SWALI: Tukisoma Ufunuo 2:17 inasema “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”..Ningependa kufahamu Sentensi hiyo ina maana gani? kwanini liwe sikio?.
JIBU: Kwasababu kuna uwezekano kabisa mtu akawa na masikio lakini asisikie!
Bwana Yesu alisema…katika Marko 8: 18
“Mna macho, hamwoni; mna masikio, hamsikii? Wala hamkumbuki?”..
Hao si viziwi Bwana aliokuwa anazungumza nao, wala sio vipofu! Bali ni mitume wake ndio aliokuwa anawaambia maneno hayo.
Kwahiyo kusikia kunakozungumziwa hapo ni kusikia kwa masikio ya ndani na si ya nje! (Yaani kuwa na uwezo wa kukichambua na kukielewa kile kitu kwa undani wake kama kinavyotakiwa kieleweke).
Hivyo na sisi tunaposoma Biblia tunapaswa tuisikie sauti nyuma ya kile tunachokisoma sio tusome tu kama habari..hapana bali kwa ufunuo…
Tunapaswa tuisikie SAUTI ya NENO lake, na sio Neno lake tu peke yake, wengi tunaisoma biblia lakini hatuisikii sauti nyuma ya kile tunachokisoma..Angalia hapa..
Zaburi 103:20 Mhimidini Bwana, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake.
Na ndio maana tunabakia kuona kama ni hadithi fulani tu Zilezile zinazojirudia kila siku.
Kwamfano Bwana aliposema kimwingiacho mtu hakimtii unajisi bali kimtokacho, hatupaswi tuanze kutafakari juu ya vyakula fulani tunavyokula kama nguruwe, kambale na nyama nyingine, au kuanza kutafakari juu ya vitu vitutokavyo mwilini kama vile majasho na mikojo n.k..badala yake tunapaswa tuelewe kwa sikio la ndani kuwa vitu vitutokavyo ndani kama vile, tamaa, matusi wivu, uasherati n.k ndio vitutiavyo unajisi, kwa maana vinatoka moyoni…Na mambo mengine yote tunapaswa tuyasikie hivyo hivyo kwa masikio la ndani.
Ndio maana sehemu nyingi utamwona Bwana akisisitiza neno hili mwenye masikio na asikie.
Bwana akubariki.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
HATARI YA KUHUBIRI INJILI TOFAUTI NA ILIYOANDIKWA KWENYE BIBLIA.
ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!
UFUNUO: Mlango wa 18
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
About the author