SWALI: Je mtu anaweza akawa hajaokoka akaombea mtu na Pepo likamtoka, na pia mtu anaweza akawa ameokoka akaombea mtu na pepo lisitoke ?
JIBU: Kuhusu swali la kwanza linalosema je mtu anaweza akawa hajaokoka kisha akaenda kuombea mtu mwenye pepo na hatimaye likamtoka?
Jibu ni la!, haiwezekani mtu ambaye hajaokoka, akawa na uwezo wa kutoa pepo, kwasababu pale alipo yupo chini ya vifungo vya ibilisi, haiwezekani akaenda kumfungua mtu ambaye ni mfungwa mwenzake, inahitaji mtu aliye huru ndio aweze kufanya hivyo.
Bwana Yesu alisema…
Marko 3:23-27
[23]Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumtoa Shetani?
[24]Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama;
[25]na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba hiyo haiwezi kusimama.
[26]Na kama Shetani ameondoka juu ya nafsi yake, akafitinika, hawezi kusimama, bali huwa na kikomo.
[27]Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake.
Ni hatari huyo mtu akijaribu kufanya hivyo, kwasababu anaweza kukutana na madhara kama yaliyowakuta wale wana wa Skewa.(Matendo 19:13-16).
Kuhusu swali la pili linalouliza Je mtu ambaye ameokoka anaweza akaombea na pepo lisitoke?
Jibu ni ndio Ikiwa mtu huyo anakiwango kidogo cha imani, si mapepo yote yanaweza yakatoka, kwasababu mashetani yanatofautiana kimadaraja (Mathayo 12:43-45), yapo yenye nguvu kubwa ya ukinzani, mengine huitwa wakuu wa giza, mengine wafalme na wenye mamlaka. (Waefeso 6:12)
Hivyo inahitaji nguvu zaidi za kiimani ambazo zinakuja kwa njia ya mifungo na maombi.
Ndio maana mitume kuna mahali walitoa kweli pepo wengi lakini kuna mahali hawakuweza kwasababu ya uhaba wa maombi. (Mathayo 17:14-21)
Lakini uhalisia ni kuwa mtu yeyote aliyeokoka, haijalishi amedumu sana katika wokovu au ni mchanga. Anayo mamlaka ndani yake ya kutoa pepo lolote lile, isipokuwa anahitaji pia na maombi ile mengine yasishindikane kwake.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
About the author