MIAMBA YENYE HATARI.

MIAMBA YENYE HATARI.

SWALI: Biblia inamaana gani inaposema “Watu hawa ni miamba yenye hatari”. Hii miamba yenye hatari ni ipi?

JIBU: Tusome..

Yuda 1:12 “Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung’olewa kabisa;

13 ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele”.

Hapa ni mtu Yuda alikuwa anawalinganisha wachungaji na mitume wa uongo kama miamba yenye hatari.

Sasa miamba inayomaanishwa hapo, si hii miamba tuionayo nchi kavu, hapana, bali ni ile miamba ya habarini ambayo baadhi yao inatabia ya kuchomoza juu hadi karibu na usawa wa bahari. Miamba hii ni hatari sana kwa mabaharia, kwasababu huwa haionekani, lakini meli inapopita karibu nayo, inaichana, kama sio kuiharibu kabisa na matokeo yake, ni aidha meli kugotea palepale, au kuzama kabisa.

Kama mabaharia wasipokuwa waangalifu, kwa kupita njia zilezile walizozithibitisha ni rahisi sana kukutana na hii miamba na kuzipoteza meli zao moja kwa moja.

Sasa hapo anaposema “Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu”;

Anamaanisha, wachungaji hawa, au watumishi hawa wa uongo ni ngumu kuwatambua, kama tu vile miamba hii hatari ilivyo ngumu kuiona habarini, pale ambapo Habari inaonekana shwari na tulivu yafaa kwa kusafiria kumbe ndipo ilipojifichia, halikadhalika, watumishi hawa wa uongo, mahali ambapo mpo katika karamu zenu za Upendo, yaani wakati ambapo mnamfurahia Mungu wenu, mnatangaza Habari njema, mkidhani kuwa wapo na nyie, kumbe ni mbwa mwitu katika mavazi ya kondoo.

Mfano wa watu hawa alikuwa ni Yuda,alitembea na Bwana Pamoja na mitume wengine, lakini haikuwa rahisi kumgundua, hadi dakika ya mwisho, utaona alipokuwa katika mlo wa jioni, kama mpelelezi, hakuna aliyemtambua isipokuwa Bwana tu peke yake.

Mtume Paulo aliliona hilo hata wakati wa kuondoka kwake akasema..

Matendo 20:29 “Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;

30 tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao”.

Hadi sasa, inasikitisha kuona watumishi wa namna hii wapo wengi katika kanisa la Mungu, ,hawaoni shida kuwadanganya watu, wengine ni wachawi, wengine ni matapeli, wengine wapo kwa lengo la kuzivuruga tu kazi za Mungu, ili watu watusiishi Maisha matakatifu, hawawahurumii watu wanaotaka kumjua Mungu, lakini cha ajabu ukiwaangalia kwa nje, wanalitaja jina la Yesu, wanaongoza makanisa, wanashiriki katika kampeni zote za kidini.

Huu ni wakati wa kuwa makini sana, Ni wakati ambao wewe kama mkristo, kuondoa uvivu wa kusoma biblia, tunadanganywa kwasababu hatuna maarifa ya kutosha kuhusu Mungu wetu na utendaji kazi wake. Hatuwezi kumshinda shetani kwa maneno tu, au kwa kumkemea, tutamshinda shetani kwa lile Neno lililokaa ndani yetu kwa wingi, ndiyo silaha ambayo Bwana Yesu aliitumia kumshinda shetani pale alipokuwa anajaribiwa nay eye kule jangwani.

Vinginevyo tukiyaendesha Maisha yetu hivi hivi tu kwa jinsi tunavyotaka, tujiandae kukutana na hii miamba yenye hatari, isiyoonekana. Tukiwa wavivu kujifunza biblia, hakuna namna tutamkwepa shetani, hakuna namna.

Bwana atusaidie.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1

UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?

FANYIKA SIPORA WA KRISTO, UNYAKUO UPO KARIBU.

USIPOTEZWE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.

JINSI YA KUSOMA BIBLIA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments