USINIPITE MWOKOZI

USINIPITE MWOKOZI

Usinipite Mwokozi wangu..

Mwanzo 18:1 “Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari.

2 Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,

3 akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba USINIPITE SASA MIMI MTUMWA WAKO.

4 Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu.

5 Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema”.

Hapo Ibrahimu Ibrahimu, alitokewa na watu watatu na hakujua kuwa..mmojawapo wa wale watatu alikuwa ni ELOHIMU (MUNGU) mwenyewe na wale wengine wawili waliosalia walikuwa ni malaika watakatifu. Ambao baadaye ndio waliokwenda nchi ya Sodoma na Gomora..Lakini Elohimu ambaye ndiye aliyekuwa mnenaji mkuu alibaki na Ibrahimu nyuma kuzungumza naye..Na Bwana Mungu akamfunulia siri kubwa sana ya jambo analokwenda kulifanya Sodoma na Gomora. Na alipomfunulia siri hizo ndipo akaenda zake.

Hapa Mungu aliamua kujidhihirisha kimwili mbele ya Ibrahimu lakini kwasasa anatembea kwa Roho.

Bwana anatabia ya kutembea huku na huko duniani kote..Sio lazima aonekane kwa macho kama alivyoonekana kwa Ibrahimu…lakini anatembea kwa namna ya Roho..Yaani Roho yake inazunguka duniani kote, inapita Taifa kwa Taifa, inapita mkoa kwa mkoa, mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyuma, inakatiza mpaka vichochoro vyote na kona zote ambazo hata watu hawajafika…inakwenda mpaka katikati  ya mbuga za wanyama na mapori ya ndani, inaingia mpaka kwenye migodi mikubwa na inamfikia mpaka mtu wa mwisho ambaye anapumua ulimwenguni…Ipo inawapeleleza wanadamu kila siku na inafikisha ripoti kwa Mungu. Roho hiyo imejigawanya mara saba (yaani Inatenda kazi kwa namna saba na nyakati saba) na ndio macho ya Mungu.

Zekaria 4:10 “…. hizi saba ndizo macho ya Bwana; yapiga mbio huko na huko duniani mwote”

Na tena biblia inasema katika Ufunuo juu ya Roho hiyo ya Mungu..

Ufunuo 5.6 “Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni ROHO SABA ZA MUNGU ZILIZOTUMWA DUNIANI KOTE.

Sasa hii Roho ya Mungu ndiyo inayoZURU watu..kumbuka ni KUZURU na sio KUDHURU..Kudhuru ni kuharibu kitu lakini KUZURU ni KUTEMBELEA KITU.  Hivyo Roho ya Bwana yenyewe inatuZURU (Tembelea) sisi kila siku. Ipo ndani yetu kila siku kila saa, lakini ipo nje inatembea huko na huko kama Mtu atembeavyo. Inatenda kazi kwa namna nyingi.

Sasa inapopita na kukutana na anayestahili Baraka basi anabarikiwa, ikimkuta asiyestahili baraka basi inampita.

Kwahiyo tunaposali ni vizuri pia kuomba…Ee Bwana UNAPOZURU WENGINE kuwapatia Mema…USINIPITE MWOKOZI.

Na pia ni wajibu wetu kujiweka katika usafi, kwasababu kwasababu Mungu ni mwenye haki, hawezi kamwe kumpa mtu asiyestahili haki, ampatie haki…hilo halipo kwa Mungu..vinginevyo atakuwa sio Mungu wa Haki…Ili awe Mungu wa haki ni lazima ampatie mtu kile anachostahili na sio kile asichostahili..Hivyo akikuzuru na kukukuta unafanya uasherati hawezi kukubariki..akikukuta unakula rushwa vile vile hawezi kukubariki…akiyazuru maisha yako na kukukuta unaishia na mwanamume/mwanamke ambaye hamjafunga ndoa atakupita..

Lakini yote katika yote usilisahau Neno hilo katika sala…USINIPITE MWOKOZI, unapozuru wengine…unapowapa wengine thawabu usinipite…Ibrahimu alimwambia Mungu USINIPITE MWOKOZI..Na pia hakumwambia tu kwa midomo bali kwa vitendo kwani tunaona alimtayarishia chakula..Na wewe na mimi ni wajibu wetu kuhakikisha tunamfanya Bwana asitupite kwa lazima..Kwa matendo yetu mema na kwa utoaji wetu tunamwambia Bwana usitupite mwokozi, kama yule mtunzi wa Tenzi alivyoandika.

Ubarikiwe.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

TENZI ZA ROHONI

SALA YA ASUBUHI

UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI.

JINSI SODOMA NA GOMORA ILIVYOKUWA INAVUTIA SANA..

USIKIMBILIE TARSHISHI.

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 2

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments