JE BWANA YESU ALIMTOKEA YUDA BAADA YA KUFUFUKA KWAKE?.

JE BWANA YESU ALIMTOKEA YUDA BAADA YA KUFUFUKA KWAKE?.

Je Bwana Yesu alimtokea Yuda baada ya kufufuka kwake?.. maana tunasoma katika 1Wakorintho 15:5 kuwa aliwatokea wale Thenashara ambao mmojawao alikuwa ni Yuda.

Jibu: Kwanza ni muhimu kujua maana ya Neno “Thenashara”.. Tafsiri ya Thenashara ni “kumi na mbili”. Maana yake popote biblia inapotaja neno hilo, iliwalenga wale Mitume 12 wa Bwana Yesu.

Na katika kipindi cha huduma ya Bwana Yesu, Yule Yuda aliyemsaliti alikuwa miongoni mwa hao Thenashara. Lakini tunaona baada ya kufa walibaki Mitume 11 tu..na kipindi Bwana Yesu anafufuka Yuda tayari alikuwa ni Marehemu kwani alijinyonga kabla hata ya Bwana kufufuka, hivyo hakuuona ufufuo wa Bwana,  Lakini tukienda mbele katika kitabu cha 1Wakorintho 15:3 tunasoma kuwa Bwana aliwatokea wote 12.. Je ni kwamba biblia inajichanganya au la?

Tusome..

1Wakorintho 15:3  “Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;

4  na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;

5 na ya kuwa alimtokea Kefa; TENA NA WALE THENASHARA;

6  baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala”

Ni kweli Bwana aliwatokea wale Thenashara (yaani Mitume 12), lakini Yule wa 12 hakuwa Yuda kwasababu biblia inasema nafasi yake ilichukuliwa na mtu mwingine aliyeitwa Mathiya.

Tusome.

Matendo 1:23  “Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya. 24  Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili,

25  ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe. 26  Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye AKAHESABIWA KUWA PAMOJA NA MITUME KUMI NA MMOJA”

Hapo anasema Mathiya akahesabiwa kuwa pamoja na Mitume 11, maana yake yeye alikuwa wa 12. Kwahiyo Mathiya alihesabika miongoni mwa Thenashara, na ndio maana hapo katika 1Wakorintho 15:5 Mtume Paulo kataja kumi na Mbili, lakini Yule wa 12 hakumlenga Yuda bali Mathiya.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Thenashara ni nini? (Marko3:16)

Je ni halali kupiga kura kanisani kuchagua viongozi?

Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?

Je! tunapaswa kukiamini Kitabu cha Henoko?

Je! Bwana Yesu alisulubiwa juu ya msalaba au juu ya mti uliokuwa wima?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments