Ni kura ya aina gani waliipiga wale watu waliosafiri na Yona..hata ikamwangukia Yona? Na je! Mungu anatumia kura kuchagua watu?
JIBU: Biblia haijasema ni kura gani ilipigwa pale, kama ni ya kurusha kete au kwamba kila mmoja aliandika maoni yake binafsi na walipoyaleta yote yakaonekana yanamlenga Yona…Hakuna ajuye, na wala biblia haijaandika..Lakini yote katika yote ni kwamba kura ilipigwa pale na ikamwangukia Yona.
Kikubwa tunachoweza kujifunza ni kwamba..Mungu anaweza kutumia njia yoyote kukamilisha kusudi lake..anaweza kutumia njia iliyo rasmi au isiyo rasmi…Kwamfano kama wewe ni mwanafunzi mzuri wa Biblia utagundua kuwa Mungu alimpa Daudi ufalme wote wa Israeli kwa njia ya fitina..Mungu Alimwahidia atakuwa Mfalme juu ya Israeli yote na akampaka mafuta kwa mikono ya Nabii Samweli…lakini siku ilipofika ya unabii huo wa kuwa Mfalme wa Israeli kutimia..hakupata ufalme kwa njia ya uchaguzi bali kwa njia ya fitina. Yaani mfalme aliyekuwa madarakani (mtoto wa Sauli )alifanyiwa fitina ndipo Daudi akaingia madarakani….
Kwani siku hiyo walitokea tu watu Fulani waliokuwa wanaishi kwenye nyumba ya Mfalme na hao watu wakamvizia mfalme aliyekuwa madarakani wakampiga na kumuua na kumkata kichwa,..na kumpelekea kile kichwa Daudi na kumwambia leo Mungu amewalipiza kisasi maadui zako. Ingawa Daudi hakukubaliana na uovu wao…lakini kukawa hakuna namna ni lazima kiti cha ufalme kikaliwe na mtu mwingine na huyo hakuwa mwingine zaidi ya Daudi (kasome 2Samweli 4:5-12).
Kwani Israeli walipoona mfalme wao kauawa kukawa hakuna namna zaidi ya kumweka Daudi Madarakani awe mfalme.. Na unabii wa yeye kuwa Mfalme juu ya Israeli yote ukatimia pale.
Hali kadhalika Mungu anaweza kumchagua mtu kwa njia yoyote ile iwe rasmi au isiyo rasmi..Na anaweza kumtumia mtu yoyote Yule kukamilisha kusudi lake, anaweza kumtumia mwovu au mwenye haki…kwa jinsi apendavyo yeye. Akitaka kumweka mtu mahali anaweza kutumia kura au asitumie kura. Mathiya alichaguliwa kwa kura kuwa miongoni mwa Mitume 12 wa Bwana Yesu kuchukua nafasi ya Yuda. Lakini Petro na Mitume wengine hawakuchaguliwa kwa kura…Na hiyo haikumfanya Mathiya asiwe miongoni mwa wale mitume 12.
Kadhalika Yona alichaguliwa kwa kura ili kuadhibiwa na Mungu. Mungu angeweza kuwaonyesha maono wale watu kuwa Yona ndio chanzo cha matatizo, lakini pale hakuitumia hiyo njia…angeweza kumtuma malaika akawatokea na kuwaambia Yona ndie chanzo cha lile tatizo lakini haikumpendeza..
Hata katika chaguzi za viongozi wa shule, kijiji, mtaa, au nchi…wote wanaochaguliwa na kushika nafasi hizo ni Mungu ndio kawaweka pale…Iwe wamewekwa kwa njia iliyo halali au isiyo halali kama ya uwizi wa kura au la!,..hiyo haijalishi..Ni Mungu ndio kawaweka pale..(Siku ya mwisho ndio watakwenda kujibu kwanini waliiba kura au kwanini hawakuwa waaminifu katika nafasi hizo)..Lakini maadamu tayari wapo katika hizo nafasi ni Mungu ndiye kawaweka…
Maraisi wote waliopo madarakani ni Mungu ndiye kawaweka katika nafasi hizo haijalishi waliiba kura au hawakuiba..haijalishi ni madiktekta au sio madiktekta, haijalishi wanamjua Mungu au hawamjui..Ni Mungu ndiye kawaweka kwa kusudi lake maalumu…wengine kwa kusudi kama la Farao, wengine kama la Yeroboamu, wengine kama la Nebukadneza, wengine kama la Mfalme wa Ashuru, wengine kama Manase, wengine kama Hezekia… Kila mmoja kawekwa pale na Mungu kwa kusudi maalumu…
Bwana akubariki.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
About the author