Mimbari ni nini? Je tofauti kati ya Mimbari na madhabahu ni ipi?

Mimbari ni nini? Je tofauti kati ya Mimbari na madhabahu ni ipi?

SWALI: Mimbari ni nini? Je tofauti kati ya Mimbari na madhabahu ni ipi?


Mimbari ni eneo lililoinuka ambalo limetengwa rasmi katika kanisa kwa ajili ya Neno la Mungu kuhubiriwa, au taarifa za kikanisa kuwasilishwa, au huduma nyingine za kiibada kutendeka kama vile uimbaji wa kwaya.

Lakini Madhabahu ni eneo la kanisa ambalo watu huenda kuomba, kutoa sadaka, kupeleka shukrani na sifa, na kushiriki meza ya Bwana (yaani mahali pa kukutana na Mungu). Madhabahuni pa Mungu sio tu pale mbele ya kanisa, bali ni lile eneo lote la kanisa. Isipokuwa tu lile la mbele ndio linasimama kama kitovu cha madhabahu yote.

Mara nyingi mimbari pia huwa palepale madhabahuni. Hivyo unaweza kusikia mtu anasema nakwenda kusimama madhabahuni kuhubiri, mwingine utamsikia anasema nakwenda kusimama mimbarani. Wote wawili hawajabadili maana.

Hivyo ikiwa unakwenda kwa kuhubiri, au kuhutubu, au kuimba kwaya kiuhalisia hapo ni sawa na unasimama mimbarani, lakini ikiwa unakwenda kwa ajili ya kuomba, kutoa sadaka, kufanya ibada kama kusifu na kuabudu, hapo huisogelei mimbari bali madhahabu ya Mungu.

Mimbarani ni mahali pa kusikilizwa, lakini madhabahuni, ni mahali pa kushiriki

Mambo ambayo hupaswi kufanya mimbarani kama mhubiri.

  • Kutoka toka sana nje ya mimbari pindi uhubiripo
  • Kufundisha maudhui ambayo yapo nje ya Neno la Mungu. Mfano, siasa, michezo
  • Kujigamba/ Kujisifu zaidi ya kumtukuza Kristo
  • Kupuuzia kujiandaa, kimaombi na kiroho, kabla ya kusimama mimbarani

Mambo ambayo hupaswi kufanya uwapo madhahabuni kama mshirika.

  • Usitoe sadaka yako kama una neno na ndugu yako.(Mathayo 5:23-24)
  • Usivae mavazi yasiyo na utukufu machoni pa Bwana
  • Usizunguke zunguke, au kuzungumza ovyo uwapo kanisani (kuwa mtulivu). Kumbuka eneo lote la kanisa ni madhabahu ya Mungu, na sio pale mbele tu.
  • Hakikisha huchelewi kufika madhabahuni pa Mungu, wala huikatishi ibada na kuondoka

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Mahali pa juu palikuwa ni wapi kama tunavyosoma katika biblia?

YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.

Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?

Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?

Kwanini madhabahu zilitengenezwa kwa mawe yasiyochongwa?

Biblia inasema tujihadhari na “Mbwa” hawa mbwa ni akina nani? (Wafilipi 3:2)

UPAKO NI NINI?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments