Aristarko ni mmoja wa wahudumu wa injili katika agano jipya. Paulo anamtaja kama mtenda kazi pamoja naye (Filemoni 1: 24), wengine wakiwa ni Luka, dema, na Marko.
> Aristarko ni mmoja wa watu walioamini injili mahali palipoitwa Thesalonike, Paulo alipokuwa anahubiri, ambao kwa mioyo yao wenyewe wakaamua kuambatana na Paulo katika ziara zake za kuhubiri injili kwenye mataifa mengine.
Matendo ya Mitume 20:4
[4]Watu hawa wakafuatana naye, Sopatro Mberoya, mwana wa Piro, na Aristarko na Sekundo, watu wa Thesalonike; na Gayo mtu wa Derbe, na Timotheo; na Tikiko na Trofimo watu wa Asia.
> Kati ya watendakazi wa Paulo waliovamiwa na kundi la mataifa ( Paulo aliwaita hayawani wakali) kule Efeso, mmojawapo alikuwa ni Aristarko. Ijapokuwa biblia haituambii kama walipigwa au kuwajibishwa vikali…Lakini ni wazi kuwa walipitia dhiki na hwenda ilikuwa ni kupigwa kwelikweli.
Matendo ya Mitume 19:29
[29]Mji wote ukajaa ghasia, wakaenda mbio wakaingia mahali pa michezo kwa nia moja, wakiisha kuwakamata Gayo na Aristarko, watu wa Makedonia waliosafiri pamoja na Paulo.
> Aristarko anatajwa pia na Paulo kama mfungwa mwenza. Kuonyesha kuwa si tu alishiriki mapigo, bali pia na vifungo pamoja na Paulo, tangu kwenye safari yake akiwa kama mfungwa kuelekea Rumi, mpaka Rumi kwenyewe alipokuwa mfungwa kwenye nyumba yake mwenyewe.
Matendo ya Mitume 27:2
[2]Tukapanda katika merikebu ya Adramitio iliyokuwa tayari kusafiri mpaka miji ya pwani za Asia, tukatweka; Aristarko, Mmakedonia wa Thesalonike, akiwa pamoja nasi.
Wakolosai 4:10
[10]Aristarko, aliyefungwa pamoja nami, awasalimu; na Marko, mjomba wake Barnaba, ambaye mmepokea maagizo kwa habari yake; akifika kwenu mkaribisheni.
Kwa ufupi, tunaweza jifunza mengi kwa watendakazi kama hawa, ambao walikuwa washirika wenza wa Paulo. Kwanza kwa kujitoa kwao kwa hiari kuitumikia injili. Lakini kuzidi kuwa thabiti hata katika mapigo na vifungo bila kuikana imani. Kwamfano tunapoisoma ile safari ya Paulo kama mfungwa kuelekea Rumi jinsi walivyopitia majanga makubwa baharini, mpaka wakakata tamaa ya kuishi, huyu aristarko alikuwa pia katika dhoruba ile.
Kufanikiwa kwa huduma ya mtume Paulo ni kwasababu ya mashujaa kama hawa walioisimama pamoja naye katika nyakati zote.
Bwana awanyanyue wakina Aristarko wengi, kwenye makanisa yetu na huduma zetu. Ili injili ya Bwana ifike na kuenea kiwepesi ulimwenguni kote.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Ndugu Yule anayezungumziwa kwenye 2Wakorintho 8:18 ni nani?
Sosthene ni nani katika biblia? (Matendo 18:17)
Mchuuzi ni nani? (Hosea 12:7).
MIMI NA WEWE TU KAZI YA MUNGU.
Rudi Nyumbani
About the author