Zawadi kubwa na ya kipee alipewa mwanadamu na Mungu, iliyomtofautisha na viumbe vingine vyote, (vya mbinguni na duniani) basi ni Uso wa Mungu.
Ni mwanadamu pekee ndiye aliyeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu (Mwanzo 1:27-28).
Biblia inaposema sura, inafananisha na mfano wa kioo, pale mtu anapojitazama kwenye kioo, anaiona taswira yake vilevile kama yeye alivyo, ikiwa ni mwenye chunusi, basi ataiona chunusi yake kwenye kile kioo, ikiwa ni mweupe vivyo hivyo ndivyo atakavyojiona.
Kwahiyo sisi ni taswira ya Mungu kabisa, lakini ifahamike kuwa taswira hiyo sio hii ya nje, yaani pua, mdogo, masikio, hapana bali ile ya ndani, yaani tabia na sifa alizonazo Mungu, sisi pia tunazo.
Sasa kazi kubwa ya shetani, aliyokuwa nayo kwa Mwanadamu ni kumbadilisha SURA yake. Ili ifanane na kitu kingine tofauti na Mungu.
Na alijua njia pekee na kubwa ambayo hubadili taswira ya mtu, ni IBADA.
Yaani kile ambacho mwanadamu anakiabudu basi moja kwa moja hufanana nacho, wala si kile anachokitazama, au anachokishika, au anachokiangalia Hapana bali kile akifanyiacho ibada, moja kwa moja kinambadilisha taswira yake.
Ndio maana amri ya kwanza na ya pili ambayo Mungu aliwapa watu wake (Kutoka 20), ni kuhakikisha hawajifanyii sanamu ya kuchonga ya aina yoyote na kuiabudu, wala hawawi na miungu mingine, ila yeye.
Kwanini? Kwasababu wamwabudupo yeye, hudumisha tabia zake, na mwonekano wake ndani yao.Lakini wanadamu walipoanza kuabudu miungu, mfano wa Baali, Arishtoreth, n.k. hawakujua kwamba moja kwa moja wanafanana nazo.
Zaburi 115: 4-8
4 Sanamu zao ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu. 5 Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni, 6 Zina masikio lakini hazisikii, Zina pua lakini hazisikii harufu, 7 Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi, Wala hazitoi sauti kwa koo zake. 8 WAZIFANYAO WATAFANANA NAZO, Kila mmoja anayezitumainia
Maandiko yanasema hapo, wazifanyao, hufanana nazo, maana yake Walikuwa vipofu rohoni, viziwi rohoni, wamepooza, kabisa, hawana uhai, ndio maana hata walipokuwa wakihubiriwa Habari za hukumu na manabii hawakuelewa wala kuona ni kitu, hata Kristo alipokuja duniani bado hawakutambua wakati wa kujiliwa kwao, sio kwamba walikuwa wanafanya makusudi, lakini ni kwasababu waliabudu miungu isiyo hai, waliabudu mashetani yasiyojua kesho yao itakuwaje, mizimu isiyojua amani ya kweli ina Ladha gani, mapepo yasiyoweza kuganga mioyo ya watu, mwishowe wakafanana nao, wakawa wakatili, wauaji, wenye wivu .
Lakini tunaposoma biblia tunadhani sanamu ziliabudiwa zamani tu, Hapana, hata sasa sanamu zipo, ambapo zinawakilishwa na vitu vyote vinavyochukua nafasi ya Mungu katika mioyo ya wanadamu.
Fedha, ni sanamu, ukiiabudu ujue utafanana nayo, simu/TV yaweza kuwa sanamu, inapochukua muda wako mwingi, kutazama maudhui zake, na kuacha kabisa kumtafuta Mungu, umeshakuwa mfu hata kama unatembea, mtu anaweza kuwa sanamu, unapomtegemea yeye zaidi ya Mungu, hapo hesabu umelaaniwa.
Lakini unapomwabudu Mungu, yaani unapomtegemea, unapomtii, unapomtumikia, unapomsujudia, ufahamu kuwa ndivyo unavyofanana na yeye, na hatimaye utakuwa hai kama yeye alivyo hai, sikuzote. Mungu anaishi milele, na wewe vivyo hivyo, Mungu ni mweza, na wewe utakuwa vivyo hivyo, Mungu ni mwenye upendo na wewe utakuwa kama yeye.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
KUSUDI LA MUNGU NYUMA YA SAFARI.
AINA ZA FARAJA BWANA AZIACHILIAZO KWA WATUMISHI WAKE.
MTU WA NNE, ANADHIHIRISHWA KWA MOTO
Print this post
Moja ya ombi kubwa la watu wa Mungu, pale wanapojikuta wameokoka, ni kubadilishwa mazingira waliyopo, wapelekwe kwenye mazingira mengine yenye uwepo wa karibu zaidi na Mungu, Kwasababu wakiangalia kwa sehemu kubwa mambo ambayo yanawakosesha huchangiwa na mazingira yao. Mazingira husika yanaweza kuwa mitaa wanayoishi, shule wanazosoma, maeneo ya kazi/ biashara walipo, watu wanaowazunguka, hata nchi yanayotokea.
Hii ni hali ya kawaida, na hufikia hatua wengi kuwaza mioyoni mwao, “Kama ningekuwa eneo Fulani, basi ningekuwa na mahusiano ya karibu na Mungu, ningekuwa mwombaji sana, ”
Lakini Je! Kuwaza hivyo ni sahihi?
Ndio kuwaza kubadilishwa mazingira yanayokosesha, ni vema, lakini kuwaza kuwa Hapo ulipo huwezi kumpendeza Mungu kwa viwango vyote ni uongo,. Kwasababu maandiko yanatuonyesha Mungu amewaweka watumishi wake katika mazingira yote, yaani mazingira rafiki na yale yasiyo rafiki, kwa mapenzi yake, na kuthibitisha kuwa kote kote, kumpendeza Mungu kunawezekana. Kwasababu dunia moja.
Bwana aliwaweka watakatifu Babeli, alikuwepo Shedraka, Meshaki, Abednego na Danieli.
Hawa waliishi katika taifa la kipagani usiokuwa wa kawaida,ni taifa lenye shinikizo kubwa la mtu kuabudu miungu hata kama hapendi, lenye mikorogo ya kila namna ya maovu. Lakini watu hawa walisimama vema na Bwana.
Waliwezaje?
Yafuatayo ni mambo ambayo yaliyatenda mpaka ufanikiwa kuishi katika viwango vyote vya ukamilifu.
1) Waliitangaza Imani yao mapema.
Mwanzoni kabisa akina Danieli walipochukuliwa Babeli, na kusomeshwa elimu ya wakaldayo,tunaona walipewa vyakula ambavyo ni najisi, lakini Danieli alisimama mapema na kumwomba msimamizi, kulishwa vyakula vingine visivyo najisi. Na Mungu akawa Pamoja nao. Wakatambulika tangu mapema kuwa wao ni watumishi wa wayahudi wasiojichangamana na desturi za kimataifa.
Hawakungoja, miaka ipite baadaye..bali mezani tu, wanaanza kutangaza misimamo yao.
Danieli 1:8-9
[8]Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi. [9]Basi Mungu alimjalia Danieli kupata kibali na huruma machoni pa huyo mkuu wa matowashi.
[8]Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi.
[9]Basi Mungu alimjalia Danieli kupata kibali na huruma machoni pa huyo mkuu wa matowashi.
Hii ni desturi ambayo na sisi, kama watoto wa Mungu babeli, tuwapo katikati ya wasioamini, tujitambulishe mapema. Hiyo itasaidia sana wao kutokukuhusisha katika matendo yao ya giza wakijua kuwa wewe ni mwamini.
Wengi wameshindwa kung’atuka katika mazingira mabovu kwasababu ya kushindwa kujitambulisha wao ni akina nani, kwa wanaowazunguka.
2) Walikuwa waombaji
Danieli akiwa Babeli, alijijengea desturi na kutwa mara tatu, kupiga magoti na kuomba, akijua kuwa nguvu ya kusimama na kuendelea mbele ilitegemea sana maombi…
Ijapokuwa alikuwa na majukumu makubwa kama waziri katika taifa lakini hakuruhusu muda wake mahususi wa maombi kuibwa.
Danieli 6:10
[10]Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
Vivyo hivyo na sisi tuwapo popote pasipofaa, hatuwezi sema hatuna muda wa sala. Ikiwa umebanwa upo muda wa chakula cha mchana kazini unaweza tumika nafasi kusogea mahali tulivu na kuomba.
3) Walikubali kujitwika misalaba yao.
Kujitwika msalaba maana yake ni kukubali kuipokea imani kwa gharama yoyote ile, yaani kama ikitokea nitatengwa kwasababu ya imani yangu, nitafungwa, nitauawa..Je nipo tayari?
Ndivyo ilivyokuwa kwa Meshaki, shedraka, Abednego, Danieli, Yusufu.
Wote hawa walikubali kutupwa kwenye matanuru ya moto, kwenye magereza, matanuru ya simba, walipojaribiwa.
Vivyo hivyo na sisi, lazima tufahamu mapema kuwa, imani haipendwi, ulimwengu sio rafiki kwetu, kama ikitokea tunalazimishwa kuikana imani je! Tutachukua hatua gani?
Wengine wameshindwa na majaribu mbalimbali ya Babeli, wameanguka katika uzinzi,wizi, upagani kwa sababu tu ya kuhofia kupoteza kazi zao, familia zao, heshima zao, mali zao, uhai wao.
Ili uweza kuishi vema Babeli, ufahamu huu wa kujitwika msalaba ni lazima uwe nao tangu mwanzo kabisa wa kuamini kwako. Kumbuka sikuzote nguvu ya kuushinda ulimwengu upo katika msalaba.
4) Waliwajibika kwa bidii na uaminifu.
Utaona hawakuwa wavivu, au walegevu, au watu wasiokuwa na shughuli zao maalumu, bali waliwajibika..Danieli pamoja na wenzake walisoma ili kupata elimu na kuwajibika katika shughuli za kifalme mpaka wakaonekana hakuna wa kufanana na wao kwa hekima na ujuzi,
Yusufu naye alisimama kwenye majukumu yake, wala hakuna mahali alionekana mlegevu. Na wote hawa walitanguliza uaminifu.
Walijua kabisa kutowajibika ni mlango mwingine wa shetani, kuinua majaribu.
Waefeso 4:27-28
[27]wala msimpe Ibilisi nafasi. [28]Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.
[27]wala msimpe Ibilisi nafasi.
[28]Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.
Hivyo na sisi pia tuwapo kwenye Babeli zetu, tuwe makini kuwajibika kwa bidii na uaminifu, tuepuke uvivu, kama watoto wa Mungu ni wajibu kujishughulisha.
Tukifanikiwa kuwa na uwiano huo mzuri, Neema ya Mungu itatusaidia.
MNARA WA BABELI
Ipi tofauti ya Falme, Mamlaka na Wakuu wa giza (Waefeso 6:12)
KWA KUWA FURAHA YA BWANA NI NGUVU ZENU.
Chanzo kibaya, Haimaanishi mwisho mbovu, chanzo chaweza kuwa bora lakini mwisho ukawa mbovu, Vilevile chanzo chaweza kuwa kibovu, mwisho ukawa mzuri.
Moja kati ya watu waliofanya uasi mkubwa mpaka Mungu akawaangamiza kwa kuwashusha kuzimu moja kwa moja wakiwa wazima, basi alikuwa ni Kora na jamii ya watu wake.
Ni mtu ambaye anatajwa hata baadaye katika agano jipya (Yuda:1:11), kama kielelezo akifananishwa na watu waasi waliopotoka wa siku za mwisho, kwasababu ya maasi yake kuwa makubwa yenye kuambukiza.
Hesabu 16:31-33
[31]Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka; [32]nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote. [33]Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni.
[31]Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka;
[32]nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote.
[33]Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni.
Lakini ijapokuwa wazazi walifanya vibaya…watoto hawakufuata njia za baba yao (Hesabu 26:11)
Kinyume chake baadaye tunaona wazao wa kora wakaambata na Bwana kwa bidii mpaka wakawa sehemu takatifu ya Mungu, yaani waimbaji wa hekaluni.
Nafasi iliyo takatifu sana.
1 Nyakati 6:31–38,
Wengine wakawa wafungua malango ya nyumba ya Mungu (1 Nyakati 9:19)
Na Kama hilo halitoshi Sehemu nyingi za Zaburi zilitungwa na wana wa Kora. Mfano wa hizo ni
(Zaburi 42, 44, 45, 46, 47, 48, 49, 84, 85, 87, 88).
Huu ni mchango mkubwa sana kwenye ufalme wa Mungu. Ambao mpaka sasa tunakula matunda yake.
Lakini si rahisi kukubali kama hao ni wana wa mtu mwasi Kora. Ni sawa na leo usikie wana wa Yezebeli ni manabii wa Bwana.., wana wa Elima-mchawi ni mitume wa Kristo.
Tufahamu kuwa rehema za Mungu, haziathiriwi na asili, au mwanzo mbovu. Maadamu moyo umegeuka kweli kweli, Bwana huanza historia mpya.
Hapo mwanzo uliitwa Kora lakini leo ukigeuka utaitwa Musa, uliitwa Sauli leo utaitwa Paulo.
Sahau yaliyopita, anza ukurasa mpya na Bwana. Wazazi wako walikosea, hata na wewe mwenyewe ukakosea, ukapata sifa mbaya, ukawa kama mfu, . LEO HII, kubali toba ya kweli, uwe kiumbe kipya, ukubaliwe na Bwana, upendwe na Bwana, utumiwe na Bwana, hata kama una asili ya sifa mbaya.
Je upo tayari leo kukata shauri kwa kutubu na kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yako?
Kama ndio basi hapo ulipo piga magoti kisha sema sala hii kwa imani kutoka moyoni ukimaanisha kabisa kutaka ukombozi wa nafsi yako leo. SEMA;
“Bwana Yesu, asante kwa upendo wako mkuu, kwa kuja duniani kunikomboka maisha yangu, katika dhambi na hukumu. Leo hii nimeamini kwa moyo wangu wote, na kupokea msamaha wa dhambi upatikanao kwa dhabihu ya damu yako takatifu. Kuanzia leo mimi ni mwana wa Mungu, nimemkataa shetani na kazi zake zote. Karibu Roho Mtakatifu ndani yangu. Ufanye makao yako sasa, nitembee kwa nguvu zako, na kukutumikia. Nimeomba nikiamini katika jina la Yesu Kristo.
Amen
Mpaka hapo utakuwa umepokea msamaha wa dhambi, hivyo hatua zinazofuata na malezi ya kiroho ili umjue Mungu, ukue kiroho, Na ubatizo ikiwa bado hujabatizwa.
Kwa mawasiliano.
Piga namba hizi : +255789001312 / +255693036618
Lakini tembelea tovuti yetu yenye mafundisho mengi zaidi ya elfu tano (5000), upate kujifunza kufuatana na mada mbalimbali za kiroho.
Mungu akubariki.
ashirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Swali: Ubatizo ni kitendo cha kuzama kwenye maji na kuibuka juu ambacho ni kiashirio cha kufa na kufufuka pamoja na YESU kiujumla ni kuwa Mpya, je mfano umeokoka halafu ukaenda mtoni peke yako kwa Imani ukazama wewe mwenyewe na kuibuka juu je ubatizo huo utakuwa batili?
Jibu: Tukirejea ubatizo wa Bwana YESU tunaona ilimpasa aende Yordani akabatizwe na Yohana, kulikuwa na uwezekano wa Bwana YESU kutokwenda kabisa kubatizwa na Yohana na akaenda mwenyewe majini.. lakini ilimpasa aende kwa lengo la kutufundisha sisi…
Mtu anapobatizwa ni ishara ya kuzaliwa (soma Yohana 3:3-5)
Yohana 3:3 “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA MARA YA PILI, HAWEZI KUUONA UFALME WA MUNGU.
4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO, HAWEZI KUUINGIA UFALME WA MUNGU”.
Sasa kwa kawaida “hakuna mtu anayeweza kujizaa mwenyewe”.. maana yake hakuna mtu asiye na baba au mama.. kila mtu ni lazima awe na wazazi wawe wema au wabaya.
Na kwa mantiki hiyo hiyo mtu anayejibatiza mwenyewe ni sawa na amejizaa mwenyewe, jambo ambalo haliwezekani.
Kwahiyo ni lazima mtu akabatizwe na mwingine aliyemtangulia kiimani, ambaye ndiye atakayesimama kama mzazi wake wa kiroho kwa wakati huo.. na si sahihi mtu kujibatiza mwenyewe na pia kwenye Biblia hapaoneshi mahali popote kuna mtu aliyejibatiza bali wote walibatizwa na wengine waliowatangulia kiimani, kuanzia Bwana wetu YESU KRISTO na mitume wote na watu wote (soma Yohana 3:13-17, Matendo 9:17-18, Matendo 8:12-14, Matendo 19:1-5).
Na Bwana mwenyewe pia alitoa agizo kwa mitume kwamba wakawabatize watu na si watu wakajibatize wenyewe (Mathayo 28:19).
Kwahiyo kwa hitimisho si sahihi kujibatiza, na pia ubatizo ni lazima kwa kila mwamini, na ni lazima uwe ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU KRISTO (Matendo 2:38)
Jina la Bwana YESU libarikiwe.
Tusomapo habari ya safari ya Wana wa Israeli kutoka Misri kuelekea Kanaani, tunajifunza mengi sana, lakini leo nataka tuangalie funzo moja la msingi sana.
Katika safari ile tunaona Mungu aliipiga Misri kwa mapigo kumi (10), ambayo ni mainzi, vyura, chawa, maji kuwa damu, mvua ya mawe, nzige, majipu, tauni, giza siku tatu na kufa kwa wazaliwa wa kwanza.
Kwa mapigo hayo, Misri iliharibika sana, iligeuka kuwa jangwa lisilo na mmea hata mmoja, nan chi ya magonjwa pamoja na misiba..mpaka waMisri wakakiri kabisa kuwa wamekwisha wote..
Kutoka 10:7 “Ndipo watumishi wa Farao wakamwambia, Mtu huyu atakuwa tanzi kwetu sisi hata lini? Wape hawa watu ruhusa waende zao, wamtumikie Bwana, Mungu wao; HUJATAMBUA BADO YA KUWA MISRI IMEKWISHA HARIBIKA?”
Kutoka 10:13 “Basi Musa akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya Misri, na Bwana akaleta upepo kutoka mashariki juu ya nchi, mchana kutwa, na usiku kucha; kulipopambazuka ule upepo wa mashariki ukawaleta nzige.
14 Na hao nzige wakakwea juu ya nchi yote ya Misri, wakatua ndani ya mipaka yote ya Misri, WALIKUWA WABAYA MNO; HAWAJAKUWAPO NZIGE KAMA HAO MAJIRA YO YOTE, WALA BAADA YAO HAWATAKUWA WENGINE JINSI HIYO.
15 Kwa kuwa waliufunika uso wote wa nchi, hata nchi iliingia giza; wakala mimea yote ya nchi, na matunda yote ya miti yaliyosazwa na ile mvua ya mawe; HAPAKUSALIA HATA JANI MOJA, MTI WALA MMEA WA MASHAMBA, KATIKA NCHI YOTE YA MISRI”.
Kutoka 12:33 “Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, TUMEKWISHA KUFA SOTE”.
Sasa mbali na kwamba MUNGU alifanya vile kuonesha uweza wake kwa Farao na kwa wana wa Israeli, lakini pia kusudi lingine la kuiharibu nchi ya MISRI, ni kuzuia au kuondoa HAMU ya wana wa Israeli kurejea MISRI.
Naamini kabisa kuwa endapo MISRI ingeachwa katika hali yake ya kustawi, yenye nafaka na uchumi kama mwanzo, ni hakika kuwa wana wa Israeli wangemsumbua sana MUSA katika safari ile na wengi wao wangerudi Misri baada ya kuona lile jangwa,
Lakini MUNGU alitangulia kuiharibu Misri kukawa hakuna chakula tena nyuma, wala maisha, hivyo ile hamu ya kuendelea kukaa Misri, haikuwepo tena kwa wana wa Israeli katika ile hatua ya kwanza, watakaaje kwenye nchi ambayo makao yake makuu hakuna mmea uliosalia?..
Kama tu katika hali hiyoya kuharibika bado wana wa Israeli walikuwa na vipindi vya kumtishia Musa kurudi Misri, vipi kama Misri ingekuwa bado ina ustawi ule ule, si ndio kabisa wasingevuka shamu?.
Kwahiyo tunachoweza kujifunza ni kuwa MUNGU anapoharibu mambo tuliyoyaacha nyuma wakati mwingine ni kwa faida yetu, kwamba tusitamani kurudia mambo ya nyuma..
Ukiona Mungu anakuharibia network zako za kazi haramu ulizokuwa unazifanya jua ni kwa faida yako, ukiona Mungu anakuondolea baadhi ya watu waliokuwa rafiki zako wakati upo Misri, fahamu kuwa ni kwa faida yako.
Ukiona watu uliokuwa unawategemea kipindi uko Misri, wanaanguka au wanashuka chini, ni kwa faida yako, ili kusudi wewe usirudi kuwatumainia baada ya kuanza safari yako ya kwenda mbinguni.
Ukiona shirika au kampuni ulilokuwa unalitegemea limeanguka baada ya wewe kuanza safari ya wokovu, usiogope na kujiona kuwa una bahati mbaya, fahamu kuwa ni kwa faida yako, usirudi nyuma wala usiweke tegemeo kwa wanadamu.
Endelea mbele katika imani, wala usitazame uharibifu unaendelea huko nyuma ulikotoka..fahamu kuwa wingu la Bwana litakuwa nawe kukuongoza na kukufikisha kule alikokusudia ufike.
Kamwe usirudi Misri, na Bwana akusaidie.
Mafanikio ni kitendo cha mtu kufanikisha jambo lolote aliloliadhimia liwe baya au zuri.
Mtu aliyedhamiria kununua shamba na akanunua, mtu huyo kafanikiwa (anayo mafanikio katika eneo hilo).
Vile vile mtu aliyedhamiria kufanya mambo mabaya mfano zinaa au ufisadi na akafanikiwa kufanya hivyo pia ana mafanikio, isipokuwa mafanikio yake hayo mwisho wake ni mbaya (yatamwangamiza).
Mithali 1:32 “Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, NA KUFANIKIWA KWAO WAPUMBAVU KUTAWAANGAMIZA”.
Lakini Baraka ni thawabu pekee itokayo kwa Mungu na kumfikia mtu akiwa hapa duniani, na hakuna baraka yoyofe inayoweza kumfikia mtu mbaya,
Tofauti na mafanikio ambayo hata mtu mwovu anaweza kuyapata, kwani hata shetani ana mafanikio ja utajiri lakini hana baraka yoyote, kinyume chake amelaaniwa.
Lakini baraka za MUNGU, ni kwa watu waliokubaliwa na MUNGU, na matokeo ya baraka za MUNGU pia ni mafanikio.
Na zipo aina kuu mbili za Baraka, ambazo ni baraka za rohoni na za mwilini.
Baraka za rohoni ni zile zinazotajwa katika Waefeso 1:3..
Waefeso 1:3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo”
Baraka za rohoni matunda yote ya Roho mtakatifu mtu anayoyapata baada ya kupokea wokovu, ambayo tunayasoma katika Wagalatia 5:22.
Na pia zipo baraka za mwilini, haya ni mafanikio katika afya na vitu vya ulimwengu huu (yaani mali).
Kumbukumbu 28:8 “BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako”.
Watu waliompokea YESU, wanayo ahadi ya baraka zote za rohoni na mwilini, ambazo ndani yake yapo mafanikio ya kiMungu.
Kwahiyo kwa hitimisho tunachotakiwa kukitafuta zaidi ni Baraka za MUNGU, na si mafanikio tu..kwani tukizipata baraka za MUNGU ndani yake pia kuna mafanikio.
Bwana atusaidie.
Jina la Bwana YESU KRISTO libarikiwe daima.
Karibu tujifunze Biblia,
Je unajua ni kitu gani kilichotukuka sana kwa MUNGU?.
Hiko si kingine zaidi ya jina lake, tangu enzi MUNGU amekuwa akijitambulisha kwa JINA na si SURA.
Ndio maana katika ile sala ya Bwana, inaanza na “Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe”..ndipo maombi mengine yafuate (Mathayo 6:9).
Na hata Bwana wetu YESU aliomba hivyo..
Yohana 12:28 “Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena”.
Na kila kitu tunafanya kwa jina la MUNGU na si kwa sura ya MUNGU. ( Wakolosai 3:17).
Kwahiyo jina ni kitu kilichotukuka sana, lakini sasa inapotokea jina la mtu au watu linapoinuliwa zaidi ya jina la MUNGU, ni jambo linaloleta Wivu mkubwa kwa MUNGU wetu soma (Kutoka 34:14).
Ndilo kosa walilolifanya watu wa Babeli..walipojenga mji na mnara ambao lengo lake ni kujijengea jina, na wala si kumjengea Bwana jina.
Mwanzo 11:4 “Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, TUJIFANYIE JINA; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote
15 BWANA akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu”.
Kama umempokea YESU yoyote uyafanyayo yafanye kwa utukufu wa jina la MUNGU na si wa jina lako.
Biashara yako iwe kwa utukufu wa jina la Bwana zaidi ya utukufu wako, watu wakiona kustawi kwako walitukuze jina la MUNGU wako na si jina lako.
Watu wakiona mwenendo wako jina la MUNGU wako litukuzwe na si litukanwe.
2 Wathesalonike 1:12 “jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani yenu, nanyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo”.
Tukienda kwa kanuni hiyo tutafanikiwa sana kiroho..
Maran atha.
Jina la Bwana YESU libarikiwe, karibu tujifunze Biblia, na leo tutajifunza umuhimu wa kuongeza nguvu za rohoni.
Biblia inasema…
Mithali 24:10 “Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache”.
Kuzimia kunakozungumziwa hapo ni ile hali ya kuzidiwa mpaka kufikia hatua ya kukata tamaa kabisa.
Kwa asili watu tuliompokea YESU hatujakusudiwa kuzimia wakati wa tabu.
Kwani tabu ni kama upepo kwa tiara, tiara inapokabiliana na upepo ndivyo inavyoruka juu zaidi.
Kama umeokoka na unaona dalili ya kuzimia au kukata tamaa au kuanguka kabisa unapokutana na tabu, ni ishara tosha kuwa nguvu zako za kiroho zipo chini.
Lakini kama changamoto na tabu kwako si kitu, na wala hazikuyumbishi..bali unasimama na kuendelea mbele kwa ushindi basi wewe nguvu zako za rohoni ni kubwa, shika sana ulicho nacho.
Sasa ikiwa umejigundua kuwa nguvu zako za rohoni ni chache, nataka nikuambie kuwa inawezekana leo hii kuzipandisha, ikiwa utakubali kufanya mambo macheche yafuatayo..
Lakini kabla ya kuyatazama mambo hayo naomba kwanza tusome andiko lifuatalo..
Isaya 40:29 “Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo”.
Kama huna nguvu ya kusimama, bali umechoka na unakaribia kuzimia kutokana na hali unazozipitia, hili ni neno lako.
Hapo ulipo piga magoti, omba toba ya kumaanisha kabisa, kisha dhamiria kutafuta ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU (Matendo 2:38), hapo Roho Mtakatifu atakuja juu yako, na kukuongezea nguvu katika nyakati zote na vipindi vyote.
Pia zingatia kuwa na vipindi vya maombi binafsi kila siku, na vipindi vya maombi ya mkesha.
Ufunuo 2:26 “Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,
27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.
28 Nami NITAMPA ILE NYOTA YA ASUBUHI”.
Je unaijua nyota ya ASUBUHI nini?
Hii si nyingine zaidi ya YESU KRISTO mwenyewe.
Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile NYOTA YENYE KUNG’AA YA ASUBUHI”.
Ahadi ya kuishi na YESU milele ni ahadi kuu sana, ni furaha isiyo na kifani kuishi na YESU milele.
Ni furaha isiyo na kifani kumtazama milele yeye aliyemwaga damu yake pale msalabani kwaajili yetu sisi tusiostahili.
Lakini ni hasara kubwa sana kukosa kuwa na YESU milele. Ndio maana katika kitabu hiko cha Ufunuo Bwana YESU mwenyewe anasema yeye ashindaye atampa “Ile nyota ya asubuhi”.
Maana yake yeye atakayeshinda atakaa na YESU milele.
Je umempokea YESU?.. Je una uhakika kwamba atakaporudi utakwenda naye mawinguni na kukaa naye milele?.
1 Wathesalonike 4:17 “Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo TUTAKUWA PAMOJA NA BWANA MILELE”.
Kama bado mpe leo YESU maisha yako kwa kutubu na kubatizwa kwa maji na kwa Roho Mtakatifu.
Shalom.
Yuda 1:7-8
[7]Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele. [8]Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili uchafu, hukataa kutawaliwa, na kuyatukana matukufu.
[7]Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.
[8]Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili uchafu, hukataa kutawaliwa, na kuyatukana matukufu.
Maandiko hayo, yanazunguzia tabia ya watu waasi ambao wameshaijua kweli lakini wamependa kuendelea katika dhambi zao.
Hivyo katika andiko hilo anasema katika kuota kwao huutia mwili uchafu…sasa huko kuota kunakozungumziwa hapo sio ile hali ya kulala na kuota ndoto…hapana bali ni maono yao, yaani ndoto zao za jinsi watakavyokuwa baadaye, namna wanavyojiona baadaye..sasa hiyo namna ndio sio nzuri bali ni ya kujitia mwili uchafu.
Kuutia mwili uchafu ni ile hali ya kuruhusu matendo yote ya mwilini kukutawala…matendo hayo yanazunguziwa vema katika Wagalatia 5:19-21
[19]Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, [20]ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, [21]husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
[19]Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
[20]ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
[21]husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Haya ndio watu wanayoyaona mbele yao, wanayoyawaza na kuyatazamia wakati wote, wanayoyaota yaje kutokea..
Fikra za watu wengi leo ni ili baadaye waishi kiasherati, wafanye anasa kwa pombe, ulafi, waibe..
Hii ni kutufunulia pia kunajisika sio mpaka mtu akatende jambo lenyewe bali ile kulitamania, tu au kulitarajia mbeleni…tayari ameshajinajisi.
Jiulize kuota kwako ni kupi? Kama mtoto wa Mungu, lazima tujue sisi yatupasa kuota maendeleo ya kazi ya Mungu, kuota ukuaji wa kiroho, kuota upendo, kuota kuingia mbingu mpya na nchi mpya,..namna hiyo humfanya mtu kuendelea katika utakaso.
Yuda alimaanisha nini kusema “wokovu ambao ni wetu sisi sote”
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 13 (Kitabu cha Hosea).