KUOTA UMETUMBUKIA SHIMONI.

KUOTA UMETUMBUKIA SHIMONI.

Ogopa wadanganyifu, ambao wanakuambia suluhisho la ndoto Fulani uliyoota labda tuseme kuota umetumbukia shimoni, au umekimbizwa na nyoka,au umezama kwenye maji au unafanya uasherati na mtu usiyemjua kwamba ukanunue dawa yao Fulani itakusaidia kutatua hilo tatizo.. Wengi wanaokuambia hivyo kama si washirikina basi uwe na uhakika ni matapeli.. Ndoto, au maono, ni mambo yanayotoka ndani ya mtu, yaani katika utu wake wa ndani, Hivyo hayawezi kutibiwa kwa tiba za nje, kama vile dawa na vidonge, Ni sawa na mtu aliyefiwa, huwezi kumwambia nenda kameze PAIN KILLER, tatizo lako la huzuni litakwishwa, badala yake utatumia njia ya kumfariji, ndipo hapo atakapogangika kwasababu ugonjwa wake ni wa moyoni na si nje..

Hivyo ni vizuri kufahamu, ndoto asili yake ni rohoni, Kwahiyo tiba yake ni lazima iwe ya rohoni na si ya  nje.

Kwa utangulizi:

Zipo ndoto za aina tatu.

  1. Ni zile zinazotokana na Mungu: Ambazo hizi zinachukua sehemu ya wastani ya ndoto anaziziota mtu kila siku.
  2. Ndoto zinazotokana na shetani: Hizi nazo zinachukua sehemu ya wastani wa ndoto mtu anazoziona kila siku.
  3. Ni zile zinazotokana na mtu mwenyewe: Hizi ndizo zinazochukua sehemu kubwa sana ya ndoto mtu anazoziota kila siku.

Sasa kama kuota umetumbukia shimoni: Mara nyingi wengine wanaota wapo ukingoni mwa shimo wanakaribia kuanguka, wengine wapo tayari chini  kabisa kwenye  shimo refu lenye giza, wengine wananing’inia ikingoni mwa shimo na kila wanapojaribu kujivuta juu watoke wanajiona ni wazito sana, wanahitaji msaada..n.k. zote hizo ujumbe wake ni mmoja. Kuwa maisha yako yapo hatarini kama hutachukua uamuzi ulisohihi Mungu anaokuagiza uufanye.

Ikiwa wewe umeokoka (yaani maisha yako yamefichwa ndani ya YESU KRISTO):  Na ndoto kama hii kuota umetumbukia shimoni imekujia kwa uzito sana, au imejirudia rudia mara nyingi, basi ongeza umakini wako kwa MUNGU,kwasababu mahali unaweza kwenda kukwamba usisonge mbele katika imani yako, pili omba sana, hususani katika mazingira uliyopo, na mambo unayoyafanya yote hakikisha unamtanguliza Mungu kwanza..Na Bwana atakuvukisha au kukukwepesha kabisa na majaribu hayo.

Soma  (Yeremia 38:6, Maombolezo 3:52-57).

Lakini kama wewe hujaokoka na unafanya mojawapo ya hivi vitu:

  • Wewe Ni mzinzi: basi ujue Mungu anakupa ujumbe huu..

Mithali 22:14 Kinywa cha malaya ni shimo refu; Anayechukiwa na Bwana atatumbukia ndani yake.

Mithali 23: 27 Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni rima jembamba.

Ukiendelea kuwa na tabia hiyo, mwisho wako utakuwa ni mbaya..Utaingia mahali ambapo utashindwa kutoka milele.

  • Ikiwa hutendi haki: Au unamuundia mwenzako visa, ili asisonge mbele, basi andiko lako ni hili.

Mithali 26: Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia.

Zaburi 7: 14 Tazama, huyu ana utungu wa uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo.

15 Amechimba shimo, amelichimba chini sana, Akatumbukia katika handaki aliyoifanya!

16 Madhara yake yatamrejea kichwani pake, Na dhuluma yake itamshukia utosini.

Hayo yote yanajumuisha watu wote waovu..Kuwa hatma ya maisha yao ni shimo refu la mauti kama hawatatubu.

Hivyo yatengeneza mambo yako kwa Mungu haraka iwezekanavyo..Kumbuka Yesu ndio njia, na kweli na Uzima (Yohana 14:6), anakuonyesha hivyo kwasababu anakupenda ili utubu umgeukie yeye, uache dhambi ayasafishe maisha yako. Ni nani ajuaye kuwa leo kukukutanisha na ujumbe huu ni kwa makusudi yake maalumu UOKOKE LEO?..Hivyo usipuuzie wito huo, mruhusu leo ayaokoe maisha yako akutoe katika shimo hilo refu la mauti ambalo upo sasa, au kama haupo basi siku si nyingi utakuwepo,ukiendelea na tabia yako.

Lakini  Ikiwa unatii na upo tayari kufanya hivyo sasa.

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Fanya Hivyo na Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

CHAGUA NI JIWE LIPI LITAKALO KUFAA KWA UJENZI.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

MAONO YA NABII AMOSI.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

NINI KINAFUATA SIKU ILE ILE YA KUOKOKA!

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments