Kutoka 14:13 “Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. 14 BWANA ATAWAPIGANIA NINYI, NANYI MTANYAMAZA KIMYA”.
Kutoka 14:13 “Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.
14 BWANA ATAWAPIGANIA NINYI, NANYI MTANYAMAZA KIMYA”.
Matokeo ya kupiganiwa na Bwana ni “Mwisho wa Manung’uniko, malalamiko, masononeko, huzuni na maumivu”.
Ndicho kilichowatokea wana wa Israeli pale walipoliona jeshi la Farao likija nyuma yao, na mbele yao kuna kizuizi cha bahari, (nyuma mauti inakuja, mbele mauti inawangojea).. wakaogopa mno na kupaniki na kuanza kumlaumu Musa, wakasahau mambo makuu waliyotendewa na Mungu masaa kadhaa na siku kadhaa nyuma, jinsi alivyompiga Farao kwa mapigo makuu.
Sasa ni rahisi sana kuwalaumu wana wa Israeli kuwa ni wajinga na wasiokumbuka!.. Lakini majaribu kama hayo hayo yanatukuta wengi leo na tunakuwa tunasahau fadhili za Mungu alizotutendea siku kadhaa au miaka kadhaa nyuma.
Hivyo unapotazama na kuona mauti mbele yako na nyuma yako unaona Giza, kiasi kwamba unajikuta unakosa utulivu na hata wakati mwingine kujiona upo katika hatari ya kutoa maneno mabaya kutoka katika kinywa chako… unapofikia hiyo hatua, basi huo si wakati wa kunung’unika, wala kulalamika, ni wakati wa wewe kumwomba MUNGU AKUPE UTULIVU.
Na unamwomba UTULIVU kwa wewe kumsihi asimame AKUPIGANIE VITA VILIVYOPO MBELE YAKO, Na ikiwa moyo wako umenyooka mbele zake basi utaona mkono wake akikupigania kama alivyowapigania waIsraeli NAWE UTAKAA KIMYA, ile huzuni itayeyuka, ile aibu itapotea, ile kiu ya kusema maneno mabaya na ya makufuru itayeyuka, nawe utajaa nyimbo za shangwe na sifa na shukrani kama wana wa Israeli walizoziimba baada ya bahari kupasuka na kuwameza maadui zao.
Kutoka 15:1 “Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia Bwana wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini. 2 Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. 3 Bwana ni mtu wa vita, Bwana ndilo jina lake. 4 Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini, Maakida yake wateule wamezama katika bahari ya Shamu. 5 Vilindi vimewafunikiza, Walizama vilindini kama jiwe. 6 Bwana, mkono wako wa kuume umepata fahari ya uwezo, Bwana, mkono wako wa kuume wawasetaseta adui. 7 Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokuondokea, Wapeleka hasira yako, nayo huwateketeza kama mabua makavu. 8 Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa, Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu, Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari. 9 Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara, Nafsi yangu itashibishwa na wao; Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza. 10 Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza; Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu”.
Kutoka 15:1 “Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia Bwana wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.
2 Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.
3 Bwana ni mtu wa vita, Bwana ndilo jina lake.
4 Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini, Maakida yake wateule wamezama katika bahari ya Shamu.
5 Vilindi vimewafunikiza, Walizama vilindini kama jiwe.
6 Bwana, mkono wako wa kuume umepata fahari ya uwezo, Bwana, mkono wako wa kuume wawasetaseta adui.
7 Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokuondokea, Wapeleka hasira yako, nayo huwateketeza kama mabua makavu.
8 Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa, Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu, Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.
9 Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara, Nafsi yangu itashibishwa na wao; Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza.
10 Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza; Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu”.
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Je Farao alikufa kwenye maji pamoja na jeshi lake au alipona?
KWANINI UBATIZO NI WA MUHIMU.
USIMWABUDU SHETANI!
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
Makasia ni nini? (Yona 1:13).
Rudi Nyumbani
Print this post
Samahani mtumishi, naomba kufahamu jambo moja tu. Haya masomo ni wewe umetunga au umeyaandika tu ni mtumishi mwingine
Ufunuo wa Neno unatoka kwa Roho Mtakatifu, na si katika tungo.. kwahiyo ni Roho Mtakatifu ndani yetu, na utukufu ni kwa BWANA YESU.