Kuhutubu ni nini?

Kuhutubu ni nini?

Kuhutubu linatoka na neno “kuhutubia”… ambalo chanzo chake ni “HOTUBA”.  Hotuba ni maneno yaliyoandaliwa ambayo mtu anaweza kuyazungumza mbele ya kadamnasi ya kuwafaa…yanaweza kuwa ya kimaendelea au ya kimikakati.

Tukirudi katika biblia….Kuhutubu ni tofauti na kuhutubu kwa watu wa kiulimwengu… Watu wa ulimwengu watahutubia mikakati ya kiulimwengu…lakini watu wa Mungu watahutubia maneno ya Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Sasa wachungaji na waalimu wanapolifundisha Neno la Mungu kwa uweza wa Roho Mtakatifu mbele ya mkutano hapo ni wanahutubu, yaani wanahutubia maneno ya Mungu ya uzima..

1Timotheo  5:17 “Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha”.

Matendo 20:7 “Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane”.

Lakini hali kadhalika watumishi wa Mungu, wenye karama ya kinabii wanaposimama mbele ya mkutano na kutoa maneno ya kinabii ya kuwajenga watu na kuwapa tumaini ya mambo yajayo hao pia ni WANAHUTUBU.

1Wakorintho 11:4 “Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake.

5 Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa”.

Kuhutubu kunakozungumziwa hapo ni kutoa unabii au kwa lugha ya kiingereza “to-prophesy”..

Shalom

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?

Mwaloni ni nini? Na je unafunua nini rohoni?

NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?

VICHEKESHO NA UTANI MADHABAHUNI

JE! MTUMISHI KUTOKUWA NA FEDHA NI ISHARA KUWA KUNA TATIZO KATIKA IMANI YAKE?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
9 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Nuru gakiza
Nuru gakiza
1 year ago

Naomba niwe natumiwa mafundisho haya mtumishi!

Victor Mwandunga
Victor Mwandunga
2 years ago

Amina. MUNGU akubariki sana kwa ujumbe huu mzuri

JOSEPH DEUS
JOSEPH DEUS
2 years ago
Reply to  Admin

Naomba niwe natumiwa mafundisho Kama aya mtumishi wa Mungu WhatsApp yangu 0714212416

Jackson samka
Jackson samka
3 years ago

Naomba niwe natumiwa mafundisho Kama aya mtumishi wa Mungu WhatsApp yangu 0763201757

Anonymous
Anonymous
3 years ago

Naomba niwe natumiwa mafundisho Kama aya mtumishi wa Mungu WhatsApp yangu 0763201757

Praygod amon
Praygod amon
4 years ago

natamani kuwa natumiwa mafunzo kama haya kwenye WhatsApp yang MUNGU awabariki sana (0678100220)