Wafilipi 4:8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.
Katika vifungu hivyo utaona neno “yoyote” limetumika sana. Ikiwa na maana yapo mengi, ya aina mbalimbali, ambayo hayajaandikwa hapo. Na hapo biblia inaegemea katika “yale yaliyo mema”.
Tukumbuke kuwa biblia haijaandika matendo yote mema mwanadamu anayopaswa kuyafanya. Kama ingekuwa hivyo basi kingekuwa ni kitabu kikubwa sana, ambacho hakuna mwanadamu yoyote angeweza kukimaliza kwa kukisoma. Lakini imetoa kama muhtasari tu, au mwongozo wa kufuata.
Kwamfano huwezi, kuona katika maandiko tunaagizwa ‘tuimbe kwaya kanisani’, lakini hayo ni moja na yenye kupendeza, au kuona tunaambiwa tuhubiri injili kwa njia ya maigizo. Lakini, tumebuni wenyewe na mwenye dhambi anapotizama filamu hizo, huwa inachangia katika kuwasogeza karibu kwa Kristo. Maadamu havitoki nje ya maudhui mema.
Au tunapotumia vipaza sauti, au tunaposambaza vipeperushi vya injili barabarani, huwezi ona agizo hilo, popote kwenye maandiko. Lakini ni moja ya yale yaliyo ya kweli.
Hivyo kwa hitimisho ni kuwa yapo mambo mengi ambayo tunaweza kuyafanya, na Bwana hatuzuii kuyatafakari, ndio maana akamalizia kwa kusema ‘yatafakari hayo’. Maana yake tutafiti na tutumie njia zote, ambazo tunaona hatma yake itakuwa ni kuujenga ufalme wa Mungu, au kuufanya upendeze zaidi.
Angalia katika ujuzi wako, angalia katika elimu yako, ni kwa namna gani utafanya jambo la ki-Mungu lenye kukuletea sifa njema kwake. Utumishi wa Mungu sio pale madhabahuni tu kuhubiri, utumishi wa Mungu ni mpana. Hivyo Hapo hapo ulipo tafakari ni kwa namna gani utaujenga ufalme wa Mungu wako, na Bwana atakupa akili njema.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mafundisho mengine:
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA TITO.
Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?
Mambo yale yaliyo mbali, na yale yaendayo chini sana,
NAFASI YAKO NI IPI KATIKA MWILI WA KRISTO?
Matulizo ya mapenzi ni nini? (Wafilipi 2:1).
Birika ni nini?, na yale Matao matano katika birika la Bethzatha ni nini?
About the author