FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?

FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?

Freemason ni nini? nini historia ya freemason?, nani mwanzilishi wa freemason na Je! Freemasons ni wa kuogopwa? Masharti ya freemason ni yapi?

Shalom! Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tuongeze maarifa ya Neno la Mungu.

Leo tutajifunza juu ya kikundi kinachoitwa “Freemasons” na jinsi gani ya kutoka au kuwasaidia ambao tayari wameshaingia humo.

HISTORIA YA FREEMASONS

Kwa kuanzia tujifunze kidogo historia ya kikundi hicho: Freemasons tafsiri yake kwa lugha ya kiswahili ni “wajenzi huru” ingawa hawatambuliki kwa jina hilo, lakini kwa asili ni kikundi cha wajenzi. Kikundi hichi kilianzishwa miaka mingi kinadai tangu wakati wa ujenzi wa hekalu la Mfalme Sulemani, japo umaarufu wake umekuja kuwa mwingi katika karne za hivi karibuni.

NANI MWANZILISHI WA FREEMASONS

Kikundi hichi kinaamini “kulikuwa kuna siri zimefichika ambazo ndizo zilitumika katika ujenzi wa hekalu la Mfalme Sulemani”...Na kama vile wakristo wanavyoamini kuwa Yesu Kristo ndiye Masihi na kiini cha siri zote za Mungu. Vivyo hivyo Na Freemasons wenyewe wanamwamini mtu mmoja anayeitwa HURAMU, Kama Masihi wao, huyu anapatikana katika kitabu cha 1Wafalme 7, ambaye ndiye aliyekuwa mtu wa mji wa Tiro ambao kwa sasa ni maeneo ya nchi ya Lebanoni. Huyu ndio kama Masihi wao, Na Mwanzilishi wa freemasons kulingana na wao.

JE FREEMASONS NI KIKUNDI CHA SIRI?

Sasa kikundi hichi ni cha Siri, tukisema ni cha siri haimaanishi watu wake hawaonekani, au majengo yao hayajulikani..Hapana! Vikundi vya Freemasons vyote vimesajiliwa na serikali zote duniani, na vinalipa kodi, kwahiyo ni watu waliowazi..Kitu pekee ambacho ni siri ni “IBADA ZAO”. Na sheria za dunia zinawalinda kufanya ibada zao kwa siri. Kama vile sheria zinavyolilinda shirika la COCACOLA kuficha formula ya utengenezaji wa vinywaji vyao.Ni watu wachache sana wanafahamu, Na hiyo yote ni kuzuia unakiliji wa bidhaa zao.(www.wingulamashahidi.org)

FREEMASON INA WANACHAMA WANGAPI?

Freemasons ina wanachama zaidi ya milioni 6 duniani kote, miongoni mwao wakiwa, maraisi, wanasiasa, wana uchumi, wanasayansi, madaktari, waalimu, viongozi wa dini, wakulima, n.k…Idadi kubwa ya wanachama hao ipo nchini Uingereza na Wales.

MASHARTI YA FREEMASON

Mshirika kabla ya kujiunga ni lazima awe ana imani ya kuwa kuna “nguvu ya Kiungu”….Hiyo ikifunua kwamba tayari hicho ni “kikundi cha rohoni” kama huamini huwezi kuwa mshirika …Wanaojiunga huko ni watu kutoka dini zote duniani, waislamu, wahindu, wakristo-jina, wabudha n.k..Baada ya mshirika mpya kujiunga anatakiwa kukusanyika na wenzake mara kwa mara katika majengo yao maalumu ya ibada yanayoitwa “Grand Lodges”..Na wanawake hawaruhusiwi kujiunga katika kikundi hicho.

ISHARA/ ALAMA ZA FREEMASONS

Ndani ya Ibada hizo kwenye majengo yao wanatumia ishara ya vitu vingi, katika vidole, mikono, miguu, na pia wana ishara za picha na vito kama pete, mikufu, stika, ribbons, na ishara za vifaa vya ujenzi kama bikari, rula, pembe tatu.n.k na Kila ishara ina maana yake. Kama vile sisi wakristo tunavyokuwa na ishara ya misalaba kanisani mwetu, Inafunua kitu kilichotendeka Kalvari.

Sasa Ibada hizo zinabadilika kulingana na vyeo, wenye vyeo vya chini hawafanyi ibada zinazofanana na wenye vyeo vya juu, na pia wenye vyeo vya chini hawafahamu siri nyingi kama wanazofahamu wenye vyeo vya juu. Hapa ndipo watu wengi wasipojua!…tutakuja kupaelewa vizuri mbele kidogo mwa somo hili…

NGAZI ZA FREEMASONRY

Sasa vyeo hivyo vimegawanyika katika ngazi kuu 33 wanazoziita “shahada” au “degrees”

Mshirika mpya anayejiunga, kuna viapo anaambiwa aape, moja ya viapo hivyo ni kukiri kuwa mwaminifu, na kutokufichua siri yoyote ya chama hicho, na pia ataambiwa akiri kwamba endapo atafichua basi atakufa, na pia anaambiwa aape kwamba atakuwa mwaminifu, na pia atakuwa tayari kushirikiana na wenzake, na kusaidiana na wenzake kwa hali na mali…(www.wingulamashahidi.org)

Na katika hatua za awali, ataambiwa tu hicho ni kikundi cha kijamii!, kinachoamini katika ujenzi, na cha kusaidiana, na wala hataambiwa siri nyingi za kikundi hicho,..Na wala hawatamkataza kurudi kusali katika kanisa lake kama ni mkristo. Ila kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda na anayozidi kupanda vyeo, ndipo ataanza kugundua kuwa sio sehemu ambayo aliambiwa pindi alipokuwa anajiunga.

SHUHUDA ZA WALIOJIUNGA NA KUTOKA FREEMASON

Wengi waliojiunga na kutoka wanasimulia…”kuwa pindi walipojiunga, hawakujua chochote na pia walikuwa wanauhuru wa kuendelea kurudi kwenye makanisa yao kuabudu” na tena walikuwa wanapingana vikali na wale waliokuwa wanakishutumu chama hicho kuwa ni chama cha kishetani” na kinachoamini mauaji.

Wengine wanasema “Nilikuwa mshirika wa chama hicho kwa miaka mingi lakini sikuwahi kujua kuwa ni chama kinachomuabudu shetani” kwasababu wote tuliokuwa ndani ya chama hicho wenye degree ndogo, tulikuwa na upendo, na tulikuwa tunasaidiana, na kupeana fursa..Mpaka nilipofika ngazi za juu ndipo nilipoelewa kuwa sio sehemu salama”..mmoja aliyekuwa na degree ya 2 aliyetolewa huko na Bwana Yesu alihojiwa… je! ulishawahi kumuona shetani ndani ya ibada zenu?…akasema la! hata siku moja, wala sijawahi kuona vitu vya kiroho kama mapepo ndani ya logde! nilikuwa naingia na kutoka tu kama ninavyoingia kanisani…Na wala nilikuwa siamini kwamba ni kikundi kibaya kwa miaka kadhaa…na wala sikuwahi kutoa kafara yeyote ya mtu! mpaka baadaye sana nilipokuja kugundua kuwa hayo yanafanyika na wenye shahada za juu na hawatuambii sisi.

Kuanzia shahada ya 30 na kuendelea ndio wanaotokewa na mapepo na kuzungumza na shetani mwenyewe, na hao ndio wanaojua siri nyingi za chama hicho kuwa ni chama cha kumwabudu shetani moja kwa moja! na agenda kubwa ya chama hicho ni “kuikimbiza dunia katika ustaarabu mpya wa ulimwengu” ambao utakuja kuhasisiwa na Mpinga-kristo, chini ya utawala wa kirumi” katika siku za mwisho, lakini wengine wa shahada za chini hawaelewi sana.(www.wingulamashahidi.org)

Freemasons pamoja na vikundi vingine vya kichawi kama Iluminati, Brotherhood, ku-klax-klan,sisterhood, vinafanya kazi zinazofanana..Vyote ni vikundi vya kumwabudu shetani. Kwahiyo sio wote waliojiunga na freemasons wanaoelewa wapo sehemu gani.

JE! FREEMASONS NI WA KUOGOPWA?

Dhana iliyopo sasa hivi, ambayo hiyo inatokana na kukosa maarifa ni kwamba mtu aliyejiunga na freemasons tayari huyo ni pepo! hapana! hiyo si kweli kama tulivyotangulia kusema wapo wengine hawajui chochote wamedanganyika tu wakidhani kuwa ni kikundi cha kijamii cha kusaidiana kama vikundi vingine, hawaelewi vizuri freemason ni nini..Sasa hao wanahitaji msaada! Kumbuka ni watu kama wewe na mimi, wanapumua, wanasikia maumivu, wana hofu kama wewe na mimi, hivyo ni wa kusaidiwa kutoka huko kabla hawajazama kikabisa kabisa humo…sio wa kuwakimbia…Wanahitaji injili ya Yesu Kristo ya msamaha wa dhambi..wengine hawaelewi wamepelekwa tu na marafiki zao, ni kama tu makahaba waliojiingiza kwenye madanguro sio wote wanaelewa madhara ya kuwa kule, wanahitaji wokovu kama wewe ulioupata.

Ukienda pasipo maarifa kwa mtu ambaye ni freemason na kumwambia wewe ni shetani! unaabudu shetani na unatokewa na shetani kila siku na kuzungumza naye na kuua watu na kuwatoa kafara! na unakunywa damu…kwasababu tu umemwona kavaa pete yenye alama zao…

Ni rahisi sana kumkosa kwasababu hivyo unavyovisema unaweza kuta havifanyi katika levo aliyopo huko…kwasababu wote wanaojiunga huko kwa mara ya kwanza ni lazima wadanganywe… Hivyo huyo ni kumweleza kwa maarifa mwanzo wa chama hicho na mwisho wake.. Na kumweleza Injili ya Yesu Kristo ya msalaba…Lakini ukikutana naye na kuanza tu! kukemea hapo hapo! na kumwogopa!…na kumhakikishia kwamba yeye ni mchawi..atakushangaa sana na hatakuelewa, na pengine atakuchukia na itamfanya azidi kuamini kuwa yupo sehemu salama zaidi. Wengi waliojiunga huko ni kwasababu wamekosa maarifa..Hivyo wanatakiwa waokolewa kwa kupewa maarifa ya Neno la Mungu. Hivyo usikose maarifa ya namna ya kuvua roho za watu!.

Biblia inasema katika

Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;..”

WATU WANAJIUNGAJE FREEMASON

Na pia jambo lingine watu wasilolijua ni kwamba Freemasons watu hawajiungi kwa kupitia Facebook, wala hawajiungi kwa kupitia vipeperushi huko barabarani, wala vinakala juu ya nguzo za umeme…Huo wote ni utapeli tu ambao watu wanadanganywa…Ni watu wa kawaida ambao wanatafuta kupata pesa za kitapeli. Na pia freemasons ni kitu kidogo sana kwa mtu aliyeokoka haipaswi kukuzwa kiasi hicho mpaka kutengeneza hofu ya kupita pembezoni mwa barabara yenye jengo la freemasons, wala kumsalimia mtu aliyejiunga huko..Hakuna chochote kitakachokupata ukiwa ndani ya Kristo kwasababu shetani ni yule yule, unayeshindana naye kanisani ndio huyo huyo huko freemason! Sasa unachoogopa ni nini? (www.wingulamashahidi.org)

WATU WALIOJIUNGA FREEMASON WANAPATAJE PESA?

Na pia usikose maarifa kuwa freemasons ni mahali watu wanakwenda kupewa pesa!! hawaendi kupewa pesa, waliotoka huko na kumpa Bwana Maisha yao, wanasema “watu wote wanaojiunga huko ni wafanya kazi” na kule hawapewi pesa kana kwamba kuna ATM inayomwaga pesa…hapana! isipokuwa waliopo kule wanapeana fursa wao kwa wao, na ndio moja ya viapo vyao… freemasons wenzao waliopo ngazi za juu katika shughuli za ulimwengu kila mmoja ana jukumu la kumwangalia mwenzake aliye chini..

Kama mmoja yupo ngazi ya juu katika serikali anamnyanyua freemasons mwenzake aliye chini, kama mmoja ni mkurugenzi basi ikitokea nafasi ya kazi anamtafuta freemason mwenzake anamchomeka hapo n.k hiyo ndio maana unaona mtu aliyejiunga anaweza kupata maendeleo ya ghafla, na endapo akijitoa wananyang’anya ile nafasi, ndio maana unaona mtu anaporomoka ghafla. Lakini sio kwamba wanapewa hela za kimajini ambazo zinatokea tu kichawi! Huko ni kukosa maarifa!

UTAJITOAJE FREEMASON KAMA UMEJIUNGA?

Hivyo kama umejiunga huko! Kumbuka kujiunga kunakozungumziwa sio kwa kupitia facebook! Au mtandaoni….Kuna watu nimekutana nao, wanakuja kuomba msaada, wamedanganywa na matapeli facebook na kuambiwa wasipotuma kiasi fulani watakufa! Na hivyo wanaogopa na kutuma pesa! Hao ni matapeli..kujiunga kunakozungumziwa ni kule kuwasili kwenye hayo maukumbi yao, na kupewa viapo na kukutana na washirika wengine. Kama umejiunga kwa namna hiyo, mlango wa kutoka upo wazi.(www.wingulamashahidi.org)

Huko ulipo upo kwenye elimu ya shetani kamili, na nguvu za giza zimekufunika..Unamwabudu shetani sasa bila kujua, lakini ipo siku utamwabudu waziwazi, hivyo unayo nafasi ya kutoka…haijalishi uliapa kiasi gani! Kuwa utakitumikia chama hicho na endapo ukitaka kutoka utakufa! Nataka nikuambie hutakufa! Zaidi ya yote ukiendelea kukaa huko ndio utakufa.

Hapo ulipo fanya jambo moja la kiimani! Tubu! Na uwaambie mimi sio mmoja wenu tena! Watakutishia lakini hakuna kitakachokupata! Kwasababu aliye upande wako ni mkuu kuliko aliye upande wao. Na usiende tena huko, wala usifanye ibada zao, wala ishara zao, choma vito vyao, uniform zao, pamoja na mihamala yao..futa na namba za washirika wenzako. Tafuta kanisa la kiroho linaloamini injili kamili ya YESU KRISTO, dumu huko, Na ukae katika mafundisho ya Kweli ya Kristo Yesu. Au wasiliana nasi kupitia boxi la maoni hapo chini.

Kumbuka washirika wote wa Freemasons watakwenda kuzimu kwasababu wanamwabudu shetani kama wasipotubu! Hivyo kama hutatubu utakwenda kuzimu….Hivyo kwa hitimisho freemason ni nini?…jibu ni kikundi cha kishetani kinachomwabudu shetani.

Bwana akubariki.

Group la whatsapp Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10


Mada Nyinginezo:

JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.

USIPIGE MATEKE MCHOKOO!

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

VITA DHIDI YA MAADUI.

UNYAKUO.

JEHANAMU NI NINI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

70 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
amos
amos
1 year ago

how to join

Anonymous
Anonymous
1 year ago

kiukwel nimekuelewa ninaiman na mwenyez mungu ila naomba kujiunga tafadhari nisaidie

MKIRISTO KAMILI HUYU
MKIRISTO KAMILI HUYU
1 year ago

bwana apewe sifa heri kula tabu kulko matexo .Asante xna muhubiri ubarikiwe sna

Isaya Kemore
Isaya Kemore
1 year ago

Ubarikiwe sana kwa elimu unayoitoa kuwaelimisha watu.

Willy kisala
Willy kisala
1 year ago

Merci trop. Je comprends

Batman
Batman
1 year ago

Hata mm nataka kujiunga jamani tena kwa hamu kabsa

isack
isack
1 year ago

Leave your messagemy name isack nina taka kujua jinsi ya na kujiunga na nyinyi

oscar
oscar
1 year ago

Leave your message thenkx umenifungua macho

amisi bin selemani
amisi bin selemani
1 year ago

asante sana mwalimu kwa mafundisho. Umeibadilisha akili yangu kwanilivyo anza kuwazia kwaajili ya umasikini,nilianza kutamani nijiunge na freemason kama nitatajiri,pia nilianza ata kuabudu ma babu kwajili ya umasikini,naamba musaada wako wa maombi ili mungu anipokeye tena upya.

alex
alex
1 year ago
Reply to  Admin

je.n kafara za aina gan mtu anatoa jameni?

NJIGA
NJIGA
2 years ago

Yesu wang

Samuel wanjala
Samuel wanjala
2 years ago

Leave your message

Longinus Owino
Longinus Owino
5 months ago
Reply to  Samuel wanjala

Nataka kujoin illuminati tafadhali nisaidie asante

Vieri
Vieri
3 months ago
Reply to  Longinus Owino

Yes

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Leave your message

urmasawa ramathaney asan
urmasawa ramathaney asan
2 years ago

wao pia wanatoxhwa ushuru how apana vilembwesawa

Anonymous
Anonymous
2 years ago

waache ujinga wafanye kazi

HAJULIKAN
HAJULIKAN
2 years ago

tumkuelew ila freemasons sio watu wabaya kw kawaida freemasons inategemea na ww unachkitakaa ktoka kwao mfano unatak utajir wa aina gan au untaka kuw nani dunian na wtakusaidia ila mswala ya kutoa kafara uyu amatudangnya kidogo yule asiye toa kafara utajiri wake n mdogo mno ktokan n yey alivyo chguw kuw utkapo takapotak kpta pesa nyngi kutoka kwao au kuw mtu mkubw dunian ndo unewza kutoa kafara ya kiumbe yeyote yule na kiumbe yeyote yule utkaye mtoa kila mmja ana limit yke mfano mzuri ntkupa apa kuku mmoja hana dhamani at nusu ya ng,ombe mmja namaasha thamni ya pesa ngo,mbe mmja ndo mwny dhaman kuliko kuku mmja nd ivyovyo ilivyo kw miung y freemasons mtu anayetoa toa kafara y mbuzi na mt anaye toa kafar ya ngo,mbe ni vitu viwili tafauti kfara ya mbuzi ni ndgo kuliko kafar ya ngo,mbe maan iyo mbzi ni mdogo kuliko ngo,mbe maan iy umeelewa mtu atakay toa kafar ya mbuzi utajiri wke si mkubw kama w uyu mtu anaye toa kafara ya ngo,mbe na kuna viumb weng wa kutoa kafara mfano ngamia, chui, kondoo na ngo,mbe n.k antegmeana na unavyo tak ww kafara gan utapend kutoa kila kitu dunian kun ch kulipi mfn unapoenda kansani lazima utoe fung la kumi na sadak ya kawaida ili MUNGU aksaidie shida zako ivoivo kwa aw freemason ndivyo walivyo kam unatak kuw mtu mkubwa lazim utoe kafar kw miungu iyo ili ikusaidie kw kumlizia kafara ambyo sjaisema ni kafara ya binadam kafar y binadamu nd kubw kuliko zote kw sabab wmanadam ndio kiumbe mwny thaman kuliko wote kw maan iyo huw ni machaguo ya mtu kuamua kutoa kafara y binadamu ivoivo kw viumbe wengine kam nilvy sema apo nyuma kafara y binadam ndio yeny utajiri mkubw kulika kiumbe yeyote dunian kafara ya majini na malaika majini wali malaika hawfai kutoa kafara

Kibonge
Kibonge
2 years ago

Mungu akubariki

MUSTAMIU HASADI
MUSTAMIU HASADI
2 years ago

ASANTE KWA MAELEZO YAKO ILA NAMIM NATAKA KUJIUNGA

Meshack yiemi
Meshack yiemi
1 year ago

Also me l need to join

Willy K
Willy K
2 years ago

Mungu akubariki Sana

Anonymous
Anonymous
2 years ago

i’m greatfull for tchngs about frmnsn nlkwa natka kugnga nafrmnsn lkn nme acha i’m 16yrs

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Asante kwa somo zuri

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Kumbe huko kuna mammbo mengi

Anonymous
Anonymous
2 years ago

Balikiwa sana kwa mafundisho mazur MUNGU azidi kukufunulia mtu mishi nawe uendelee kunilisha zaidi

NICHOLAUS LENARD ABEID
NICHOLAUS LENARD ABEID
2 years ago

Nahitaji kujiung freemason kwa sababu moyo wangu umelizia sijalazimishwa na mtu yeyote

Anthony
Anthony
2 years ago

Asante umenifungua macho.

Steven Gidioni
Steven Gidioni
2 years ago

Asante ubalikiwe

Adam
Adam
2 years ago

Umenifungua macho yangu asante sana mungu akubaliki

Ohuru Milton
Ohuru Milton
3 years ago

Nimebarikiwa sana na nimeshukuru kwa ujumbe huu. Mola akujalie na akuzidishie neema zake uwe wake na akuongezee imani yako. Mwamini akuongoze. Umekuja kwa mponyaji.{Yesu Kristo}

PETER
PETER
3 years ago

NATAKA KUJIUNGA

Alex
Alex
3 years ago

mungu akubariki

Anonymous
Anonymous
3 years ago

Leave your message OK nimeelewa

Elvis onchoke
Elvis onchoke
3 years ago

I want to join freemason plz help me0759893142

Anonymous
Anonymous
3 years ago

Ameen

marcos benjamim joão
marcos benjamim joão
3 years ago

nataka kwingya

Samuel ndegwa
Samuel ndegwa
3 years ago

I won’t twe join because I need money

OSCAR MAINA SIFUNA
OSCAR MAINA SIFUNA
3 years ago

Ni lazima tu ni join eluminati ju sina pesa ninaona ka sina pesa ni vigumu kuwa duniani oky please i want to join na nitamwabudu lucifa na nitapokea mali yake i need a car aina ya veight by

Anonymous
Anonymous
3 years ago

asante umenisaidia sana akili yangu umeifungua kabisa bwana yesu asifiwe mungu akubariki

Max viketi
Max viketi
3 years ago

plz nataka ku jon

Senior OCs
Senior OCs
3 years ago

To GOD be the glory Halleluyah……let’s praise the lord for his almighty.

Anonymous
Anonymous
3 years ago

Asante sana tumsifu yesu kristo amen

silvesta
silvesta
4 years ago

namwamin mungu ndyo mweza ktk maisha yangu yote

Hassan
Hassan
4 years ago

Amin mungu juu

Anonymous
Anonymous
4 years ago

atukuzwe mungu wa mbinguni

Prospa kavano
Prospa kavano
4 years ago

Vp mm nataka kujiug filimason

Anonymous
Anonymous
4 years ago

Ubarikiwe

Anonymous
Anonymous
4 years ago

Apo nimekwelewa haswa

Christina muheza
Christina muheza
3 years ago
Reply to  Anonymous

Mimi nataka kujiunga

Harrison
Harrison
4 years ago

hakuna yeyote kama mungu

Dennis murangiri
Dennis murangiri
3 years ago
Reply to  Harrison

Mimi nataka kujiunga chama Freemason

Max Faida
Max Faida
4 years ago

Kiukweli nimeelewa sana ,Mungu wa mbinguni akubariki sana na Neema ya Bwana wetu Yesu kristo iendelee kutufunika siku zote za maisha yetu.

Kevoo
Kevoo
4 years ago
Reply to  Admin

Mungu akubariki sanaa

Sekuri olivier
Sekuri olivier
3 years ago
Reply to  Admin

Pole sana kwa wale walio jiunga na Freemasons bila kujua yesu awaangazie nuru yake watoke huko jehenama