SHETANI ANAITHAMINI HATA MAITI YAKO.

SHETANI ANAITHAMINI HATA MAITI YAKO.

Biblia inatupa mwangaza wa jinsi shetani alivyomaanisha kweli kuwaangamiza wanadamu japokuwa sisi hatulijui hilo.. Unaweza ukadhani siku ukifa tu, ndio basi shetani anakuwa amemalizana na wewe. Huo mtazamo ni wakuuondoa kabisa kichwani..

Embu jaribu kifirikia kile kisa cha Musa, baada ya Kufa, ni nini kilitokea baadaye?..

Utasoma kwenye kitabu cha Yuda, Malaika Mikaeli alikuwa akihojiana naye sana na juu ya mwili wa Musa.. Tusome..

Yuda 1:9 “Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.

Kumbuka hiyo ni baada ya Mungu kumuona Musa ni mwaminifu na amevipiga vita vyema, mwendo ameumaliza, na Imani ameilinda, Na sasa baada ya kufa Mungu anampa maagizo malaika Mikaeli amchue aende kumzika mahali pa siri pasipojulikana na watu (Soma Kumbukumbu 34:5-6).. Lakini shetani kwa kulijua hilo kuwa hawezi kumpata Musa tena, hawezi kumletea tena jaribu ili atende dhambi amshinde kwani roho yake tayari haipo pale ilishamtoka na kwenda sehemu nyingine siku nyingi..

Lakini yeye bado aliona fursa ya kuushitaki na mwili wa Musa pia, alitaka Mungu auache tu ardhini, alitaka usizikwe kipekee vile na Mungu, au alitaka aupate yeye kwa shughuli zake za kuwapotosha watu waabudu mahali alipozikwa, au mifupa yake….shetani japokuwa alijua ni muozo tu ule, na mavumbi, lakini hata hilo alililia apewe, bado anashughuli nao.

Alikuwa anahojiana na Mikaeli, pengine kwa kumwonyesha ubaya wake aliokuwa anaufanya duniani au madhaifu yake, kama alivyokuwa anamshitaki Ayubu ili tu Mungu aghahiri asizike mwili wake kipekee..Lakini tunasoma alishindwa kwasababu Musa alikuwa ni mtakatifu wa Mungu.

Sasa tujiulize, ikiwa maiti tu ya mtakatifu, ibilisi anaigombania, mfano tu wa wale askari walioligombani vazi la Yesu pale msalabani, ambalo walijua halikuwa na faida yoyote kwao,..Sisi je tutawezaje kumkwepa kirahisi huyu adui wa roho zetu ikiwa hatutakuwa milki ya YESU KRISTO?

Shetani haitaki tu roho yako, ingekuwa heri aishie hapo ..Lakini Akishaipata bado atataka na familia yako pia, atataka na afya yako, atataka na watoto wako, atataka na nyumba yako, na mali zako ulizozitaabia… pengine, atapelekea mashitaka mbinguni kuwa hata hizo nguo unazovaa ni mali yake.. Na siku ile ukifa hata huo mwili wako, pia atautaka kwa Mungu..Sasa jiulize ikiwa wewe ni mwenye dhambi ni nini kitamshawishi Mungu asimpe vyote hivyo?

Ndio hapo Kaburi lako badala lilindwe na Mungu, ndio shetani analifanya kuwa VILINGE VYA WACHAWI WAKE, mwili wako uliozikwa kwa heshima na wabunge wenzake, unafukuliwa na wachawi ili kuchukuliwa viungo ambavyo vitawasaidia katika shughuli zao za kiganga..Si ni kwasababu wewe ni mali yake?..shetani kashinda hoja mbinguni juu yako…anazo point za kutosha za kupewa mwili wako, na Mungu ni Mungu wa haki, anahojiana na shetani na vile vile pia anampa haki zake kama anastahili.

Hata sasa bado ukiwa hai, hivyo vyote ulivyonavyo shetani anavijengea hoja kwa Mungu, kwanini visiwe vyake?….Umetoka kuzini, na umeshajua Neno la Mungu linakataza kufanya hivyo, unatoka asubuhi unakwenda kazini..wakati upo njiani shetani kashafika mbele za Mungu na kusema…mwangalie Yule mtu ambaye unasema ni mtumishi wako ametoka kuzini..na masaa chache tu alitoka kulisoma neno lako linalomwambia usizini..hivyo huyu ni wangu, nataka nimtumie majeshi ya mapepo nimuue!…na malaika wa Mungu wanapojaribu kutafuta hoja mbili tatu za kukutetea wanapokosa..shetani anapewa haki yake, na wewe unakabidhiwa chini ya mikono yake..kwasababu ni wake yeye…

hivyo unajikuta unapata matatizo ambayo si ya kawaida..

Ndugu haya mambo sio hadithi za kutunga ni vitu vinavyoendelea katika roho kabisa…Je unajua tafsiri ya jina “shetani”?…Shetani maana yake ni “mchongezi/mshtaki” biblia imetoa tafsiri yake hiyo…Hivyo kazi yake ni kukuchongea mbele za Mungu..hata unapochukia tu, tayari kashafika mbele za Baba kupeleka mashtaka..Hivyo sio wa kujiungamanisha naye kabisa.

Unaweza kuona tupo hatari kubwa kiasi gani ndugu yangu.. Ulimwengu huu ni wa mashaka na hofu ikiwa tu Yesu Kristo sio kimbilio lako. Aliposema pale Yohana 17:15 “Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu” . Alimaanisha kweli wale wanaomkimbilia watalindwa na Yule mwovu shetani, mshitaki wao.

Hivyo yasalimishe maisha yako leo kwa Kristo, ndani ya hichi kipindi kifupi tulichobakiwa kabla Kristo hajarudi. Dalili zote zinathibitisha Unyakuo ni wakati wowote,..Na shetani hilo analijua na ndio maana na yeye anafanya kazi sana kwasababu anajua muda wake ni mchache..

Hivyo ingia zizini mwa Bwana kama bado upo nje. Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kweli kuziacha, nenda kabatizwe kama ulikuwa hujafanya hivyo katika ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Yesu Kristo ambalo ndio jina la Baba, mwana na Roho Mtakatifu. Kisha utapokea Roho Mtakatifu ambaye ndiye atakayokusaidia na kukulinda hadi siku ile ya mwisho.

Ubarikiwe sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

MTU ASIYE PAMOJA NAMI YU KINYUME CHANGU.

NAO WAKADHANI YA KUWA YUMO KATIKA MSAFARA;

Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu ni wakina nani?

 

Je! Ni kweli ubatizo wa maji hatuuhitaji tena?

Kwanini Kristo hakuitwa Imanueli badala yake akaitwa Yesu?

JE NI DHAMBI KUWA NA MAHUSIANO KABLA YA NDOA?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments