwa ajili ya Bwana.
3 Panda shamba lako miaka sita, na miaka sita lipelee shamba lako la mizabibu, na kuyachuma matunda yake;
4 lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ni Sabato kwa Bwana; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu.
Unaona, haikuishia hapo tu kwenye mwaka wa 7, bali pia miaka hiyo miaka 7, ikipita mara saba tena, kuna sabato nyingine itakayokwepo katika mwaka unaofuata..yaani 7×7 =49, ikiwa na maana, mwaka wa 50 ni sabato ya pumziko na maachilio, inayojulikana kama YUBILEE.
Walawi 25:11 “Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa. 12 Kwa kuwa ni yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani. 13 Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake”.
Walawi 25:11 “Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa.
12 Kwa kuwa ni yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani.
13 Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake”.
Haiishii hapo tu, tutakuja kuona mbele kidogo, sabato nyingine ambayo Mungu ameificha katika maandiko, ambapo ipo katika miaka 1000 kwa ajili ya wateule wake.
Sasa ikiwa tumeshafahamu, sabato ni PUMZIKO, na sio siku fulani, au mwezi fulani, au mwaka fulani, tutafahamu sasa kuwa hata wana wa Israeli kutolewa Misri na kupelekwa Nchi ya Kaanani, ni kwamba walikuwa wanaingizwa katika Sabato yao, (yaani rahani mwao,) ambayo Mungu alikuwa amewaandalia.
Lakini biblia inatuonyesha kuwa sio wote waliweza kuingia katika hiyo raha ya sabato yao, kutokana na kutokuamini kwao na matendo yao kuwa maovu. Si wote waliweza kuingia katika nchi ibubujikayo maziwa na asali isipokuwa wale wawili tu lakini wengine wote waliosalia Mungu aliwaua kule jangwani.
Waebrania 3:8 “Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha, Siku ya kujaribiwa katika jangwa, 9 Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima, Wakaona matendo yangu miaka arobaini. 10 Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki, Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa; Hawakuzijua njia zangu; 11 KAMA NILIVYOAPA KWA HASIRA YANGU, HAWATAINGIA RAHANI MWANGU. 12 Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai. 13 Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. 14 Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho; 15 hapo inenwapo, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha. 16 Maana ni akina nani waliokasirisha, waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa? 17 Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa? 18 Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale”.
Waebrania 3:8 “Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha, Siku ya kujaribiwa katika jangwa,
9 Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima, Wakaona matendo yangu miaka arobaini.
10 Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki, Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa; Hawakuzijua njia zangu;
11 KAMA NILIVYOAPA KWA HASIRA YANGU, HAWATAINGIA RAHANI MWANGU.
12 Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai.
13 Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
14 Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;
15 hapo inenwapo, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha.
16 Maana ni akina nani waliokasirisha, waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa?
17 Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?
18 Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale”.
Unaona? Wengi wao walishindwa kuingizwa katika pumziko lao, kutokana na kuasi kwao.. Lakini sasa bado biblia inatuambia, sabato yao ilikuwa ni kivuli tu sabato halisi inayokuja huko mbeleni ambayo Mungu aliwaandalia watu wake, waaminifu. Mtume Paulo alisema kama ingekuwa Yoshua amewapa raha yenyewe, basi Daudi asingeandika tena mahali fulani huko mbeleni juu ya watu wa Mungu kuingia rahani mwa Mungu.
Waebrania 4:7 “aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo,kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu. 8 Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye. 9 Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu”.
Waebrania 4:7 “aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo,kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu.
8 Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye.
9 Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu”.
Umeona? Sisi kama watakatifu tunaomngojea Bwana bado hatujaingia kwenye raha yetu, au sabato yetu, ambayo Mungu alituandalia tangu zamani.. Sasa kumbuka Mungu huwa anapenda kutumia namba SABA, hasaa kuwakilisha sabato yake, kwa kustarehe kwake siku hiyo.
Na biblia inatuambia kwa Mungu miaka elfu moja ni sawa na siku moja. (2Petro 3:8). Sasa kama ulikuwa hujui ni kwamba tangu wanadamu tuumbwe, hadi sasa imeshapita miaka 6000, aidha inaongezeka kidogo sana, au inapungua kidogo sana. Lakini tupo katika mduara huo huo wa miaka elfu 6. Yaani Tangu Adamu mpaka Nuhu, inakadiriwa ni miaka elfu 2 ilipita, na tangu Nuhu Mpaka kuzaliwa kwa Yesu vilevile inakadiriwa ni miaka elfu 2 ilipita, na tangu kuzaliwa kwa Yesu hadi sasa tunajua ni miaka elfu 2 tupo, kwahiyo jumla ni miaka elfu sita.
Na kama tunavyofahamu kwa Mungu miaka elfu ni sawa na siku moja, kwahiyo mpaka sasa ni kama siku 6 tu kwa Mungu zimepita, na siku ya saba ni sabato yake. Hivyo miaka elfu moja ijayo itakuwa ni sabato ya Mungu kwa watu wake.
Hapo ndipo lile Neno la UTAWALA WA MIAKA ELFU MOJA linakuja kutimia, ambalo Kristo atatawala na watakatifu wake hapa duniani, dunia ikiwa katika hali ya amani na furaha tele.. Kwa maelezo marefu juu ya utawala huu wa amani, tutumie ujumbe inbox tukupe somo lake.
Wakati huo dunia hii itakuwa kama paradiso, kwasababu hakutakuwa na shida wala taabu, wala mateso, tutamfurahia Mungu wetu kwa Muda mrefu sana wa miaka elfu moja, wakati huo sio wa kukosa ndugu yangu..lakini inasikitisha kuona kuwa wengi wetu hatutaingia katika raha hiyo kwa mfano tu wa kuasi kwa wana wa Israeli kule jangwani..
Hizi ni nyakati za za kumalizia hakutakuwa na kanisa lingine zaidi ya hili, yaani sisi ndio tutakaoshuhudia tendo zima la UNYAKUO, Jiulize wewe utakuwa wapi wakati huo utakapofika ndugu yangu, Na ndio maana mtume Paulo ametuonya na kutuambia..
Waebrania 3:12 “Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai. 13 Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi”.
Waebrania 3:12 “Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai.
13 Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi”.
Waebrania 4:11 “Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi”.
Huu sio wakati wa kutanga tanga na huu ulimwengu, Huu ni wakati wa kuelekeza macho yetu mbinguni, tuhakikishe kuwa hata tukifa tutakuwa katika ufufuo wa kwanza, na unyakuo ukipita basi tunaenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni, ambapo tutakula ile karamu ya mwana kondoo kisha tutarudi kutawala na Bwana hapa duniani.
Je! Umeokoka? Kama bado unasubiri nini? Tubu dhambi zako mfuate Yesu, akupe uzima wa milele.
Maran Atha.
UTAWALA WA MIAKA 1000.
UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.
KAMA MKRISTO FAHAMU ZIPO HATUA UTAPIGISHWA NA MUNGU.
Nini maana ya “yasiyokuwapo hayahesabiki”(Mh 1:15)
Tafakari sana kabla hujafikia hitimisho Fulani ambalo ndio litakuwa la kudumu katika maisha yako.
Kuna watu wengi sana ambao shetani kawafumba macho, na kuwafanya wasifikiri vyema kabla ya kufikia hitimisho la maisha yao.
Kwamfano kuna watu wanatazama mwenendo wa watumishi wa uongo, au waliorudi nyuma, na kuhitimisha kwamba kamwe hawataokoka..kisa tu wameona hao watumishi wakifanya mambo ya ajabu yasiyopatana na wokovu kabisa.. Mtu wa namna hii tayari kafikia hitimisho la maisha yake bila kutenga muda wa kutafakari/ kufikiri sana.
Ndugu ni kweli umezunguka kila mahali hujaona mchungaji mkamilifu kama ulivyotaka wala ulivyotegemea…Lakini hiyo isikupe nafasi ya kusema hutamtafuta Mungu kamwe wala hutaokoka..Kwasababu ni kweli hujaona mchungaji mkamilifu lakini yupo aliye mkamilifu ambaye hakutenda dhambi kabisa hata moja, yaani YESU KRISTO, habari zake zimeelezwa kwa urefu katika maandiko, Umekataa kumsikiliza mchungaji wako kwasababu umeshuhudiwa kafumaniwa katika uzinzi, umekataa kumsikiliza muhubiri fulani maarufu kwasababu kakengeuka kawa kama watu wa kidunia n.k.. Lakini yupo mmoja aliye mkamilifu YESU KRISTO, mfuate huyo hao wengine waache.. Unafikiri utajitetea vipi siku ile ya hukumu?.
Utasema Bwana mimi nilikata tamaa ya kuendelea na wokovu kwasababu mchungaji wangu alinitaka kimapenzi, hakuwa mkamilifu,..ni kweli mchungaji wako anayo dhambi lakini alikuwepo YESU AMBAYE BADO NI MWAMINIFU, hana dhambi, mchungaji mkuu.. ungemfuata huyo Yesu, umwache mchungaji wako..Lakini wewe umewatapika wote…Utajitetea vipi siku ile???… kama vigezo vya utakatifu Bwana Yesu kavikidhi vyote, hana kosa wala hatia…Tafakari sana kabla ya kufanya maamuzi, usitafakari juu juu tu.
Bwana Yesu alisema maneno haya..
Yohana 8.46 “Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?”
Mchungaji wako anayekuchunga anayo dhambi, pengine umemshuhudia akisema uongo, umemshuhudia akizini, lakini ni wapi Yesu umemshuhudia akisema uongo, ni wapi umemshuhudia akizini? …lakini wewe umemkataa Yesu aliye mkamilifu sawasawa na Mchungaji wako,..ni nani sasa utakayemkubali mwenye vigezo unavyovitaka wewe??…..Ndio maana anauliza swali hilo hapo juu “Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi?” … Yesu hana dhambi hata moja unamkataa…utamkubali nani kwamfano ukiulizwa hilo swali?….siku ile utajitetea vipi mbele ya Bwana?.
Utasema mimi ni kijana, siwezi kuishi maisha bila kufanya uasherati, kwasababu naishi mazingira ya vishawishi vingi…. Siku ile ataletwa kijana aliye mzuri kimwonekano kuliko wewe na aliyeishi katikati ya mazingira magumu kuliko wewe, lakini aliweza kuushinda uasherati kwa kishindo kikubwa…Hapo utazungumza nini cha kujitetea??.
Unajua ni kwanini biblia inasema watakatifu watauhukumu ulimwengu??
Ni kwa njia hiyo ya wanavyoishi…kama kuna dada ambaye mnaishi naye mtaani anavaa vizuri katikati ya dunia hii ya wanawake walioharibika akili, siku ya hukumu atawahukumu wanawake wote waliokuwa wanavaa vibaya…na atawahukumu si kwa maneno, bali maisha yake ndio yatawahukumu hao wengine…wakati hao wengine wanasema Bwana ilikuwa haiwezekani kila duka lilikuwa linauzwa nguo fupi, yeye atasimamishwa na kuulizwa alizipata wapi hizo ndefu..na hivyo maisha yake kuwa hukumu kwa wengine, (hiyo ndio maana ya watakatifu watauhukumu ulimwengu 1Wakorintho 6:2)
Kwahiyo usifikiri kwa vyovyote vile siku ile kuna kushinda hoja mbele ya kiti cha hukumu.. hakutakuwa na hoja yoyote ya kushinda, ndio maana leo hii..tunapata nafasi hii ya kukumbushwa kutafakari kwa makini kabla ya kufanya maamuzi.
Leo hii umeuacha wokovu kwasababu ya mchungaji wako, Rudi mgeukie Yesu Mchungaji mkuu asiye na dhambi, leo hii maneno ya muumini mwenzako yamekufanya usiupende wokovu au ukristo, ni wakati wa kumtazama Kristo na si mwanadamu.. Leo hii umevunjwa moyo na wakristo wenzako, au kiongozi wako katika imani, hata ikakufanya ukate tama kabisa ya kuendelea na wokovu…Ni wakati wa kuyaweka hayo mawazo pembeni kwasababu, shetani anataka ufikiri hivyo hivyo mpaka siku ya hukumu, ili ukose cha kujitetea siku ile.
Na kama hujampokea Yesu kwasababu nyingine yeyote, huu ni wakati wa kufanya hivyo, tunaishi siku za hatari sana, na adui yetu shetani ana wakati mchache sana, amewekeza nguvu nyingi katika kuwafanya watu wasione mbele, badala yake wawe bize kutafuta mambo ya kidunia na kuwa na vijisababu vidogo vidogo vya kuhalalisha huo usingizi wa kiroho..Hiyo amka leo. Kristo anarudi, parapanda inakaribia kulia, na mwisho wa dunia kufika.
Mafundisho mengine
Nini maana ya K.K, na B.K? (B.C na A.D).
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
UWE MWAMINIFU HATA KUFA.
MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.
Jina kuu la Bwana wetu Yesu libarikiwe.
Ni siku nyingine tena Bwana ametupa pumzi yake kuiona, leo tutajifunza somo linalohusiana na utakaso kwa mtakatifu. Lakini kabla hatujafika kwenye utakaso, ni vizuri tufahamu kwanza mtakatifu ni mtu wa namna gani kibiblia..
Wengi tunafahamu labda mtu mpaka aitwe mtakatifu ni lazima awe ameshakaa kwenye wokovu miaka mingi,, lakini kibiblia sio hivyo. Bali pale mtu anapoamua kuokoka, pale anapoamua kuacha maisha yake ya dhambi, na kumgeukia Bwana Yesu, na kusafishwa na damu yake, na kubatizwa, wakati huo huo anakuwa tayari kashafanyika kuwa mtakatifu, haijalishi mambo mengine yatakuwa hayajaondoka vizuri ndani yake,..Kile kitendo tu cha kumpokea Yesu maishani mwake, mtu huyo mbinguni ni mtakatifu kwasababu hana deni la dhambi, anakuwa sawasawa tu na mkristo mwingine aliyekaa katika wokovu kwa miaka 50.
Lakini tatizo linakuja ni pale ambapo mtu huyo anadhani akishampokea Yesu, ndio basi inatosha, Nataka nikuambie hilo halipo katika safari ya ukristo. Utarudi nyuma tu siku sio nyingi, na utakatifu wako utakufa na utakuwa kama vile mtu ambaye hajaokolewa.
Fahamu baada ya kuwa mtakatifu, hatua inayofuata kwako ni lazima iwe Kujitakasa.. Ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya..
Ufunuo 22:11 “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na MTAKATIFU NA AZIDI KUTAKASWA”.
Unaona inasema mtakatifu azidi kutakaswa, ikiwa na maana ukiwa mtakatifu hupaswi kubakia pale pale sikuzote, ni jukumu lako kujitakasa siku baada ya siku. MTAKATIFU ni kama BETRI ya simu. Pale inaponunuliwa ndani yake huwa imeshaumbiwa nguvu ya kutosha ya kuifanya simu iwake kwa muda wa miaka mingi sana hata 10 na zaidi. Lakini Betri hiyo haitegemei tu ile nguvu iliyowekwa ndani yake kuipa uhai simu siku zote, hapana, bali inatarajia pia iwe inachajiwa mara kwa mara, hata kila siku, ili kuzisisimua nguvu zilizoko ndani yake iendelee kuifanya simu iwake kwa muda wote huo.
Lakini kama isipochajiwa, ni wazi kuwa hautaweza kuwasha simu, na matokeo yake ni kuwa itakuwa kama jiwe tu lisilokuwa na maana yoyote, haijalishi kuwa ndani yake kuna nguvu nyingi kiasi gani.Vivyo hivyo na utakatifu nao.. utakatifu bila utakaso Umekufa.
Unapookoka leo hii, unapoamua kumpa Yesu maisha yako, hiyo peke yake haitoshi zipo hatua za kuanza kupiga, ili kuufanya ule utakatifu kuwa hai ndani yako siku baada ya siku. Yapo maisha unapaswa uanze kujizosha kuishi ili Mungu aweze kukutakasa (kukutia nguvu ) ya kuendelea kuishi maisha ya utakatifu siku baada ya siku .
Warumi 6:22 “Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, MNAYO FAIDA YENU, NDIYO KUTAKASWA, na mwisho wake ni uzima wa milele”.
SASA MTU ANAJITAKASAJE?
Kwanza ni kwa kukujifunza Neno la Mungu kwa bidii: Unapookoka, ni jukumu lako kusoma Neno na kusikiliza Neno, hususani mafundisho yanayolenga utakatifu. hiyo itakusaidia kujua biblia inasema nini katika kila jambo unalotaka kulifanya. Hivyo kuwa rahisi kujiepusha na mambo ambayo hayampendezi Mungu.
1Petro 1:22 “Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo”.
Pili ni kwa kuwa mwombaji na kufunga: Maombi ni nguzo nyingine inayomtia mtu nguvu ya kuendelea kudumu katika utakatifu Mungu anaouhitaji ndani ya mtu. Usipokuwa mwombaji huwezi kudumu katika wokovu, huwezi kuyashinda majaribu kwa namna yoyote ile. Vilevile na katika kufunga, kunakusaidia kufikiria zaidi mambo ya rohoni kuliko ya mwilini na matokeo yake kuzishinda tama zake.
Tatu ni kwa kujizoeza kuishi maisha yampendezayo Mungu: Kujizoesha ni jambo lingine la msingi sana, kwamfano mtu aliyejizoesha kuamka alfajiri sana, huwa inafikia wakati kuamka kwake asubuhi kunakuwa ni kwepesi sana tofauti na Yule ambaye hajajizoesha kuamka mapema.. Vivyo hivyo na katika Utakatifu, tukijizoesha kuishi maisha ya haki, baadaye yanakuja kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku yenyewe bila hata kutumia bidii nyingi.
1Timotheo 4:8 “Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye”.
Nne, Ni kwa kuifanya kazi ya Mungu: Kuitenda kazi ya Mungu ikiwemo kuwahubiria wengine ni chaji nzuri sana ya utakatifu. Kwasababu inakufanya ukae katika uwepo wa ki-Mungu muda mrefu, kwasababu unamlazimisha Roho Mtakatifu aje kufanya kazi na wewe, na sikuzote alipo Roho Mtakatifu, lazima uwepo utakatifu.
Hivyo kwa kuhitimisha, ni jukumu la kila mmoja wetu KUJITAKASA kila siku, ili aendelee kudumu, hakunaga Utakatifu wa kusema mimi nimeokoka, halafu huonyeshi bidii yoyote, hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe, utasema tu kwa mdomo lakini kwa matendo utakuwa mbali nao. Ni lazima tujichaji (tujitakase) ili tuweze kudumu kwenye huo utakatifu. Siku hizi za mwisho Bwana Yesu alitusisitiza sana kufanya hivyo, kwasababu maovu yameongezeka, na yeye yupo mlangoni kurudi.
2Petro 1:8 “Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo. 9 Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, AMESAHAU KULE KUTAKASWA DHAMBI ZAKE ZA ZAMANI.
2Petro 1:8 “Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.
9 Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, AMESAHAU KULE KUTAKASWA DHAMBI ZAKE ZA ZAMANI.
Mimi na wewe tusisahau utakaso wa kila siku.
Maran atha.
Nini maana ya ‘Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu’ ?
TUSIWE WATU WA KUPUNGUKIWA AKILI.
MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.
Nini maana ya ‘kuhuluku’ kama tunavyosoma katika biblia?
Kwanini Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wasikisaze chakula?
SWALI: Naomba kufahamu maana ya mstari huu ; Mithali 16:1 “Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana”.
JIBU: Mstari huu unatukumbusha kuwa si kila jambo tunalolipanga katika maisha tunaweza kulitolea maamuzi yake asilimia mia. Ni kweli Mungu anaturuhusu tupange mipango yetu mingi kwa jinsi tupendavyo, lakini tunapaswa tukumbuke pia sio kila mpango tulioupanga ni lazima uje kama tulivyotarajia.
Kwamfano utaona Balaamu alipomwendea Mungu ili kuwalaani Israeli, jibu la Mungu lilikuwa ni kuwabariki badala ya kuwalaani. (Hesabu 22-24). Utaona alikwenda kweli na mipango yake kwa Mungu ili kumridhisha Balaki, akidhani utakuwa ni vema pia kwa Mungu, lakini badala yake aliambiwa aibariki Israeli badala ya kuilaani.
“Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana”
Hivyo tunapopanga mipango yetu, tunapaswa tujinyenyekeze kwa kusema Bwana akipenda kama biblia inavyotuasa hapa,
Yakobo 4:13 “Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; 14 walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. 15 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi. 16 Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya”.
Yakobo 4:13 “Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida;
14 walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka.
15 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.
16 Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya”.
Unaweza kweli ukawa umepanga uje kuwa daktari ukubwani, lakini mipango yako au ndoto zako ghafla zimevuruguka kuona kwamba unalazimika kwenda kusomea kitu ambacho hujakipenda, sasa unapokuwa katika hali kama hiyo na wewe ni mkristo kumbuka huu mstari.. “Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana”
Unaweza ukawa umepanga, ufanikishe jambo fulani, mwaka uliopita lakini haujafanikisha kutoka na vikwazo fulani, pengine ukaanza kulaumu kwanini haikuwezekana, sasa ukijikuta katika hali kama hiyo na wewe ni mkristo ambaye unaouhakika umeokolewa na Kristo, hupaswi kuwa na huzuni, ujue ipo mipango mingine mzuri zaidi ambayo Mungu kaiweka mbele yako, pengine unaweza usiione sasa hivi, lakini baadaye ukaiona na kumshukuru Mungu, na kusema asante Mungu kwa kunipitisha njia hii leo.
Hivyo kila jambo ulifanyalo, usilipe asilimia mia kwamba ni lazima liwe kama ulivyolipanga, kumbuka wewe sio Mungu, anayejua kesho kwa asilimia yote ni Mungu peke yake..Kwahiyo wewe amka asubuhi, panga mipango yako, kisha mshirikishe Mungu na umalizie na Neno IKIWA ITAKUPENDEZA MUNGU..
Ikiwa imempendeza basi litafanikiwa kama ulivyopanga lakini ikiwa halikumpendeza basi atakuandalia njia nyingine iliyo bora zaidi.
Shalom.
Tofauti kati ya lijamu na hatamu ni ipi kibiblia?
JE SALA YA ROZARI TAKATIFU NI YA KIMAANDIKO?
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
CHAPA YA MNYAMA
JIBU: Tusome mstari wenyewe.
Mhubiri 1:15 “Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa, Wala yasiyokuwapo hayahesabiki”.
Hapo utaona vipengele viwili, cha kwanza ni: Yaliyopotoka hayawzi kunyoshwa. Na cha pili ni yasiyokuwapo hayahesabiki.
Tukianza na hicho cha kwanza cha Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa,..Tukumbuke kuwa kitabu cha Mhubiri ni kitabu kinachoeleza juhudi za mwanadamu za kutafuta suluhu ya mambo yote yaliyopo duniani kwa nguvu zake mwenyewe pasipo kumuhusisha Mungu. Na ndio maana utaona mhubiri ambaye ndiye aliyejibidisha katika kufanya hivyo, mwisho wa siku anaishia kusema ni UBATILI Mtupu, mambo yote na hekima yote ya mwanadamu ni ubatili tu, ni sawa na kuufuata upepo ambao mwanzoni unaweza kukupa matumaini kuwa utakufikisha mahali, lakini mwishowe unapotea tu ghafla njiani, hujui ulipoelekea umekuacha tu hewani. Ndivyo alivyo mwanadamu anayehangaika kukimbizana na ulimwengu huu.
Sasa aliposema “Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa” Ni kuwa aliona, kuna mambo ambayo yalikatazwa na Mungu, au kwa namna nyingine tuseme hayapo katika uhalisia wake, na pengine anaweza kuyaweka sawa na kuyafanya yaonekane yanafaa katika jamii, Umeona? Ndipo kwa hekima yake akajaribu kufanya hivyo aone kama yatakuwa kweli ni sawasawa, lakini mwisho wa siku akagundua hata ufanyaje kile kilichokataliwa na Mungu (yaani kupotoshwa) hakiwezi kufanywa kiwe sawasawa. Ni kujitafutia tu matatizo na shida zisizokuwa na sababu.
Mbeleni kidogo utaona anasema..
Mhubiri 7:13 “Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye?
Ni kama leo tu, watu wanatafuta namna ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja..wanajaribu kufanya kila mbinu, ionekane kuwa ile ni ndoa iliyokubaliwa na Mungu, lakini bado haiwezi kuwa ndoa, na hilo wanalijua, wengine mpaka wanajibadilisha jinsia waonekane kama wanaume, au wanawake, lakini bado zile jinsia zao zinaendelea kubakia nao ndani yao.. Na matokeo yake wanaishia kupata matatizo mabaya ya kiafanya na kuishia kufa.
Ndivyo walivyo hata na mashoga, wanapojaribu kuwa kama wanawake, maumbile yao yanaharibika wanashindwa kukaa hata katika jamii na watu wengine wakihofia aibu. Kwasababu yaliyopotoshwa hayawezi kunyoshwa, Unaona? Si hilo tu Wapo wengine wanajichubua ngozi zao ili wabadili rangi ya miili yao wawe weupe, sote tunajua mwisho wao watu wa namna hiyo ni nini, ni kuishia kupata kansa ya ngozi na kufa.
Inastaajabisha leo hii, kuona wanawake nao wanasema suruali ni mavazi ya jinsia zote. Haijalishi wataihalalisha vipi wataitengeneza kwa muundo gani unaoonekana wa kike, lakini bado vazi la suruali litabakia kuwa vazi la kiume tu, wewe unayejaribu kukinyosha kitu ambacho Mungu kakipotosha kwako unajitafutia matatizo na hukumu.
Unaweka mawigi, kucha za bandia, ili uonekane wa tofauti na Yule wa kwanza ambaye Mungu alikuumba..Embu Itafakari vema kazi ya Mungu, na uache kukinyosha kile ambacho Mungu kakipotosha. Hiyo ndio maana ya kifungu hicho.
> Sasa tukirudi kwenye kile kipengele cha pili ambacho kinasema “Wala yasiyokuwapo hayahesabiki”.
Hii dunia imejawa na mambo mengi ya Mungu, ambayo bado mwanadamu anazidi kuyavumbua kila siku, lakini mpaka sasa takwimu zinaonyesha, bado asilimia 86 ya viumbe havijajulikana duniani, japokuwa ameishi duniani kwa muda mrefu sasa
Mambo yasiyojulikana ni mengi kuliko yanayojulikana, wanasayansi wanalijua hilo, kila siku wanavumbua mambo mapya, wanashangaa kumbe na hili lipo na lile lipo..Hiyo inawafanya wawe buzy usiku na mchana kutafuta na kutafiti tu, siku zinakuja siku zinakwenda, wanaendelea tu hivyo hivyo, wanasahau mpaka na mambo ya msingi ya roho zao.. Wanadhani katika kuvumbua huko ndio siku moja watapata jawabu la maisha ya mwanadamu hapa duniani.
Mhubiri anasema hayo yote ameshayafanya, lakini amegundua ni ubatili mtupu, kwamba yasiyokuwepo hayahesabiki, hata kama nitakuwa buzy miaka yangu yote kutafiti, kamwe sitavumbua yote. Ni sawa na kuufuata upepo. Huoni leo hii wanadamu walivyo buzy na mambo ya duniani wanasahau mambo ya mbinguni ambayo ni ya kudumu milele? Kiasi kwamba huwezi kuwaeleza chochote, nje ya sayansi wanayojitumainisha nayo.
Lakini Mhubiri mwishoni anatoa jumla ya mambo yote, anasema, linalompasa mwanadamu kufanya ni KUMCHA MUNGU, NA KUZISHIKA AMRI ZAKE (Mhubiri 12:13) basi. Na wewe pia hakuna mahali popote utakapoweza kupata jawabu la maisha isipokuwa kwa Kristo tu peke yake. Hii dunia itakutesa sana, lakini Ukimpa leo maisha yako,ayaongoze, ukaanza naye upya ameahidi kukupa pumziko la roho, hiyo ni ahadi yake.
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Hivyo kama upo tayari leo kutubu na kuanza naye upya, basi fungua hapa kwa maelekezo ya sala ya Toba..>>. SALA YA TOBA
Maana ya huu mstari ni ipi? Mithali 14:4 ‘Zizi ni safi ambapo hapana ngombe;bali nguvu za ngombe zaleta faida nyingi’.
Kiango na Pishi ni nini (Mathayo 5:15)?
Ukoma wa nyumba ulifunua nini zamani?
NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.
Kuhuluku ni Neno lingine linalomaanisha KUUMBA.
Kwamfano tukisema Mungu kahuluku jua na mwezi, tunamaanisha kuwa Mungu ameumba jua na mwezi.
Vifuatavyo ni baadhi ya vifungu ambavyo vinalielezea Neno hilo;
Isaya 43:1 “Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu”.
Isaya 45: 12 “Mimi nimeiumba dunia, nimemhuluku mwanadamu juu yake; Mimi, naam, mikono yangu mimi, imezitanda mbingu, na jeshi lake lote nimeliamuru”.
Isaya 45: 7 “Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na KUHULUKU UBAYA; Mimi ni Bwana, niyatendaye hayo yote”.
Katika huu mstari wa mwisho utaona anasema sio tu ameumba vitu vya asili na wanadamu au mambo mema tu peke yake, hapana, bali anasema yeye pia ni Mungu anayehuluku UBAYA, Yaani anaumba ubaya. Jambo ambalo wengi hatulijui.
Ndio Mungu anaumba ubaya ndugu yangu,. Alipoleta gharika ule ulikuwa ni ubaya, lengo lilikuwa ni kuwagharikisha watu wote waovu waliokuwa duniani wakati ule. Embu Soma maneno haya anavyosema;
Ayubu 38:22 “Je! Umeziingia ghala za theluji, Au umeziona ghala za mvua ya mawe, 23 Nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba, Kwa siku ya mapigano na vita”?
Ayubu 38:22 “Je! Umeziingia ghala za theluji, Au umeziona ghala za mvua ya mawe,
23 Nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba, Kwa siku ya mapigano na vita”?
Unaona?
> Aliposhusha pia ule moto na kibiriti, wakati wa Sodoma na Gomora ule ni uovu aliouumba yeye mwenyewe mahususi kwa ajili ya watenda dhambi.
> Alipoleta tena Tauni mara kadha wa kadha kwa taifa la Israeli pale walipomwasi na kumkasirisha kule jangwani na sehemu nyinginezo, ule ulikuwa ni ubaya aliohuluku, kwa watu waasi.
> Vilevile alivyoleta CORONA ulimwengu ni Ubaya uliotoka kwake yeye mwenyewe kutuadhibu sisi wanadamu tunaoishi duniani leo hii kwa matendo yetu maovu. Hakuna mwanasayansi yoyote aliyeuunda ugonjwa huo, Huo ni ugonjwa uliotoka kwa Mungu mwenyewe kama pigo.
> Lakini hayo yote ni mwanzo tu ubaya wenyewe ambao Mungu alishaundaa tangu zamani kwa watenda dhambi wote ikiwemo ibilisi pamoja na mapepo yake yote. Na ubaya wenyewe ndio lile ZIWA LA MOTO.
Hivyo Mungu ni wa kumuogopa sana.. Ni kweli yeye ni Mungu wa rehemu na neema nyingi, kwa wale wamtiio, lakini pia ni wa ghadhabu na hasira nyingi, kwa waovu wote. Na ndio maana leo hii anakupa Muda wa kutosha wa kutubu ili umgeukie yeye akusemehe dhambi zako. Usifurahie unatenda dhambi halafu hakuna chochote kinachokutokea, usifurahie unaua, unafanya ushirikina, unazini, lakini Mungu hakufanyi chochote ukadhani utaendelea kuwa hivyo milele. Upo ubaya mbele yako. Na ni jukumu lako kufahamu hilo ili siku ile usije ukasema sikuambiwa.
Hivyo tubu dhambi zako umgeukie Mungu, akuoshe, ili ushiriki wema wa Mungu na sio ubaya wake.
Kama upo tayari kufanya hivyo leo, basi fungua hapa kwa ajili ya SALA YA TOBA, na Maelekezo mengine >> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Pia Tazama tafsiri ya maneno mengine ya kibiblia chini.
Chuo cha vita vya Bwana ni kipi?(Hesabu 21:14)
NAYE AKASIMAMA JUU YA MCHANGA WA BAHARI.
Ngome ni nini? Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?
Ni kwanini mifugo ya Yakobo iliongezeka kwa wingi kiasi kile?
Nyinyoro ni nini?
Kiango ni kifaa maalumu cha kushikilia au kuning’inzia taa, tazama picha, kwa jina lingine kinaitwa kinara. Na nilazima kinyanyuke au kiwe sehemu ya juu kidogo, ili kuruhusu mwanga wa hicho kilicho juu yake (yaani taa) kuangaza mahali pote.
Na Pishi ni bakuli dogo, au kapu ndogo. Tazama picha,
Hivi ni vifungu ambavyo utaweza kukutana na maneno hayo;
Mathayo 5:15 “Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani”.
Marko 4:21 “Akawaambia, Mwaonaje? Taa huja ili kuwekwa chini ya pishi, au mvunguni? Si kuwekwa juu ya kiango”?
Luka 11:33 “Hakuna mtu awashaye taa na kuiweka mahali palipositirika, au chini ya pishi; bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuuona mwanga”.
Soma pia Luka 8:16
Hivyo mpaka hapo tunaweza kupata picha sasa Bwana Yesu alimaanisha nini kutoa mfano huo, kuwa tunapoamua kuokoka hatupaswi kuuficha wokovu wetu, kuuweka chini ya bakuli bali ni sharti tuungaze kwa watu wote, kwanza kwa matendo yetu na pia kwa kuwahubiria ili kusudi kwamba wavutwe na wao katika wokovu tulionao.
Na ndio maana pale kwenye Mathayo 5:15 akamalizia na kusema..
16 “Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni”.
Tazama maana nyingine ya maneno ya biblia chini.
Bwana Yesu alimaanisha nini aliposema; Mafarisayo Hupanua HIRIZI zao, na kuongeza MATAMVUA yao?
GOGU NA MAGOGU, Katika biblia ni nani?
“Shinikizo” ni nini kibiblia, Na maana yake rohoni ni ipi?
Uga ni nini? Na kazi yake ni ipi kibiblia?
SIFONGO NA SIKI NI NINI?
Shalom, jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe milele.
Karibu tujifunze Neno lake.
Ukisoma kitabu cha Ufunuo sura ya 12, utaona habari kuu inayouzungumziwa pale ni kuhusu mapambano ambayo aliyafanya tangu akiwa mbinguni, na anayoendelea kufanya hadi sasa.
Utaona mapambano hayo yamegawanyika katika vipengele vikuu vitatu. Cha kwanza vita ile aliyoifanya mbinguni akiwa na malaika zake, ambayo alishindwa, na matokeo yake akatupwa chini,
Kipengele cha pili utaona ni ile vita aliyoifanya na yule mwanamke aliyemzaa mtoto mwanaume, ambaye nchi ilimsaidia. Na mwanamke yule analiwakilisha Kanisa la Israeli kwa ujumla. Wakati Bwana Yesu anazaliwa, utaona shetani kwa kupitia Herode alikuwa ameshaanza kuleta maafa Israeli, kwa kuwaaua wale watoto wote waliozaliwa wakati mmoja na Yesu, lengo likiwa ni kumwinda Yesu, afe, Lakini Mungu akamuhamisha Kristo akilimbilie Misri kwa muda, na hiyo ilikuwa ni kulinusuru taifa zima.
Na kipengele cha tatu na cha mwisho ambayo ndio kiini cha somo letu la leo Ni vita ambayo shetani aliita kwa uzao wake wote wa huyo mwanamke uliosalia. Yaani wote watakaofanana na Kristo, waisraeli wa rohoni, hao ndio anamalizia kufanya nao vita , na vita hiyo ni endelevu, ilianza tangu kipindi kile Kristo anaondoka duniani, mpaka leo hii, na itaisha na unyakuo.
Lakini kuna jambo moja la kuona pale, shetani alipoanza kufanya vita na kanisa la Kristo, hakusimama mbinguni tena au nyuma yetu kuleta mafuriko, kama alivyofanya kwa yule mwanamke, hapana, bali biblia inatuambia alikwenda kusimama JUU YA MCHANGA WA BAHARI.
Ufunuo 12:13 “Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume. 14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo. 15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule. 16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake. 17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake AFANYE VITA JUU YA WAZAO WAKE WALIOSALIA, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; NAYE AKASIMAMA JUU YA MCHANGA WA BAHARI”.
Ufunuo 12:13 “Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.
16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.
17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake AFANYE VITA JUU YA WAZAO WAKE WALIOSALIA, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; NAYE AKASIMAMA JUU YA MCHANGA WA BAHARI”.
Sasa mchanga wa bahari unawakilisha nini?
Hapo inaposema kwenye mchanga wa habari inamaanisha kwenye ufukwe, yaani alikwenda kusimama ufukweni, mpakani, kati ya habari na nchi kavu. Hii ikiwa na maana vita vyake hasa vipo pale mpakani, kuhakikisha kinachotoka habarini hakiji nchi kavu. Na hata kama kikitokea kimevuka nchi kavu, basi hakitapita hivi hivi tu.
Sasa kibiblia habari au palipo na maji mengi inawakilisha ulimwengu,(Ufunuo 17:15) ..Na nchi kavu ni wokovuni..Bwana Yesu alimwambia Petro njo nami nitakufanya kuwa mvuvi wa watu. Yaani kuwatoa watu kutoka kwenye ulimwengu na kuwaleta katika Nuru ya wokovu,
Hii ikiwa na maana mtu yeyote ambaye hajaokoka, kwamba yupo baharini, hivyo akishaokoka, ni anakuwa anahamishwa kutoka kwenye maji na kuletwa nchi kavu.
Hivyo sasa tunamwona hapa shetani kasimama ufukweni, lengo lake likiwa ni kukipinga kile kinachotoka kule kuja nchi kavu. Kumpinga mtu Yule ambaye anataka kutoka kwenye dunia na kuja katika wokovu. Mtu yule nayetaka kuacha kuishi maisha yake machafu na kuja katika maisha mapya ya utakatifu. Hapo ndipo vita vya ibilisi vilipo haswaa.
Hapo ndipo utakapokutana na shetani, hakuna mahali pengine utamwona ibilisi kwa uwazi wote kama hapo. Ndio vita vyake vilipo. Hatahangaika na wewe ambaye sikuzote upo dhambini, wala hutamwona akikugasi, lakini siku ambapo unafanya uamuzi ndipo utakapomwona akitaka kukusumbua, kama vile alivyotaka kumwangamiza Kristo tu alipozaliwa duniani.
Lakini ni wajibu wetu kumshinda, na tunamshinda kwa damu ya mwanakondoo na kwa Neno la ushuhuda wetu sawasawa na
Ufunuo 12:11 “Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa”.
Hivyo kaa ukijua kuwa pale unapotaka kufanya badiliko la kweli la maisha hapo ndipo pa muhimu sana, na shetani analijua hilo na ndio maana anasimamia hapo, kwahiyo ni wajibu wako kumshinda, haijalishi ataleta vita vya aina gani, Kumbuka hizi ni siku za mwisho, na Bwana Yesu alisema, ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu ndio watakaouteka. Mathayo 11:12
Kwahiyo huna sababu ya kuanza kuogopa kudharauliwa, au kuchekwa, au kutengwa au kudhihakiwa kisa tu umeamua kuokoka au kuishi maisha ya wokovu. Jitwike msalaba wako umfuate Yesu, ili upokee taji la ushindi ufikapo kule.
Bwana akubariki
JINSI DHAMBI ILIVYO NA SHINIKIZO KUBWA SANA.
ROHO ANENA WAZIWAZI
JIFUNZE KUTOA KATIKA HAZINA YAKO VITU VIPYA NA VYA KALE.