Jina la Bwana YESU libarikiwe, karibu katika kujifunza Neno na Maombi.
Utangulizi: Kusoma Neno bila Maombi, au kuomba bila Neno la kusimama nalo ni sawa na kitamba cha bendera kisicho na mlingoti, kupitia mfululizo huu na tafakari hizi tutapata mwongozo sahihi wa kuomba kwa kusimama na maandiko ya Biblia.
Biblia inataja ulimi wa mtu, kama kiungo kiharibifu kuliko viungo vyote katika mwili.
Yakobo 3:5 “Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana. 6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum”.
Yakobo 3:5 “Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum”.
Sasa kwasababu ulimi ni kiungo hatarishi,maana yake kinaweza kumfanya mtu kuanguka moja kwa moja pasipo kuamka tena, hivyo andiko hili halijahifadhiwa ndai ya Biblia liwe tangazo la taarifa tu, kwamba tujue hatari ya ulimi halafu basi.
Hapana, si lengo la maandiko yote ya Biblia, bali maandiko yote yana lengo la sisi kusoma, na kujitengeneza kulingana na andiko hilo kwa njia ya kuomba…hivyo tumia muda kuomba maombi yafuatayo
1. OMBA UTAKASO WA ULIMI.(tumia Dk. 30 au zaidi).
– Takasa kinywa chako, kwa kutubia maneno yote mabaya na mazungumzo yasiyofaa yaliyotoka kinywani mwako na omba utakaso kwa damu ya YESU.
2. MWOMBE BWANA AKAKUTENGENEZE MANENO YA KINYWA CHAKO.
– Ukanene kwa hekima.
Zaburi 49:3 “Kinywa changu kitanena hekima,
Na fikira za moyo wangu zitakuwa za busara”
Ukanene kweli siku zote usiseme uongo.
Mithali 8:7 “Maana kinywa changu kitasema kweli, Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu”.
3. OMBA ULINZI WA KINYWA.
Mithali 13:3 “Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake; Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu”.
– Usiwe mtu wa kupayuka.
Zaburi 141:3 “Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu”
– Usifanye dhambi (mf. Uongo, usengenyaji, matukanio, malalamiko na faraka).
Ayubu 31:30 “(Naam, sikukiacha kinywa changu kufanya dhambi Kwa kuutaka uhai wake kwa kuapiza);
4. KEMEA KILA ROHO INAYOJIINUA KUKUKOSESHA KUPITIA ULIMI (KINYWA) CHAKO.
Kemea kwa jina la YESU KRISTO kila pando la la uongo, usengenyaji ndani yako, kanisani kwako, familia yako na wakristo wenzako wote.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
1. SHEREHE.
Katika Biblia hamna neno “sherehe” lakini kuna neno “sikukuu”.
Sherehe ni shughuli (tukio) la kijamii linayofanyika kwa lengo la kuadhimisha, kukumbuka jambo fulani (kama vile harusi, mahafali, siku ya kuzaliwa, ushindi n.k),
Na sherehe huwa inaambatana na michezo, au hotuba, au ibada au michezo, kutegemea na aina ya sherehe..(na katika Biblia hatuna neno sherehe).
Kama jina sherehe lilivyo maana yake linahusisha “shangwe” au “shamra shamra”.
2. SIKUKUU.
Sikuukuu ni neno linalopatikana kwenye Biblia, na tafsiri ya Neno Sikukuu ni “Siku iliyo kuu”. (Yaani siku yenye ubora kuliko nyingine)
Na katika Biblia zinatajwa sikukuu kadha wa kadha, ambazo hazikuwa kwa lengo la ibada na tafakari za kiMUNGU, mfano wa sikukuu hizo ni sikukuu ya vibanda, pasaka, na baragumu.
Kwa urefu juu ya Sikukuu hizo na maana zake kiroho fungua link ifuatavyo.
https://wingulamashahidi.org/archives/1858Karamu.
3. KARAMU.
Karamu ni neno linalopatikana kwenye Biblia ambalo lina maana ya tafrija yenye mandalizi ya chakula.
Kwa ufupi ni shughuli yoyote ndogo au kubwa yenye malengo makuu ya kula vyakula na kufurahi kutokana na tukio fulani jema.
Katika Biblia kunatajwa karamu mbalimbali mfano wa hizo ni ile Abramu aliyowafanyia wale Malaika wawili waliomtembelea.
Mwanzo 19:1 “Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi. 2 Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha. 3 Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. AKAWAFANYIA KARAMU, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala.”
Mwanzo 19:1 “Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.
2 Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha.
3 Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. AKAWAFANYIA KARAMU, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala.”
Na ile Abramu aliyomfanyia mwanae baada ya kuachishwa maziwa.
Mwanzo 21:8 “Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Ibrahimu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya.”
Lakini ipo karamu iliyo kuu katika Biblia ambayo haipaswi mtu yoyote kuikosa ambayo ni ile ya Mwanakondoo.
Kwa urefu juu ya karamu ya mwanakondoo ni fungua link ifuatayo..
https://wingulamashahidi.org/archives/1280
Jibu: Kwa asili Kuomba sio karama bali ni “Agizo”.
Na agizo la kuomba si la mtu mmoja bali ni la watu wote wenye karama zote,
Kwasababu hata mwenye karama ya kinabii ni lazima awe mwombaji kwa lengo la kuinoa karama yake au kuwaombea wale aliowapa unabii..
Vile vile mwenye karama ya uponyaji ni lazima aombe na kufanya maombezi ili mgonjwa/wagonjwa wapone.
Mwenye karama za lugha ni ivyo hivyo ni lazima aombe ili anene kwa lugha, matendo ya miujiza ni ivyo hivyo ni lazima maombi yahusike ili miujiza itendeke.
Nabii Eliya hakushusha moto kutoka mbinguni kwa uweza wa MUNGU bila kuhusisha maombi, aliomba kwanza ndipo muujiza ukatendeka..na karama zote zinaendeshwa na maombi.
Sasa tunarudi kwenye swali, je kuna karama ya kuomba na maombezi?.
Jibu ni La! Hakuna hiyo karama, kwasababu agizo haliwezi kuwa karama..
Lakini sasa kama ni hivyo inakuwaje wapo watu wenye uwezo wa kuomba kwa kina na masafa marefu kuliko wengine?.
Kuna sababu kuu mbili (02) za hali hiyo ya baadhi ya watu kuwa na uwezo mkubwa zaidi ya wengine, na sababu ya pili ina uzito zaidi kwa mujibu wa swali Letu.
1. MAZOEZI YA UTAUWA.
Najua unajiuliza mazoezi ya Utauwa ni kitu gani?…tusome maandiko yafuatayo kisha tufafanue.
1 Timotheo 4:7 “Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; NAWE UJIZOEZE KUPATA UTAUWA. 8 Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye”
1 Timotheo 4:7 “Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; NAWE UJIZOEZE KUPATA UTAUWA.
8 Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye”
Kiswahili kingine cha mazoezi ya utauwa ni “mazoezi ya uungu”.. yaani mtu anakuwa na mazoezi ya kutosha ya maagizo ya MUNGU kama maombi, mifungo, na uinjilisti…kiasi kwamba anakuwa ni mtu anayejizoeza kuhubiri mara kwa mara, au kuomba mara kwa mara jambo linalofanya uwezo wake wa kuomba, kuhubiri au kufunga kuongezeka kila iitwapo leo.
Sasa kundi hili linalojizoeza utauwa huwezi kushindana nalo wewe unayejizoeza kulala kutwa kuchwa au kula mara tatu kwa siku.
Wewe utasali dakika mbili na kulala mwenzio atasali masaa 5 bila kuchoka, wewe utabaki kusema fulani ana karama ya kuomba kumbe ni uvivu wako tu uliovikwa na ibilisi.
Hiyo ni sababu ya kwanza…
2. KARAMA YA MASAIDIANO.
Hii ndio karama inayochanganywa na wengi..
1 Wakorintho 12:28 “Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha”.
Katika karama hii ya masaidiano ndio hapa kuna watu wanakuwa na mzigo wa kuomba kwaajili ya wengine kwa muda mrefu kwasababu ndani yao kuna msukumo wa kusaidia.
Ile roho ya kutamani kusaidia inamfanya mtu aidha atoe vitu vyake au muda wake katika maombi na kuomba mpaka ule mzigo utakapoisha ndani.
Kwahiyo kwa hitimisho hamna karama ya maombi kwenye Biblia, bali ya masaidiano ambayo inahusisha maombi au kitu kingine chochote cha kumsaidia mtu mwenye uhitaji.
Je wewe ni mwombaji?. Kama sio. fahamu shetani kafaulu pakubwa sana kukupata, kuelewa faida za maombi kwa undani wasiliana nasi kupitia namba zifuatazo, tutakupa masomo husika bure.
Shalom.
Kuna kauli ambayo tunayo sana kwenye vinywa vyetu…Hususani pale boss au kiongozi wetu anapomalizana nasi katika mpango fulani na kutuaga..tunasema “bwana unaniachaje”?
Maana yake, baada ya kukaa chini yake muda mrefu, au kumtumikia, kuna namna anapaswa akuandalie mazingira ya kukufanya uendeleze lile jambo lake, au lako mwenyewe.. ndio hapo utaona wanawaachia watumwa wao aidha viinua mgongo, mitaji, au fedha za matumizi.
Hili linaonekana ni jambo zuri kufanywa na bwana au kiongozi yeyote mwenye busara.
Lakini kwa Yesu mambo yalikuwa tofauti, kwenye kauli yake ya mwisho alipokuwa anapaa.. Mitume hawakuachwa na lolote, na zaidi wanaambiwa wakashuhudie habari zake kutoka pale Yerusalemu walipo, waende uyahudi, Samaria na mpaka mwisho wa nchi.
Ukitafakari kwa ukaribu jambo hilo linahitaji rasilimali nyingi za kifedha, kiuchumi n.k. lakini hawakuachiwa hata senti kumi.
Ukiwa na mawazo kuwa kiongozi wako wa kiroho akuandalie rasilimali za kujikimu kimaisha, ndio ukamtumikie Bwana vizuri, ndugu utavunjika moyo..kwasababu yeye mwenyewe alipoitwa hakuandaliwa rasilimali, Na hilo halikuanzia kwake, lilianzia kwa mitume, hadi kwa wote waliofuata baadaye yao. Tena ungekuwepo nyakati za mitume ungevunjika moyo mara kumi zaidi.
Kumbuka Yesu anaonekana kama “Bwana mgumu” kwa baadhi ya watumwa. Usipokuwa makini unaweza kumwona pia hivyo.
Kivipi?
Mkumbuke yule aliyepewa talanta moja aliona ameachwa bila màandalizi mazuri kimtaji…akabakia tu kulalamika na kusema huyu Bwana wangu ni mgumu sana.… hii talanta moja aliyoniachia nitafanyia nini, Hata chakula cha siku moja tu hainitoshi, Bado anataka nimletee vingi, anataka kuvuna asipopanda… Ninakwenda kumwekea pesa yake. Nikafanye mambo yangu akirudi nimpe sitaki lawama.
Hakujua uamuzi huo ni kosa kubwa..
Luka 19:20-26
[20]Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso. [21]Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda. [22]Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda; [23]basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake? [24]Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi. [25]Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi. [26]Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho.
[20]Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.
[21]Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.
[22]Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;
[23]basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake?
[24]Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi.
[25]Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi.
[26]Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho.
Ukiona unasubiri ufanyiwe na Yesu kwanza kitu fulani ndipo uwe na hamasa ya kuifanya kazi.
Kuwa makini. ROHO MTAKATIFU TAYARI YUPO NDANI YAKO UMESHAPEWA. Hakuna kingine zaidi ya hiko. Simama kwenye huduma yako, Timiza utume wako.
Ubora wa Kuhubiri au kufundisha haupimwi kwa elimu kubwa ya biblia, au mifano mizuri, au utashi fulani wa kupangilia maneno. Hapana, bali ni uwezo wa kupenya katika mioyo ya watu.
Haimaanishi kuwa na elimu ya biblia haichangii ubora wa fundisho au hubiri..inachangia sana lakini hiyo ni kama gamba la juu sana..ambalo linaweza lisitoe pia matokeo yoyote.
Pale fundisho linapoweza kuingia ndani ya moyo wa mtu, kupambanua, kuchoma, kulainisha, kupindua-pindua, kukarabati, kuponya hadi kumfanya mtu kuwa na mwitikio wa dhahiri wa nje. Hilo ndio linaitwa fundisho au hubiri kibiblia.
Sasa tendo hilo mpaka kufikiwa, si jambo rahisi hata kidogo, hakuna utashi wa kibinadamu unaweza kufanya hivyo.
Kwasababu hakuna anayejua ndani ya mtu mwingine kuna nini?
Lakini lililo gumu zaidi ni kuwa hata yeye mwenyewe hajijui vema, kama anahitaji matengenezo katika eneo fulani la moyo wake. Anaweza akawa ana hofu akadhani huwenda chanzo cha hofu hiyo ni ule ugonjwa uliomshika, kumbe chanzo ni kingine kabisa.
Kwasababu mwanadamu mwenyewe moyo wake ni fumbo kubwa.
Yeremia 17:9
[9]Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?
Umeona jinsi ilivyo ngumu sana. Ikiwa yeye mwenyewe hajijui, wewe mtu wa tatu utayajulia wapi yaliyomo moyoni mwake? Lakini Mungu anataka uyahubiri yahusuyo moyo wake.
Usifikiri unapomwona mtu, labda ana huzuni, au furaha au ana tabia za ulevi, wizi, , ukadhani anahitaji fundisho linaloendana na hiyo tabia unayoiona kwa nje.
Unaweza ukakosa shabaha kwa maili nyingi sana, ukifikiri tu hivyo.
Utamwona analia, pengine ni mgonjwa, amefiwa, amepoteza kila kitu kama ilivyokuwa kwa Ayubu na wewe unamfuata na fundisho la faraja, ukadhani kuwa ndio uponyaji wake utakapotokea.
Kumbe Mungu anajua anataka makemeo, na makaripio ili aponywe.
Wakati mwingine utasimama kwenye mkusanyiko wa watu wengi labda mia. Huko huko wapo wanaohitaji faraja, wanaohitaji unabii, wanaohitaji maonyo, wanaohitaji maarifa, wanaohitaji kufunguliwa. Sasa wewe unasimama na fundisho lako lenye mlengo mmoja wa makemeo, unadhani wote watahudumiwa na hilo. Kama ukikosa namna ya ki-ungu, unaweza ukawa unazungumza maneno yako.
Na lengo la Mungu ni watu wote wahudumiwe na Neno.
Hapo ndio linakuja suala la hakuna mbobezi wa fundisho au hubiri. Inahitaji hekima nyingine itokayo juu, ya kuhubiri usichokuwa na ufahamu nacho, au ujuzi nacho.
Siku ile ya Pentekoste, kilichotendeka mpaka ikapelekea watu wale kuchomwa mioyo, na hatimaye kuamini kwa idadi ile kubwa ya watu.
Haikuwa kwasababu walipaza sauti sana, au walihubiri kwa ujasiri sana, au maneno yao yalikuwa na elimu kubwa ya theolojia..
Hapana angalia utaona yalikuwa ni maneno ya kawaida kabisa… lakini yaliyoundwa na Roho Mtakatifu kwa namna ambayo yalipenya katika moyo wa kila mmoja.
Utaona, hatua ya kwanza walinena kwa lugha ambazo hata wao wenyewe hawakuzijua, lugha hizo zilikuwa zinawahubiria wengine.. zinanena mambo yao ya sirini, zinawakemea, zinawafariji, zinawaponya, zinawashuhudia Kristo.
Mpaka baadaye wanamaliza kunena tayari injili imeshahubiriwa wasijue ni kitu gani kimehubiriwa.
Petro aliposimama kumalizia maneno yake, wote wamenywea wanasubiri tu kupewa maelekezo ni nini cha kufanya baada ya pale..
Matendo ya Mitume 2:37
[37]Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
Hao ni watu wasio na elimu yoyote, walikuwapo waandishi, na mafarisayo wenye elimu lakini hakuna matokeo yoyote ya mafundisho yao.
Hata leo hii mimi na wewe.. Tujue kuwa kuhubiri na kufundisha hakutegemei sana ujuzi, au utashi, bali kunategemea zaidi Roho Mtakatifu.
Kwanini Roho Mtakatifu?
Kwasababu yeye ndiye anayeweza kuzama ndani ya mioyo ya watu na kujua shida zao, na kuwaponya.
Ni nini tunapaswa kufanya, ili fundisho likazame moyoni, lisitoke kwa makisio yetu?
Jambo kuu ni Kuwa na maandalizi ya kutosha.
Maandalizi hayo yapo kwa namna mbili.
1) Kumwandalia Roho Mtakatifu njia ya kuanzia..Ndio hapo unahitaji kwanza kusoma na kuandaa somo / fundisho. Kumbuka Ni lazama utenge muda kuandaa fundisho ambalo utalihubiri. Andika, na ujue pa kuanzia, bila kuwa na maandalizi hayo, unasema nitaenda tu kuzungumza. Ujue tayari umeizuia njia ya Roho Mtakatifu kufundisha.
2) Lakini hilo peke yake halitoshi, hatua nyingine ni kuomba maingilio ya Roho Mtakatifu yawe makubwa. Hapo ndipo unatenga muda mrefu wa kuomba, ili Roho Mtakatifu akatembee kwenye vyumba vya ndani kabisa ambavyo wewe hujui, wakati utakaposimama na kufundisha, kushuhudia.
Sasa ukimaliza hapo. Jiandae kwenda kusema ulichokusudia.. kumbuka mhubiri anayetumia dakika kumi kufundisha lakini amekuwa na maandalizi ya masaa matano kwenye kusoma na maombi. Ana nguvu zaidi ya yule atakayefundisha masaa matano, halafu alijiandaa kwa dakika tano.
Mwisho Ukienda kufundisha na kuona mazungumzo yako yanasogea nje ya mada, au taarifa nyingine zinakuja kichwani mwako tofauti na zile ulizoziandika kwenye daftari ujue ni kazi za Roho Mtakatifu usizizuie.
Baadaye utakuja kusikia tu shuhuda, na hata kama hazitasemwa, ujue Neno lako halijakwenda bure.
Tukiwa wahubiri na waalimu wa namna hii. Roho nyingi za watu zitaokolewa.
Kuhubiri ni kusema tusichokijua, cha wengine.
Shalom
Jina la Bwana YESU libarikiwe, karibu katika kujifunza Neno na Maombi. Kusoma Neno bila Maombi, au kuomba bila Neno ni sawa na kitamba cha bendera kisicho na mlingoti, kupitia mfululizo huu wa tafakari hizi tutapata mwongozo sahihi wa kuomba kupitia maandiko ya kwenye Biblia.
PENDO LA MUNGU.
Bwana YESU alitufundisha kuwa Amri ya kwanza ni “Kumpenda Bwana na ya pili ni kuwapenda majirani kama nafsi zetu”.
Mathayo 22:36 “Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 37 Akamwambia, MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE, NA KWA ROHO YAKO YOTE, NA KWA AKILI ZAKO ZOTE. 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO. 40 Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii”.
Mathayo 22:36 “Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
37 Akamwambia, MPENDE BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE, NA KWA ROHO YAKO YOTE, NA KWA AKILI ZAKO ZOTE.
38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.
40 Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii”.
Na tena alisema…
Yohana 14:21 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
1. OMBA ONGEZEKO LA UPENDO WA MUNGU NDANI YAKO (Tumia dakika 30)
i. Kwa moyo wako wote.
ii. Kwa roho yako yote
– Hapa utamwomba Bwana kuwa upendo wako ukatoke rohoni, katika kumtafuta kwasababu Neno linasema waabudua watamwabudu baba katika roho na kweli.
iii. Kwa akili zako zote.
– Hapa utaomba Bwana akuwezeshe kumtumikia yeye kwa ujuzi aliokupa, (ule wa asili na ule wa kujifunza) kama ni msomi basi kupitia elimu yako hiyo umtumikie MUNGU, na kuyafanya mapenzi yake.
iv. Kwa Nguvu zako zote.
– Nguvu zinaweza kuwa za mwili kama wewe ni kijana, lakini pia zinaweza kuwa za kifedha, katika maeneo hayo yote mwombe BWANA akusaidie uweze kumpenda MUNGU na kufanya mapenzi yake, Utoe muda wako au mali zako katika kumtumikia MUNGU.
2. OMBA UPENDO KWA JIRANI. (Tumia dakika 30)
Neno la MUNGU linatufundisha kuwa “Tujaponena kwa lugha zote na kufanya ishara zote kama hatuna Upendo sisi sio kitu”
1Wakorintho 13:1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao”.
Na tena inasema…
Waebrania 13:1 “Upendano wa ndugu na udumu”.
i. Omba Upendo kwa ndugu wa kiroho (Wachungaji na washirika wenzako)
ii. Omba Upendo kwa ndugu wa kimwili (Wana familia)
3. KEMEA KILA ROHO INAYOJIINUA KUPOOZA UPENDO WA MUNGU, NA WA KINDUGU
Kemea kwa jina la YESU KRISTO kila pando la chuki kanisani kwako, katikati yako na wakristo wenzako, katikati yenu kama familia.
Jina la Bwana YESU libarikiwe, karibu katika kujifunza Neno na Maombi. Kusoma Neno bila Maombi, au kuomba bila Neno ni sawa na kitamba cha bendera kisicho na mlingoti, kupitia mfululizo huu wa tafakari tutapata mwongozo sahihi wa kuomba kupitia maandiko ya kwenye Biblia.
MAPENZI YA MUNGU.
Bwana YESU alisema si kila aniambiaye Bwana Bwana atakayeingia katika ufalme, bali yule afanyaye mapenzi ya Baba wa mbinguni.
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Sasa basi kama kigezo cha kuingia mbinguni ni “KUFANYA MAPENZI YA MUNGU”, hivyo tukimwomba MUNGU atusaidie kuyajua na kuyafanya mapenzi yake tutakuwa tunaomba jambo sahihi kabisa.
1. OMBA KUYAJUA MAPENZI YA MUNGU KWAKO (Tumia dakika 30)
Katika Eneo la kiroho.
Katika Eneo la kimaisha.
Katika Eneo la kifamilia.
2. OMBA KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU. (Tumia dakika 30)
Utauliza katika kuyatenda mapenzi ya MUNGU kuna haja ya kuomba?. Jibu ni Ndio! Kwasababu pasipo yeye kutusaidia sisi hatuwezi kufanya lolote. (Soma Yohana 15:5).
Katika Eneo la kifikra
Katika eneo la Viungo
3. KEMEA KILA ROHO INAYOKUZUIA WEWE KUYAFANYA MAPENZI YA MUNGU.
Zipo roho za adui zinazozua kuyafanya mapenzi ya MUNGU, roho hizi zinazuia fikra zako za ndani zisifikiri, wala kupenda kuyafanya mapenzi ya MUNGU, ndio hapo utatamani kwenda kushuhudia habari za wokovu, ndani ya fikra zako woga unaingia au aibu au kukosa ujasiri, tumia muda kuzikemea.
Pia zinazuia viungo vyako visiwe tayari kufanya mapenzi ya MUNGU, ndio hapo utatamani kwenda kuhubiri au kwenda kufanya kazi yoyote iliyo halali na ghafla udhaifu wa mwili utaingia kama uchovu, uvivu, au ugonjwa. Hivyo chukua muda kukemea roho hizo na Bwana atakufungua.
1Petro 4:2 “Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. 3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali; 4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana”.
1Petro 4:2 “Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.
3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;
4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana”.
Bwana akubariki usikose sehemu ya Pili ya Mwongozo huu wa Neno na Maombi, kwa msaada zaidi wasiliana nasi kwa namba tajwa hapa chini.
– Hapa utamwomba Bwana akufunulie kuyajua mapenzi yake katika kazi unazozifanya au elimu, ni kipi sahihi unapaswa ukifanye ukiwa hapo kazini, ni watu gani sahihi unapaswa ushirikiane nao ili usifanye kinyume jambo nje na mapenzi ya MUNGU pia kama unatafuta kazi, basi omba MUNGU akakufunulie kazi sahihi na kukuongoza hapo.
iii. Katika eneo la kifamilia.
– Hapa omba Bwana akakuoneshe mapenzi yake kuishi na mke, mume, na watoto, au wazazi pia ombea wanafamilia yako wote wakayajue mapenzi ya MUNGU na kuyafanya.
2 Wafalme 13:20 “Elisha akafa, nao wakamzika. Basi vikosi vya Wamoabi wakaingia katika nchi mwanzo wa mwaka.
21 Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka, akasimama kwa miguu”
Kumbukumbu la Torati 30:15 “Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya”.
Mathayo 16:24 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.
26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
27 Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake” .
Ulishawahi kutafakari kwanini yule mwanamke aliyemzaa yule mtoto wa kiume, kupewa uwezo wa kukimbilia nyikani, kama njia ya kuepushwa na joka lile?
Kwanini asichuliwe mashambani, au mjini, au milimani, kinyume chake iwe nyikani.
Ufunuo 12:13-14
[13]Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume. [14]Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
[13]Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
[14]Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
Nyikani ni mahali ambapo hapana uzuri wowote, hapana mahitaji yoyote ya msingi, mahali pasipovutia, kwasasa tunaweza kusema ni nyakati za ukame, ambazo huoni, jambo lolote, huoni hatua yoyote dhahiri,ijapokuwa unajitahidi sana..huoni mafanikio yoyote, huoni mazingira rafiki..
Wakati mwingine ni kipindi cha kupungukiwa kwa muda mrefu, upo pale pale.
Tunapofikia hatua hii, mara nyingi tunamlilia Mungu atuondoe huko, tunahuzunika, tunanyong’onyea, tunasinyaa kiroho, tunamlilia Mungu kwa juhudi nyingi atuvushe..
Ni kweli kabisa jangwa si zuri, lakini wakati mwingine Bwana hulitumia kutuepusha na yule mwovu. Njia pekee iliyompasa huyu mwanamke kuepushwa na joka lile, ilikuwa ni kukimbilia jangwani, na si vinginevyo.
Hivyo ujikutapo katika nyakati mbalimbali ngumu, maadamu upo ndani ya Kristo na unaendelea vema katika imani, fahamu pia huko ulipo Mungu anakuandaa na unatimiza kusudi la Mungu.
Tuwapo katika mazingira yoyote, suluhisho si kulalamika bali ni kuomba, kushukuru na kuitafuta hekima.
WhatsApp