JIBU: Vita vipo vya aina mbili, 1) Vita vya kuishindania Imani …na 2) Vita vya kuishindania Injili,
Vita vya kuishindania Imani Tunasoma katika
Yuda 1:3 “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.
4 Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.”
Na hii ndio vita dhidi ya mafundisho potofu ambayo ambayo yanapindua imani zetu na dhidi ya dhambi ambayo inatenda kazi katika viungo vyetu …Wagalatia 5:17 “Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka”.
Waebrania 12:4 “Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi;”…
Na kila mtu aliyezaliwa mara ya pili anapambana kwenye hii vita. 2. Aina ya pili ya Vita ni vita vya kuipigania injili, na hivi ndivyo Mtume Paulo alivyokuwa anavizungumziwa hapo katika hiyo 2 Timeotheo 4:7 , si vita vya kimwili bali ni vita katika safari yake ya kuhubiri injili, akipambana na majaribu na nguvu zote za yule mwovu katika kuwaleta watu kwa Kristo,
….. 2 Wakorintho 10:3 “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;
4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo”;
Kazi ya kuhubiri Injili, siku zote shetani haifurahii hata kidogo, atanyanyua vikwazo vingi, na kuleta majaribu mengi..hivyo kusababisha vita vikali vya mapambano visivyoisha, ndio maana utaona Mtume Paulo alipitia kufungwa magerezani, kuchapwa bakora, kupigwa mawe kusalitiwa na kukumbwa na kila hatari katika safari yake ya kuhubiri injili.…
2 Wakorintho 11:3 “……. mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi.
24 Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja.
25 Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini;
26 katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang’anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo;
27 katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi”.
Kwahiyo hapo aliposema amevipiga vita vizuri anamaanisha, “kuwa Ameishindania injili ipasavyo” hakuacha kuishindania kwasababu ya mateso amevumilia na kuvuta wengi kwa Kristo, na ndio maana juu kidogo mstari wa 5 utaona anamwambia Timotheo naye ashindanie Injili vivyo hivyo. Na kila mtu ambaye atakwenda kuhubiri Injili ni lazima akutane na hivyo vita na lazima apambane, na kushinda na kuhakikisha kwa gharama yoyote, anakwenda kuzivua roho za watu..Bwana Yesu alisema
Mathayo 10:16 “Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
17 Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga;18 nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa”.
2) Nitailindaje imani maana mimi nahitaji kulindwa na Mungu.
Ni vipi mkristo wa leo atailea na kuilinda imani?Utailinda Imani, kwa kuishika Imani…Na unaishika Imani kwa kukaa na kudumu katika Neno la Mungu..kila siku ukihakiki ni lipi limpendezalo Bwana,(Waefeso 5:10) na kujiepusha na Ulimwengu…Na jukumu la kuilinda Imani ni la mwanadamu si la Mungu, sisi ndio tunajukumu la kushika kile tulichonacho asije mtu akaitwa taji yetu Biblia inasema hivyo…
soma Ufunuo 3:11 na 1 Wakorintho 10:12. 3).je! kunao Mwendo wa kuumaliza, ni upi? Maandishi haya yamekua maarufu sana kwa mazishi, nisaidie tafadhali.Mwendo unaozungumziwa hapo, ni mwendo wa riadha, Safari yetu ya kwenda mbinguni inafananishwa na mashindano ya kukimbia mbio ndefu…tunapompa Kristo Maisha yetu ndio tunaanza mbio, na tunapoondoka duniani ndio tunakuwa tumeumaliza mwendo, kwahiyo hapo Mtume Paulo aliposema Mwendo ameumaliza, alikuwa yupo karibu sana na wakati wa kufariki kwake, Roho Mtakatifu alimshuhudia kuwa muda wake wa kuishi uliobakia sio mwingi…
Ukisoma juu kidogo mstari wa 6, utaona jambo hilo. Na maandishi haya yamekuwa yakiandikwa kwenye makaburi ya wapendwa wetu kuwafariji wafiwa, lakini kimsingi kama Maisha ya aliyekufa hayakuwa ya kikristo, wala hakupigana vita vyoyote vya kuitetea injili wala kushindana na dhambi, basi maneno hayo ni hewa tu! Hayana msaada wowote kwa aliyekufa.
Bwana akubariki.
Mada Nyinginezo:
TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.
ZIFAHAMU NAMBA KATIKA BIBLIA NA MAANA ZAKE.
About the author