Nini maana ya ”Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana”?

Nini maana ya ”Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana”?

Je! katika biblia mstari huu una maana gani? ”Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza’’? (Mithali 11:1)? ..Hiyo mizani ya hadaa ni ipi?


JIBU: Katika maisha ya kawaida Bwana anataka tuwe na haki, katika mambo yetu tunayoyafanya kila siku iwe ni katika biashara zetu au kazi zetu…Unapouza kitu uza kulingana na thamani ya kitu chenyewe unachouza, usizidishe thamani ya kitu kile ili upate faida kubwa vile vile usipunguze kipimo cha kitu kile ili upate faida kubwa…

USIPANDISHE THAMANI.

Kwa mfano kama wewe ni muuzaji wa mchele, na umenunua kilo moja kwa shilingi elfu mbili, na bei inayoziwa sokoni ni shilingi elfu na mia tano kwa wateja…Na unajua kabisa faida yako inapaswa iwe ni shilingi mia tano kwa kila kilo, au ikizidi sana mia 7.

Lakini wewe unakwenda kuuza kwa bei ya juu kuliko inavyotakiwa ili wewe upate faida kubwa bila kujali kuwa unamkandamiza yule unaye muuzia kisa tu anaouhitaji mkubwa wa kitu hicho..Labla tuseme unauuza mchele ule kwa shilingi elfu 4 kwa kilo moja..Hivyo kwa kufanya hivyo, Ni machukizo kwa Bwana. Hiyo ni mizani ya hadaa, hutendi haki.

USIPUNGUZE KIPIMO;

Vilevile Bwana hapendezwi na kupunguza kipimo cha bidhaa ile kwa hila, kwamfano unapunguza kwa makusudi kiwango cha upimaji, aidha katika mizani yako ili usiuze kingi upate faida kubwa..Hilo nalo ni chukizo kwa Bwana…Hiyo nayo ni mizani ya hadaa, hutendi haki.

Vilevile katika kazi nyingine zote tunazozifanya iwe ni kwa Mungu, au mashuleni, au  mahakamani, tunapaswa tuamue kwa haki bila kumpendelea mtu, kwa kutokujali fedha, au heshima, au cheo, au jinsia,..Bwana anapenda haki, na palipo na haki ndipo kiti chake cha enzi kilipo…..(Zaburi 97:2)

Zaburi 89: 14 Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako, Fadhili na kweli zahudhuria mbele za uso wako.

Na ndio maana biblia inasema .. Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu. (Mathayo 5:48)

Bwana akubariki.

Mada Nyinginezo:

TWEKA MPAKA VILINDINI.

WALIO NA HEKIMA NDIO WATAKAOELEWA.

UNYAKUO.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments