Jibu: Turejee..
Kumbukumbu la Torati 11:15 “Nami nitakupa nyasi katika MAVUE yako kulisha wanyama wako wa mifugo, nawe utakula na kushiba”.
“Mavue” ni kiswahili kingine cha “mashamba”….shamba likiwa moja linaitwa “VUE” yakiwa mengi “MAVUE”.
Kwahiyo hapo anaposema “Nitakupa nyasi katika mavue yako”.…maana yake nitakupa nyasi katika mashamba yako.
Hii ni ahadi ya Mungu kwa wana wa Israeli, na ni ahadi ya MUNGU kwetu pia, ikiwa tutayashinda
Tuanzie ule mstari wa 13..
Kumbukumbu 11:13-15 “Tena itakuwa, mtakaposikiza kwa bidii maagizo yangu niwaagizayo leo, kwa kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kumtumikia kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote, 14 ndipo nitakapowapa mvua ya nchi yenu kwa wakati wake, mvua ya masika, na mvua ya vuli, upate kuvuna nafaka yako, na divai yako, na mafuta yako. 15 Nami nitakupa nyasi katika MAVUE YAKO kulisha wanyama wako wa mifugo, nawe utakula na kushiba”.
Kumbukumbu 11:13-15 “Tena itakuwa, mtakaposikiza kwa bidii maagizo yangu niwaagizayo leo, kwa kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kumtumikia kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote,
14 ndipo nitakapowapa mvua ya nchi yenu kwa wakati wake, mvua ya masika, na mvua ya vuli, upate kuvuna nafaka yako, na divai yako, na mafuta yako.
15 Nami nitakupa nyasi katika MAVUE YAKO kulisha wanyama wako wa mifugo, nawe utakula na kushiba”.
Neno hili pia tunalisoma katika
Maandiko yafuatayo…
1Samweli 25:15 na 1Samweli 30:11.
Je umempokea Bwana YESU KRISTO?..
Kama bado unasubiri nini mpendwa?..Fahamu ya kuwa kwa jinsi unavyozidi kuendelea kuishi maisha ya dhambi
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Print this post
Neno utakaso mara nyingi, tunalitazama katika jicho la Mungu kututakasa sisi(1Thes 5:23), lakini pia sisi kujitakasa wenyewe (1Petro 1:22), lakini tunasahau kuwa Kristo naye tunamtakasa… maandiko yanasema hivyo katika,
1 Petro 3:14
[14]Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu.
Kama Kristo anatakaswa? Swali ni je! Anatakaswaje wakati yeye ni mkamilifu?
Hapo anasema;
‘mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu’.
Kumbe ni mioyoni mwetu, sio kwamba yeye mwenyewe tumtakase mahali alipo(hawezi kutakaswa kwasababu yeye ni msafi). Mioyo yetu ndio humfanya aonekane kivingine.
Kutakasa ni kukifanya kitu kiwe kisafi au kiwe kikamilifu tena, kurejee katika hadhi yake iliyopotezwa.
Sasa kumtakasa Yesu moyoni, ni sawa na kumfanya Yesu awe jasiri tena, ajae utukufu wake, ajawe na raha na fahari yote ndani ya mtu.
Haya ni mambo ambayo ukiyatenda/ kuyakubali basi unamtakasa sana Yesu moyoni mwako
Sawasawa na hilo andiko hapo juu anasema..
Zipo nyakati ambazo utachukiwa bure kwasababu umekataa uongo, au utafukuzwa kazi kwasababu umekataa rushwa, au utafungwa kwasababu unahubiri injili ,au utapigwa kwasababu unakemea dhambi..
Nyakati kama hizi wengine huzikwepa, na kuamua kusimama na maovu ili tu kuepusha madhara yatakawapata… hawajui kuwa wanamweka Kristo kando.
Matokeo yake Yesu anakosa kutukuzwa ndani yetu, kwasababu yeye naye alikubali kuteswa kwa kusimamia ukweli na haki, akapigwa, akasulubiwa kwa kifo cha aibu.. Hivyo atakapoona watu pia wanafuata Nyayo zake, hutakasika sana, hujitukuza sana ndani ya huyo mtu, hujithibitisha kuwa kazi yake kamilifu huendelea kumulika gizani.
Hivyo usikwepe mapito yenye gharama, wala usihuzunishwe nayo maadamu ni haki unayoisimamia. Mtakase Kristo.
Lakini pia..
Waefeso 1:6-7
[6]Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa. [7]Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
[6]Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.
[7]Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
Kwa jinsi unavyoitambua kazi ya Kristo aliyoitenda kwa ajili yako pale msalabani kwamba kwa kupigwa kwake umepokea neema na ukombozi kupitia msamaha wa dhambi ndivyo unavyomtakasa Kristo moyoni mwako.
Tumia muda mwingi kutafakari juu ya neema ya wokovu, kisha msifu na kumtukuza na kumshukuru juu ya hilo. Kristo anapoona umeithamini kazi yake, huinuka sana moyoni mwako.
Utakumbuka yule mwanamke kahaba na Miriamu ndugu yake Martha walivunja vibweta vya marhamu vyenye thamani nyingi, wakampaka Yesu kichwani na miguuni, mpaka wengine wakasema ni upotevu mkubwa sana..lakini Yesu alipoona alisema wametenda kazi njema juu yake, (Marko 14:3-9, Luka 7:36-50).
Jifunze kumtolea Kristo sadaka zaidi hata kipimo chako cha sikuzote, sio kwamba unamshawishi Yesu kwa vitu, (yeye hashawishi na hivyo)..Lakini anapendezwa sana, na watoaji, anatakasika sana pale unapofanya kitu cha ziada kwa ajili ya Mungu wako. Jifunze kutoa sana sadaka.
Yesu anajaa utukufu na waombaji…utakumbuka alikuwa na mitume kumi na wawili…lakini waliokuwa tayari kudumu naye katika masafa ya ndani ya kimaombi walikuwa ni watatu; yaani Petro Yohana na Yakobo.
Na wakati ule alipopanda juu ya ule mlima mrefu(Mathayo 17), ghafla walimwona katika utukufu mwingine wa ajabu, nguo zake zilikuwa zikimeta-meta kwa weupe mkuu.. wakashangaa na kuingiwa na hofu..
Lakini Yesu asingeweza kubadilika mbele yao, kama wangekuwa mbali na yeye katika maombi.
Hivyo unapozama sana katika uombaji, ndivyo unavyomtakasa Kristo ndani yako. Anajiona safi na mkamilifu.
Kwa hitimisho ni kuwa, unapokubali mateso pamoja na Yesu, unapo msifu sana kwa kazi yake ya msalaba, unapotoa sadaka zako nyingi na unapokuwa mwombaji.
Moyoni unahesabika kuwa unamtakasa Bwana wako sana.
Shalom, Mungu akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
WALAWI WALIKUWA WENYE MIOYO YA ADILI KWA KUJITAKASA KULIKO MAKUHANI.
Kanisa kama sehemu ya maisha ya mwamini mpya.
SHUGHULIKA NA HASIRA INAYOKAA KIFUANI
Kama ni msomaji wa biblia, Neno hilo utakutana nalo katika baadhi ya vifungu kwenye Zaburi..
Zaburi 11:2
[2]Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta, Wanaitia mishale yao katika upote, Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.
Zaburi 21:12
[12]Kwa maana utawafanya kukupa kisogo, Kwa upote wa uta wako ukiwaelekezea mishale.
Upote ni ule uzi mwembamba unaofungwa kwenye uta, ambao mshale huwekwa pale kwa kuvutwa na kurushwa.
Upote hutengenezwa kwa ngozi na wakati mwingine kamba za mimea imara.. ni lazima utengenezwe kwa malighafi imara, ili isikatike pale unapovutwa.
Kwasababu hizi ni zana za kivita…kiroho hufunua pale mbili. Adui hutengeneza upote wake, ambao hurushia watu mishale ya moto ili kuwaua kiimani (Waefeso 6:16), ili kuweza kuishinda, biblia inatufundisha daima tuibebe ngao ya Imani.
Lakini pia Bwana Yesu anao upote wake ambao kwa huo hutupa silaha zake kwa adui zetu, sawasawa na hiyo Zaburi 21:12, Na silaha za Kristo zina nguvu sana sio tu kumlenga adui lakini pia kuangusha ngome.
Maboma na makao ya shetani.
2 Wakorintho 10:4-5
[4](maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) [5]tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
[4](maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
[5]tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
Lakini Nguvu ya silaha hizi hutegemea na hali ya mtu kiroho katika maeneo matatu;
1) kimaombi,
2)Utakatifu
3) Injili.
Mwamini wa namna hii ambaye huchukia dhambi, huubiri injili na huzingatia kudumu katika maombi ya masafa,
Kiroho ni askari imara na mwenye silaha zenye nguvu sana, ziwezazo kumuharibu ibilisi.
Kuwa askari kamili wa Kristo
Mtambo/mitambo ni nini kibiblia?
Na kipenu ni nini (Isaya 1:8)
Kutawa ni nini? Sawasa na Luka 1:24
Warumi 6:23
[23]Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Kwenye vifungu hivyo tunaonyeshwa kuwa Mungu hutoa zawadi(karama), lakini dhambi inalipa mshahara.. Na mpaka ilipe mshahara ni lazima kazi fulani ilifanyika..
Watu wengi hawajua kuwa kila tendo moja la dhambi, huhesabu mshahara fulani na mwishoni mtu huyo hulipwa wote, hata kama hakujua.
Unapokwenda kuzini leo, unarudia tena na kesho, na kesho kutwa hivyo hivyo, mshahara unajilimbikiza, siku isiyo na jina utashangaa tu ghafla mshahara wako huo hapo umekufikia…
Ndio hapo mauti ya kiroho au ya kimwili au ya jambo fulani humfikia mtu.
Sasa inapofikia wakati wa mshahara wengi hujifanya haiwahusu, lakini utaupokea tu.. upende usipende…wengi humdharau Yuda kwanini alijinyonga, si kwamba alipenda lakini ulikuwa ni wakati wa mashahara, ukiona leo watu wanakutana na madhara makubwa kwasababu ya dhambi zao, sio kwamba wana bahati mbaya, bali ni wakati wa mshahara.
Epuka dhambi, ikimbie dhambi.
Shalom
WhatsApp
Yeremia 2:13
[13]Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji.
Ndugu Ipo tofauti kati ya chemchemi na birika, chemchemi ni chanzo cha asili ambacho hutoa maji yake yenyewe, haihitaji kuchimbwa, wala kukarabatiwa lakini birika ni hivi visima ambavyo mtu hutumia jasho lake kuchimba na hutegemea mvua ili kuwa na maji, lakini bado huvujisha maji yake chini ya ardhi ndio maana baadaye hukauka…maji ya visima kikawaida hayawagi masafi sana kwasababu hayatembei, ni rahisi kuona vyura, ngala, ruba, tofauti na ya chemchemi.
Sasa Bwana anasema watu wake wamefanya makosa MAWILI. Kwanza wamemuacha yeye aliye chemchemi ya maji ya uzima, Maana yake wana kiu, lakini hawataki maji yaondoayo kiu…hicho huitwa kiburi, au dharau na matokeo ya kiburi ni maangamizi. Ni sawa na mtu anajijua kabisa ni mgonjwa halafu analetewa tiba anasema sinywi dawa zako.
Lakini kama hilo halitoshi, wanaenda kufanya kazi ya kuunda chemchemi zao bandia, kwa kuchimba wenyewe ili wajihifadhie maji yao ambayo ni ya muda…hii ndio huitwa ibada ya sanamu..watu wanapoona fedha inaweza kusimama badala ya Mungu, hiyo ni sawa na kujichimbia birika ..wanapoona elimu, ushirikina, anasa, ulevi, ujuzi..vinatosha kuwa mbadala wa Mungu ni kujichimbia birika lako mwenyewe..
Ndio maana wanataabika, kutafuta ukweli wote ndani yake hawapati, wanapata raha za kitambo baada ya hapo ni majuto kurudi.
Ndugu tulia kwa Kristo ambaye alishamaliza kuunda chemchemi yake, kwake yeye huhitaji kutendea kazi, nenda tu unywe maji, kiu ya dhambi na mambo mengine maovu ya kidunia ife, uishi maisha ya amani na kustawi. Maji hayo ukinywa hata ukifa utakuwa unaishi, na kumpokea Yesu ndio kuyapokea maji. Ukimwamini Yesu na kumfanya Bwana na mwokozi wa maisha yako, na kumtii baada ya hapo ujue ndani ya roho ya maji yameshawasili.
Yohana 4:13-14
[13]Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; [14]walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
[13]Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;
[14]walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
Achana na mabiriki.
Mungu atusaidie.
Nini maana ya “Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, ndivyo alivyo mwanamke mzuri asiye na busara.”
Mithali 11:22 “Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, ndivyo alivyo mwanamke mzuri asiye na busara.”
Kabla ya kujua kwa undani maana ya mstari huu, hebu tujifunze kidogo juu ya Nguruwe, na pete inayowekwa puani mwake.
Nguruwe ni mnyama mwenye sifa ya uchafu, na asiyekuwa na ustaarabu, anaweza kuoshwa na baada tu ya kumaliza kuoshwa akarudi kwenye matope..Biblia inatuthibitishia hilo..
2Petro 2:22 “Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.”
Sasa pamoja na tabia hiyo ya uchafu na kukosa ustaarabu nguruwe waliyonayo, bado wana tabia nyingine ya kuchimba chimba chini ya ardhi, au kwenye mashamba na kwenye zio kwa kutumia “pua zao” kwa lengo la kutafuta chakula, au utofauti wa mazingira.
Tabia hiyo ya kuchimba chimba kwa kutumia pua, inawafanya kubeba tabia nyingine ya uharibifu usiokuwa wa kawaida,
Sasa wafugaji wa nguruwe ili kulidhibiti hilo, huwa wanaweka pete katika pua zao lengo ni ili wanapojaribu kuchimba chimba kwa kutumia pua zao, basi ile pete iliyowekwa puani iwaumize na waache au kupunguza tabia hiyo ya uharibifu.
Sasa hizi pete si za urembo, bali zinakuwa kama Hereni kwenye pua ya nguruwe, na zinakuwa ni za chuma..tazama picha juu..
Sasa inapotokea Mfugaji anamwekea nguruwe pete ya dhahabu badala ya chuma isiyo na thamani..itakuwa ni jambo la ajabu sana na la kushangaza..kwani nguruwe kamwe hajawahi kuthamini kitu cha thamani, na hata yeye mwenyewe hajithamini soma Mathayo 7:6
Sasa anapowekewa kitu cha thamani puani mwake, ni kitu cha ajabu na kinachoshangaza..
Kwa mantiki hiyo hiyo Biblia inajaribu kuufananisha uzuri wa mwanamke na PETE YA DHAHABU, na mwanamke asiye na busara inamfananisha na NGURUWE.
Kwamba Mwanamke aliye na uzuri wa uso halafu akakosa busara ni sawa na kitu cha thamani kilichowekwa mahali pasipostahili.
Mwanamke mzuri wa uso/wa nje halafu hana heshima kimwonekano ni sawa na pete puani mwa nguruwe,
“Uzuri” na “Busara” ni lazima viende pamoja, lakini ukiwa ni mzuri halafu huna busara ya kiMungu, unafananishwa na nguruwe.
Sasa swali ni je hii busara inapatikana wapi?
Chanzo cha Busara halisi ni YESU KRISTO, kwamba unapompokea YESU na kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha, basi hapo tayari umeshafungua mlango wa busara kuumbika nakuanza kufanya kazi ndani yako.
Na kazi hiyo ya kujaza busara ndani yako ni ya Roho wa Mungu atakayeingia ndani yako baada ya wewe kuokoka….Utaanza kuona kiwango chako cha hekima kinaongezeka, na ueledi katika masuala ya kiroho na kimwili.. na hiyo busara itaulinda uzuri wako wa nje na ule wa ndani kama maandiko yanavyosema..
Mithali 2:10 “Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza nafsi yako; 11 Busara itakulinda; Ufahamu utakuhifadhi”
Mithali 2:10 “Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza nafsi yako;
11 Busara itakulinda; Ufahamu utakuhifadhi”
Wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale nguruwe. Akawapa ruhusa.
USITUPE LULU ZAKO MBELE YA NGURUWE.
Je? ni sahihi kwa watu wa MUNGU kutumia majina ya wanyama kuwaita wengine.
Inaruhusiwa Kula nyama ya Nguruwe kwa Mkristo wa Kweli?
Kwanini Mungu aliwazuia walemavu wasimtumikie madhabahuni kwake?(Walawi 21:16-24)
Zaburi 42:8
[8]Mchana BWANA ataagiza fadhili zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami,..
Biblia inataja nyakati mbili, ambazo mwamini anazipitia..nazo ni mchana na usiku.
Mchana ni nyakati za matumaini, nyakato za kuona njia, za kufanikiwa, za amani…hizi ni nyakati ambazo Bwana anasema ataagiza fadhili zake…maana ya fadhili ni kujitoa kwa upendo wa juu sana..Mungu huwafadhili watu wake hata katika nyakati za furaha, na amani.
Lakini pia anasema wakati wa usiku wimbo wake bado utakuwa nasi…usiku ni wakati wa huzuni, wakati wa upweke, wakati wa ukame wa kiroho, wakati wa majaribu, na mapito n.k.
Ni nyakati ambazo huoni chochote…kwasababu usiku sikuzote ni nyakati za ukimya na upofu..
Lakini pia huko Bwana anasema juu ya watu wake kuwa WIMBO WAKE, utakuwa pamoja nao.
Wimbo humaanisha faraja, kicheko, shangwe, yaani hatawaacha wawe kama walio gizani wanyonge, wapweke, bali kama watu wafurahishwao na nyimbo nzuri sana..
Kama mwana wa Mungu, nyakati za majaribu, Bwana yupo pamoja na wewe, nyakati ambazo huzielewi upo wimbo wake ndani yako.
Wakristo wafikiapo hatua hii huukimbia wimbo wa Bwana na kutazama zaidi changamoto zao, shida zao, magumu yao, na mengineyo kana kwamba Mungu amewaacha,
Lakini kama ukibakisha fikra zako kwake…utaona bubujiko kubwa sana likitiririka ndani yako, kwa jinsi ile ile ulivyokuwa katika nyakati za nuru..
Kwasababu hii ni ahadi yake. Na kamwe hawezi kudanganya. Unapojifunza kutulia uweponi mwa Mungu, kimaombi, kwa kutafakari, uwapo kwenye hizo nyakati hafifu..ghafla tu utaona furaha, amani, ushindi, kicheko, uwepo wa Bwana vinajaa ndani yako.
Kamwe usiukandamize wimbo huu?
UYATIE MACHOZI YANGU KATIKA CHUPA YAKO EE! BWANA.
JITIE NGUVU KWA BWANA MUNGU WAKO.
MAISHA YA UVUGUVUGU, YANAMFANYA MUNGU AUMWE.
Mithali 29:20
Je! Umemwona mtu mwenye kuhamaki katika maneno? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye
Mtu mwenye kuhamaki.
Ni mtu anayezungumza maneno kwa haraka, yaani anayezungumza bila kufikiri, au kujizuia.
Vitu kama mizaha, ugomvi, hasira, uongo, na mafarakano, huzaliwa na tabia kama hii ya watu kunena bila kufiriki.
Kwamfano, mtu anaweza kukutukana, na wakati huo huo hasira ikawaka ndani, sasa kwasababu huwezi kujizuia, unajikuta unarudisha majibizano, hatimaye na wewe unafungua kinywa chako unatukana.
Au labda unatambua jambo Fulani ambalo si jema, na pengine ukilisema linaweza lisiwe na maana yoyote, kinyume chake likazua ugomvi, au kumuabisha mwingine, au sintofahamu, lakini wewe kwasababu huwezi jizuia unalisema, mwishowe matatizo yanazuka makubwa yasiyokuwa na lazima.
Watu wanaoapa, ni matokeo ya kunena bila kufikiri, mafarisayo ambao walitenda dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ni kwasababu ya maneno ambayo hayana hekima nyuma yake.
Mathayo 12:36 Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.
Mpaka hapo unaweza kuona ni kwanini mpumbavu anaweza kuonekana ana afadhali kuliko mtu mwenye kuhamaki.
Mstari huu unatukumbusha nguvu iliyopo katika maneno, biblia inasema ulimi ni kama moto ni kiungo kidogo lakini kinawasha misitu, hivyo hatuna budi kuwa wazito katika kunena, tukifiri kwanza ndipo tuseme. Yakobo 1:19
19 Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
Maneno yana nguvu, kila siku yatupaswa tujifunze kudhibiti vinywa vyetu.
KUMBUKA NI AMRI MPYA!
KARAMA TUZIPATAZO KWA MSAADA WA WATU WENGI.
JIBU: Wakiwa jangwani wana wa Israeli walitenda makosa ya aina mbili.
Makosa yaliyopoteza Ahadi ndio yalikuwa yale ya kutokuamini. Mfano Mungu alipowatoa jangwani, na kuwavusha, mara nyingi walionyesha hali ya kutoamini, Kosa ambalo liliwafanya Mungu aghahiri kuwafikisha kule alipowaahidia, ambapo ni nchi ya Kaanani ibubujikayo maziwa na asali, Na kilele cha kosa hilo kilikuja pale wale wapelelezi waliporudi katika kuichunguza nchi, na kutoa ripoti za kule, kwamba wao wanaonekana kama mapanzi, hivyo wote wakaanza kulia na kutaka kurudi Misri, Ndipo Mungu akakasirika sana na kuapa kuwa wote hawataiona hiyo nchi ya Kaanani isipokuwa Kalebu na Yoshua, kwasababu wao hawakuonyesha kutokuamini.
Hesabu 14:21-24
21 lakini hakika yangu, kama niishivyo, tena kama dunia hii nzima itakavyojawa na utukufu wa Bwana; 22 kwa sababu watu hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na ishara zangu, nilizozitenda huko Misri, na huko jangwani, pamoja na haya wamenijaribu mara hizi kumi, wala hawakuisikiza sauti yangu; 23 hakika yangu hawataiona hiyo nchi niliyowaapia baba zao, wala katika hao wote walionidharau hapana atakayeiona; 24 lakini mtumishi wangu Kalebu, kwa kuwa alikuwa na roho nyingine ndani yake, naye ameniandama kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo aliyoingia; na uzao wake wataimiliki
Lakini hiyo haikumaanisha kuwa hawatakwenda mbinguni, kwasababu wapo waliotubu,hata wakati ule ule
Kwahiyo kusema adhabu ile ndio iliwapelekea moja kwa moja kupoteza mbingu si sahihi.
Kwasababu Mungu aliendelea kutembea nao kwa wingu lake, baadaye akawainua viongozi, wa kuwaaamua na Pamoja na wazee, akawamwagia Roho wake, (Hesabu 11:25). Hivyo kama Mungu kasingekuwa nao, basi hayo yote yasingefanyika, kwasababu Mungu hawezi kuwaongoza wafu.
Lakini yapo makosa ambayo yaliwagharimu adhabu ya kupoteza kabisa uzima wa milele. Na makosa kama hayo ndio yale ya makusudi kabisa, mfano wa hayo ni yale ya kuvunja amri za Mungu, kama vile kutengeneza sanamu ya ndama na kuiabudu, Kuzini, kuwa na miungu mingine, na kuhalifu sabato za Mungu .
Makosa kama hayo ndio yaliyopelekea kupoteza uzima wa milele, ndio maana ukichunguza utaona watu kama hawa walipokea adhabu za moja kwa moja. Hivyo ni kuwa makini sana na neema ya Mungu.
Hata sasa, zipo dhambi za aina mbili zinazozungumziwa kwenye maandiko, dhambi za mauti, na dhambi zisizo za mauti.
Kwa urefu wa maelezo yake, pitia hapa>>> DHAMBI YA MAUTI
Mungu akubariki.
Je shauri la kuipepeleza Kanaani lilitoka kwa wana wa Israeli au kwa BWANA?
Kwanini Roho Mtakatifu amzuie Paulo kuipeleka injili Asia? (Matendo 16:6-7).
Yohana 13:34
[34]Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
Hapo mwanzo nilipokuwa nautafakari huu mstari, nilijiuliza maswali Yesu anaposema “AMRI MPYA..
Ni amri ipi hiyo mpya?
Maana ukitafakari anasema “mpendane” kwani kupendana ni amri mpya?
Mbona ilikuwepo tangu zamani? Na ilijulikana
Mambo ya Walawi 19:18
[18]Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi BWANA.
Kupendana kulifundishwa tangu zamani za torati…lakini mpaka Kristo anasema amri mpya maana yake kupendana anakokusema yeye ni tofauti na kule kulivyodhaniwa…
“Ndio maana akasema…Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.”
Yaani mpendane kwa mfano wa upendo wangu, sio mfano wa upendo mwingine.
Upendo wa upeo.
Yohana 13:1
[1]Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo.
Upeo ni ukomo wa mwisho kabisa…Yesu hakutupenda kwa wakati fulani tu…bali alitupenda (sisi tuliomwamini) mpaka mwisho, kabisa kutoka moyoni..
Ikiwa na maana alipiga gharama ikitokea huyu amenisaliti, Amenikana, amenizunguka…je nitakoma kumpenda?…hivyo akaamua kukubaliana na yote…liwalo na liwe nimempenda, na nitampenda mpaka mwisho..
Ndio maana ijapokuwa alijua Yuda atamsaliti, na Petro atamkana, hakuacha kuwapenda…sasa huo ndio upendo wa Kristo mpya..upendo wa upeo
Leo ni rahisi kupenda mtu kwa mema, au mazuri anayoyadhihirisha sasa…lakini ikitokea baadaye yule uliyemsaidia anakusaliti, uliyemhudumia anakudharau, uliyemsomesha hatimaye amekuwa na cheo kikubwa kuliko wewe sasa anakucheka,..hapo hapo unaanza kuumizwa, hata kumchukia, na kumlalamikia…sasa huo sio upendo wa upeo….ni upendo wa nyakati…lakini ikiwa anakutendea mambo yote hayo halafu hujali hapo ndio upendo ule mpya wa Kristo anapodhihirika.
Bwana anataka tupige gharama ya kuanzia mwanzo hadi mwisho…ukiamua kumpenda mtu..basi mpende daima. Bila sharti.
Upendo mpya.. ni ule wa kupenda wanaokuchukia, ule wa zamani ulikuwa mpende akupendaye, asiyekupenda achana naye.(Mathayo 5:43-44).. kilele cha upendo huu mpya ni kuwa tayari kugharimika lolote kwa ajili ya wengine..(Yohana 15:13)
Je amri hii mpya tunayo?
2 Yohana 1:5
Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.
Bwana awe nawe.
Shalom.
NYAKATI TOFAUTI- TOFAUTI ZA UPENDO.
JAWA NA UPENDO UNAOTAFUTA.
JE UPENDO WAKO UMEPOA?