Arkipo ni nani katika biblia?

Arkipo ni nani katika biblia?

Arkipo ni mmoja wa wahudumu wa agano jipya. Ambaye alikuwa na ushirika wa karibu na mtume Paulo katika kazi ya kuieneza injili.

Paulo alipokuwa anamwandikia waraka Filemoni, anamtaja Arkipo kama ASKARI mwenzake.

Filemoni 1:1-2

[1]Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo aliye ndugu yetu, kwa Filemoni mpendwa wetu, mtenda kazi pamoja nasi, 

[2]na kwa Afia, ndugu yetu, na kwa Arkipo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako. 

Lakini pia katika waraka ambao Paulo aliundika kwa Wakolosai tunaona katika salamu zake za mwisho, anatoa agizo maalumu kwa mtu huyu kwa kumwambia, aiangalie sana huduma Ile aliyopewa na Bwana ili aitimize.

Wakolosai 4:17

[17]Mwambieni Arkipo, Iangalie sana huduma ile uliyopewa katika Bwana, ili uitimize. 

Kuonyesha kuwa alikuwa na sehemu ya huduma kwa hawa watakatifu wa Kolosai. Ijapokuwa biblia haijatueleza ni huduma ya namna gani.

Lakini ni kwanini amwambie vile?

Paulo anasisitiza kuwa huduma hiyo amepewa na Bwana, (ikiwa na maana si mwanadamu)..huwenda alidhani alichokirimiwa hakikuwa na msukumo kwa Bwana, ni yeye tu mwenyewe ameanza kukitenda..Au watu wamekipuuzia au kukiona cha kawaida, hivyo na yeye pia akakiona cha kikawaida, hakitakiwi kutiliwa mkazo sana.

Au Pengine Arkipo alipitia kuvunjwa moyo, au mashaka fulani, na hiyo ikampelekea kutowajibika vya kutosha katika nafasi yake.

Hivyo Paulo anamtia moyo kwa kumwambia huduma hiyo ni ya Mungu, hivyo hakikisha unaitimiza.

Ni lipi la kujifunza kwa Arkipo.

Hata sasa kila mtu aliyeokoka ni askari wa Bwana. Na hivyo amepewa huduma ndani yake, kufuatana na karama aliyokirimiwa ambayo anapaswa aiangalie na kuitimiza.

Kama askari wa Bwana ni lazima tufahamu kuwa tutakumbana na vita na kuvunjwa moyo, na kutaabishwa, na dhiki, na kupungukiwa, na taabu za namna mbalimbali lakini pia Raha katika huduma.

Kwa vyovyote vile Hatupaswi kupoa, au kulegea, au kuvinjika moyo. Bali tubakie tufahamu kuwa ipo siku tutatolea hesabu uwakili wetu.

Kama askari ya Kristo Timiza huduma yako

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mhunzi ni nani? (Isaya 54:16)

Mwandishi wa kitabu cha Filemoni ni nani?

Mwandishi wa kitabu cha Filemoni ni nani?

Kuwanda ni kufanya nini?

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments