Kama wewe ni msafiri utakuwa umegundua kuwa nyasi zilizopo katikati ya barabara zenye vumbi huwa haziathiriwi na tairi za gari.
Utakuta barabara inapitiwa kila siku na magari yenye tairi zenye nguvu na nzito lakini katikati ya barabara utaona mstari wa nyasi, zilizo salama kabisa.
Ikifunua kuwa si kila kilichopo katikati ya hatari kipo hatarini, kuna watu wanaonekana kama wapo katikati ya changamoto na hatari nyingi lakini wapo salama, na kuna wengine wanaonekana kama wapo pembezoni (mahali salama) lakini ndio wapo hatarini.
Watu waliosimama kweli na YESU, wanaonekana ambao hawasogezi mguu wao kulia wala kushoto, ni watu wanaoonekana wamwisho kabisa duniani, na wenye wanaopotea, watu waliojikana nafsi kwaajili ya YESU ni watu wanaonekana wamepotea,
Watu wanaotukanwa, na kudhalilika kwaajili ya misimamo yao ya kiimani wanaonekana kama wamepotea lakini ukweli ni kwamba wao ni mfano wa nyasi zilizopo katikati ya barabara, hazikanyagwi wala kuathiriwa na tairi za magari.
Siku zote wanasimama na Zaburi 23..
Zaburi 23:1 “BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji”
Kama ulikuwa unasuasua katika Imani na Wokovu, huu ni wakati wako wa kusimama katika njia kuu.
Simama kwa imani na tembea kwa ujasiri katikati ya njia yako ya wokovu, usisogeze mguu wako kushoto wala kulia nawe utakuwa salama, na utaona wema wa MUNGU.
Mithali 4:25-27 “Macho yako yatazame mbele.
26 Ulisawazishe pito la mguu wako, Na njia zako zote zithibitike;
27 Usigeuke kwa kuume wala kwa kushoto; Ondoa mguu wako maovuni”.
Vile vile kama bado haujaokoka, fahamu ya kuwa hizi ni siku za mwisho, na Bwana amekaribia sana kurudi. Na upendo wake kwako ni ule ule usio na mwisho,
YESU anawapenda watu wote wa kike na kiume, wakubwa kwa wadogo, walio na maradhi na wenye afya, wenye uwezo na wasio na uwezo,
Maandiko yanasema kwa moyo mtu huamini hata kupata Haki na kwa kinywa hata kupata wokovu.(Warumi 8:9-10).
Leo hii mwamini moyoni na mkiri kinywani ubadilike na kuwa mwana wa MUNGU, Mzao wa mbinguni.(1Peteo 2:9).
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Print this post
Waebrania 12:22 “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi”
Nyakati za Nabii Musa,Ulikuwepo mlima uliojulikana kama mlima wa Mungu, au Sinai, au mlima Horebu.
Katika mlima huo, Mungu aliposhuka hakuruhusiwa mtu mwingine kuusogelea isipokuwa Musa tu peke yake, hata mnyama aliyekaribia alikufa.
Kwani ulikuwa umejaa utukufu wa MUNGU, ulioambatana na radi na umeme na ngurumo zinazotisha.
Na kutokana na hali hiyo, ni Musa tu peke yake ndiye aliyepata kibali cha kuusogelea mlima huo na kusikia sauti ya MUNGU, wengine wote walibaki chini, kusubiria kusikia kile Musa alichoambiwa na MUNGU.
Lakini katika agano jipya, tunasoma kwamba upo mlima mfano wa huo, lakini si katika mwili bali katika roho, na mlima huo una utukufu mkubwa kuliko ule wa Sinai, Musa alioupanda.
Mlima huu wa rohoni, nao pia unaitwa Sinai, ambao umejaa malaika wa Mungu, na wenye utukufu mwingi.
Tofauti na mlima ule wa kwanza wa mwilini ambao ni Musa tu ndiye aliyeruhusiwa kuupanda, mlima huu wa rohoni unapandwa na mtu yeyote aliye ndani ya imani kamili ya YESU KRISTO.
Waebrania 12:21 “Na hayo yaliyoonekana jinsi yalivyokuwa ya kutisha, hata Musa akasema, Nimeshikwa na hofu na kutetemeka.
Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi”,
Na faida za kuupanda mlima huu (Sinai ya rohoni) ni kwamba mtu atapata nafasi ya kumkaribia MUNGU zaidi na kumsikia MUNGU zaidi kuliko Musa alivyomsikia kule Sinai,
Pia atashuka na utukufu mkuu zaidi ya ule Musa aliokuwa nao aliposhuka hata uso wake ukang’aa.
Swali linarudi je wewe ni miongoni mwa watu walioufikia huo mlima wa MUNGU?.
Lakini labda utajiuliza pia mtu ataufikiaje huo mlima?..
Biblia imetupa majibu..
Zaburi 24:3 “Ni nani atakayepanda katika mlima wa BWANA? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? 4 Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila. 5 Atapokea baraka kwa BWANA, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake”.
Zaburi 24:3 “Ni nani atakayepanda katika mlima wa BWANA? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?
4 Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila.
5 Atapokea baraka kwa BWANA, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake”.
Sasa tunapataje mikono safi na mioyo myeupe, itakayotufanya tustahili kufika katika mlima huo mtakatifu?.
Njia ni moja tu, kumwamini Bwana YESU, Kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha na kupokea Roho Mtakatifu, na kila siku kuishi maisha ya utakatifu.
Kwa njia hiyo basi tutaweza kufikia kilele cha baraka, kwani ni Neema kuu tulipewa ya sisi kuufikia mlima wenye utukufu zaidi ya ule Musa aliopanda.
2 Wafalme 3:16-17
[16]Akasema, BWANA asema hivi, Fanyeni bonde hili lijae mahandaki. [17]Kwa kuwa BWANA asema hivi, Hamutauona upepo, wala hamtaiona mvua, ila bonde hilo litajaa maji; nanyi mtakunywa, ninyi, na ng’ombe zenu, na wanyama wenu.
[16]Akasema, BWANA asema hivi, Fanyeni bonde hili lijae mahandaki.
[17]Kwa kuwa BWANA asema hivi, Hamutauona upepo, wala hamtaiona mvua, ila bonde hilo litajaa maji; nanyi mtakunywa, ninyi, na ng’ombe zenu, na wanyama wenu.
Ilifika wakati wana wa Israeli, walikwama, baada ya kuona wapo katika eneo ambalo ni kame kupita kiasi, na hawana msaada, nguvu zimewaishia maadui zao wapo karibu kuwaangamiza..
Wakalia sana, Lakini baadaye wakapata akili ya kumlingana Mungu kwa kuulizia kupitia nabii wake Elisha. Lakini maagizo waliyopewa hayakuwa bado marahisi sana, kama walivyotegemea.
Hawakufanyiwa muujiza wa maji kutokea mwambani kama kipindi cha Musa, au mvua kushuka mbinguni…bali waliambiwa wachimbe mahandaki…yaani mashimo makubwa sana…pale jangwani..
Fikiri umechoka umeishiwa nguvu, halafu unaambiwa uchimbe mashimo..upige sururu chini, upige jembe chini, utoe jasho la kutosha si jambo jepesi..
Lakini baadaye tunaona Mungu anawaambia hamtaona mvua bali hayo mabonde yote yatajaa maji. Na ndivyo ilivyokuwa. Kwa waliochimba sana walipata maji sana, kwa waliochimba kidogo walipokea maji sawasawa na mashimo yao.
Je nini Bwana alikuwa analifundisha kanisa lake.
Katikati ya jangwa, Si muda wa kulia na kusumbuka, kinyume chake shika jembe lako, chepe lako anza kuchimba mashimo.
Kwanini watu wengi hawaioni mvua ya Mungu ya neema au baraka za rohoni zikidumu kwao lakini kwa wengine hudumu…sio kwamba Mungu anaupendeleo…hapana…bali wale wengine tayari wameshachimba mashimo marefu ya kuhifadhi maji mengi…Kwasababu mvua au umande wa Mungu sikuzote hushuka au hupanda juu ya nchi yote lakini wale wenye visima ndio hudumu na maji yake mda mrefu kwa wengine hudumu tu kwa muda mfupi pale juu, baadaye kidogo hupotelea ardhini…
Kuchimba handaki ni kudumu sana katika maombi, pamoja na kutendea kazi kile ulichokitaka kwa Mungu…
Kwa mfano unamwomba Mungu akupe mke/mume mwema, labda leo huoni kutokea kwa yoyote upo jangwani tu, unakaribia kukata tamaa…hakikisha unazidisha sana maombi, lakini pia unajitunza na kuanza kujifunza mafunzo ya kuwa mke/mume mwema, unaonyesha kivitendo zile sifa za mke mwema/mume mwema anazopaswa awe nazo kibiblia, kwamfano wewe ni mwanamume unafahamu kuwa yapo majukumu ya kibaba mbele yako, kwamba unapaswa uwajibike kwa kipato cha familia yako, lakini hilo kama hulisumbukii na bado unatarajia Bwana akuletee mke..ni kweli atakuletea, atapandisha umande wa maji juu ya nchi lakini hatimaye atashindwa kudumu na wewe katika hatua za awali akiona huwezi kusimama kwenye wajibu wako…baadaye utalalamika mbona wanawake wananikimbia..vilevile mwanamke akikosa tabia njema..wanaume watakuja na kumkimbia baadaye…kwasababu hakuwa na muda wa kujichimbia mahandaki yake, kitabia.
Kila eneo liwe la kihuduma, kikazi, kiafya..wekeza sana kwenye mahandaki kwasababu mvua/ umande utakuja tu…kwasababu kwa Mungu kushusha baraka si jambo la kulisumbukia sana, yeye anawanyeshea mvua waovu na wema alisema hivyo (Mathayo 5:45) bali kuzihifadhi hizo baraka ndio ugumu ulipo.
Mwanzo 2:6
[6]ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.
Wekeza kwenye maombi na kutendea kazi imani yako kwa vitendo. Zaidi ya kutarajia tu Mungu atende mwenyewe.
Bwana akubariki