Jina la Bwana YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze Biblia, Neno la Mungu wetu lilo njia na Mwanga wa njia yetu (Zab. 119:105).
Je! Umeokoka na kuna dhambi ambayo bado hujaiacha na hujui ufanye nini?.. Twende pamoja katika ujumbe huu utapata kitu au suluhisho la tatizo ulilo nalo.
Awali ya yote ni muhimu kufahamu kuwa, mtu anapoamua kwa dhati kabisa kutoka moyoni mwake kumfuata YESU, basi zile dhambi zote zilizokuwa zinamtesa ni lazima zife ndani yake!, lakini inapotokea mtu kaokoka lakini bado mambo ya kale yanamsumbua kuna SHIDA!
Fanya hivi ili upone hilo tatizo… ACHA HIYO DHAMBI!..ACHA KUITUMIA HIYO DHAMBI!. Huenda bado hujaelewa.. ni hivi.. ACHA HIYO DHAMBI.
Kitu chochote ukiacha kukitumia kinaisha nguvu na hatimaye kinakufa kabisa/kinapotea…hata chuma kisipotumika kinapata kutu na hatimaye kuharibika kabisa..Moto usipochochewa unakufa (Soma Mithali 26:20) na Dhambi isipotumika inakufa…Hiyo ndio tabia ya dhambi wengi tusiyoijua.. kuwa dhambi ina tabia ya KUFA.
Warumi 6:11 “Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa WAFU KWA DHAMBI na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu”.
Ukitaka kushinda dhambi ya “Kujichua”.. “Acha Kujichua”… Ukitaka kuacha dhambi ya Uzinzi acha uzinzi, ukitaka kuacha dhambi ya ulevi, acha ulevi, ukitaka kuacha matusi, acha kutukana, ukitaka kuacha hasira acha hasira..
Mithali 28:13 “Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye NA KUZIACHA atapata rehema”.
Utauliza.. “nitaachaje”.. Wazo linapokuja kichwani la kwenda kufanya hivyo, unaanza kulikataa likiwa huko huko kichwani, na kukubaliana na matokeo ya maumivu, kwasababu inakuhitaji kuingia gharama kushindani na dhambi….lakini ukijilegeza na kuitii dhambi itazidi kustawi ndani yako.
Ukishaikataa kichwani, ni wakati wa kuutiisha mwili wako, na kusema utafanya unachokisema na unachokitaka na sio mwili unachokitaka!… nakuhakikishia ukimaanisha kufanya hivyo, dhambi itakosa nguvu ndani yako!.. Kwani unapoamka kila siku asubuhi na kukatisha usingizi wako ili uwahi kwenye majukumu yako, mwili huwa unapenda??..
Huwa haupendi katika siku za mwanzo lakini unakuwa unajilazimisha tu…mpaka ile ratiba inapokaa akilini kiasi kwamba unafika wakati ukifika tu ule muda wa kuamka usingizi wenyewe unakata..kwanini!..ni kwasababu tayari umeshauua usingizi majira yale uliyozoea kuamka.. kwahiyo ukifika tu huo wakati hauhitaji kengele, tayari kengele ipo kwenye ubongo wako na usingizi unakuwa haupo huo muda..
Na dhambi ni hivyo hivyo, unaiacha na kuilazimisha isikae maishani mwako, na mwisho itakufa tu… mahali pale ulipozoea kukutana ili kulewa, zikifika zile saa hata kiu haipo, mitaa ambayo ulikuwa ukikatiza ni lazima utamani kulewa, sasa utaikatiza bila shida yoyote.
Aina ya watu ambao ulikuwa ukiwaona huwezi kuvumilia, unawaka tamaa…utafika wakati utawaona ni watu wa kawaida sana, tena utajishangaa ulikuwa ni mtu wa namna gani?
Rushwa ulizokuwa unakula, ambazo huwezi kufanya jambo bila kuhonga, utajishangaa hutamani tena kuchukua/kutoa rushwa..
Lakini ni lazima uingie gharama katika hatua za awali, usikubali kujilegeza.. na kusubiri muujiza wa wewe kuacha hayo…amua kubadilika kwa KUACHA DHAMBI.. ACHA DHAMBI, ACHA DHAMBI..Hakuna dawa nyingine zaidi ya hii ACHA!, na MUNGU atakusaidia..
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.
Je tamaa ni dhambi kulingana na Yakobo 1:15?
Ipi tofauti kati ya sadaka ya dhambi na sadaka za hatia?
NITAACHAJE DHAMBI?.
Biblia inamaana gani iliposema “Dhambi ilipozidi, Neema ilizidi kuwa nyingi Zaidi”.
SWALI: Mara nyingi biblia inataja “shuhuda za Mungu” Je hizi shuhuda ni zipi?
Mfano katika vifungu vifuatavyo Neno hilo utaliona;
Zaburi 119:2
[2]Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote.
Zaburi 119:22
[22]Uniondolee laumu na dharau, Kwa maana nimezishika shuhuda zako.
Zaburi 119: 24
[24]Shuhuda zako nazo ndizo furaha yangu, Na washauri wangu.
Zaburi 119:99
[99]Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo.
Soma pia…Zab 119:119, 144, 132:12
Hizi shuhuda ni zipi?
Shuhuda ni neno linalozaa ushuhuda au kushuhudia.
Ni kitendo cha kuthibitisha ukweli wa jambo.
Kwamfano nikisema yule “mtu ni mkarimu”. Hapo nimemshuhudia kwasababu nimeona kitu hicho ndani yake, aidha amenitendea mimi ukarimu au kamtendea mwingine..
Tofauti na kama angejisemea mwenyewe..
Hivyo Mungu naye ana vitu amevihakiki kuwa ni kweli, na hizo ndizo zinazoitwa shuhuda zake..
Mpaka jambo Mungu amelihakiki mwenyewe ni kutuhakikishia kuwa hatupotei tukilifuata, tofauti na kama tungeshuhudiwa na wanadamu…kwasababu shuhuda za wanadamu zina udanganyifu mwingi nyuma yake.
Yesu Kristo ni mwana wa Mungu na ndiye uzima wetu.
1 Yohana 5:7-12
[7]Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. 9… Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe. [10]Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe. [11]Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. [12]Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.
[7]Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.
9… Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe.
[10]Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.
[11]Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.
[12]Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.
Huu ndio ushuhuda mkuu wa Mungu, na huu ndio tuliopewa tuuhubiri kwa ulimwengu pia kwamba kwa Yesu kuna ukombozi, na uzima..
Matendo ya Mitume 4:33
[33]Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote.
Sisi (tulioamini) ni wana wa Mungu Huu ni ushuhuda mwingine wa Mungu mwenyewe ndani yetu kupitia Roho wake Mtakatifu.
Warumi 8:16-17
[16]Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; [17]na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
[16]Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;
[17]na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
Si Kristo tu peke yake ni mwana wa Mungu, na sisi pia tunapomwamini tunafanyika watoto wake (Yohana 1:12 )watoto wa Mungu mfano wa Kristo.
Hivyo tunapopitia mateso kama yeye, hatupaswi kuwa na hofu au manung’uniko, kinyume chake ndio tujipige vifua vyetu kushangilia, kwani hata yule wa pekee(Yesu), aliyapitia hayo…kwasababu kama vile alivyopata mateso na alivyorithi utukufu vivyo hivyo na sisi tutarithi utukufu wake.
Mungu anataka tutembee kwa ujasiri hapa duniani, tusiishi kama yatima, tuishi tukijua kuwa tunaye Baba mbinguni anayetutazama na kujishughulisha sana na mambo yetu yote, kwasababu yeye mwenye ametuthibitisha kuwa sisi ni wana wake…Kama yeye ametuthibitisha nafsi yako kwanini ipinge? Wanadamu kwanini wapinge, ulimwengu kwanini upinge?
Hivyo kwa hitimisho ni kuwa tunaposema tumezishika shuhuda zake maana yake ni kuwa tumeamini wokovu na uzima utokao kwa Kristo Yesu, lakini pia tumekubali kuwa wana wa Mungu, yaani tukubali dhiki kwa ajili ya jina lake, tuishipo maisha ya kumpendeza yeye, lakini pia kupokea tumaini la utukufu lililo mbele yetu.
DHAMBI HAIWEZI KUKAA NA MSHAHARA WAKO.
USHUHUDA WA RICKY:
FUNGUA KINYWA CHA ROHO MTAKATIFU KIHUDUMU.
WhatsApp
Jibu: Turejee..
Kumbukumbu la Torati 11:15 “Nami nitakupa nyasi katika MAVUE yako kulisha wanyama wako wa mifugo, nawe utakula na kushiba”.
“Mavue” ni kiswahili kingine cha “mashamba”….shamba likiwa moja linaitwa “VUE” yakiwa mengi “MAVUE”.
Kwahiyo hapo anaposema “Nitakupa nyasi katika mavue yako”.…maana yake nitakupa nyasi katika mashamba yako.
Hii ni ahadi ya Mungu kwa wana wa Israeli, na ni ahadi ya MUNGU kwetu pia, ikiwa tutayashinda
Tuanzie ule mstari wa 13..
Kumbukumbu 11:13-15 “Tena itakuwa, mtakaposikiza kwa bidii maagizo yangu niwaagizayo leo, kwa kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kumtumikia kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote, 14 ndipo nitakapowapa mvua ya nchi yenu kwa wakati wake, mvua ya masika, na mvua ya vuli, upate kuvuna nafaka yako, na divai yako, na mafuta yako. 15 Nami nitakupa nyasi katika MAVUE YAKO kulisha wanyama wako wa mifugo, nawe utakula na kushiba”.
Kumbukumbu 11:13-15 “Tena itakuwa, mtakaposikiza kwa bidii maagizo yangu niwaagizayo leo, kwa kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kumtumikia kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote,
14 ndipo nitakapowapa mvua ya nchi yenu kwa wakati wake, mvua ya masika, na mvua ya vuli, upate kuvuna nafaka yako, na divai yako, na mafuta yako.
15 Nami nitakupa nyasi katika MAVUE YAKO kulisha wanyama wako wa mifugo, nawe utakula na kushiba”.
Neno hili pia tunalisoma katika
Maandiko yafuatayo…
1Samweli 25:15 na 1Samweli 30:11.
Je umempokea Bwana YESU KRISTO?..
Kama bado unasubiri nini mpendwa?..Fahamu ya kuwa kwa jinsi unavyozidi kuendelea kuishi maisha ya dhambi
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.
Neno utakaso mara nyingi, tunalitazama katika jicho la Mungu kututakasa sisi (1Thes 5:23), lakini pia sisi kujitakasa wenyewe (1Petro 1:22), lakini tunasahau kuwa Kristo naye tunamtakasa… maandiko yanasema hivyo katika,
1 Petro 3:14
[14]Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu.
Kama Kristo anatakaswa? Swali ni je! Anatakaswaje wakati yeye ni mkamilifu?
Hapo anasema;
‘mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu’.
Kumbe ni mioyoni mwetu, sio kwamba yeye mwenyewe tumtakase mahali alipo (hawezi kutakaswa kwasababu yeye ni msafi). Mioyo yetu ndio humfanya aonekane kivingine.
Kutakasa ni kukifanya kitu kiwe kisafi au kiwe kikamilifu tena, kurejea katika hadhi yake iliyopotezwa.
Sasa kumtakasa Yesu moyoni, ni sawa na kumfanya Yesu awe jasiri tena, ajae utukufu wake, ajawe na raha na fahari yote ndani ya mtu.
Haya ni mambo ambayo ukiyatenda/ kuyakubali basi unamtakasa sana Yesu moyoni mwako
Sawasawa na hilo andiko hapo juu anasema..
Zipo nyakati ambazo utachukiwa bure kwasababu umekataa uongo, au utafukuzwa kazi kwasababu umekataa rushwa, au utafungwa kwasababu unahubiri injili ,au utapigwa kwasababu unakemea dhambi..
Nyakati kama hizi wengine huzikwepa, na kuamua kusimama na maovu ili tu kuepusha madhara yatakayowapata… hawajui kuwa wanamweka Kristo kando.
Matokeo yake Yesu anakosa kutukuzwa ndani yetu, kwasababu yeye naye alikubali kuteswa kwa kusimamia ukweli na haki, akapigwa, akasulubiwa kwa kifo cha aibu.. Hivyo atakapoona watu pia wanafuata Nyayo zake, hutakasika sana, hujitukuza sana ndani ya huyo mtu, hujithibitisha kuwa kazi yake kamilifu huendelea kumulika gizani.
Hivyo usikwepe mapito yenye gharama, wala usihuzunishwe nayo maadamu ni haki unayoisimamia. Mtakase Kristo.
Lakini pia..
Waefeso 1:6-7
[6]Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa. [7]Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
[6]Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.
[7]Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
Kwa jinsi unavyoitambua kazi ya Kristo aliyoitenda kwa ajili yako pale msalabani kwamba kwa kupigwa kwake umepokea neema na ukombozi kupitia msamaha wa dhambi ndivyo unavyomtakasa Kristo moyoni mwako.
Tumia muda mwingi kutafakari juu ya neema ya wokovu, kisha msifu na kumtukuza na kumshukuru juu ya hilo. Kristo anapoona umeithamini kazi yake, huinuka sana moyoni mwako.
Utakumbuka yule mwanamke kahaba na Miriamu ndugu yake Martha walivunja vibweta vya marhamu vyenye thamani nyingi, wakampaka Yesu kichwani na miguuni, mpaka wengine wakasema ni upotevu mkubwa sana..lakini Yesu alipoona alisema wametenda kazi njema juu yake, (Marko 14:3-9, Luka 7:36-50).
Jifunze kumtolea Kristo sadaka zaidi hata kipimo chako cha sikuzote, sio kwamba unamshawishi Yesu kwa vitu, (yeye hashawishi na hivyo)..Lakini anapendezwa sana, na watoaji, anatakasika sana pale unapofanya kitu cha ziada kwa ajili ya Mungu wako. Jifunze kutoa sana sadaka.
Yesu anajaa utukufu na waombaji…utakumbuka alikuwa na mitume kumi na wawili…lakini waliokuwa tayari kudumu naye katika masafa ya ndani ya kimaombi walikuwa ni watatu; yaani Petro Yohana na Yakobo.
Na wakati ule alipopanda juu ya ule mlima mrefu(Mathayo 17), ghafla walimwona katika utukufu mwingine wa ajabu, nguo zake zilikuwa zikimeta-meta kwa weupe mkuu.. wakashangaa na kuingiwa na hofu..
Lakini Yesu asingeweza kubadilika mbele yao, kama wangekuwa mbali na yeye katika maombi.
Hivyo unapozama sana katika uombaji, ndivyo unavyomtakasa Kristo ndani yako. Anajiona safi na mkamilifu.
Kwa hitimisho ni kuwa, unapokubali mateso pamoja na Yesu, unapo msifu sana kwa kazi yake ya msalaba, unapotoa sadaka zako nyingi na unapokuwa mwombaji.
Moyoni unahesabika kuwa unamtakasa Bwana wako sana.
Shalom, Mungu akubariki.
WALAWI WALIKUWA WENYE MIOYO YA ADILI KWA KUJITAKASA KULIKO MAKUHANI.
Kanisa kama sehemu ya maisha ya mwamini mpya.
SHUGHULIKA NA HASIRA INAYOKAA KIFUANI
Swali: Je nikiomba kazi kwa mwaka mmoja na ikatokea fursa ambayo inanitaka nitoe rushwa kidogo ili niingie kazini, je hilo ni Jibu la Maombi yangu, au ni jaribu?
Jibu: Hilo si jibu la Maombi, bali ni “Jaribu” linaloletwa na ibilisi mbele yako. Majibu ya Maombi hayana njia za mkato, yanakuwa yamenyooka na yenye kibali.
Lakini inapotokea tunaomba jambo kwa Mungu atutendee, halafu inatokea fursa nyingine iliyo kinyume na Neno la MUNGU, hilo ni jaribu na tunapaswa tulishindwe.
Mfano mwingine ni pale mtu ameomba hitaji fulani kwa Mungu labda fedha ya kodi, halafu inatokea fursa ya wizi, utakaokamilisha kile kiasi.. sasa hiyo fursa si kutoka kwa MUNGU hata kama inakupa wepesi mkubwa wa kupata kile kiasi, bali ni Jaribu la maombi yako, na ni lazima kulishinda.
Au unaomba mume halafu anakuja Mume wa Mtu kutaka kukuoa, hayo sio majibu ya maombi bali ni majaribu..
Na yapo mambo mengine mengi, yanayokuja kwa sura ya Majibu ya Maombi, lakini nyuma yake ni Majaribu ya maombi.
Sasa ni kwa namna gani tunaweza kutofautisha Majibu na Majaribu?.
Hakuna njia nyingine zaidi ya “KULIJUA NENO LA MUNGU”..Na hatulijui Neno la Mungu kwa kukariri mistari ya Biblia, au kuelezewa bali kwa “KUJIFUNZA BIBLIA”.
Huwezi kujua dhambi ni nini kama hauijui Biblia..
Warumi 7:7 “Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani”.
Pia hatutaweza kuyajua majaribu ya ibilisi kama hatutalijua Neno la MUNGU ndani ya Biblia takatifu.
Weka desturi za kusoma Biblia kwa kujifunza, usiwekeze tu peke yake katika Maombi na ukaliacha Neno la Mungu pembeni, ukiwa mtu wa namna hiyo, ibilisi atakuletea majaribu ukidhani ndio majibu ya maombi yako, na kufanya mfungo wako au maombi yako kuwa si bure.
Wakolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu”.
Bwana atusaidie.
NYAKATI TOFAUTI- TOFAUTI ZA UPENDO.
MAJARIBU 10 WANA WA ISRAELI WALIYOMJARIBU MUNGU.
NI KWA NAMNA GANI TUTASHINDA MAJARIBU?
KISIMA BADO KINA MAJI, KIFUKUE TENA.
FAIDA NYINGINE YA MAOMBI YA KUSHUKURU.
Kama ni msomaji wa biblia, Neno hilo utakutana nalo katika baadhi ya vifungu kwenye Zaburi..
Zaburi 11:2
[2]Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta, Wanaitia mishale yao katika upote, Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.
Zaburi 21:12
[12]Kwa maana utawafanya kukupa kisogo, Kwa upote wa uta wako ukiwaelekezea mishale.
Upote ni ule uzi mwembamba unaofungwa kwenye uta, ambao mshale huwekwa pale kwa kuvutwa na kurushwa.
Upote hutengenezwa kwa ngozi na wakati mwingine kamba za mimea imara.. ni lazima utengenezwe kwa malighafi imara, ili isikatike pale unapovutwa.
Kwasababu hizi ni zana za kivita…kiroho hufunua pale mbili. Adui hutengeneza upote wake, ambao hurushia watu mishale ya moto ili kuwaua kiimani (Waefeso 6:16), ili kuweza kuishinda, biblia inatufundisha daima tuibebe ngao ya Imani.
Lakini pia Bwana Yesu anao upote wake ambao kwa huo hutupa silaha zake kwa adui zetu, sawasawa na hiyo Zaburi 21:12, Na silaha za Kristo zina nguvu sana sio tu kumlenga adui lakini pia kuangusha ngome.
Maboma na makao ya shetani.
2 Wakorintho 10:4-5
[4](maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) [5]tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
[4](maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
[5]tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
Lakini Nguvu ya silaha hizi hutegemea na hali ya mtu kiroho katika maeneo matatu;
1) kimaombi,
2)Utakatifu
3) Injili.
Mwamini wa namna hii ambaye huchukia dhambi, huubiri injili na huzingatia kudumu katika maombi ya masafa,
Kiroho ni askari imara na mwenye silaha zenye nguvu sana, ziwezazo kumuharibu ibilisi.
Kuwa askari kamili wa Kristo
Mtambo/mitambo ni nini kibiblia?
Na kipenu ni nini (Isaya 1:8)
Kutawa ni nini? Sawasa na Luka 1:24
Jina la Mwokozi Mkuu YESU KRISTO, libarikiwe.
Kabla ya kusogea mbele kujifunza ujumbe huu, ni vizuri tukarejea sehemu ya kwanza ya ujumbe huu inayosema “FAHAMU JINSI YA KUPATA MAMLAKA YA DAMU YA YESU”
Katika ujumbe huo tuliona ni kwa namna gani tunaweza kuwa na uhalali wa kuitumia Damu ya YESU, ikiwa tutakuwa ndugu zake, fuatilia ujumbe huo hapa >>>FAHAMU JINSI YA KUPATA MAMLAKA YA DAMU WA YESU.
Sasa kuna umuhimu mkubwa sana wa “KUYAJUA” na “KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU”.. Kwani hiyo ndio tiketi ya ‘KUMWONA MUNGU’ siku ya mwisho.
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni”.
Na tena Neno la Mungu linatusisitiza kutafuta kuyafanya mapenzi ya Mungu kwa bidii muda tuliobakiwa nao hapa duniani..
1Petro 4:2 “Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali KATIKA MAPENZI YA MUNGU, WAKATI WENU ULIOBAKI WA KUKAA HAPA DUNIANI”.
Sasa Mapenzi ya MUNGU yamegawanyika katika sehemu kuu Mbili.. 1) Mapenzi ya Mungu kwa Mtu binafsi, na 2) Mapenzi ya Mungu kwa watu wote.
Ni lazima tufanye Mapenzi ya Mungu katika migawanyiko yote hii miwili.. ni kama sheria, zipo sheria ulizojiwekea wewe, na zile ulizowekewa na nchi, ni lazima zote uziishi. Hali kadhalika yapo mapenzi ya Mungu kwako wewe au mimi binafsi, na yale Mapenzi ya Mungu kwa watu wote.. hebu tutazame moja baada ya lingine.
1. MAPENZI YA MUNGU KWA MTU BINAFSI.
Hili ni kusudi ambalo Mungu anataka ulifanye ukiwa hapa duniani kupitia karama, au nafasi uliyopewa na MUNGU. Ni lazima ufahamu duniani umeitiwa kufanya nini wewe kama wewe.. Kama umeitwa kuwa Askofu, au mwalimu, au mchungaji, au nabii, au mtume, au mwinjilisti, au mtu mwenye kukirimu, au mshauri, au mwingine yoyote katika nafasi yoyote ile kwa ajili ya ufalme wa MUNGU.
Usipojua mapenzi ya MUNGU ni yapi ni ngumu kuishi kwa kumpendeza MUNGU, kwasababu utafanya jambo lisilompendeza Mungu, utaishi mahali pasipompendeza Mungu, utaenda katika njia ambayo Mungu hajaikusudia juu yako.
Na mapenzi ya Mungu yanatofautiana kwa mtu na mtu.. anavyotembea mwingine si sawa na utakavyotembea wewe,..lakini wewe umekusudiwa njia yako tofauti na mwingine, ni lazima uijue.
Sasa unajuaje kusudi/mapenzi ya Mungu kwako?
Njia ya kwanza ni ya kumpokea YESU na kutubu dhambi.. baada ya hapo, kuomba huku ukidumu katika kumpenda MUNGU, Roho Mtakatifu atakuongoza katika kusudi lake, na ukikaa katika kusudi/mapenzi ya MUNGU, utaona amani ya kiMungu ndani yako, na pia mafanikio katika utumishi huo.
Na utakapojaribu kuacha njia hiyo utaona mambo hayaendi kabisa..hapo utajua kuwa ulikuwa kwenye njia sahihi ya mapenzi ya MUNGU.
2. MAPENZI YA MUNGU KWA WATU WOTE.
Baada ya kujua mapenzi ya MUNGU kwako ni yapi, kwamba unapaswa ufanye nini, wakati mwingine uishi wapi, au utembee na nani safari bado haijaisha ni lazima pia uyajue mapenzi ya MUNGU kwa watu wote, aliyoyakusudia kila mtu ayaishi.
Sasa hayo mapenzi ya MUNGU kwa wote ni yapi?.. Tusome maandiko yafuatayo..
1Wathesalonike 4:3 “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; 4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; 5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.
1Wathesalonike 4:3 “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;
5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.
Kumbe mapenzi ya Mungu kwetu sote ni KUTAKASWA (Yaani utakatifu), na TUEPUKANE NA UASHERATI (wa mwilini na rohoni) na TUJUE KUIWEZA MIILI YETU KATIKA UTAKATIFU na HESHIMA.
Hapa ndipo shetani anapofumba macho wengi.. ni kweli tumejua mapenzi ya MUNGU kwetu ni kumtumikia, kumwimbia, kuhubiri, kufanya uinjilisti, lakini tumekosa kujua kuwa mapenzi ya MUNGU kwetu wote (kama watu wa Mungu) ni kuishi maisha matakatifu, yenye staha mwilini na rohoni.
Utakuta mkristo ameokoka anamwimbia Mungu, anahubiri na kweli wito wa MUNGU ndio uliomweka hapo, lakini tazama uvaaji wake, tazama maisha yake ya sirini, ni dhambi tupu imetawala.
Ni lazima kuyafanya mapenzi ya Mungu katika migawanyiko yote.
Bwana atusaidie sana kuliona hili, na yeye ni mwaminifu hajatuitia kwa hukumu bali tupate Baraka na faida, usiukimbie utakatifu ndugu mpendwa katika KRISTO, pasipo huo hatutaweza kumwona MUNGU (Waebrania 12:14).
Na kwa nguvu zetu hatutaweza kuishi maisha hayo ya usafi, lakini kwa msaada wa Roho Mtakatifu yote yanawezekana, tafuta ujazo wa Roho Mtakatifu.
Ipi tofauti ya utakatifu na utukufu?
CHAGUA UTAKATIFU MWAKA HUU.
JAWA SANA MOTO ULAO.
JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?
UVUKISHE MIPAKA UPENDO WAKO.
Warumi 6:23
[23]Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Kwenye vifungu hivyo tunaonyeshwa kuwa Mungu hutoa zawadi (karama), lakini dhambi inalipa mshahara.. Na mpaka ilipe mshahara ni lazima kazi fulani ilifanyika..
Watu wengi hawajua kuwa kila tendo moja la dhambi, huhesabu mshahara fulani na mwishoni mtu huyo hulipwa wote, hata kama hakujua.
Unapokwenda kuzini leo, unarudia tena na kesho, na kesho kutwa hivyo hivyo, mshahara unajilimbikiza, siku isiyo na jina utashangaa tu ghafla mshahara wako huo hapo umekufikia…
Ndio hapo mauti ya kiroho au ya kimwili au ya jambo fulani humfikia mtu.
Sasa inapofikia wakati wa mshahara wengi hujifanya haiwahusu, lakini utaupokea tu.. upende usipende…wengi humdharau Yuda kwanini alijinyonga, si kwamba alipenda lakini ulikuwa ni wakati wa mashahara, ukiona leo watu wanakutana na madhara makubwa kwasababu ya dhambi zao, sio kwamba wana bahati mbaya, bali ni wakati wa mshahara.
Epuka dhambi, ikimbie dhambi.
Shalom
Yeremia 2:13
[13]Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji.
Ndugu Ipo tofauti kati ya chemchemi na birika, chemchemi ni chanzo cha asili ambacho hutoa maji yake yenyewe, haihitaji kuchimbwa, wala kukarabatiwa lakini birika ni hivi visima ambavyo mtu hutumia jasho lake kuchimba na hutegemea mvua ili kuwa na maji, lakini bado huvujisha maji yake chini ya ardhi ndio maana baadaye hukauka…maji ya visima kikawaida hayawagi masafi sana kwasababu hayatembei, ni rahisi kuona vyura, ngala, ruba, tofauti na ya chemchemi.
Sasa Bwana anasema watu wake wamefanya makosa MAWILI. Kwanza wamemuacha yeye aliye chemchemi ya maji ya uzima, Maana yake wana kiu, lakini hawataki maji yaondoayo kiu…hicho huitwa kiburi, au dharau na matokeo ya kiburi ni maangamizi. Ni sawa na mtu anajijua kabisa ni mgonjwa halafu analetewa tiba anasema sinywi dawa zako.
Lakini kama hilo halitoshi, wanaenda kufanya kazi ya kuunda chemchemi zao bandia, kwa kuchimba wenyewe ili wajihifadhie maji yao ambayo ni ya muda…hii ndio huitwa ibada ya sanamu..watu wanapoona fedha inaweza kusimama badala ya Mungu, hiyo ni sawa na kujichimbia birika ..wanapoona elimu, ushirikina, anasa, ulevi, ujuzi..vinatosha kuwa mbadala wa Mungu ni kujichimbia birika lako mwenyewe..
Ndio maana wanataabika, kutafuta ukweli wote ndani yake hawapati, wanapata raha za kitambo baada ya hapo ni majuto kurudi.
Ndugu tulia kwa Kristo ambaye alishamaliza kuunda chemchemi yake, kwake yeye huhitaji kutendea kazi, nenda tu unywe maji, kiu ya dhambi na mambo mengine maovu ya kidunia ife, uishi maisha ya amani na kustawi. Maji hayo ukinywa hata ukifa utakuwa unaishi, na kumpokea Yesu ndio kuyapokea maji. Ukimwamini Yesu na kumfanya Bwana na mwokozi wa maisha yako, na kumtii baada ya hapo ujue ndani ya roho ya maji yameshawasili.
Yohana 4:13-14
[13]Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; [14]walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
[13]Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;
[14]walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
Achana na mabiriki.
Mungu atusaidie.
Matumizi ya damu ya YESU hayaishii tu katika kutamka, kwamba tukiwa na haja na jambo tunatamka “Kwa Damu ya YESU” na jambo lile linatokea au linatii… hapana ni zaidi ya hapo, kwasababu hata mashetani wanamjua Bwana YESU na Damu yake.
Hivyo hayatishiki na mtu wa kawaida kulitaja jina la YESU au Damu ya YESU na huku mtu huyo hana uhalali, au mamlaka ya kutumia Jina hilo, soma kilichowatokea Wana saba wa Skewa (Matendo 19:4) unaweza kuelewa zaidi.
Sasa Mamlaka ya kutumia DAMU YA YESU, tunapataje?
Tunapata mamlaka ya kutumia DAMU YA YESU kwa kanuni moja tu!, nayo ni ile ya kuwa na UNDUGU WA DAMU NA YESU?
Utauliza mtu anaweza kuwa na undugu wa Damu na YESU na mwingine asiwe nao?..
Ndio!, hiyo inawezekana kabisa na nitakuonyesha kimaandiko…Lakini tambua jambo moja kuwa ili mtu aitwe ndugu yako ni lazima muwe na mfanano wa damu, mnaweza msifanane sura, au mwonekano lakini bado damu ikaeleza undugu mlio nao (hiyo imethibitika kisayansi na wanadamu).
Na YESU KRISTO anao ndugu zake wa damu.. sasa tunawajuaje?.. tusome maandiko yafuatayo Mathayo 12:47
Mathayo 12:47 “Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe. 48 Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani? 49 Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu! 50 Kwa maana ye yote ATAKAYEYAFANYA MAPENZI YA BABA YANGU aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu”.
Mathayo 12:47 “Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe.
48 Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani? 49 Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu!
50 Kwa maana ye yote ATAKAYEYAFANYA MAPENZI YA BABA YANGU aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu”.
Umeona? Ndugu za YESU wana sifa gani?… hawana sifa ya usomi, au uzuri, au ukuu au umaarufu… bali ni wale wote WANAOFANYA MAPENZI YA BABA ALIYE MBINGUNI.
Kumbe ili tuwe NDUGU WA DAMU WA YESU, ni lazima TUYAJUE na KUYAFANYA MAPENZI YA BABA MBINGUNI?.
Je unayajua mapenzi ya MUNGU kwako?.. Kama huyajui je unawezaje kuwa na ujasiri wa kuitumia DAMU YAKE, na ilihali huna muunganiko wowote na hiyo DAMU?
Ni lazima uyajue mapenzi ya MUNGU, na KUYAFANYA.. ili ile damu iweze kunena mema juu yako (Waebrania 12:24).
Je wewe ni ndugu wa YESU?… Je unayajua Mapenzi ya MUNGU kwako?.. kama bado huyajui au huna uhakika kama unayafanya mapenzi yake au la!, basi usikose sehemu inayofuata ya somo hili inayozungumzia MAPENZI YA MUNGU.
Waebrania 2:11 “Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake; 12 akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa. 13 Na tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye. Na tena, Tazama,mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu. 14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, 15 awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa”.
Waebrania 2:11 “Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;
12 akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa.
13 Na tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye. Na tena, Tazama,mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu.
14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,
15 awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa”.
Bwana atusaidie..
MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.
Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela.
SAFARI YA KUUONA USO WA MUNGU.
Tofauti kati ya kuhukumu na kulaumu ni ipi?
Nini tofauti ya kushuhudia na kuhubiri?